Friday, March 30, 2018

KUSULUBIWA, KUFA, NA KUFUFUKA KWA YESU KRISTO

Image may contain: text
Leo nataka tutafakari kwa pamoja somo muhimu sana katika maisha ya Ukristo.Moja ya Misingi ya Imani yetu Wakristo ni tunaamini kuwa Yesu Kristo alisulubiwa, akafa na kuzikwa na hatimaye akafufuka siku ya tatu. 

Endapo imani hii itakuwa ni uongo na tukio hilo kama litakuwa halijawahi kutokea ni wazi kuwa imani ya Ukristo ni batili. “I Korintho 15:13-19” Ni wazi kuwa unapozungumzia kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo ni lazima uamini kuwa Yesu alisulubiwa yaani alipata Mateso yaliyosababisha kifo chake na hatimaye akafufuka na kama hivyo sivyo basi Ukristo ni imani mbaya na mbovu kuliko zote.

Upinzani dhidi ya Kusulubiwa, Kufa na Kufufuka kwa Yesu Kristo.

Kwa kuwa shetani anafahamu kuwa kusulubiwa kwa yesu Kristo na kufa na kufufuka ndio nguzo muhimu katika imani ya Ukristo ametumia jitihada kubwa sana katika kuhakikisha kuwa watu hawataamini hata kidogo kuwa Yesu alisulubiwa, akafa na kufufuka. Aidha ziko Imani nyingine ambazo kwa makusudi au kwa Bahati mbaya zinapinga vikali kuhusu kusulubiwa na kufa na kufufuka kwa Yesu na kutumia ujanja mwingi hata wa kupotosha maandiko ili tusiamini kuwa kweli Yesu alisulubiwa na kufa na kuzikwa na kufufuka siku ya Tatu.

Kwa mfano: Waislamu wanaamini kuwa Yesu hakusulubiwa.Waislamu wanaamini kuwa Yesu hakusulubiwa na kufia Msalabani ndivyo wanavyoamini na kufundishwa na ndivyo Quran inavyofundisha (Surat al Imran 3:54-55, an Nisaa 4:157-158) aya hizi ndizo zinawathibitishia kuwa Yesu Masihi hakusulubiwa na kufia msalabani na huunganisha madai haya kwa kutumia aya zifuatazo katika Biblia.

Wanafundisha kuwa Yesu hakufa msalabani sawa na maneno yake mwenyewe kuhusiana na Ishara ya nabii Yona (Yunusi) sawa na (Mathayo 12:38-40) hivyo kama ilivyokuwa kwa Yona katika tumbo la nyangumi alikuwa hai na Yesu alikuwa hai katika uso wa nchi.

Wanahoji kama ilikuwa ni mapenzi ya Mungu Yesu afe msalabani kwanini aliomba kule bustanini Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke?(Mathayo 26:39, Marko14;35, Luka22:42)

Waislamu wanaamini kuwa Mungu aliyasikia maombi ya Yesu Masihi na kumuokoa katika mauti sawa na (Yohana 9;31,11:41-42,Waebrania 5:7)Wanaamini kuwa kuna uthibitisho wa kibiblia kuwa Mungu aliyasikia maombi yake na ndio maana alianza kumshughulikia mkewe Pilato katika ndoto na Pilato mwenyewe (Mathayo 27:19)

Wanaamini kuwa Pilato alifanya jitihada binafsi ili kumuokoa Yesu na mauti na kwa kufanya yafuatayo;-

Kunawa mikono kuonyesha kuwa Yesu hana hatia na kuwa yeye hahusiki na damu yake mtu huyo

Kumfungulia Baraba ili kupata mbadala wa Yesu

Kuchelewesha hukumu kwa kuipeleka kesi kwa Herode kwani alijua kuwa sabato inakaribia, Pia kwa asili kifo cha msalabani ni kifo cha polepole hivyo kwa mtu mwenye afya kama Yesu aliyekuwa na uwezo wa kufunga siku arobaini (40) hangeweza kufa msalabani kiurahisi na ushahidi unaonekana kwa wenziwe waliosulubiwa pamoja nae kuwa walilikatwa miguu (Yohana 19:31-32).Waislamu wanahoji kama Yesu alikufa kweli kwanini maiti yake ilitoka maji na damu?Wanahoji zaidi lugha ya kibiblia inayoonyesha Pilato akishangazwa na taarifa kuwa Yesu amekwisha kufa mara! (Marko 15:42-44). Wanahoji kuwa jambo lingine la kushangaza ni muonekano wa Yesu mwenyewe baada ya kufufuka kuonekana na Mariam Magdalena akiwa na mavazi kama mtunza Bustani jambo linaloashiria kuwa aliyapata hapo (Yohana 20;13-15)Waislamu wanahoji kuwa kama Yesu alikufa kweli kwa nini hatuna ushahidi toka kwa Yusufu wa Armathaya na Nikodemo waliomzika na sio Mathayo na Marko au Luka ambao hawakuwepo na walikimbia? Na wanahitimisha kwa kudai kuwa maisha ya Yesu yaliyosalia aliishi nchini India katika jimbo la Kashimir na alikuwa na Tomaso aitwe Pacha (yaani alifanana na Yesu) na aliishi miaka 120 huko na alizaa mtoto wa kike na Mariam Magdalene na alifia huko na kaburi lake liko hata leo

Waislamu wanadai hata wayahudi walitilia shaka kifo cha masihi (Mathayo 27:63).

Waislamu pia huamini kuwa Biblia ilitiwa chumvi katika maeneo yanayohusiana na kifo na kufufuka kwa Masihi kwa madai yafuatayo;-

Unapofungua Biblia yako katika ukurasa unaokaribia injili ya Mathayo utaona kuna maelezo ya vifungu vya Mabano na Parandesi za aina mbili 1. Ya mviringo mfano ( ) hii inahusu ufafanuzi. 2 ya mraba mfano huu [ ] hii inahusu maneno yanayoonekana katika nakala kadhaa za zamani za kale ila hayaonekani katika nakala nyingine yaani za sasa

Hoja:- Kama hivyo ndivyo waislamu wanashangaa kwa nini hizi nakala nyingine yaani za sasa zisionyeshe tukio la muhimu la kufa na kufufuka kwa Yesu hasa ukizingatia kuwa Mathayo anashindwa kuelezea tukio la kupaa kwa Yesu.(Marko 16;9-19) ziko kwenye kifungo cha mraba kuonyesha nakala nyingine za kale je nakala za sasa zimeshindwaje kuonyesha tukio hili la kufufuka na kupaa kwa Yesu?

Yohana pia anashindwa kuonyesha tukio hili la kupaa kwa Yesu?· Je tunawezaje kumuamini Luka ambaye alikuja baadae na hakuwa miongoni mwa wale 12.Hoja kama hizi za waislamu je unafikiri hazipaswi kujibiwa? Na kushughulikiwa je mkristo wa kawaida tu je hawezi kusilimishwa? Ni muhimu tukajibu hoja hizi ili kuondoa utata utakao zuia yamkini hata waislamu wenyewe kuokoka na kuifahamu kweli.KWA NINI TUNAAMINI KUWA YESU ALISULUBIWA ?Wakristo tunaamini kuwa Yesu amesulibiwa na alikufa na hatimaye alifufuka toka kwa wafu na sasa yuko mkono wa kuume wa Mungu Baba mbinguni,Hapa ndipo mahali penye moyo wa Imani yetu Wakristo wote na kwa ufupi huu ndio Ukristo wenyewe na ndio maana shetani kwa makusudi kabisa anapingana sana na swala zima linalohusiana na kusulibiwa, kufa na hata kufufuka kwa Yesu (1Korintho 15;12-19). Kwa bahati mbaya mstari huu nilioutumia hapa ni moja ya mistari inayotumiwa sana na makafiri katika kudanganyia watu kuwa Kristo hakufufuka nitashughulukia mstari huu wakati wa kujibu hoja hii kuwa Kristo amefufuka.

Lakini kabla ya jambo hilo nilikuwa nataka kwanza nikurudishe nyuma katika historia iliyokuwako wakati wa Muhamadi ambayo iliathiri uelewa wake na wa watu wa nyakati zake kuhusu Ukristo na kufa kwa Yesu na kufufuka kwake jambo ambalo linaathiri waislamu wa nyakati hizi tulizonazo kushindwa kulielewa swala hili ni Muhimu kufahamu kuwa wakati wa Muhamadi kulikuwepo na imani potofu zenye mafundisho ya uzushi kuhusu Ukristo,ambazo zilichangia uelewa potofu kumhusu Kristo na kifo chake cha msalabani, uelewa ambao ulimkumba Muhamadi na unaathiri waislamu wa nyakati hizi.

Kwa mfano Kama ni msomaji mzuri wa Quran utakuta kuna kundi la watu wanaitwa “Manasara” Kundi hili hufikiriwa kuwa ni Wakristo lakini wakristo wengi wa leo wakiulizwa kama wanajifahamu kuwa wanaitwa hivyo watakushangaa! Manasara Ni mojawapo ya makundi ya imani potofu yaliyokuwa yameenea sehemu za Arabia Na huko Makka, jamii ya kundi hili walikuwa ni wakristo wa kiyahudi ambao imani yao ilikua ikiamini kati ya ukristo na dini ya kiyahudi hawa ndio Muhamadi aliwafahamu kwa hivyo utaona lile wazo la kuwafikiri wakristo katika quran limejengeka kwa misingi ya imani ya Kinasara.Imani nyinginezo zilizokuwepo ambazo zilichangia mawazo potofu kuhusu kifo cha Yesu ni pamoja na kundi la imani potofu lijulikanalo kama Gnosticism hawa waligawanyika katika makundi makuu kama matano hivi nitayataja makundi hayo kwa lugha ngeni kwa kukosa tafasiri ya Kiswahili ya maneno hayo ingawa wakati wa kuyafafanua utaelewa kile walichokuwa wakikiamini na ndilo jambo la muhimu kwako.1. Basilides. Hili Ni kundi lililofundisha kuwa Yesu asingeweza kuteseka hata kidogo Kwa sababu wakati woote mateso Ni Kwa mtu muovu tu Na mwenye dhambi, Hivyo mtu aliyetumwa na Mungu kama Yesu na aliyekuwa mwenye haki kama yeye hangeweza kuteseka.Waliamini kuwa Yesu alichukua sura ya Simon wa Kirene, na Simon wa kirene alichukua sura ya Yesu, Hivyo kwa asili wayahudi walimsulibisha Simon badala ya Yesu, na hivyo Yesu alisimama pembeni akiwasanifu.

2. Docetism. Hili ni kundi lililofuyndisha kuwa Yesu alikuwa ni Roho tu.Hivyo matukio yoote yanayohusu kuzaliwa, kukua, kula, kunywa, kulala nk.hayakuwa mambo halisi “ it was an illusion, some thing that does not really exist” Kumbuka wazo hili kuwa Yesu ni roho limo katika Quran.

3. Cerenthus. Hili Ni kundi lililofundisha kuwa wakati Yesu alipobatizwa Yesu halisi alishuka kutoka mbinguni kuja Kwa Yesu mtu Kwa umbo Kama njiwa, akafanya miujiza, na kuhubiri ufalme na kumtambulisha baba. Wakati wa kusulibiwa Kristo wa kiroho aliondoka zake na Kristo mwanadamu alikufa na akafufuka baadae.

4. Manichaeism. Kundi hili lilifundisha kuwa sio Yesu aliyekufa msalabani isipokuwa ni mwana wa mwanamke mjane huenda ni yule aliyefufuliwa katika (Luka. 7; 11-17)

5. Carpocrates. Kundi hili lilifundisha kuwa sio Yesu aliyesulibiwa lakini ni mojawapo ya wafuasi wake, Yesu alikuwa pembeni akiwasanifu wayahudi kwa kukwepa mateso waliyotaka kumtendea kisha baadae akapaa mbinguni.Unafikiri kwa mtindo huu wa imani potofu zilizokuwepo Muhamad na waislam wengine je wanao mtazamo sahihi kuhusu Ukristo?

Tukirudi nyuma kwenye andiko la Wakoritho 15;12-19 ambalo waislamu hulitumia katika kupotosha kuwa Yesu hakusulibiwa ni muhimu kufahamu kuwa hapa Paulo mtume alikuwa anacheza na falsafa ya maneno hasa kwa sababu Wakoritho wenyewe walikuwa wanafalsafa Paulo aliwataka wakoritho kufikiri vema (Logicaly) na kwa kuanzia na haya hii ni muhimu msomaji akafahamu mazingira na historia ya andiko kabla ya kujisomea hovyo na kufasiri hovyo kama makafiri wafanyavyo;-Kihistoria, kuhusiana na andiko hili kulikuwa na tatizo miongoni mwa wakoritho kuhusu ufufuo wa Wakristo waliokufa katika Bwana huko koritho ya kuwa hawatafufuka kwa sababu wafu hawafufuliwi, shida ya wakoritho haikuwa katika ufufuo wa Kristo mwenyewe hili waliliamini na kwa kweli lilikua ni kiini cha injili ya mitume na waliyoiamini wakati ule.

Paulo anajibu hoja hii akitumia uzoefu au tabia ya watu ya wakati ule iliyokuwa inaendelea pale Koritho ili kuwasilisha kweli kitaalamu mtindo huu unaitwa “Ad-Homeinem” Wakoritho walikuwa wamekata tamaa kuwa hakuna kiama (Ufufuo wa wafu) hasa kwa waamini wenzao waliokuwa wamekwisha kufa (I koritho 15;12-34.)Huku wakati huohuo wakiamini kuwa Yesu yuko hai na kuwa alisulibiwa,alikufa na alifufuka ! jambo hili lilikuwa wazi kwao.

Paulo anajibu kwa kujenga hoja zifuatazo;-

a). Wakoritho 15;16- Kama wafu hawafufuliwi Kristo naye hakufufukaa!(Maana yake ninini?) jibu Kama mnaweza kuamini kuwa Yesu amefufuka katika wafu mnashindwaje basi kuamini kuwa Ndugu zenu waliokufa katika bwana watafufuka? Kwa vipi kwa maana Kristo ndio limbuko lao yaani wa kwanza wao ona mst 20.

b). Wakoritho 15;29- (“ au je wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje kama wafu hawafufuliwi kamwe ;kwanini kubatizwa kwa ajili ya wafu?) maana yake kulikuwa na desturi zinazozunguka jamii ya wakoritho ambapo watu walibatizwa kwa niaba ya wafu wao waliokufa kabla ya kubatizwa (ingawa zoezi hilo lilifanywa na wapagani na sio wakristo) Paulo anahoji je watafanyaje kama wafu hawafufuliwi? Maana yake hata hao waliofanya hayo walifanya wakiamini kuwa kuna ufufuo.

c). Wakoritho 15;32 - Kama hakuna ufufuo na tule na tunywe; maana yake kama kifo ndio mwisho wa yoote na hakuna ufufuo yanini kujinyima starehe za dunia kwa ajili ya Mungu? watu na wastarehe wale wanywe maana tutakufa!.Kwa maana nyingine Paulo alimaanisha kuwa ufufuo wa Yesu Kristo ni ishara iliyokuwa wazi kuwa siku moja Mungu atafufua wafu kama alivyo fufuka kristo ndio maana quran inasema yeye ndie Ishara ya kiama.

Ushauri mwingine kwa wasomaji wa Biblia ni kuwa tofauti na Quran ambayo kila aya inajitegemea, Kanuni za usomaji wa Biblia zinamuongoza msomaji kusoma fungu zima la juu na chini ili kupata maana kamili inayokusudiwa na mwandishi huyo kumbuka vitabu vingine ni nyaraka yaani barua unawezaje kuisoma barua nusunusu kisha ukapata maana aliyoikusudia mwandishi?

Kwa mfano Wakoritho 15;12-19 inakamilishwa kwa kusoma Wakoritho 15;1-11 na Wakoritho 15;20-28 nk. Kwa mfano swasa ukisoma fungu lile la kwanza Paulo anasisitiza kuwa Yesu alisulibiwa, alikufa na alifufuka na aliwatokea watu wengi baada ya kufufuka kwake unaona? Jambo la kushangaza ni kuwa waislamu hawajui namna ya kuisoma biblia bali hudandia treni katikati ya safari na unajua matokeo, kwa kuwasaidia tu Hebu niwahoji wanaharakati wa kiislamu kwamba ninyi mnamkataa Paulo mtume na mnamuona kua ni muongo na aliharibu dini sasa iweje leo myaamini maandiko haya kipande ambacho kimeandikwa na Paulo?

Baada ya kufafanua aya hizo hapo juu sasa tuchambue aya katika quran yaani (Imran 3;54-55, An Nisaa 4;157-158). Linganisha na injili inayoitwa ya Barnaba uk 14. Sura ya 215; Aya hizi zinadai Mungu alibadili hila za wayahudi maana yeye ni mbora wa kupindisha hila na hivyo alisulubiwa mtu mwingine Yesu akanyakuliwa mbinguni? Ukiachia imani potofu ambazo zilichangia uelewa huu mimi ninashangazwa na Quran kuwa ni kitabu cha Mungu au cha majahili? Maana aya hizi zinamtukanisha Mungu kwa kuonyesha wazi kuwa Allah ni mjuzi wa kufanya utapeli na kuwa hana nguvu ya kufufua ila ana nguvu ya kudanganya watu eti waone sura ya Yesu anasulibiwa na kumbe ni mtu mwingine! Wanaharakati wa kiislamu ni lazima watubainishie hili;-

Kama Yuda ndiye aliyesulibiwa badala ya Yesu je Yesu ndiye aliyejinyonga?

Je Mungu Mtakatifu asiyeweza kusema uongo aliamua kuwadanganya Askari, Pilato, Herode, Yusufu wa arimathaya, Nikodemo, wanafunzi waliokuwa karibu kama Yohana, Mariam mama yake na Mariam Magdalene hawa wote walidanganywa na Mungu alipokuwa anapindua hila za wayahudi? (Yohana 19;25,26-27).

Je Mungu angeweza kuwaumiza na kuwadanganya watu watakatifu waliokuwepo?

Hata Mariam (Quran 3;36,19;16). Waliguswa na mateso haya na kulia huku wakiangalia mpaka mtu anakufa wakidhani ni Mwanae kumbe eti Mungu alikuwa anacheza kamchezo ka utapeli, Nani atakuwa mwenye makosa pale wanafunzi akiwemo Paulo walipohubiri kuwa Yesu amesulibiwa na kuwa aliukufa na akafufuka na zaidi ya yoote walikubali kufa kwa ajili ya injili hii,Je malaika pia ni waongo pale waliposema na wanawake kuwa Yesu amefufuka? Ona (Mathayo 28;5-7, Matendo 2;23-24). Injili inamtukuza Mungu kwa kuonyesha uwezo wake kuwa yeye anao uwezo wa kufufua tofauti na allah ambae kwake kufanya hila ni jambo jepesi kuliko kufufua?

Mungu ambae sisi tunajifunza habari zake katika Biblia hawezi kusema uongo (Hesabu 23;19, 1Samuel 15;29, Malaki 3;6, Tito 1;2; Yakobo 1;17), Aya zote hizi zinabainisha jinsi Mungu alivyo mkweli, Kristo mwenyewe alisema kuwa atakufa na atafufuka pia ni mkweli.Inasikitisha kuona Mungu wa Muhamad na wa waislamu akifanya hila? Sisi tunaamini kuwa Mungu wa kweli aliyefunuliwa kwetu kupitia Yesu Kristo ni wa kutumainiwa lakini kumuamini Mungu wa kwenye Quran inatutia mashaka na kutupotezea tumaini “ Hawezi kufufua ila anaweza kufanya utapeli?”Hoja kuhusu Ishara ya nabii Yona (Yunusi).Waislamu wanadai kuwa Ishara hii inathibitisha kuwa Yesu hakufa bali alikuwa hai, na pia Hakukaa siku tatu kamili kaburini,mara nyingi humnukuu Yesu katika matamshi yake katika (Mathayo 12;33-40).Hili nalo ni jambo la kushangaza sana nah ii inatusaidia kujua kuwa unapozungumza na mwislamu aneyeamini hivyo kuwaq unazungumza na jahili au maaamumah wasiojua kabisa maandiko wala hawana utaalamu nayo ila hudandia tu na kwa bahati mbaya ni kama watu wanaodandia gari kwa mbele jambo ambalo unajua nini kinaweza kutokea kwa kuwa mimi ni mwalimu hebu fuatana nami tena tupate kulichambua andiko hilo.

Ni wazi kuwa waislamu hawajui kanuni ya uchambuzi wa agano la kale (Torati) na uhusiano wake na agano jipya (Injili).Kitaalam mambo mengi katika agano la kale yalikuwa ni ya kinabii (kivuli) cha mambo halisia katika agano jipya.“Mfano mimi ninampenda mke wangu na mwanangu,ninaposafiri husafiri na picha zao,na inapotokea nimerudi nyumbani sihitaji picha zao tena kwa sababu sasa ninae mke wangu na mwanangu halisi”

Hivi ndivyo Mungu alivyowatumia manabii wengi katika agano la kale kutoa unabii kuelekea kwa Kristo (Kolosai 2;16-23) Hivyo ishara ni picha tu ya tukio halisi lililotokea au litakalotokea,mfano rahisi ni jinsi ambavyo zamani wayahudi walikuwa wanandama mwezi kama wafanyavyo waislamu wengi leo, Mwezi ukiingia gizani na unapotoka huitia nuru dunia hii ilikuwa ni ishara ya kuja kwa Masihi Yesu kristo ambaye yeye ni nuru ya ulimwengu (Yohana 1;6-14). Hivyo kwa kua masihi alikwisha kuja duniani naye ndiye nuru halisi na tumekwisha kumjua na amekwisha tia nuru mioyoni mwetu, Wakristo hatuitaji tena kuandama mwezi maana mwezi ulikuwa ni kivuli tu (copy)Bali kristo ni halisi (Original).

Kwa msingi huu basi tukio la nabii Yona ingawa lilikuwa la kweli kwake kama tukio halisi hata hivyo lilikua ni Ishara au unabii wa tukio halisi litakalompata Kristo. Hakuna shaka kuwa kuna uwezekano Yona alikuwa hai ndani ya tumbo la Nyangumi, wala hatuambiwi kua alikufa kasha akafufuka toka kwa wafu na labda kwa ajili ya hili waislam hufikiri kuwa ndivyo ilivyokuwa kwa Yesu kuwa alikuwa hai pale kaburini. Kwanini Yesu alitumia mfano wa Yona? Yesu alikuwa na maana gani. Mstari wa 40 wa Mathayo 12 unasema.“Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, Hivyo ndivyo mwana wa Adamu atakavyikuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wanchi ”Ni wazi kuwa mtu anapotafasiri unabii vivuli (Types) na uhalisia wa jambo huwezi kuchukua kila kitu kama kilivyo ila unachukua wzo la jumla au ile dhana mfano (Yohana 3;14).“Na kama vile Musa alivyomuinua yule nyoka kule jangwani vivyo hivyo mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu”Hivyo unaweza kuona wazi Yesu anasisitiza na kamavile. Hapa anazungumzia ile dhana ya kuinuliwa juu (Kusulubiwa). Nyoka aliinuliwa kuleta uponyaji kwa wayahudi waliokuwa wakiumwa na nyoka, Kristo aliinuliwa kuleta uponyaji kwa ulimwengu kutoka katika dhambi na madhara yake.

Sasa tukitafasiri Biblia au mfano ule wa yona kama waislamu wanavyotaka je mfano huu tutaufafanua vipi? Nyoka alikuwa wa shaba na alikuwa hana uhai je Kristo naye alikuwa na mwili wa shaba na aliinuliwa akiwa amekwishakufa? Maana hivi ndivyo waislamu wanavyo itafasiri Biblia!. Hivyo ni wazi Yesu alikuwa anazungumzia lile wazo la Yona kufichika katika Tumbo lanyangumi kwa siku tatu.

Ufahamu kuhusu siku tatu Mchana na usiku.

Wote tunakubali kuwa Yesu alikufa na akafufuka siku ya tatu bila shaka. Lakini kwa waislam hii ni hoja! Wao wanadai kuwa Yona alikaa tumboni mwa nyangumi suku tatu usiku na mchana na hivyo kutimiza masaa 72 lakini kwa.Lakini yesu hakukaa masaa zaidi ya 33 tu. Ijumaa saa 9 alikufa na alizikwa na jumapili saa 12 aliffufuka ,hivyo alikaa usiku wa ijumaa na jumamosi tu na mchana mmoja tu wa jumamosi,hivyo waislamu huona hakuna uwiano wa unabii wa yona na uhalisia wa tukio la Kristo. kuhusiana na siku tatu. Shida waliyonayo waislamu hapa ni kukimbilia kutafasiri kitabu kisichokua chakwao huku wakiwa hawana utaalamu wa kutosha na kanuni za kuitafasiri biblia,Ni muhimu kufahamu kuwa kuna tofauti kubwa kati ya kizazi cha leo na lugha,tamaduni,historia na nyakati yaani Muda,hivyo unapotaka kuifasiri biblia unakumbana na mambo hayo manne kufikia wakati tulionao.Hivyo kuna mengi yakufahamu kati ya nyakati za muandishi na nyakati tuliopo na matumizi ya mambo yale manne katikati ya hayo.Kama tunavyoona katika kielelezo hapo juu Unapotaka kuifasiri biblia leo lazima kuna vikwazo kutoka kujua maana iliyokusodiwa na mwandishi yaani wakati ule, vikwazo utakavyokumbana navyo ni pamoja na muda,Tamaduni,Lugha na Historia. Mfano kitabu cha kutoka kiliandikwa miaka 3500 iliyopita je unafikiri tamaduni za wakati ule zinaewza kuwa sawa na leo? Je ni Muda gani umepita? Je mtindo wa lugha usemi nk ni sawa na wa leo? Ni lazima tujue kuwa mtindo wa lugha na semi zinatofautiana sana akifufuka mtu aliyefariki mwaka 1984 na kukuta usemi wa neno vijisenti nk anaweza asielewe nini kinazungumzwa! Hivi ndivyo ilivyo pia kwa suala la usemi wa Siku tatu mchana na Usiku.Kitu ambacho wanaharakati wa kiislamu wanashindwa kukielewa ni kuwa kuna tofauti kati ya waebrania wa karne zile na tamaduni za Kiingereza na Kiswahili cha nyakati za leo. Kwa mujibu wa tamaduni za Wayahudi wa nyakati hizo wao walihesabu hata sehemu ndogo tu ya siku kamasiku nzima, hivyo Yesu kuzikwa Ijumaa, akashinda Jumamosi, akafufuka jumapili mapema alfajiri. Kwamujibu wa tamaduni na kalenda na lugha za kiyahudi; Yesu alikuwemo kaburini siku tatu (Mathayo 27;64)na ndio maana walilinda kaburi.kumbuka mitume pia walihubiri juu ya siku hizo tatu (Matendo 10;40).Swala hili halikuwa na shaka katika injili ya mitume. (1Koritho 15;3-4).Hivyo ishara ya Yona inawathibitishia waislamu na maadui wa ukristo uhakika ya kuwa Yesu alisulibiwa,alikufa na alifufuka siku ya tatu na si vinginevyo.

Ufahamu kuhusu maombi ya Yesu kwa Baba aokolewe na mauti.

Baadhi ya waislamu na hasa wa madhebu ya ahmadia huwa wanatumia baadhi ya mistari kama vile (Mathayo 26;39.Marko 14;35;Luka 22;42) kuhoji kuwa kama yalikuwa ni mapenzi ya Mungu afe msalabani kwanini aliomba “ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke” na wanatumia aya zifuatazo kujithibitishia kuwa Mungu alimsikia (Yohana 26;39 11;11-42 na Ebrania 5;7). Kabla ya kushughulikia mengineyo hebu tushughulikie hoja hii ya kusikiwa kwa maombi ya Yesu.Waislamu wengi hawamjui Yesu kama jinsi ambavyo hawamjui Mungu, wale wakristo wanaomfahamu Kristo vizuri wanafahamu lile fundisho maarufu la unyenyekevu wa Yesu (The Doctrine of Kenosis),Fundisho hili lafundisha jinsi ambavyo kitu Fulani cha ulimwengu wa kiroho kinavyoweza kuvaa mwili wa kibinadamu (Incarnation) na kufanya shughuli za kibinadamu; (Kwa waislamu majini hufanya hivyo).Kristo kwa asili maisha yake hayakuanzia katika tumbo la mariam yeye alikuwako tangu mwanzo. (Yohana 1;1-5,14).Quran inasema “Yesu ni Roho” Hivyo alipotungwa mamba tumboni mwa mariam alikuwa anachukua mwili wa kibinadamu (Filipi 2;5-8) na kwa tendo hili tunapata Mungu mwanadamu yaani Immanuel Mungu pamoja nasi (Mathayo 1;23) hata hivyo kwa unyenyekevu wake Yesu hakutumia uwezo wake wa kiungu,bali aliishi kama mtu wa kawaida, angeweza kubadili mawe kuwa mkate lakini hakufanya hivyo na angeweza kuagiza majeshi kumi na mawili ya malaika lakini hakufanyahayo.Yesu mwenye asili ya kiungu wakati huohuo akiwa mwanadamu anayeishi bila kuutumia uwezo wa kiungu kama mwanadamu alihisi njaa, alichoka,alikula na zaidi ya yoote aliogopa kifo na mauti kama binadamu yoyote. Yesu aliomba ikiwezekana kikombe hiki kimuepuke.Lakini si kwa mapenzi yake bali ya Baba yake hivyo kwa kuwa ilikuwa ni mpango wa Mungu Yesu kufa kwa ajili ya ulimwengu alitumwa malaika kumtia nguvu kukabiliana na kifo cha msalaba hivyo hatimaye alisulubiwa, alikufa na kufufuka kama majibu ya kuokolewa na mauti unaona!

Hii ni tofauti na mauti iliyomkuta Muhamadi ambaye alihaha na kuogopa kufa sana badala ya kumtumainia mungu,Muhamad alisema “Enyi watu! Hakika kukata roho kuna machungu makubwa” (Maisha ya nabii Muhamad uk 80 kifungu cha tatu)Hivyo Yesu asife bali kuokolewa na mauti baada ya kifo.

Kwa mujibu wa IVP Bible background commentary (New Testament) inasema “Wayahudi wanaamini kuwa Mungu alisikia maombi ya Yesu na Mungu aliyajibu kwa kumfufua na sio kwa kuikwepa mauti yenyewe bali kwa kufufuka kutoka mautini”· The applied New testament commentary by Thomas Hale inasema hivi “Yesu aliomba aokolewe na mauti ya msalaba (Marko 14;35-36) lakini Mungu hakuchukuliana na Maombi hayo, Mungu angeweza kumuokoa kutoka mautini lakini hakuchagua hivyo, ingawaje siku ya tatu alimfufua toka kwa wafu”Matendo 2;22-28.

Kwa kufundisha kinyume na ukweli huu waislamu wanataka kutuambia kuwa Yesu ni Muongo,huku quran inathibitisha kuwa hakuwa na dhambi.Yesu mwenyewe alisema anautoa uhai wake (Yohana 10;14-18) Yesu mwenyewe anawachanganya wislamu kwa kuwa yeye mwenyewe ni njia kweli na uzima hivyo aliutoa uhai wake yeye mwenyewe na kuutwaa tena.Yesu Kristo hakuwa na Hatia ya aina yoyote.Yako madai ya Baadhi ya waislamu kuwa biblia inathibitisha kua Mungu aliyasikia maombi maombi ya Yesu na kuanza kuwashughulikia mke wa Pilato ambae alimtahadharisha Pilato kujihadhari na hukumu dhidi ya Kristo andiko hili hutumika (Mathayo 27;19), Pia wanaorodhesha kile kinachodaiwa kuwa ni jitihada za Pilato kumnusuru Masihi na mauti kwa kunawa mikono,Kumfungulia Baraba ili kupata mbadala wa Yesu (Luka 22;36) na kile kinachodhaniwa kuwa ni kuchelewesha hukumu kwa kumpeleka Masihi kwa Herode.Nikianza kuwajibu waislamu hoja hizi nataka kukazia kwanza kichwa cha Habari hapo juu cha kifungu hiki Yesu Kristo hakuwa na hatia ya aina yoyote.Hakuna mtu Yeyote aliyemshuhudia Masihi kuwa na Dhambi(Yohana 8;46).Yeye hakutenda dhambi wala hakuwa na hila ya aina yoyote soma mistari hii (2 Korintho 5;21, Ebrania 4;15, 1Petro 2;22).Masihi alitafutiwa kubambikizwa hatia katika Mazingira makuu matatu ambayo ni Kumtafutia makosa ya 1) Kidini, 2) Uhaini dhidi ya Serikali ya Kikoloni ya Rumi na 3) Uhaini dhidi ya ufalme wa kiyahudi Jimbo la Galilaya kwa Herode, katika mazingira hayo yote hakuna aliyepata kosa wala hatia inayostahili auwawe.

Mashitaka Ya Kidini.

Yesu alipokamatwa kwanza alipelekwa kwa Anasi mkewe Kayafa.na aliyekua kuhani mkuu kabla ya Kayafa.Hapa kwa anasi ilionekana wazi kuwa Hakuwa na hatia Soma (Yohana 18;12-14,19-23).Baadaye ndipo walimpeleka kwa Kayafa aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule ambapo hapo walitafuta ushahidi hata wa uongo ili wamuue wasiuone (Mathayo 26;57-68).

Mashitaka mbele ya Serikali ya Rumi.

Biblia iko wazi kuwa walipoona kuwa hakuna hatia walimpeleka kwa Pilato ambae Kihistoria alikuwa liwali katili na aliyeamuru wengi kusulubiwa, Pilato pia hakuona hatia ya aina yoyote na alijua kuwa alitolewa kwa Husuda; Ni wazi kuwa kuteseka kwa mkewe Pilato dhidi ya hukumu ya Masihi kulikuwa kunaweka bayana kuwa Masihi hakuwa na hatia ya kidini, kisiasa na kihaini;Kufunguliwa kwa Baraba ilikuwa ni desturi ya Pilato kila inapokaribia sikukuu, jambo ambalo hufanywa na viongozi wengi wa Kisiasa hata leo, Baraba alijulikana wazi kuwa ni muuaji na muhaini hata hivyo mioyo ya watu wenye dhambi iliona vema kuchagua uovu kuliko wema na hivyo “Walipenda giza kuliko Nuru”(Mathayo 27;11-23).Pilato aliona ni vema Masihi apelekwe kwa Herode labda hatia ingeonekana,Hivyo hapa hakukuwa na jitihada za Pilato au mkewe kumuokoa Masihi na mauti ya Msalaba bali ni kuweka wazi kwa ulimwengu kuwa Masihi Hakuwa na Hatia iliyostahili Yeye kuuawa isipokuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu mimi na wewe (Isaya 53;1-9).Mashitaka Mbele ya Mfalme Herode.Biblia inathibitisha wazi kuwa Pilato alipoona kuwa Masihi hana hatia na kupata uhakika kuwa ni mgalilaya aliamuru apelekwe huko nako ambapo hawakuona hatia dhidi yake (Luka 23;3-15). Hatua zote hizi zilikuwa na lengo lilelile la kutudhihirishia sisi walimwengu kuwa Kristo hakuwa na Dhambi nay a kuwa alikuwa ni Mwana kondoo wa mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.Yesu anahukumiwa Kifo.

Baada ya kuthibisha wazi kuwa Yesu hakuwa na hatia ni wazi kuwa hakimu yeyote ambaye ameapa kusimamia haki anawezaje kukubali kumhukumu kifo mtu asiye na hatia?

Akitaka kujihadhari na damu isiyo na hatia pilato alinawa mikono (Mathayo 27;24-25) ni wazi kabisa kuwa Hukumu ya Kristo ilichangiwa na mpango kamili wa Mungu, uchaguzi wa watu waovu, shinikizo la wayahudi dhidi ya Pilato, Hofu binafsi ya Pilato ambaye aliogopa ghasia, kupoteza cheo, hadhi na manufaa yake mwenyewe Ingawa alijua wazi kuwa Masihi hakuwa na hatia na alithibitisha hivyo mara Kadhaa (Mathayo 27;18, Yohana 19;4,6) lakini kumbuka kuwa ni yeye ndiye aliyeidhinisha hatimaye kutoa hukumu ya kifo dhidi ya Kristo.hii ndio ilikuwa Hatima,Ni lazima tujiulize kama ni kweli Pilato alikuwa na nia ya dhati ya kumuokoa Kristo na mauti?kulikuwa na ulazima gani basi kutoa hati ya hukumu ya kifo mbona waovu wengine walifungwa magerezani kwa muda? Hata Yohana mbatizaji si aliwekwa Gerezani Tangu lini kesi ya hukumu ya kifo ikasikilizwa siku moja na siku hiyohiyo kutolewa hukumu yake? Ni lazima Tujue kuwa pilato anawajibika katika hatia ya kuhukumu isivyo halali hivyo anayo dhambi (Yohana 19;11-19).

Yesu alifia Msalabani.

Kwa sababu ya athari za imani potofu zilizokuweko Nyakati za Muhamad na upinzani wa makusudi dhidi ya Injili Wanaharakati wa kiislamu wanatilia mashaka kama kweli Yesu alifia Msalabani kwa madai kadhaa yafuatayo;-Kukatwa miguu kwa wanaume waliosulubiwa pamoja naye (Yohana 19;42-44)Kushangaa kwa Pilato kama Yesu amekwisha kufa (Marko 15;44-45).Kutoka kwa damu na maji kwa Yesu baada ya kufaKwa kuzingatia historia kuwa kifo cha Msalabani ni cha Polepole;Ukweli kuwa Yesu alifia Msalabani unathibitishwa na matukio hayo hapo juu, Tendo la askari wa kirumi kuvunja miguu ya wanaume wale wengine wawili linathibitisha kuwa Yesu alifia msalabani; (Yohana 19;32-33). Kuacha kumvunja Yesu miguu ni uthibitisho kuwa Yesu amefia msalabani, Haingekuwa rahisi kabisa kwa askari wa kirumi kuliachia swala hili kama Isingekuwa Yesu amekufa! Kwa mujibu wa taratibu za wakati ule askari wa kirumi kushindwa kutekeleza wajibu aliopewa ni kujitakia hukumu ya kifo, wao walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa watu hao wanafia msalabani kama hukumu yenyewe ilivyoamuru na kwa kuwa wanaume wale wengine walikawia kufa ilikuwa ni lazima wakatwe miguu ili wafe.

Kushangaa kwa Pilato kuwa Yesu amekwisha kufa Mara hakutokani na jitihada zake za kutaka kumuokoa Yesu,bali mshangao wake ulifuatiwa na Kupata uhakika kuwa Yesu amekufa toka kwa Akida wa kikosi kilichomsulubisha Kristo Jambo lililomfurahisha alipothibitisha hilo (Marko 15;44-45) wahubiri wa kiislamu husoma mstari wa 44 tu na kusimamia uongo.

Kwa mujibu wa historia na tabia za jeshi la askari wa kirumi, ilikuwa ni kosa linalostahili kufa kwa kushindwa kusimamia wajibu waliopewa mfano pale, Petro alipofunguliwa kimuujiza na malaika na kutoka gerezani, askari wote waliokuwa zamu na usimamizi wa siku ile waliuawa soma (Matendo 12;18-19). Jambo lingine lifananalo na hilo ni pale gereza lilipojifungua kimuujiza baada ya maombi ya Paulo na Silla ambapo vifungo vyao na vya wafungwa wengine viliachia mkuu wa gereza alichagua kujiuwa kwani ni hukumu bmayo angeipata tu kama Wafungwa wangekuwa wamekimbia (Matendo 16;27). Hivyo kama askari wa kirumi alipewa jukumu na akashindwa kutekeleza jukumu alihukumiwa kifo, ni wazi kuwa akida wa kikosi kilicho tumwa kumhukumu Masihi kifo angeshindwa kusimamia jukumu lake angeuawa nafikiri ndio maana alithibitisha kwa kumchoma mkuki ubavuni yaani kwenye moyo (Yohana 19;34).Tendo la kuchoma mkuki katika moyo halikufanywa kwa wale waliokatwa miguu kwani walikuwa hai na kama Yesu angalikuwa hai lile tendo la kusokomeza mkuki ubavuni ilikuwa ni Ishara ya kummalizia kabisa!

Ni lazima Waislamu wajue pia kuwa Tendo la Kristo kutokuvunjwa miguu ni la kinabii na lilitabiriwa katika torati na zaburi soma (Zaburi 34;20), Jambo hili lilikuwa linadhihirisha kuwa Kristo ndiye Pasaka ya kweli,Moja ya amri waliopewa wana wa Israel kabla ya ukombozi kule Misri ni kumla mwana kondoo wa pasaka bila Kumvunja mifupa yake soma (Kutoka 12;46).

Swala la Maiti ya Yesu kutoa maji na Damu;

Tendo hili nalo hutumiwa na waislamu kushutumu kuwa Yesu alikuwa amezimia tu kwani maiti haiwezi kutoa damu na maji,Hii nayo inashangaza sana hebu soma kwanza (Yohana 19;31-36).

Tendo la kutoka maji na damu liko miongoni mwa matukio yaliyo wazi yanayothibitisha kuwa Yesu alifia msalabani, Yohana mwanafunzi wa Yesu aliyependwa sana anathibitisha kuwa ushuhuda huu ni kweli kwanini? Kwa sababu yeye alikuwa karibu kabisa na Msalaba wa mateso wa Kristo (Yohana 19;25-27), pia mama yake Yesu ambaye wakati huu alikuwa mtu mzima anayejua maiti ninini naye alikuwa karibu kama shuhuda ya kuwa Yesu alikufa.Sitaki kuchukua Muda kujadili swala hili, wala sihitaji utafiti wa kisayansi kujua kuwa mtu aliyekufa anatoa damu ya namna gani na aliye hai anatoa damu ya aina gani,lakini kwa ufahamu wangu mdogo wa sayansi Damu ni muundo wa chembechembe hai za aina kuu mbili yaani chembechembe hai nyekundu na nyeupe, hizi ndizo zinaunda damu,mtu aliye hai anapoumia kwa kujikata hutoka damu yaani mchanganyiko wa chembechembe hizo, Mtu anapokufa chembechembe hizi huganda,na endapo mtu anatoa damu na maji maana yake, chenbechembe hizo zinazounda damu zimeachana hivyo huu ni uthibitisho wa wazi kuwa mtu huyo amefariki,kwa habari ya maiti kutoa damu tumeshuhudia watuwengi wakiwa wamekufa na siku mbili au tatu zikapita na wanaweza kutoa damu ni zaidi sana mtu aliyeuawa muda si mrefu ni rahisi kutoa damu, hivyo maji na damu ni uthibitisho kuwa Yesu alikufa Msalabani.

Kama hilo aliaminiki maandalizi na taratibu za mazishi ya kiyahudi ilikuwa ni pamoja na maiti hiyo kuzongwazongwa kwenye sanda ya kitani namna walivyokuwa wanafungasha ilikuwa hatakama uko hai kuna uwezekano ukafa(Yohana 11;43-44 19;40).Nafikiri kama Yesu alikuwa hai wasingeweza kigiza mchezo huu wa kufungasha maiti kama ilivyokuwa desturi yao hivyo aina hii ya ufungashaji wa maiti inathibitisha kuwa Yesu alikufa hakika pale msalabani na alizikwa! Na siku ya tatu alifufuka.

Kwanini Yesu alikufa mapema zaidi ya wahalifu wale wawili wengine?

Mazingira ya kifo cha Msalabani kwa Yesu.

Yako madai kutoka kwa wanaharakati wa kiislamu kuwa Yesu alikuwa na afya nzuri na ndio maana aliweza kufunga siku arobaini na kutembea kwa miguu sehemu mbalimbali, na kutokana na mazingira ya hukumu ya kifo cha msalabani kilikuwa ni kifo cha polepole isingekuwa rahisi Yesu kufa msalabani mapema na ushahidi ni kwa wale wahalifu wengine waliolazimika kukatwa miguu ili wafe mapema.

Nataka kuwajibu waislamu hoja hii kwa ufupi kuwa waalifu wale wengine wawili walibeba misalaba yao na kwenda kusulubiwa moja kwa moja bila mateso ya aina yoyote mbadala. Lakini kwa Bwana Yesu yeye alikamatwa Mapema alfajiri katika siku hii hatuambiwi kama alihudumiwa kwa chakula au la? lakini bila shaka wafungwa wale wengine walihudumiwa gerezani kama kawaida, akiwa hajala kitu alianza kuteswa (Mathayo 26;67), Tunaambiwa kuwa alipigwa makonde na makofi, hatuambiwi ni kwa kiasi gani,

Pia tunaambiwa kuwa alipigwa mijeledi ambayo kwa mujibu wa historia Enzi za Warumi, Mtuhumiwa alivuliwa nguo zote na kuwambwa kwenye nguzo au kuinamishwa kwenye nguzo fupi na kufungwa mikono yake na kuchapwa na kifaa maalumu,Kifaa hiki cha kuchapia yaani mjeledi kilikuwa ni kifaa chenye Mpini mfupi wa mbao ambapomikanda kumi na mbili ya ngozi iliambatanishwa ikiwa na vipande vya chuma au mifupa iliyofungwa kama shanga kwenye kila mkanda,vipigo vilifanywa na wanaume wawili mmoja upande huu na mwingine upande huu.

Kipigo hicho kilipelekea nyama ya mwili kupurwa au ku katwa katwa kiasi cha kuweza kuathiri mishipa ya fahamu, vena na ateri na hata kuumiza viungo vya ndani vya vya tumbo na wakati mwingine vilitoka nje jambo hili pekee lilifanya watuhumiwa wengi kufa wakati wa kupigwa mijeledi,Mijeledi ilikuwa inaharibu kabisa sura ya Mtu ukweli ilikuwa ni adhabu yenye kutisha sana,Inawezekana kabisa kushindwa kwa Yesu kuubeba msalaba wake na kuanguka mara tatu na hatimaye kusaidiwa na Simon mkirene kulitokana na kuchoshwa na kipigo cha mijeledi alichopata (Mathayo 27;32, ).

Achilia mbali kule kusimikwa kwa taji la miiba kama mfano wa taji kichwani ambapo kulitoboa maeneo ya kichwa na mishipa, kubeba ule msalaba, Na baadae kugongomelewa masumari mazito ya chuma yenye umbo la mraba miguuni na kusimamishwa na kuchuruzika madamu kwa masaa masaa tkribani sita hivi,misuli inavutwa Ngozi inaharibika,huku kukiwa na dhihaka na matusi na shutuma ili kuteswa kiakili katika hali kama hii hata kama ulikuwa unalia huwezi kulia tena ni rahisi kuhisi kuwa Mungu amekuacha! Acha kiu ya maji ambayo kwa mateso kama haya mtu alalamika kua ana kiu maana yake kutokana na kumwagika kwa damu nyingi akiomba maji akinywa anakufa (Yohana 19;28). Hivyo kuomba maji kwa Yesu kunaashiria alikuwa amefikia hatua ya kukata roho na kwakweli ALIKUFA!. Mateso haya kwa kweli yalichangia Yesu kufa mapema kuliko wale wengine.

Pamoja na mateso hayo yoote aliyoyapata Masihi ambayo yalichangia kufa kwake mapema kabla ya wale wawili,Inashngaza eti kuona wahubiri wa kiislamu wanakosa shukurani na kugundua Upendo mkuu aliokuwa nao Yesu kwa ajili ya ulimwengu na wao pia badala yake wandhihaki kazi hii ya huruma kwa wanadamu na wanafanya jitihada za kuipinga kazi hii kwa makusudi hii ndio shukurani wanayomlipa Mungu kuupinga msalaba jaribu kuwaza ni hukumu gani itawapata watu wa jinsi kama hii kwa kushindwa kumuamini Yesu na kushikamana na marehemu Muhamad na kusahau kuwa mateso ya Kristo yalikuwa ni kwa ajili yao.

(Isaya 53;2b-5). “…Yeye hana umbo wala uzuri, Na tumuonapo hana uzuri hata tumtamani, Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko; Nakama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu,Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu, Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu na Kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu. Alichubuliwa kwa Maovu yetu, Adhabu ya amani Yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona….”Isaya nabii alitabiri vema na kuonyesha wazi kuwa ni kifo cha namna gani Masihi angekufa soma aya hizo hapo juu za unabii wa Isaya kumhusu Masihi, Hivi karibuni wataalamu wa Biblia walifanya utafiti wa kutosha kuhusu Mateso yaliyompata Masihi na kujaribu kuyaigiza katika filamu iitwayo “The passion of Christ”Tunaweza kusema kuwa lile kilichoigizwa katika filamu ile ni sahihi kabisa na kuna uwezekano kuwa mateso hayo yalikuwa zaidi ya kile kilichoigizwa,Lakini lile wazo la nabii Isaya limeweza kufikiwa kwa aslimia zaidi ya themanini!

Kaburi alilozikwa Bwana Yesu kisha akafufuka, liko wazi hata leo, Watu wengi huenda mahali hapo kwa shughuli za kutalii tu. Eneo hili huitwa Garden Tomb, Yaani Bustani ya Kaburi, Mungu amepatunza mahali hapa hata leo hii ili watu wapate kusadiki kuwa Yesu yu hai.

Hoja Kuhusu Wasiwasi wa Wayahudi kuhusu kifo cha Yesu.

Hii ni mojawapo ya hoja ambayo Waislamu huitumia kuwa tendo la viongozi wa kiyahudi kuomba kaburi la Yesu lilindwe lilikuwa linamaanisha kuwa Yesu aliteremshwa Msalabani akiwa amejeruhiwa tu yaani aklwa hai. Hivyo waliomba kwa Pilato kaburi lilindwe sawia asije akakimbia (Mathayo 27;63). Soma Mstari huu kwa makini, Hapo utagundua tatizo,la Waislamu, jinsi wasivyojua kusoma Biblia! Sawa na kanuni zake,Hapa kanuni iliyokiukwa Inaitwa kanuni ya kifungu kizima “The principle of Context” Wakati wanaharakati wa kiislamu wakifikiri kuhusu Yesu kupona na kutoroka, Hofu ya Wayahudi hapa ilikuwa ni kuibiwa kwa Maiti kisha watu kuambiwa kuwa amefufuka!. (Mathayo 27;63-66).Hapa kuna mambo mawili hasa ambayo wayahudi walikuwa wakiyahofu ndani yake kuna kweli kuu ambazo zinafunuliwa kwetu, angalia sentensi ifuatayo kwa makini

“…Tumekumbuka kwamba yule Mjanja alisema alipokuwa akali hai…”

Sentensi hii inatuthibitishia kuwa wayahudi, na viongozi wao walikuwa na uhakika bayana kuwa Yesu alifia msalabani,na kua alizikwa,angalia maneno yale “….alisema alipokuwa akali hai” maana yake sasa amekufa! Hapa walikuwa wakifanyia kazi maneno ya unabii wa Yesu mwenyewe kuwa hata baada ya kuuawa kwake siku ya Tatu atafufuka (Luka 9;22).

Hofu yao kuu ilikuwa kwamba kufufuka kwa Yesu Masihi kungeathiri,Mipango na umaarufu wao kumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa unamwendea yeye hususani pale alipomfufua lazaro Yohana 12;9-19, ikiwa umati mkuu ulikuwa unamwamini Yesu na hivyo kusababisha wao kupanga kumuua Yohana 12;47-53, unafikiri wangefurahi kuona yeye mwenyewe akifufuka? Kwao Yesu aliitwa muongo na kuwa kwa uongo wake watu walimwamini na kama akifufuka uongo wa mwisho utapita ule wa kwanza, Hata hivyo yeye ndiye kweli halisi (Yohana 1;16-17).

Hofu yao ilikuwa kufufuka kwa Yesu kungeleta kuaminiwa zaidi na heshima zaidi kuliko mwanzoni hii ndio ilikuwa hofu ya maadui wa Kristo, hata leo wale wanaotaka kupunguza heshima ya kristo huushambulia msalaba na ujumbe wake (1Korintho 1;18).

Ningependa kutoa ushauri wa bure kwa waislamu kuwa wanapoisoma biblia wawe na mioyo yenye utii,mioyo safi na si kwa lengo la kuikosoa, Mtu yeyote aliyeharibika moyo hawezi kulifasiri neno la Mungu kwa halali.Moja ya kanuni za mwanzo kabisa za kulitumia neno la mungu kwa halali ni pamoja na utii “The principle of Obidient”

Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye HekimaRev. Innocent Mkombozi Kamotekwa maoni na ushauri ikamote@yahoo.comImeratibiwa na Max Shimba Ministries Org.
x

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW