Wednesday, August 7, 2019

UTATU UNATHIBITISHWA KWA AYA NA HISABATI

Tuanze kwa kusoma aya :
1 Yohana 5:7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 

Aya ya Biblia inasema ifuatavyo:

WAKO WATATU: 1 + 1 + 1 = 3
1. Baba
2. Neno - Yesu
3. Roho Mtakatifu
Hawa Watatu wanashuhudia Mbinguni.

HAWA WATATU NI UMOJA: 1 * 1 * 1 = 1

MUNGU NI WA MILELE: 
∞ INFINITY

Zaburi 90: 2 inatuambia kuhusu uzima wa milele wa Mungu: "Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu." Kwa kuwa wanadamu hupima kila kitu kwa wakati, ni vigumu sana kwetu kumpata mimba Ya kitu ambacho hakina mwanzo, lakini kimekuwa, na kitaendelea milele.


1. Baba ni wa Milele: Hana Mwanzo wala Mwisho 
2. Mwana ni wa Milele: Hana Mwanzo wala Mwisho 
3. Roho Mtakatifu ni wa Milele: Hana Mwanzo wala Mwisho 

YESU NI WA MILELE 
Yesu Kristo, Mungu wa mwili, pia alithibitisha uungu Wake na uzima wake wa milele kwa watu wa siku yake kwa kuwaambia, "Kabla Ibrahimu hajazaliwa, mimi ni" (Yohana 8:58). Ni wazi kwamba Yesu alikuwa akidai kuwa Mungu kwa mwili kwa sababu Wayahudi, waliposikia maneno hayo, walijaribu kumtupa kwa mawe. Kwa Wayahudi, kujitangaza kuwa Mungu wa milele kulikufuru na kustahili kifo (Mambo ya Walawi 24:16). Yesu alikuwa akidai kuwa ni wa milele, kama Baba yake ni milele. Mtume Yohana pia alitangaza ukweli huu kuhusu hali ya Kristo: "Katika mwanzo kulikuwa Neno, na Neno lilikuwa pamoja na Mungu, naye Neno lilikuwa ni Mungu" (Yohana 1: 1). Yesu na Baba yake ni moja kwa moja, wanapo bila muda, nao wanagawana sawa katika sifa ya milele.

ROHO MTAKATIFU NI WA MILELE 
Roho wa Mungu / Bwana / Kristo: (Mathayo 3:16, 2 Wakorintho 3:17, 1 Petro 1:11) Majina haya yanatukumbusha kwamba Roho wa Mungu ni kweli sehemu ya Mungu wa Utatu na kwamba Yeye ni sawa sawa na Mungu kama Baba na Mwana. Anatufunuliwa kwa kwanza wakati wa uumbaji, wakati "akitembea juu ya maji," akiashiria sehemu yake katika uumbaji, pamoja na ile ya Yesu ambaye "alifanya vitu vyote" (Yohana 1: 1-3). Tunaona Utatu huo wa Mungu tena wakati wa ubatizo wa Yesu, wakati Roho akishuka juu ya Yesu na sauti ya Baba inasikika.

SASA TUFANYE HISABATI:
Umilele katika Mahesabu au Hisabati unashika na au onyeshwa kwa alama hii 
∞. Kwa Kiingereza wanasema in "INFINITY"

Tukitumia Hisabati ya kawaida kabisaa utaona ∞ + ∞ + ∞ = ∞
BABA ∞ + MWANA ∞ + ROHO MTAKATIFU ∞ = ∞

1 + 1 + 1 = 3 Wapo Watatu wanao shuhudia Mbinguni: There are THREE that bear witness in heaven.

1 X 1 X 1 = 1 Hawa Watatu ni Umoja: These THREE ARE ONE

∞ + ∞ + ∞ = ∞
Mungu Baba hana Mwanzo wala Mwisho: The Father has no beginning or the end= ETERNAL=∞
Neno-Yesu hana Mwanzo wala Mwisho: 
The Word "Jesus" has no beginning or the end= ETERNAL= ∞

Roho Mtakatifu hana Mwanzo wala Mwisho: The Holy Spirit has no beginning or the end= ETERNAL= ∞

Sasa naiweka tena aya:
1 Yohana 5:7  Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.  For there are three that bear witness in heaven: the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these THREE ARE ONE. ~ 1 John 5:7

NATUMIA KUJUMLISHA KWA KIZIO CHA TATU:

Kuhusu swala la UTATU, Linahusisha NAMBA TATU na hivyo sheria yake lazima iwe ya "TERNARY ADDITION" na sio "BASE TEN ADDITION" kama wengi wenu mnao tumia hiyo hesabu bila ya hata kufahamu kuwa addition yenu MNATUMIA SHERIA YA "BASE TEN" .

SASA NINI MAANA YA TERNARY ADDITION:

1. Ternary namba inatumia BASE 3, tofauti na BASE 10 ambayo mkihesabu na kufikia namba 9, unarudi kwenye 1 na kuongeza "SIFURI" = 10. SASA, katika Ternary addition, unapo hesabu namba mwisho wako ni NAMBA MBILI na inayo fuata ni 10, kama kwenye "BINARY ADDITION" namba yako ya mwisho ni MOJA http://www.allaboutcircuits.com/…/d…/chpt-2/binary-addition/ .
Ninafahamu wengi wenu labda hamjawai soma Hesabu za juu na mnaweza pata walakini, lakini ingia hapa na ujifunze mwenyewe Ternary addition 
http://homepage.cs.uiowa.edu/~jones/ternary/arith.shtml

SASA TUANZE KUTHIBITISHA UTATU WA MUNGU KWA KUTUMIA HESABU

MSINGI WA TERNARY ADDITION UNATUMIKA:

A. (1 + 1 + 1) Ternary = 10 Ternary

UNAONA JAWABU LAKO NI Ternary (10)

SASA namba zetu tumesha zipunguza na kufikia Tenary 10. Ikiwa na maana kuwa, MSINGI UNAO FUATA NI KUZIJUMLIZA HIZO NAMBA " DIGITS MBILI ZA MOJA NA SIFURI KWA KUTUMIA msingi ule ule wa Ternary addition.

B. (1 + 0) Ternary = 1 Ternary.

SASA TUMESHA PATA JIBU LETU KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA KWA KUTUMIA HISABATI, na leo nimewajibu wale wote ambao HESABU SIO SOMO LAO KUWA UTATU UNAJIBIKA HATA KWA KUTUMIA HISABATI.

SASA NENDA KAMUULIZE MKUFUNZI WAKO WA HISABABI YAFUATAYO:

A. Ternary ya (1 + 1 + 1 ) = ?

B. Ternary ya ( 1 + 2) = ?

UKISHA PEWA JIBU MUULIZE TENA HUYO MKUFUNZI WAKO
C. Ternary ya (1 + 0 ) = ?

HAKIKA MUNGU NDIE MWANZILISHI WA HISABABTI na hakuna asilo liweza.

Mungu awabariki sana, na leo UMESHA JIBIWA KUWA UTATU UNATHIBITISHIKA HATA KWENYE HISABATI.

KURIDHIKA NA YALE TULIYOFUNULIWA .

A. BABA anaitwa MUNGU ( 1 WAKORINTHO 8:6 ).

B. MWANA ( YESU ) anaitwa MUNGU ( ISAYA 9:6; YOHANA 20:26-29 ).

C. ROHO MTAKATIFU anaitwa MUNGU ( MATENDO 5:3-4 )
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1 na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.

Shalom

Max Shimba bond-servant of Jesus Christ Mighty God. Titus 2:13TRINITYHOW COMPLEX IS TRINITY?

 
1 + 1 + 1 = 3 There are THREE that bear witness in heaven.

1 X 1 X 1 = 1 These THREE ARE ONE

∞ + ∞ + ∞ = ∞
The Father has no beginning or the end= ETERNAL=∞
The Word "Jesus" has no beginning or the end= ETERNAL= ∞
The Holy Spirit has no beginning or the end= ETERNAL= ∞

For there are three that bear witness in heaven: the Father, the Word, and the Holy Spirit; and these THREE ARE ONE. ~ 1 John 5:7

Shalom

Max Shimba bond-servant of Jesus Christ Mighty God. Titus 2:13WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW