Monday, October 17, 2016

MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI "NGUVU ZA GIZA"


Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaidia familia yako.
Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.
Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.
MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI:
Baba katika Jina la Yesu:
1. Ninayaharibu na kuyateketeza mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/ mababa, ndugu zangu katika Jina la Yesu.
2. Nina zilaani na kuziteketeza kwa damu ya Yesu roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo maagano katika maisha yangu na naziteketeza na kuzivunavunja kwa Jina la Yesu.
3. Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo, au majini ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu.
4. Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa, katika jina la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.
5. Ee Bwana Yesu, shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu, iliyoandaliwa kwa ajili yangu, katika jina la Yesu
6. Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la Yesu
7. Upanga wa moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina la Yesu
8. Ee Bwana, nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au anataka kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.
9. Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina kungo’a katika jina la Yesu.

10. Baba nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu yangu lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.
11. Agano lolote la siri ambalo ni la uovu, ninakuvunja katika jina la Yesu
12. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote
13. [Imba wimbo huu kama unaweza, kama huwezi usilazimshe: Kuna nguvu ya ajabu, damuni mwa Yesu ]
14. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu
15. Ee Bwana, badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka
16. Kila nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu, ninakuamuru kurudi moja kwa moja, kwa mtumaji katika jina la Yesu.
17. Ee Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.
18. Nina jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na adui,katika jina la Yesu.
19. Nina jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la Yesu.
20. Ee Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate kila pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.
21. Nina ipitisha Damu ya Yesu, katika mifumo yote ya mwili wangu [mfumo wa damu, wa fahamu, wa chakula, wa upumuaji, wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya urithi wa vitu viovu katika jina la Yesu.
22. Damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu [Figo, moyo, mapafu, macho, masikio, n.k] katika jina la Yesu
23. Nina vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la Yesu.
24. Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la Yesu
25. Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu, katika jina la Yesu
26. Mapepo, majini, mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze] sasa katika jina la Yesu.
27. Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu, ninalibatilisha kwa ajili yangu katika jina la Yesu
28. Nina vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu, lilipachikwa kwenye nafsi yangu katika jina la Yesu
29. Nina batilisha laana zote, mikosi, majanga, ajali, maradhi yote yaliyoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
30. Muombe Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya kutotii neon lake[kumb 28:]
31. Pepo lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi, toka, katika jina la Yesu
32. Laana zote katika maisha yangu, badilika na kuwa Baraka, katika jina la Yesu
33. Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini, sema kwa kumaanisha “vunjika, vunjika, vunjika” katika jina la Yesu. Nina jitenganisha na nyinyi katika jina la Yesu.
• Laana zote za udhaifu wa kiakili na kimwili
• Laana zote za kushidwa katika kila ninalofanya
• Laana zote za umaskini
• Laana zote za kuvunjika kwa familia
• Laana zote za kuonewa na kudharauliwa
• Laana zote za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile kujinyonga n.k
• Laana zote za magonjwa sugu
• Laana zote za kishirikina
• Laana zote za kuharibikiwa mambo ya uzazi na viungo vya uzazi
• Laana zote za kufanya kazi kwa bidii pasipo kuiona faida
• Laana zote za kulowea mambo ya uovu kama vile zinaa, pombe, sigara n.k
34. Jitamkie maneno ya Baraka wewe mwenyewe, kwa mfano kwa kusema “hakutakuwa na umaskini tena, magonjwa tena n.k katika maisha yangu katika jina la Yesu.
35. Nina jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika jina la Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina jitenganisha” katika jina la Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.
36. Nina tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la Yesu.
37.[Weka mikono yako juu ya kichwa chako] Nina vunja kila mamlaka za giza katika maisha yangu, katika jina la Yesu.Rudia “nina vunja katika jina la Yesu.
38. Taja mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
• Mamlaka zote za mizimu na miungu ya familia, ukoo, na kabila
• Mamlaka zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya familia, ukoo, kabila
• Mamalaka zote zilizoshika rimoti za kudhibiti familia, ukoo, kabila
• Mamlaka zote ovu ndani ya Familia, ukoo, kabila nk
39. Kila mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo unaweza kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]
40. Nina zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza katika jina la Yesu
41. Nina zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la Yesu
42. Nina agiza nyundo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya giza zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.
43. Ee Bwana tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi ya maisha yangu,
44. Makuhani wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na upanga wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.
45. Mkono wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya ninayoomba kauka katika jina la Yesu.
46. Nina waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la Yesu
47. Nina rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.
48. Ninafuta/ninaliondoa jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
49. [Weka mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
50. [Weka mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu.
51. [Taja kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama ni mwili wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye madhabahu za giza” katika jina la Yesu. Tamka hivyo mara saba.
52. Nina jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika jina la Yesu
53. Damu ya Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza
54. Nina tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina la Yesu.
55. Nina jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu
56. Nina jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika jina la Yesu.
57. Ninajitenganisha na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.
58. Nina iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu
59. Nina iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza katika jina la Yesu
60. Nina vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa jina la Yesu
61.Ee bwana, damu ya mnyama yeyote iliyomwagika kwa niaba yangu, Naipoteze nguvu ya agano sasa, kwa jina la Yesu
62. Kila tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu, na ikae kimya sasa, kwa damu ya Yesu
63. Ninajifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila, kiukoo, kabila katika jina la Yesu.
64. Nina jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa jina la Yesu
65. Ee Bwana kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu yangu katika jina la Yesu.
66. Damu ya agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo, naiikemee damu ya agano na nguvu za giza ilijipanga kinyume name. Kwa jina la Yesu
67. Nimepewa mamlaka ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza . kwa jina la Yesu.
68.Agano lolote la damu na nguvu za giza lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye mwili wangu, nalivunjike sasa.Kwa jina la Yesu
69. Ninapokea vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa na adui kupitia maagano na nguvu za giza. Kwa jina la Yesu.
70. Nina vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu . Kwa jina la Yesu AMEN.
BAADA YA KUFANYA HAYO MAOMBI, SASA ENDELEA KUSOMA UJUMBE WA MUNGU KWAKO:
Mtegemee Roho Mtakatifu kwa maana atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu. Na kwa kufuata maagizo ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi vitakwisha. Soma Wagalatia 5:16-25, Luka 22:40-46. Kudumu katika maombi, kuenenda kiroho na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata misingi hiyo ndipo unafunguliwa vifungo kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda kazi ndani yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia ni muhimu kujua ya kwamba sala ya toba pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na sio imani tu bali na juhudi binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu wanaotaka kupokea miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la Mungu na kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha ama makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi katika kukua kiimani.
Kuwa hodari katika Bwana ili upate ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani”
Maana ya kuwa hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake liwe ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika kupambana na muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili kuweza kupingana na hila za muovu shetani.
Mungu akubariki sana
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

22 comments:

Unknown said...

Nimebarikiwa sana na maombi haya!!!!

Unknown said...

Barikiwa sana Mtumishi wa Mungu,na Mungu akuinue zaidi na zaidi,hakika mafundisho na maombi atoayo Mungu kupitia kwako yamefanyika baraka kwa wengi

Unknown said...

Amina mtumishi wa mungu 0754228974

Unknown said...

Amina mtumishi wa mungu 0754228974

Unknown said...

Pst umenibariki mafunzo nawe utabariwa amen

Thobias J.Chengula said...

Nimebarikiwa Mungu akutunze ili masomo haya tuendelee kuyapata.Thobias Chengula-Ruvuma Mbinga

Annet said...

Asante sana
Nimebarikiwa sana na Haya Maombi
Bwana yesu akibarikk sana sanap

Unknown said...

Amen, nimebarikiwa na maombi haya naamini MMungu atanifungua katika changamoto ninayopitia katika Jina la Yesu

Unknown said...

Amen, nimebarikiwa na maombi haya naamini MMungu atanifungua katika changamoto ninayopitia katika Jina la Yesu

James uncle JJ said...

be blessed our prophet

Unknown said...

Amina! Nimebarikiwa sana kwa maombi yako Mtumishi wa MUNGU.
Ubarikiwe sana.

Unknown said...

Thanks, nimebarikiwa Sana , Asante

Anonymous said...

Thank God for this prayer

Joune said...

Mungu akubariki sana mtumishi. Hakika nilihitaji sana sala hii. Kwa uweza waje nitafunguliwa. Amina

Stevanwalt said...

Mungu amenibariki sana kupitia maombi haya.

Unknown said...

Amen naamin yesu amesikia

Anonymous said...

Hallelujah Bwana Yesu azidi kukubariki, nimebarikiwa na neno pia maombi, asente.

Unknown said...

Asnt Sana mtumishi wa mungu nime balikiwa na mungu akupe Imani zaidi

Health info said...

Barikiwa sana kwa uchambuzi yakinifu wa maandiko kutoka kwa ndugu zetu waislamu

Health info said...

Barikiwa sana uchambuzi yakinifu wa ndugu zetu waislamu

Health info said...

Barikiwa sana

Unknown said...

Barikiwa sana Mtumishi wa Mungu na Mungu akuinue zaidi na zaidi. Hakika mafundisho na maombi atoayo Mungu kupitia kwako yamefanyika baraka kwa wengi.

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW