Monday, March 18, 2019

KWARESMA NA JUMATANO YA MAJIVU NI NINI NA ILIANZIA WAPI?


No photo description available.

Kwenye somo letu la leo, tutajifunza maana ya Kwaresma na Jumatano ya Majivu kama inavyo fuatwa na Kanisa la Katoliki. 

Hii mada ninaifundisha kwa sababu ya swali ninilo ulizwa na sina budi kulijibu kiuwazi. Sio kusudio la hii mada kukosoa wala kukubali, bali ni kueleza na kujifunza maana yake. 

KWARESMA ni kipindi cha mfungo kwa waumini Wakatoliki. Mfungo huu ni wa siku arobaini. Kipindi hiki kinaanza na ibada ya kupakwa majivu kwenye paji la uso (siku ya Jumatano ya Majivu) ikiwa ishara ya kuanza toba. Kujikubali kwamba tu wakosefu na pia kujutia makosa yetu tunayotenda kinyume na mapenzi ya Mungu. 

Jina la Jumatano ya Majivu, lilianza kutumika rasmi mwaka 1099 na Papa Urbani II: mwanzoni iliitwa “Mwanzo wa Mfungo”. Majivu yatumikayo hutokana na matawi yaliyobarikiwa Jumapili ya Matawi ya mwaka uliopita. Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma. Ni wakati wa kumwilisha utamaduni wa Injili ya upendo!

Kipindi cha Kwaresma kinawaandaa waumini Wakatoliki kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka yaani ufufuko wa Yesu Kristo. Ufufuko ndio msingi mama wa imani ya Wakatoliki; “…na kama Kristo hakufufuka, basi mahubiri yetu hayana maana na imani yetu haina maana…” (1 Wakaritho15:14). 

Jina hili yaani Jumatano ya Majivu, lilianza kutumika rasmi mwaka 1099 na Papa Urbano II: mwanzoni iliitwa “Mwanzo wa Mfungo”. Majivu yatumikayo hutokana na matawi yaliyobarikiwa Jumapili ya Matawi ya mwaka uliopita. Kwaresima ni kipindi cha siku arobaini za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma. Ni kipindi kinachotualika kumwilisha ndani mwetu utamaduni wa upendo, kwa kufunga na kuwasaidia maskini zaidi. Kipindi hiki cha Kwaresima ni safari ambayo kilele chake ni adhimisho la fumbo la ukombozi wetu yaani mateso, kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Kipindi cha Kwaresma kinadai mambo makuu matatu: Kwanza, kufunga yaani kubadili aina na kiasi cha chakula ambacho mtu huwa anakula kila siku, kiasi kipungue na aina pia ya chakula. Kama wewe umezoea kula milo mizito yenye kila aina ya mahanjumati basi Kwaresma badilisha na ule kawaida kabisa. 

Kufunga hakuishii tu katika kufunga chakula bali kuzuia mianya yote inayomfanya mtu atende dhambi. Hili ndilo jambo la kuzingatia. Kama tunavyosoma katika Kituo cha 14 cha njia ya msalaba kinachosema kwamba; “Pamoja nawe kaburini, zika dhambi na ubaya wa moyo, Yesu tuwe Wakristo kweli. Twakupa, twakupa sasa mapendo.” 

Ni kipindi cha kujinyima na kujikatalia: Pili, kufanya matendo ya huruma au kutoa sadaka, yaani kile ambacho mtu anajinyima basi akipeleke kwa wenye shida. 

Tatu, kuongeza muda wa kusali hasa kwa kusoma Neno la Mungu, yote haya matatu yanaelezwa vizuri sana katika kitabu cha Nabii Yoel 2:12-18. 

Kwa Wakatoliki, tendo hili la Kwaresma huwa linajionyesha kwa kufuata njia ya msalaba ambayo huwa inafanyika siku ya Ijumaa na sehemu nyingine siku ya Jumanne. Bila ya kujali ni siku ngapi za njia ya msalaba mtu anahudhuria. Kinachozingatiwa zaidi ni kuona kuwa vile vituo vyote kumi na nne vya njia ya msalaba vina maana katika maisha ya ufuasi wa Yesu Kristo au tunahudhuria ibada kwa kutekeleza wajibu wa kuonekana kwamba tunapitia vituo vyote kumi na nne kwa masikitiko ya usoni kumbe moyoni ni mkavu kabisa. 

Vituo vya njia ya msalaba havitukumbushi tu machungu na magumu aliyopitia Yesu bali kikubwa zaidi ni sisi waumini tunakumbushwa kujitoa na kuacha mapenzi na makusudi ya mtu yanayomjengea ubinafsi, ili aweze kumfuata yeye aliyejitoa kwa ajili yetu maskini kwa matajiri. Yesu hadai kwamba mwumini lazima apate adha na mateso ya kimwili, lakini anataka kila mfuasi wake awe tayari kutimiza mapenzi ya Mungu ambayo kwayo yanadai zaidi kutimiza na kuishi amri ya mapendo ambayo imeonekana kupitia kwa Yesu Kristo.

Ushiriki wa njia ya msalaba haumfanyi mtu kumtafuta Mungu au kuwa karibu na Mungu tu, bali ushiriki wa ibada ya njia ya msalaba unatufanya na kutulazimu tukuze mapendo kwa ndugu zetu kwa kukwepa na kuogopa kuwafanyia mabaya. Neno haki linakuza na kudumisha upendo, kinyume cha hapo kunakuwa na magomvi, matabaka yasiyo ya lazima, uonevu, unyanyasaji, udhalilishwaji na ubadhirifu wa kila namna na ndipo ufisadi unajikita kwa sababu haki imepindishwa na kutekwa na wenye nguvu. 

Haki katika safu hii naiweka katika maana mbili; kwa upande mmoja haki ina maana ya usawa, uadilifu au uwajibikaji kuhusu sheria ya mambo ya kawaida ya jumuiya ya mwanadamu. Hii tunaweza inaitwa ‘justice’. Sheria ya kutambua haki hii imeandikwa kwenye moyo wa kila mwanadamu na inaitwa dhamira; “…Mwenendo wao unaonyesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. 

Katika siku za Agano la Kale na pia katika Agano Jipya, kama tulivyosikia katika Maandiko Matakatifu ya kuwa ikiwa mtu alikuwa ametenda dhambi, alivaa nguo za magunia na kujipaka majivu katika mwili wake (Rej. Yer 6:26). Tendo hili tunalofanya leo la kupakwa majivu, linatokana na desturi hiyo ya kiroho ya kufanya toba. Katika ulimwengu wa wayahudi majivu yalikuwa ni alama ya huzuni, masumbuko, uchungu au uduni (Rej. Ayubu 2:8, 30:19; Zab 102:10). Baadaye utamaduni huu wa kupakana majivu ulitumiwa na wakristo wa kwanza kama alama ya toba.

Mwaka 600 hivi, Papa Gregory Mkuu aliifanya siku ya Jumatano ya Majivu kuwa siku ya kwanza ya Kwaresima na akaongeza urefu wa kipindi hiki cha toba hadi siku arobaini. Miaka ya 800 hivi, baadhi ya makanisa yaliadhimisha ibada ya Jumatano ya majivu kwaajili ya wadhambi waliokubuhu katika dhambi na waliojulikana. Sasa pale walipoamua kufanya toba ndio walipakwa majivu. Hivi wakati huu si wote walipakwa majivu ila tu wale waliokuwa wadhambi waliojulikana wazi, kama vile Malaya, wauaji, waasi n.k. Kuanzia karne ya 11, Kanisa lilipanua ibada hii na kuwahusisha waamini wake wote na si wadhambi waliokubuhu tu.

Tendo hili liliambatana na matendo mbalimbali ya kufunga, kusali, kutoa sadaka, kuonesha mapendo kwa wengine na matendo mengineyo ya huruma. Leo hii mwenyezi Mungu kwa kinywa cha Nabii Yoeli, anatuita tumrudie Yeye kwa mioyo yetu yote, kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza. Tunaambiwa tuirarue mioyo yetu, na siyo mavazi yetu. Katika siku za Agano la Kale, watu walikuwa na desturi ya kurarua mavazi yao kama ishara ya kufanya toba. Hata hivyo, walikuwepo wengine waliokuwa wakiyararua mavazi yao kama ishara ya nje tu, na kumbe ndani ya mioyo yao hawakuwa na nia ya kufanya toba ya kweli. Mioyo yao ya ‘jiwe’ haikuweza kubadilika! Watu hawa hawakuwa wameyaacha mambo ya kiulimwengu na kuanza kuyaishi maisha mapya, maisha ya kumcha Mungu.

Nabii Yoeli, anatutaka sisi waamini kumrudia Mungu. Katika hili Nabii Yoeli haiti mtu mmoja mmoja, bali anatoa wito kwa watu wote, akisema, “Pigeni tarumbeta katika Sayuni, takaseni saumu, kusanyikeni kusanyiko kuu; kusanyikeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyikeni wazee kusanyeni watoto na hao wanyonyao maziwa” (Rej. Yoe 2:15). Mtakatifu Paulo, katika Waraka wake wa pili kwa Wakorintho, anatusihi tukubali kupatanishwa na Mungu kwa njia ya Kristo. Mungu Baba alimtuma Mwanawe wa pekee, Yesu Kristo, aje kutukomboa kwa kuteswa na hata kufa msalabani. Mungu asiyejua dhambi alimfanya Yesu Kristo kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye (Rej. 2Kor 5:21).

Yesu Kristo hakujua dhambi, lakini alifanywa kuwa dhambi; vivyo hivyo sisi tusio haki tunafanywa kuwa haki katika Yeye. Sisi wadhambi tulistahili kifo hiki cha aibu nakutisha, kifo cha msalaba lakini Yesu Kristo kwa Upendo aliokuwa nao akakubali kutoa Maisha yake kufa msalabani kwa ajili yetu. Katika Injili Yesu anatuonya kuhusu unafiki wa mafarisayo yaani mtindo wa kufanya matendo mema ili kuonekana machoni pa watu wengine. Yesu anasema ya kuwa Mafarisayo hao wamekwisha kupokea thawabu yao kwa njia ya hao watu wengine wanaowatazama na kuwastaajabia, na pia kuwasifia. Watu wa namna hii, anasema Yesu, hawatapokea tena thawabu mbele ya Mungu Baba aliye Mbinguni. Katika kipindi hiki cha Kwaresima, matendo yetu mema yasiwe yale yanayolenga kujionesha hadharani au kwa watu wengine, bali yawe ni mawasiliano binafsi kati yetu na Mungu yaani kujenga muungano na Mungu wetu Mtakatifu sana kwa sala, sadaka na kufunga.

Dhamira zao zinashuhudia pia jambo hili, maana fikra zao mara nyingine huwashitaki, na mara nyingine huwatetea…” (Warumi 2:15). Sheria kama hizi hazijaandikwa kwenye vitabu bali ziko katika moyo wa mtu, mbali na kuwa haiko katika vitabu lakini bado inambana mwanadamu ajue haki ni nini na apange kanuni ili kuendesha haki katika jamii. Utambuzi wa haki hii haikuandikwa lakini bado unamwezesha mwanadamu afahamu yaliyo sawa au yanakwenda kinyume na Mungu. 

Kipindi hiki cha Kwaresma kinatubana zaidi kuhakikisha tunadumisha upendo kwa kutenda haki katika taasisi zote za kiserikali na dini, kwani sote twahesabika kuwa tu wadhambi twaweza tukawahadaa wanadamu wenzetu lakini Mungu bado anaona mioyo yetu kama Nabii Amosi anavyotuambia; “…maana mimi najua wingi wa makosa yenu na ukubwa wa dhambi zenu; ninyi mwawatesa watu wema, mnapokea rushwa na kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.” (Amosi 5: 12). 

Ninawashukuru sana wasomaji kwa ushauri. Nimejisiki niko na watanzania wengi karibu kupitia tafakuri hii. nawapenda sana! Mungu awabariki. 

Shalom,

Max Shimba Ministries Org.

KWANINI MAJINA YA KISLAMU HUFANANA NA MAJINA YA MAJINI?

Image may contain: 1 person
Nilitafakari jambo kwa makini kwanini majina ya kislamu hufanana na majina ya majini, kama maimuna shwaibu, Hassan, Fatuma, Muhammed, Athuman, Sharif, Farid, nk. Kwa ujumla hutakutana na jinni ambalo lina jina la Kikristo majini yoote yana majina ya kiislamu anaeleza Desmon Mkumbo mmoja ya wataalamu wa huduma ya Biblia ni jibu Tanzania. Majini au mapepo pia huhubiri Uislamu kwa nguvu na huhusika kusilimisha watu ukiwa na ugonjwa au pepo limekupagaa ukipelekwa kwa sheikh au maalim akusomee duwa utapewa masharti ya kubadili dini,jina, kusilimu au kuswali haya ni maagizo ya majini Mwenye masikio na asikie!.
Mtume Muhammad alikuwaa anatumia Uchawi?
Muhamad alikwenda Yerusalem akafika pale lilipokuwa Hekalu la wayahudi wenyewe waislamu hupaita Baittil maqdis kwa usiku mmoja kwa kutumia mnyama aitwae “Buraq” Mnyama huyu ni jinni lenye sura ya mwanamke mzuri na mwili wa Farasi (Soma kitabu Maisha ya nabii muhamad uk 28 kifungu cha mwisho) jambo hili lilimfanya akataliwe zaidi na watu wa makka wakisema ni MCHAWI MKUBWA na hawako tayari kumuamini mchawi, Hizi ni khadithi chache tu ambazo zinatudhihirishia kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya Uislamu na Majini, Mashetani na mambo ya uchawi au ushirikina katika uislamu tutachambua mtazamo wa Quran kuhusu viumbe hao ikiwa ni pamoja na mashetani, Malaika na majini. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) ametufundisha dua ya kusoma kabla ya mtu kuigia chooni, akasema:
Ukweli ni kwamba uislamu unajua vizuri majini na namna ya kuwatumia katika shghuli mbalimbali za kiuchawi.
Mtume anasema "
Mmoja wenu anapoingia chooni basi aseme;
"Allaahumma inniy audhu bika minal khubuthi wal khabaaith."
Muhammad anafundisha namna ya kujikinga na wachawi unapoingia Chooni.....lakini jambo linaloshangaza Muislamu ameoneka kumtii shetani anapoingia chooni kwa kuomba msamaha kwa mapepo ya kike na kiume maana baadhi ya mapepo huishi chooni!!!
Je uislamu siyo dini ya shetani? Tafakari.
Katika Biblia tunaona kipindi Yesu alipotwaa mwili na kuja duniani, hao majini, au mashetani au Ibilisi au Mapepo wachafu yalimfahamu na yalianza kulalamika mbele zake.
Mathayo 8:28-31 “ Naye alipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo (Majini) walikutana naye, wanatoka makaburuni wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama wakapiga kelele wakisema tuna nini nawe mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya muhula wetu………………. (Marko 5:1-9).
Majini hayo yanafahamu kuwa Yesu ndiye atakayewahukumu ila yalichoshangaa ni kwamba mbona amewahi kabla ya kipindi chenyewe cha yeye Yesu kuyahukumu kwenda Jehanamu ya Moto?
Yesu alikuja duniani ili kumwokoa mwanadamu kutokana na mateso ya hayo majini au mashetani kwa sabahu katika Ufunuo 12:12 Malaika Mikael alipokuwa anawafukuza hao malaika waasi yaani hao majini au mashetani alisema OLE WA NCHI NA BAHARI ndiyo maana Yesu ilibidi aje duniani kupambana na huyo shetani, Joka, Ibilisi kwa niaba yetu maana sisi tusingeweza na wale, majini walisema kumuambia Yesu ukitutoa tuache tukawaingie Nguruwe na Ngurume wale wapatao 2000 waliona bora kufa baharini kuliko kuishi na viumbe hivi majini au mashetani miilini mwao na hivyo kutimiza ujumbe wa malaika Mikaeli “ Ole wa nchi na bahari”. Baharini ni sehemu mojawapo ambapo majini huishi.
Je Nguruwe ni Bora kuliko Uislamu?
Itaendelea sehemu ya pili.
Tafakari
Hoji mamboo
Chukua Hatua.
Yesu anakupenda

Israel yapeleka kitabu cha Biblia mwezini


BIBLIA NDIO KITABU PEKEE NA CHA KWANZA KUFIKA MWEZINI
ISRAEL imetuma chombo cha anga za mbali ambacho kimeanza safari yake ya miezi miwili kabla ya kutua mwezini kikiwa na Biblia na vitu vingine mbalimbali ambayo vitaachwa huko.
Gharama za kuisafirisha Biblia ni jumla ya Dola Milioni mia moja za Kimarekani.
Chombo hicho kilichorushwa majira ya saa 8:45 usiku wa Alhamisi kutokea Cape Canaveral, Florida, Marekani, kikiwa kinasafirishwa na roketi ya Falcon 9 kutoka kampuni binafsi ya SpaceX inayomilikiwa na bilionea Elon Musk, kina uzito wa kilo 585 na kimepewa jina la Beresheet linalomaanisha “Mwanzo” kwa lugha ya Kihebrania.
Beresheet imeweka rekodi ya kuwa chombo cha kwanza kilichopelekwa mwezini kwa ufadhili binafsi na chombo cha kwanza kwa taifa la Israel na endapo kitafanikiwa kutua mwezini, Israel itajiunga na Marekani, Urusi na China kama nchi pekee zilizowahi kufanikiwa kutua vyombo kwenye uso wa mwezi.
Chombo cha ”Mwanzo” kikifanikiwa kuingia kwenye mzunguko wa dunia na kuzunguka kwa muda wa wiki tatu, kitakutana na nguvu ya mvuto wa mwezi na kinatarajiwa kutua mwezini Aprili 11, 2019, ambapo kitapiga picha na kuzituma duniani kwa siku mbili kabla ya kujizima.
“Mwanzo” kimebeba vitu mbalimbali vya kuvipeleka mwezini vikiwemo kumbukumbu za Myahudi aliyepona katika Mauaji ya Hitler, Biblia ya dijitali, bendera na wimbo wa taifa la Israel na michoro mbalimbali ya watoto.
Inasemekana gharama ya chombo hicho hadi kupaishwa kwake, ni ndogo zaidi ya gharama za vyombo vingine viliyvowahi kufanya safari kama hiyo.
Shalom

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA TISA)

Image may contain: 1 person, text
MALAIKA MKUU RAFAELI
Malaika Rafaeli (kwa Kiebrania רָפָאֵל, Rāfāʾēl, "Mungu anaponya" au "Mungu, ponya!") ni malaika anayetajwa na Kitabu cha Tobiti katika Deuterokanoni na vile vile yupo kwenye kitabu cha Henoko. Kwa hiyo anaheshimiwa na madhehebu yanayokubali kitabu hicho kama sehemu ya Biblia. Katika Uislamu ni sawa na malaika Israfili.
Vitabu vya deuterokanoni (kutoka Kigiriki "deuteros" = ya pili na "kanon" = orodha) ni maandiko ya Agano la Kale yanayotazamwa na Wakatoliki, na baadhi ya Waorthodoksi na ya Makanisa ya Kale ya Mashariki kama sehemu kamili ya Biblia.
Wayahudi na Waprotestanti wengi huviita apokrifa na kuvitazama kama vitabu vinavyostahili kuheshimiwa lakini si sawa na Biblia yenyewe.
Raphael, Malaika Mkuu. Kiebrania ya kawaida, "Mungu ameponya", "Mungu anaponya", "Mungu, tafadhali uponya", na mchanganyiko mwingine wa maneno mawili. Malaika Mkuu wa Kiyahudi na Ukristo, ambaye hufanya kila aina ya uponyaji. Neno la Kiebrania kwa daktari wa dawa ni Rophe aliyeunganishwa kwa neno moja la mizizi kama Raphael. Raphael mara nyingine huonyeshwa (kwa kawaida kwenye medalili) kama amesimama samaki kubwa au akiwa akifanya samaki waliopatikana wakati wa mwisho wa mstari kwenye fimbo ya uvuvi.
YAHWEH-RAPHA: "Bwana anayeponya" (Kutoka 15:26) — "Mimi ni Yehova anayekuponya" kwote katika mwili na nafsi. Katika mwili, kwa kuhifadhi na kuponya magonjwa, na katika roho, kwa kusamehe uovu.
Malaika Wakuu walikuwa daima kuwakilishwa katika sehemu nne. Kitabu cha Henoko majina yao Michael (moja katika malipo ya sehemu bora ya watu), Gabriel (ni malipo ya nyoka, Garden na Kerubim), Urieli (malaika wa ngurumo na tetemeko, yaani Ufunuo 11:13,16; 16:18) na Raphael (maana Mungu imekuponya; Yeye ni malaika wa roho za watu yaani Angel ya Kiyama). Raphael jina labda ni kumbukumbu ya Satanel uvunjaji umba wakati aliasi na kupoteza jina el au suffix na hivyo cheo chake. Shetani alikuwa hivyo kuondolewa kama alivyofunika kerubi. Raphael jina inaweza pia kutaja maridhiano ya ufufuo.
Majina ya malaika muhimu pia ni pamoja na Raguel (ambaye anachukua kisasi juu ya dunia na taa, yaani mwingine malaika wa Ufunuo) na Saraqael (yeye ni malipo ya roho ambaye kusababisha watu kwa dhambi, yaani yeye ni malaika wa kuzimu shimo) (Knibb, The Ethiopic Book of Enoch, Oxford Clarendon, 1982, Vol. 2, Ch. 20.1-2, pp. 106-107). Malaika walikuwa sita katika idadi na hii ni idadi iliyotajwa katika Mchungaji wa Herme kama kuwa katika umbo kati. Mchungaji wa Herme kubainisha Michael malaika mkuu kama katika Sinai ambaye alitoa sheria. Vitendo kubainisha kuwa katika Kutoka kama Kristo. Hivyo, pamoja na vifungu Daniel 10:13,21; 00:01, Yuda 9 na Ufunuo 00:07 ambapo yeye ni mkuu wa jeshi la Bwana, ambayo ni nafasi ya kura ya Kristo, si ajabu kwamba Kanisa ilikuwa kwa kutambua Kristo kama Michael, kabla ya kufanyika kwake.
Kulingana na Johannes Trithemius (1462-1516), Raphael ni mmoja wa malaika wa 7 wa Apocalypse (maoni haya yanatokana na Enoch 20) na huhesabiwa kati ya Sephiroth takatifu ya 10.
Raphael pia anaelezewa kama mmoja wa wanachama wa 7 ambao wanasimama mbele ya Mungu, pamoja na mtawala wa Cherubim na Malaika Mkuu katika uongozi wa mbinguni. Malaika Mkuu, pamoja na Zarachiel, pia ana mamlaka juu ya Raquia, Mbinguni ya Pili.
Malaika wa huruma na uponyaji - Raphael.
Mtawala wa Mbinguni ya Tatu. Whem Oses alitembelea Paradise ilikuwa mbingu ya tatu. Inaaminika pia kuwa "Malaika walioanguka" wamefungwa gerezani huko Raquia.
Kutoka kwa neno la Kiebrania rapha ambalo linamaanisha "daktari" au "mponyaji". Raphael ni mkulima mwenye nguvu na husaidia na aina zote za uponyaji - wanadamu na wanyama. Anasaidia kuponya mwili haraka, mawazo na roho ikiwa inaitwa.
Raphael: ni Mtazamaji wa Kaskazini.
Katika Kanisa Katoliki, "Biblia" ya Kanuni, "Tobit" (Tobit) 5-6 yaliyotajwa katika aya hii: "Rafael alijibu: 'Ndiyo, mimi mara nyingi kwenda Medea, jamaa sana na mitaa mtaa! "
"Tobit" (Tobit) 15-12 kwamba: ". ...... Jina langu ni Raphael, wamesimama mbele ya kiti cha enzi cha mmoja wa wale malaika saba kumtumikia Bwana"
KWA KIFUPI MALAIKA WAKUU 7:
Ufunuo 8
1 Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa.
2 Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.
1. Malaika Mikaeli anayeongoza wizara ya ulinzi/malaika mlinzi.
Malaika Mikaeli (kwa Kiebrania מִיכָאֵל, Micha'el au Mîkhā'ēl, maana yake Nani kama Mungu; kwa Kigiriki Μιχαήλ, Mikhaḗl; kwa Kiarabu ميخائيل, Mīkhā'īl) anaheshimiwa kama malaika mkuu katika imani ya dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu.
2. Malaika Gabrieli anayeongoza wizara ya habari na mawasiliano/malaika mpasha habari.
Katika dini zinazotaka kufuata imani ya Abrahamu, Gabrieli (kwa Kiebrania גַּבְרִיאֵל|Gavri'el|Gaḇrîʼēl, Mungu ni nguvu yangu; kwa Kiarabu جبريل, Jibrīl or جبرائيل Jibrāʾīl) ni malaika aliyetumwa na Mungu kuleta ujumbe wa pekee.
3. Malaika Rafaeli anayeongoza wizara ya afya/malaika mponyaji.
Malaika Rafaeli (kwa Kiebrania רָפָאֵל, Rāfāʾēl, "Mungu anaponya" au "Mungu, ponya!") ni malaika anayetajwa na Kitabu cha Tobiti katika Deuterokanoni. Kwa hiyo anaheshimiwa na madhehebu yanayokubali kitabu hicho kama sehemu ya Biblia. Pia anatajwa katika kitabu alichoandika mtume Bartholomayo.
4. Malaika Urieli anayeongoza wizara ya nuru/Malaika wa nuru.
Urieli(kwa kiebrania אוּרִיאֵל , "Mungu ni nuru yangu") ametajwa katika kitabu cha Ezra wa pili(2 Ezra) kilichopo katika Biblia ya waorthodox.
5. Malaika Selafieli anayeongoza wizara ya utaratibu/Malaika wa utaratibu.
Selafieli(kwa kiebrania שׂרפיאל , "Mkuu wa utaratibu juu ya malaika") ametajwa katika kitabu cha Enoko kilichopo katika biblia ya waorthodox.
6. Malaika Barachieli anayeongoza wizara ya heri/malaika wa heri.
Barachieli( kwa kiebrania ברכיאל , "Heri na Mungu" kiarabu بُراقيل "Buraqil") ametajwa katika kitabu cha Enoko kilichopo katika biblia ya waorthodox.
7. Malaika Jegudeli anayeongoza wizara ya kusifu/Malaika wa sifa.
Jegudeli(kwa kiebrania יהודיאל‎ , Yehudiel "sifa ya Mungu" au "Mungu wa wayahudi") ametajwa katika kitabu cha Enoko kilichopo katika biblia ya waorthodox.
Ufunuo 5
6 Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

"Jesus Knocks on Muslim Imam's Door" -- Zak Gariba on Full Circle -- 1/2

INJILI YA BARNABA

No photo description available.
Beleshi Linalochota Waislamu na Kuwatupia Kwenye Shimo la Kuzimu
Ulimwengu wa Kiislamu, kama kawaida yake, unatia juhudi kubwa sana katika kuuchafua Ukristo ili angalau uweze kuendelea kuwashikilia walio ndani yake; na pale inapowezekana, kuwadanganya Wakristo wasiojua Ukristo wala Uislamu.
Kuna mambo mawili makubwa ambayo huwa yananishangaza sana kuhusiana na masuala ya kiroho. Kwanza ni jinsi ambavyo wakuu wa dini wa Kanisa Katoliki wanavyotumia miaka na miaka kusomea dini na Biblia, kisha wanakuja kuishia kufundisha mambo yaliyo nje ya Biblia!!! Kwa mfano, wanawaambia waumini wao kuwa wafu wanatuombea kule mbinguni au kwamba unaweza kufanya misa huku duniani halafu ndugu yako aliyekufa akiwa na dhambi na, kwa ridhaa yake alikataa wokovu, eti atasamehewa dhambi na Mungu atamuingiza mbinguni!!!
Jambo la pili linalonishangaza sana ni kitendo cha Uislamu na Waislamu kutumia uongo kwa juhudi kubwa sana ili kutetea dini yao na kuwafanya waumini wao waendelee kubakia kwenye Uislamu.
Kama dini yenyewe haiwezi kujitetea kwa njia ya neno inalolihubiri, bali inabidi uisaidie kusimama kwa kutumia uongo, kwa nini basi unaitetea? Na kwa nini hasa unaiamini?
Siwashangai wale wasioelewa, lakini nawashangaa wale wanaojua kuwa, “Hapa ninasema uongo ili kumtetea Allah!” Yaani, wanafanya makusudi kusema uongo kwa lengo la kumtetea Mungu ambaye tunatarajia na tunaamini kuwa ana uwezo wote!!!!
Ama kweli duniani kuna mambo!!!
Nikirudi sasa kwenye mada ya leo, mojawapo ya silaha za uongo inayotumiwa na Waislamu kwa lengo la kuinua dini yao ni kusambaza na kuhubiri kile kinachojulikana kama “Injili ya Barnaba.”
Injili ya Barnaba ni nini?
Hiki ni kitabu kikubwa (karibu sawa na injili zote nne za Biblia zikijumuishwa pamoja - maana kina sura 222). Kitabu hili kinaeleza maisha ya Yesu na kudai kwamba kimeandikwa na mmoja wa mitume wa Yesu aliyeitwa Barnaba.
Nakala za zamani kabisa za kitabu hiki ambazo zinajulikana ni mbili – moja kwa Kiitaliano na nyingine kwa Kihispania. Zote zinaonyesha kuwa ziliandikwa kwenye karne ya 15 au 16 baada ya Kristo.
Kwa nini injili ya Barnaba ni ya bandia?
Unaposoma injili hii, unagundua kuwa ni ‘forgery’ au ni ya bandia kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu ziko wazi lakini zingine zinahitaji jicho la karibu zaidi ili kuzitambua.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu hizo:
1. Mwanzoni tu mwa injili hii, Yesu anaitwa ‘Kristo’ (Christ). Imeandikwa: “Dearly beloved the great and wonderful God hath during these past days visited us by his prophet Jesus Christ …” Lakini unavyoendelea kusoma unakuta kwamba Yesu anakataa kwamba yeye si ‘Masihi’. Kwa mfano, katika sura ya 42 imaendikwa: Jesus confessed, and said the truth: "I am not the Messiah."
Neno ‘Kristo’ (Christ) ni tafsiri ya Kigiriki ya neno la Kiebrania ‘masihi’ (Messiah). Kwa hiyo, Kristo na Masihi ni neno lilelile. Licha ya hivyo, katika maisha yao yote, Wayahudi walikuwa wakimtarajia Masihi. Hivyo, hili lisingekuwa ni neno geni kwao kiasi cha kumfanya mwandishi ashindwe kulielewa.
Mbali na hayo, Barnaba halisi anayejulikana kwenye Biblia aliishi kwenye kisiwa cha Kipro (Cyprus) ambako wenyeji wake walizungumza Kigiriki. Na Barnaba mwenyewe alikuwa ni Mwebrania. Kwa hiyo, asingeweza kamwe kushindwa kuelewa kuwa maneno haya yanabeba maana ileile katika lugha mbili tofauti ambazo alizizungumza zote.
Kwa hiyo, huu ni ushahidi kwamba mwandishi wa Injili ya Barnaba ni mtu ambaye hakujua Kigiriki ndiyo maana mwanzoni tu mwa injili yake hii anamwita Yesu ni Christ, ilhali ndani anamfanya Yesu aseme kuwa yeye si Messiah!
2. Quran inasema kwamba Yesu ni Masihi. (Tazama Sura 3:45). Na Biblia nayo inasema kuwa Yesu ni Masihi. Kama wewe Mwislamu unaamini kuwa Quran ni kitabu cha kweli; na kwamba kile inachokisema ni kweli, iweje basi uamini injili ya Barnaba inayosema kuwa Yesu si Masihi na usiamini Biblia inayosema kuwa Yesu ni Masihi kama ambavyo Quran yako inasema?
3. Katika sura ya 3, ‘barnaba’ huyu anatuambia kuwa Herode na Pilato walitawala Yudea wakati Yesu alipozaliwa. There reigned at that time in Judaea Herod, by decree of Caesar Augustus, and Pilate was governor in the priesthood of Annas and Caiaphas. Wherefore, by decree of Augustus, all the world was enrolled; wherefore each one went to his own country, and they presented themselves by their own tribes to be enrolled. Joseph accordingly departed from Nazareth, a city of Galilee, with Mary his wife, great with child, to go to Bethlehem (for that it was his city, he being of the lineage of David), in order that he might be enrolled according to the decree of Caesar…….. While Joseph abode there the days were fulfilled for Mary to bring forth.
Herode alitawala Israeli kati ya mwaka 37-4 kabla ya Kristo. Unaweza kusoma HAPA au kwingineko kokote. Lakini Pilato alitawala miaka zaidi ya ishirini baadaye, yaani kati ya 26-36 baada ya Kristo. Unaweza kusoma HAPA. Sasa, kwa kuwa Barnaba aliishi pamoja na Yesu, wakati ambapo Pilato alikuwa mtawala, inawezekanaje akafanya kosa lililo wazi kama hili? Hili ni kosa linaloweza tu kufanywa na mwandishi ambaye hakuishi nyakati za Yesu au nyakati za Pilato.
4. Katika sura ya 20 tunaambiwa na ‘barnaba’ kwamba Yesu alisafiri baharini kutoka Galilaya hadi Nazareti. Imeandikwa: Jesus went to the sea of Galilee, and having embarked in a ship sailed to his city of Nazareth. Hebu tafuta Nazarethi kwenye ramani HAPA, kisha uangalie kama mtu anaweza kusafiri kwa chombo cha majini kutoka kwenye Bahari ya Galilaya hadi Nazarethi.
Nazarethi iko kilometa takriban 14 kutoka Bahari ya Galilaya. Ni mtume gani wa Yesu angeweza kusema jambo kama hili – ukichukulia kwamba Yesu na mitume wake walikuwa wakitembea sana kwenye maeneo haya? Hii inaonyesha tu kwamba mwandishi wa injili ya Barnaba hajui jiografia ya Nazarethi au Galilaya.
5. Yehova aliagiza kwenye Biblia kwamba watu washerehekee mwaka wa Yubile kila baada ya miaka 50. Imeandikwa: Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile. Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa (Walawi 25:10-11).
Mwaka 1300 B.K, papa Boniface VIII alitangaza kimakosa kuwa Wakristo wanatakiwa washerehekee siku hiyo kila baada ya miaka 100. Lakini, mwaka 1350 B.K, papa aliyefuata, yaani Clement VI, alirudisha utaratibu wa kawaida wa kusherehekea yubile kila baada ya miaka 50. Kwa hiyo, kwa kipindi cha miaka 50, yaani kuanzia 1300 hadi 1350, watu walikuwa wakijua kwamba yubile inasherehekewa kila baada ya miaka 100. Soma HAPA.
Na huyu mwandishi wa Injili ya Barnaba kwenye sura ya 82, anamwekea Yesu maneno mdomoni kwamba eti alisema: “insomuch that the year of jubilee, which now comes every hundred years, shall by the Messiah be reduced to every year in every place."
Hivi, kama ukiona sinema ambayo mtu anakwambia hii ni ya mwaka 1910, na inaonyesha watu wamevaa mavazi ya zamani na nyumba ni za zamani, lakini humo ndani kwa nyuma ukaona bendera ya taifa la Tanzania inapepea utawaza nini?
Kihistoria inajulikana kabisa kwamba bendera hiyo haikuwapo mwaka 1910. Maana ya kuwapo kwake kwenye sinema hiyo ni moja tu – kwamba hiyo ni sinema ya uongo!
Sasa, suala la yubile ya kila miaka 100, kwa mara ya kwanza, lilikuja mwaka 1300. Halafu waislamu mnataka kuwaambia watu kuwa injili ya Barnaba iliandikwa na mtume aliyeishi na Yesu kwenye karne ya Kwanza, yaani miaka 1300 kabla ya jambo hili linalohusiana na yubile ya kila miaka 100 kutokea. Au huyu mheshimiwa 'barnaba' alikuwa anaongea kinabii?
Kwa msomaji unayependa KWELI, hili linakuonyesha kitu gani? Bila shaka jibu liko wazi kwamba mwandishi wa injili hii aliishii baada ya mwaka 1300. Amka!!!
Barnaba wa karne ya 1 asingeweza kamwe kuandika au kusema jambo kama hili; na zaidi ya yote Yesu…?!
6. Katika sura ya 178, injili ya Barnaba inatuambia kuwa ili ufike paradiso ni lazima uvuke mbingu 9. Ikimaanisha kuwa, paradiso ni ya kumi. Imeandikwa: Truly I say to you that the heavens are nine, ……. And truly I say to you that paradise is greater than all the earth and all the heavens together.
Katika karne ya 14 kule Italia kulikuwa na mshairi maarufu aliyeitwa Dante Alighieri. Katika mojawapo ya vitabu vyake, Dante anazungumzia jambo hilihili. Yaani anasema kuwa ili kufika paradiso unatakiwa kuvuka mbingu tisa!!! Unaweza kusoma HAPA.
Na inajulikana, kama nilivyosema mwanzo wa makala haya kuwa, nakala za zamani kabisa zinazojulikana za injili ya Barnaba ni mbili – moja ya Kiitaliano na nyingine ya Kihispania. Na hizi zinajulikana kuwa ni za kwenye takriban karne ileile ya Dante. Waswahili wanasema, mwenye macho haambiwi tazama!!
7. Sura ya 193 ya Injili ya Barnaba inaongelea juu ya kifo cha Lazaro ambaye alifufuliwa na Yesu. Kisha Yesu anasema kuwa saa yake (ya kufa) ikifika naye atalala vilevile kama Lazaro na atafufuliwa mara moja. Imeandikwa: 'My hour is not yet come; but when it shall come I shall sleep in like manner, and shall be speedily awakened.'
Lakini unapofika kwenye sura ya 216 na 217, wakati ambapo Yesu amekamatwa ili auawe, tunaambiwa kuwa Mungu alimwondoa kimiujiza (kama Quran inavyosema) na badala yake mungu huyu (anayeonekana kuwa ni mwongo) akamvika Yuda sura ya Yesu na Yuda akauawa kwa kuwa watu waliomjia Yesu walidhani kuwa Yuda ndiye Yesu.
Swali ni kuwa, je, si Yesu katika sura ya 193 ndiye aliyesema kwamba angekufa na kufufuliwa? Mbona basi Mungu anamkimbiza na kumficha badala ya kutimiza lile ambalo Yesu alilisema?
Mwenye macho haambiwi tazama!!
8. Sura ya 54 inasema kuwa mafarisayo walikuwapo wakati wa nabii Eliya. Lakini historia inaonyesha kuwa Mafarisayo walitokea kuanzia karne ya pili kabla ya Kristo. Soma HAPA au kwingineko.
Lakini nabii Eliya aliishi kwenye karne ya 9 kabla ya Kristo. Soma HAPA. Hiyo ina maana kuwa aliishi takriban karne 7 kabla mafarisayo hawajatoke. Sasa iweje huyu barnaba atuambie kuwa mafarisayo walikuwapo nyakati za Eliya?
9. Sura ya 80 inatumbia kwamba Danieli alichukuliwa na Nebukadreza kupelekwa Babeli akiwa na miaka miwili. Imeandikwa: Daniel as a child, with Ananias, Azarias, and Misael, were taken captive by Nebuchadnezzar in such wise that they were but two years old when they were taken; and they were nurtured among the multitude of idolatrous servants.
Unaposoma Biblia inatuambia kwamba: Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. (Dan. 2:1).
Matokeo yake Nebukadreza alitaka waganga na wataalamu wa kutafsiri ndoto wamwambie maana ya ndoto ile. Kila mmoja alishindwa lakini Danieli alitafsiri ndoto ile baada ya kumwomba Yehova.
Matokeo yake, Biblia inasema: Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli. (Dan. 2:46-48).
Sasa, Nebukadreza aliota ndoto hii akiwa katika mwaka wa pili wa kutawala kwake. Kama alimchukua Danieli kutoka Israeli katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake, hiyo ina maana kwamba, Danieli alitafsiri ndoto ile akiwa na miaka mitatu; na pia alifanywa kuwa liwali (mbunge) akiwa na miaka hiyohiyo mitatu!
10. Jambo jingine ambalo ni kichekesho kikubwa kuhusiana na hii injili ya Barnaba ni kuwa Yesu hakuwahi kuwa na mtume aliyeitwa Barnaba. Mitume wa Yesu wanajulikana. Unaweza kusoma Mathayo 10:2-4; Luka 6:13-14.
Sasa, Barnaba ni nani?
Huyu alikuwa ni mwanafunzi aliyemwamini Yesu baadaye wakati Yesu tayari alishafufuka na kupaa kurudi mbinguni. Wakati mitume alioacha Yesu walipohubiri injili ya Yesu, mmoja wa watu waliosikia na kuiamini na kuokolewa alikuwa ni Yusufu (Joseph), mwenyeji wa Kipro (Cyprus).
Huyu aliuza shamba lake akaleta fedha kwa mitume ili wenye uhitaji waweze kugawiwa. Mitume walimpa jina la Barnaba likiwa na maana ya ‘mwana wa faraja.’
Imeandikwa: Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji. Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume. (Matendo ya Mitume 4:33-37).
Kwa hiyo, Barnaba hakuwa mmoja wa mitume wa Yesu!
Je, unadhani baada ya ushahidi huu kidogo (maana upo zaidi) bado utashikilia kuwa Injili ya Barnaba ni ya kweli? Unafikiri ni nani aliiandika? Kama umewahi kuisoma injili hii, ni kitu gani kitakachokufanya upinge hoja kwamba injili hii iliandikwa na mwislamu aliyeishi Italia katika karne ya 14, 15 au 16 ambaye alikuwa anajaribu kumhalalisha Muhammad kama ambavyo ninyi Waislamu mmeendelea kufanya hadi hivi leo – maana injili yenyewe 'inamfagilia' Muhammad?
Waswahili husema: Mwenye macho haambiwi tazama na pia sikio la kufa halisikii dawa. Je, wewe ni mwenye macho au ni sikio la kufa?
Jiponye mwenyewe.
Utadanganywa hadi lini?
Tafakari.
Hoji mambo.
Chukua hatua.

WADADA WA KISOMALI WANAENDELEA KUUKUBALI UKRISTO NA KUMKANA MUHAMMAD

Image may contain: 1 person, text and closeup


Maisha ya Maonyesho na Ubatili
Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? 
(Yeremia 17:9).
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. (Wagalatia 6:4).
Katika somo lililopita nililoliita Nia ya Ndani ya Moyo niligusia kuhusu umuhimu wa kuwa makini na nia zetu pale tunapomwendea Mungu, maana Mungu anajali sana hizo nia ambazo ndizo zinazoamua endapo atayakubali maombi yetu au tutaishia kupata hasara.
Katika somo hili namwomba Mungu anisaidie kufafanua kwa uwazi zaidi kile ambacho hasa kinaweza kuwa kinaendelea ndani ya mioyo yetu, ambacho ndicho anachokiona Mungu wetu pale anapotutazama.
Katika nyakati za Biblia kulikuwa na dhambi ambazo, labda niziite kuwa ni “za jumuiya.” Dhambi za namna hii zingeweza kutendwa na mtu mmoja lakini athari zake zikaangukia familia au hata taifa zima – ingawaje wengine wanakuwa hata hawakushiriki au hawakujua kwamba mkosaji halisi alikuwa anatenda dhambi hiyo.
Kwa mfano, Mfalme Daudi alipofanya kosa la kuwahesabu Israeli, alisababisha vifo kwa watu ambao hawakuhusika na kosa lake. Imeandikwa: Basi Bwana akawaletea Israeli tauni tangu asubuhi hata wakati ulioamriwa; nao wakafa watu toka Dani mpaka Beer-sheba sabini elfu (2 Samweli 24:15).
Pia, tunasoma kuhusu wana wa Israeli kwa ujumla kuhesabika kuwa wametenda dhambi kutokana na kosa la mtu mmoja, yaani Akani. Matokeo yake walishindwa kwenye vita na kakabila kadogo sana ka Ai.
Imeandikwa: Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli. (Joshua 7:1).
Mbali na hivyo, kosa la Akani pia lilisababisha kuangamia kwa familia yake yote. Imeandikwa: Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori. Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe. (Yoshua 7:24-25).
Lakini ilifika mahali ambapo Bwana akasema: Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapoipanda nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, mbegu ya mwanadamu na mbegu ya mnyama. … Siku zile, hawatasema tena, Baba za watu wamekula zabibu kali, na meno ya watoto wao yametiwa ganzi. Bali kila mtu atakufa kwa sababu ya uovu wake mwenyewe; kila mtu alaye zabibu kali, meno yake yatatiwa ganzi. (Yeremia 31:27, 29-30).
Na tena, ingawaje tunatakiwa kabisa kubebeana mizigo, kwa maana ya kusaidiana kwa upendo ili kuleta furaha, amani, uponyaji, n.k., lakini inapokuja kwenye hatima ya suala la dhambi na athari zake kwa yule azitendaye, imeandikwa: … kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe. (Wagalatia 6:5).
Ndugu zangu, ninachotaka kusema hapa ni kwamba, Mungu anatupima kibinafsi katika kila jambo tunalojihusisha nalo hapa duniani. Kama ambavyo unaona kwamba ukinunua muda wa maongezi kwenye simu, hauwezi kamwe kuidanganya mitambo ili kwamba eti uongee hata kwa nusu sekunde na usikatwe pesa. Haiwezeani! Ukibonyeza tu, hata kama ingekuwa ni usiku wa manane, lazima mtambo utatambua na pesa yako itakatwa mara moja kulingana na kiwango cha upigaji simu wako!
Hiyo ni teknolojia ya kibinadamu. Mungu ni zaidi! Hakuna sekunde yoyote katika maisha yetu inayompita. Hakuna!! Na kila kitu kinawekwa kumbukumbu mbinguni – kiwe ni tendo linaloonekana kwa nje au ni wazo lililojificha moyoni!! Ndiyo maana imeandikwa kwamba Mungu atazihukumu siri za wanadamu (Warumi 2:16).
Je, ni kwa nini unafanya yale unayoyafanya?
Hakuna mwanadamu anayejua kile kinachoendelea moyoni mwako. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? (1 Wakorintho 2:11). Roho yako, au wewe mwenyewe (pamoja na Bwana) ndio mnaojua kile kinachoendelea ndani ya moyo wako. Na kwangu vivyo hivyo! Na kwa mwingine vilevile!
Sasa, kwa nini unafanya yale unayoyafanya? Nia yako ni nini?
Katika mambo ya kawaida kabisa ya kila siku maishani mwetu ni lazima kujiuliza swali hili: Kwa nini ninafanya hivi? Makusudi yangu ni nini?
Kwa nini unataka nguo ya gharama kubwa wakati ziko za gharama ndogo za ubora uleule?
Kwa nini unataka uwe na magari kumi?
Kwa nini unataka kumiliki maduka matano?
Kwa nini unachubua ngozi yako?
Kwa nini umebadili rangi ya nywele zako?
Kwa nini umechora ‘tattoo’ kwenye mwili wako?
Kwa nini unavaa mavazi yanayoacha wazi sehemu za mwili wako ambazo hazitakiwi kuachwa wazi?
Kwa nini umevaa mlegezo?
Kwa nini ulitoa mchango mkubwa sana kwenye harusi ya yule ndugu?
Kwa nini umevaa nyusi za bandia?
Kwa nini ukiwa kanisani unaonyesha sura ya unyenyekevu lakini ukiwa nje haufanyi hivyo?
Simu yako ni ya gharama. Kwa nini unapenda kuitoatoa mbele za watu hata kama haupigi au haujapigiwa?
Kwa nini umevaa cheni na unafungua vifungo vya shati lako?
Kwa nini umevaa nguo inayoacha maziwa nje?
Kwa nini ulimsaidia yule mtu aliyeomba msaada?
Mengi ya mambo haya ni ya kawaida kabisa katika maisha yetu ya kila siku na hayana ubaya hata kidogo!! Hakuna ubaya kuwa na magari kumi, nyumba tano, simu ya shilingi milioni moja, n.k. Hakuna ubaya!
Swali hapa ni moja tu: Moyo wako au moyo wangu unakuwa unanisukumaje mbele za watu? Kwa lugha rahisi, je, ninapenda kujionyesha? Ninaona fahari fulani watu ‘wanaponitambua’? Ninakuwa na shauku kila mtu ajue kuwa mimi ni wa kiwango cha juu? Je, kila wakati nakuwa naangalia kwa jicho la chati ili kubaini kama kuna watu wananitupia angalau jicho sawasawa na ninavyotamani wafanye?
Ni hakika kabisa hivi ndivyo maisha ya wengi wetu yalivyo. Ni maisha ya maonyesho, maonyesho, maonyesho tu! Ni maisha ya kusaka sifa na umaarufu! Ni maisha bandia! Hatumfikirii Bwana bali tunawafikiria wanadamu. Tunatamani kusifiwa na wanadamu.
Kwa watu wa dunia hii ni sawa kabisa. Lakini je, kwa Mungu nako ni sawa? Kwa wapendwa nako inatakiwa iwe hivyo?
Je, kanisa litatofautishwaje na dunia kama nalo linafanya mambo haya? Je, ni kwa kiasi gani haujanaswa na mtego huu? Ni kwa kiasi gani haujaingia kwenye kapu hili?
Kwa nini unafanya yale unayoyafanya?
Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake. (Wagalatia 6:4).
Labda binti au msichana unasema, “Sasa nisipojipodoa na kujipamba nitapataje mume?” Dada yangu, kama Mungu ni Baba yako, basi lia na Yeye. Kibinadamu unaonekana kuna mantiki kabisa. Inaonekana kana kwamba usipojihangaisha kwa namna Fulani, basi utakosa mume. Lakini Bwana anapotutazama anasikitika kwa sababu hayo si maagizo yake. Maagizo yake yanasema: Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona. (2 Wakorintho 5:7). Kwa kuwa: Mwenye haki ataishi kwa imani. (Warumi 1:17).
Jambo moja la msingi sana, si kwa akina dada tu, bali kwa kila mwanadamu, ni kufika mahali pa KUAMUA kuwa, “Mimi nitasimama na Bwana peke yake! Awe amenipa kile ninachokiomba au hakunipa. Basi!!”
Huku ndiko kuyatoa maisha YOTE kwa Bwana. Lakini hii haitufanyi tuache kuomba kwa bidii zote yale ambayo mioyo yetu ina shauku nayo.
Ni hasara sana kuishi maisha ambayo yanataka tu kuwavutia wanadamu na kutaka kusifiwa nao. Hayo ni maisha ya UBATILI mkubwa.
Bwana anatuagiza katika sura ya sita ya Kitabu cha Mathayo:
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. (Mathayo 6:1-8).
Japo hapa Bwana anaongelea zaidi suala la utoaji sadaka na maombi, lakini, kimsingi, yuko kinyume na maisha ya maonyesho mbele za watu. Tukifanya mambo kwa nia ya kuonekana mbele za watu ni kweli kabisa tutafanikiwa katika hilo. Tutasifiwa na kupata umaarufu huu batili wa dunia. Lakini hiyo ndiyo itakuwa thawabu yetu.
Simaanishi kuwa sasa basi uwe mchafumchafu kwa sababu tu eti hauko hapa kuifurahisha dunia bali Bwana! La hasha! Uchafu pia ni dhambi. Ninachomaanisha ni mtu kufanya mambo yake hasa kwa ajili ya Bwana. Ni kufika mahali ambapo kila kitu ninachofanya ni kwa ajili ya kumtukuza Bwana wangu, Yesu Kristo. Kama kwa jambo hilo dunia itanisifu, sawa. Kama haitanisifu, nako sawa pia. Lakini kusifiwa na wanadamu kusiwe ndio sababu ya msingi inayonisukuma kufanya jambo lolote.
Bwana anaagiza: Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu. (1 Wakorintho 10:31).
Siamini kamwe kwamba mtu aliyeamua kwa dhati kuyafanya yote kwa utukufu wa Mungu atahangaika na mambo haya. Tunahangaika nayo kwa kuwa tu tumenaswa na ubatili wa dunia.
Ni nani yuko tayari kumwangalia Bwana pekee na kuachana na ulimwengu huu? Ni nani ee Bwana aliye tayari kutafuta kwa bidii sifa kutoka kwako badala ya sifa za wanadamu? Ni nani aliye tayari ee Bwana kujikagua katika KILA wazo, neno na tendo, KILA sekunde ya maisha yake?
Hakika yake Bwana hatuwezi. Hatuwezi kabisa bila neema yako. Tusaidie kuishi maisha matakatifu badala ya kushiriki na kuwa sehemu ya giza la dunia hii. Maana umesema kuwa sisi ni nuru ya ulimwengu. Lakini badala yake tumemezwa na giza; na sasa tunatafuta kila sababu [hata za kimaandiko] za kuhalalisha mambo haya ya giza. Tupe ufunuo wa rohoni ee Roho Mtakatifu ili tujue umuhimu na kuwa na utayari wa kubadilishwa na kupewa mioyo mipya inayoweza kukutii. Ni katika jina la Yesu naomba. Amina.

A devout Muslim woman who harbored a deep hatred of Christians converted to Christianity after Jesus.

Image may contain: 1 person, sitting, table and indoor
By LEAH MARIEANN KLETT ( news@gospelherald.com )
A devout Muslim woman who harbored a deep hatred of Christians converted to Christianity after Jesus appeared to her in a dream and told her to visit a local church.
An Assyrian woman attends a Mass on March 1, 2015, inside Ibrahim al-Khalil church in Jaramana, eastern Damascus, in solidarity with the Assyrians abducted by Islamic State fighters in Syria. Photo courtesy of REUTERS/Omar Sanadiki
A devout Muslim woman who harbored a deep hatred of Christians converted to Christianity after Jesus appeared to her in a dream and told her to visit a local church.
According to Christian Aid Mission, the young woman, whose name was not disclosed for security reasons, lived in Turkey's Black Sea coast along with her strict Muslim family. One Sunday, she showed up at the church of Pastor Matta, the leader of an indigenous ministry reaching Turkey's 96-percent Muslim population.
Through tears, she told the pastor she had seen him preach on weekly Web posts of the church's services.
"I did not know you, and I hated the Christians, and for this reason I was intending to make fun of you when I started watching your videos in the Internet," she said. "But the things I was hearing from you spoke to me of the love I was always looking for, and the words of faith and courage were doing away with my fears."
Her heart transformed by the truth of the Gospel, the young woman converted to Christianity. However, fearing for her life, she was hesitant to attend a worship service. That is, until Jesus appeared to her in a dream.
"In my dream, Jesus led me to the church, telling me, "What are you still waiting for? Follow my way,'" she told the pastor. "And I saw all of you in there waiting for me, smiling at me. Before I met you, I saw you in my dream. Thanks be to God."
Pastor Matta said he returned home after talking with her and looked up her Facebook page. He was stunned to find she frequently shared her newfound faith with her family and friends.
"I then told her to be careful in doing this because of the resentment she might cause," he said. "I am still worried because of the likely opposition of her family and of her surroundings, and I please ask you to pray for her so that she may grow in the faith, and may gain an entrance to a university of another city."
He added, "This is really a miracle. If these things happened 2,000 years ago, they are still happening today. This young girl still wearing her headscarf, having hundreds of friends in Facebook, does not stop spreading the gospel to others."
Turkey is ranked 37th on Open Door USA's World Watch List of countries where Christians face the most persecution, and has received the maximum score in the violence category.
CAM notes that Christians in Turkey face increasing hostility and discrimination from their Muslim counterparts. Pastor Matta shared the story of a Muslim man who recently put his faith in Christ and is now in serious trouble from his family.
"Since his family found out about his conversion, he is constantly threatened by them that he is to be disowned," he said. "He is very young and pure in heart and loves the Lord. Please pray for him, that he may feel the presence of God supporting him and that he may endure this time of trial. And pray also for wisdom for us to give him right counsel when he comes to us with his problems
He added, "These kinds of situations occur very often in our country, sometimes with wolves entering our church disguised as sheep and threatening the children of God, and at other times with family pressures," he said. "But nonetheless, the work of the Lord is not arrested."
Voice Of the Martyrs Canada, which supports Christian radio broadcasts in the region, told BosNewsLife that despite the large numbers of Christians fleeing the Middle East due to terrorism, persecution, and war, scores of Muslims are making the decision to embrace Christianity. The organization revealed that many Muslims hear the gospel through radio and online sermons.
"There are thousands upon thousands coming to Christ," VOMC revealed. "We are in regular contact with our FM stations in Iraq and have talked with many people who have family in the Middle East."
"Some of our Middle Eastern broadcasters have shared testimonies [about many turning to Christ] with us, which they hear directly from listeners when visiting there ..."

BIBLIA NI KITABU KILICHO TOKA KWA MUNGU


Biblia ni zawadi ya Mungu, na tunapaswa kumushukuru sana kwa zawadi hiyo. 

Biblia ni kitabu kilicho tofauti na vitabu vingine. Inatujulisha mambo ambayo hatungejua. Kwa mfano, inatuelezea namna dunia na mbingu zenye kujaa nyota viliumbwa, na namna mwanaume na mwanamuke wa kwanza waliumbwa. Kanuni za Biblia ni za kweli na zinaweza kumusaidia mutu ajue namna ya kushindana na magumu na mahangaiko ya maisha. Inatufasiria namna Mungu atatimiza kusudi lake na kufanya maisha yawe mazuri sana duniani. Kweli, Biblia ni zawadi yenye kufurahisha kabisa!

Biblia inapatikana katika luga zaidi ya 2 500, yote nzima ao kwa sehemu; kwa hiyo watu wengi duniani wanaweza kuipata (zaidi ya 90%). 

Biblia zaidi ya milioni moja zinagawanywa kila juma! Mamilioni na mamilioni ya Biblia zimekwisha kuchapishwa, iwe yote nzima ao kwa sehemu. Kwa kweli, hakuna kitabu kingine kinacholingana na Biblia.

Biblia ‘imeongozwa na Roho ya Mungu.’ (2 Timotheo 3:16) Maana yake nini? Biblia yenyewe inajibu hivi: “Wanadamu walisema yaliyotoka kwa Mungu kama walivyoongozwa na Roho Mtakatifu.” (2 Petro 1:21) 

Kwa hiyo, Biblia yote nzima ni “neno la Mungu.”​—1 Wathesalonike 2:13.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

MUUJIZA WA BWANA YESU NDANI YA MSIKITI

Huu ni ushuhuda wa dada mmoja wa kutoka Indonesia ambaye, japokuwa zamani alikuwa Mwislamu (na sasa ni Mkristo), Bwana Yesu alimwokoa kimiujiza yeye pamoja na watu wengine kutoka kwenye janga na mauti ya sunami na tetemeko ambavyo vilisababisha vifo vya mamia kwa mamia ya watu
Je, ni nini kilisababisha hadi Bwana Yesu akaingilia kati wakati ule ambapo kifo kilikuwa hakikwepeki?
Fuatilia ushuhuda huu wa kushangaza, ambao kwa maneno yake mwenyewe, dada huyu anasimulia kile kilichotokea, hadi kufikia mahali ambapo yeye na watu hao wakamwamini Bwana Yesu bila hata mahubiri ya moja kwa moja ya Injili. Bwana alihubiri mwenyewe:
Usiku uliotangulia janga lile la sunami na tetemeko, dada huyu aliota ndoto ambayo ilimpa mawazo mengi sana lakini hakujua ina maana gani. Katika ndoto ile, alijiona kuwa anajenga nyumba yake mwenyewe. Kuta tayari zilishasimama lakini kulikuwa hakuna paa; ambalo kwa kawaida huwa ni ishara ya ulinzi. Na nje ya nyumba kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamezunguka nyumba hiyo.
Kulipokucha, dada huyu aliamka na kuendelea na kazi za kawaida za nyumbani. Alikuwa akisafisha vyombo. Ghafla kulitokea tetemeko. Anasema kuwa, “Nilimweleza mume wangu asubuhi ile wakati wa tetemeko kuwa, labda hii ni ishara kuwa watu wengi watakufa. Niliota jambo hili usiku wa leo.
Anaendelea kusema, “Kisha dakika moja baadaye, tetemeko liliisha. Kwa hiyo tulitoka nje. Tutoke nje! Tutoke nje! Halafu maji ya bahari ambayo yalionekana yana kimo kirefu kama urefu wa minazi miwili yalikuwa yakija kuelekea ufukweni.
“‘Tutaenda wapi sasa? Tutaenda wapi sasa?’ kila mmoja aliniuliza. Nikachanganyikiwa kabisa! Nikasema, ‘Ile ni nyumba ya Mungu! Ile ni nyumba ya Mungu!” (yaani msikiti).
“Sote twendeni humo. Nilianza kuomba. Nilijisahau kuwa mimi ni Mwislamu. Nilianza kuomba kama Wakristo wanavyoomba. Nilisema, ‘Bwana Mungu, tulinde kwa wakati huu. Usituharibu Bwana. Usiwe na hasira nasi, Ee Mungu. Tusamehe. Tusamehe dhambi zetu. Bwana Yesu, usiniache.
“Kila mmoja wetu alikuwa akirukaruka, akisema, ‘Bwana Yesu! Bwana Yesu! Ghafla, maji yaliyokuwa yakija, yalikomea kama meta moja hivi kutokea tulikokuwa.”
ya kuona hivyo, dada huyu anaendelea kusema, “Sote tulikuwa tukilia, ‘Asante Bwana Yesu. Kila mmoja aliamini kuwa Bwana Yesu alituokoa wakati ule. Hakuna mwingine wa kumgeukia ila Yeye tu.”
Yanayofuata ni maelezo ya msimuliaji, Dr. Randy Richards, ambaye alikuwa mmoja wa watoa misaada wa kujitolea (Tsunami Relief Volunteer) kwenye eneo hilo:
“Mara maji ya bahari yalipokoma, walienda sehemu zenye mwinuko wa juu, kwenye milima. Na baadaye waliporudi, kila upande kuzunguka msikiti, kulijaa miili ya watu waliouawa na maji ya bahari.
“Akasema,” (yaani yule dada), ‘Hapo ndipo nilipotambua maana kamili ya ile ndoto yangu.’
“Nyumba ilikuwa haijakamilika. Haikuwa na paa. Haikuwa na ulinzi. Hawakuwa na Yesu. Na kama ilivyokuwa kwenye siku za Nuhu, kila mtu aliangamia. Kwa hiyo, watu wote hawa ambao walikuwa wamezunguka nyumba ambayo ilikuwa haijakamilika, waliangamia.
Randy anaendelea kusema, “Yesu aliamua kuwaokoa watu wale kwa ajili ya ushuhuda. Sijui anakusudia nini, lakini hakika ameyabadilisha kabisa maisha ya watu wale; na ushuhuda uko pale.”
INGIA HAPA NA ANGALIA VIDEO YA USHUHUDA https://www.youtube.com/watch?v=1yU87JMtzEo
Yanayofuata ni maneno yangu blogger:
Ndugu unayesoma ushuhuda huu, sijui wewe umo kwenye nyumba ya namna gani? Je, ni nyumba yenye paa au ni nyumba isiyo na paa?
Hebu sikia maneno ya Bwana Yesu mwenyewe:
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. (Mathayo 7:24-27).
Njoo kwa Yesu leo ili upone. Nje ya Yesu, hakika yake, kuna mauti, upotevu na uangamivu pekee. Hakuna uzima isipokuwa kwa Yesu peke yake!

ALLAH KATEREMSHA AYA NA KUSEMA WATAKAOINGIA PEPONI NI WATU WENYE CHUKI

Image may contain: 23 people
Sura Al-Nahl 16:28
[Kuhusu wale wanaoingia mbinguni] – Malaika watasema kwa wale ambao watawafanya wafe katika usafi (utakatifu), ‘Amani na iwe juu yenu. Ingieni paradiso kutokana na matendo yenu.’
LAKINI, QURAN HIYO HIYO INASEMA:
Sura Al-Hijr 15:45-47
Wenye haki (watakatifu) watakaa kwenye bustani na chemchemi za maji, kwa amani na usalama wataingia humo. Nasi tutaondoa chuki yote ndani ya mioyo yao.
Maswali:
1. Katika 16:28, inaonekana kwamba watakaiongia peponi ni watu walio safi kwa sababu malaika wamesababisha watu hao wafe wakiwa safi. Lakini 15:45-47 inaonyesha kuwa wataingia peponi wakiwa na chuki mioyoni mwao. Je, chuki ni sehemu ya usafi?
2. Je, aya hizi zimetoka kwa mtoaji yule yule?
3. Kama chuki ni mbaya kiasi cha kuhitajika kuondolewa mioyoni mwa Waislamu wanaoingia peponi, iweje wakiwa duniani wanaagizwa kuwachukia wale wasio Waislamu (kama tulivyoona kwenye 4:101)?
HITIMISHO
Hizi ni baadhi tu ya aya ambazo zinaonyesha kuwa quran au Allah anasema jambo moja hapa, kisha anajipinga mwenyewe katika sehemu nyingine.
Na ukweli huu, ninavyodhani,unamaanisha kuwa, ama:
1. Si kila aya iliyo kwenye quran ni maneno ya Mungu muumba vyote – maana Mungu huyo hawezi kufanya mambo kama hayo; au
2. Quran haitokani na Mungu bali imetokana na chanzo kingine, ndiyo maana inaonyesha tabia za viumbe za kujisahau au kutojua mambo yote, hususan yajayo.
Nadhani siku ya mwisho Muhammad atawakana watu wote wanaomwamini maana atakuja kusema kwamba, “Mimi niliwaambia kuwa wakitaka kujua kama quran inatoka kwa Allah waangalie kama quran inajikanganya. Sasa waliona kuwa inajikanganaya, lakini wao wakendelea tu kuiamini.
Pia Muhammad atawakana wale wote wanaomwamini na kumfuata kwa sababu yeye mwenyewe anasema wazi katika sura Al-Ahqaf 46:9,
... nor do I know what will be done with me or you. I follow only what is revealed to me.
Yaani,
... na wala mimi sifahamu kile nitakachotendewa wala kile ninyi mtakachotendewa. Mimi nafuata tu kile ninachofunuliwa.
Swali ni kwamba, je, kama mtu mwenyewe anakiri kuwa hajui hatima yake wala hatima ya wale wanaomfuata, je, kama ni kweli Mungu wa mbinguni ndiye aliyempatia quran, je, angekaa kimya kweli juu ya suala la HATIMA za wanadamu? Yaani jibu la mtu atakuwa wapi MILELE lingeachwa hewani tu hivihivi? Na kama Muhammad hajui hili na bado anataka watu wamfuate, je, ni hilohilo tu asilolijua au yapo na mengine asiyoyajua? Bila shaka hii inaashiria kuwa yako mengi asiyoyajua.
Sijui kwa kweli! Kama nilivyosema, mimi kwa mambo haya ni maamuma tu. Kwa hiyo, inawezekana niko nje kabisa ya kile kinachomaanishwa. Nitafurahi kama ndugu zangu Waislamu mtanisaidia kujua mambo haya.
Lakini kwa ule upande ambao mimi naufahamu zaidi, yaani Ukristo, Bwana Yesu anasema: Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. (Yohana 14:6). Yaani, hakuna namna ya kwenda mbinguni isipokuwa kwa kumwamini Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi. Hiyo ndiyo namna pekee ya kufika mbinguni. Tafakari!

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW