WAISLAM NYIE MNA MA-ALLAH WANGAPI?
Hebu rejea kwenye Kuran kwanza:
Suratul Anbiyaa 91. Na mwanamke aliye linda uke wake, na TUKAmpulizia katika roho YETU, na TUKAmfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.
Ndugu zanguni, Allah ameanza vituko vyake hapa. Katika Koran Allah anadai kuwa hana msaidizi Suratul Baqarah: aya 106 ― 107 Lakini katika aya tuliyo isoma hapo mwanzoni - Suratul Anbiyaa 91 tumeona kuwa Allah anatumia wingi alipo kuwa akielezea jinsi alivyo mpa ujauzito Maryam na au labda wenzetu wana MA-ALLAH WENGI.
Waislam, nyie mna Ma-Allah wangapi?
ULE UTATA UNAOWASUMBUA WATU KILA KUKICHA, JE! HAWA WANAOTUMIA WINGI KATIKA QURAN NI MUNGU AU NI WENGINE?
ALLAH ANAMUUMBA ISA BIN MARYAM KWA KUTUMIA WINGI:
Kuran imejaa utata, hebu soma hapa Suratul Attahriim 12. Na Mariamu binti wa Imrani, aliye linda ubikira wake, na TUKAmpulizia humo kutoka ROHO YETU, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu vyake, na alikuwa miongoni mwa wat'iifu.
HAPA: Allah anasema kwa undani zaidi TUKAmpulizia ROHO YETU. Hivi huyu Allah ni kweli alikuwa Mungu au ni madai ya Muhammad na rafiki yake Jibril? Mbona alisema kuwa yeye hana msaidizi wala Mwana? Kivipi Allah anatumia wingi katika kumuumba Isa Bin Maryam? Kumbe Waislam mna Ma-Allah wengi.
Aya zaidi kuhusu Maryam na kupata ujauzito za Isa: Suratul Anbiyaa 91.
Endelea hapa tena:
ALLAH ANAMUUMBA BINADAMU KWA KUTUMIA WINGI:
Suratul Hijr 26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
HAPA tumesoma kuwa Allah anamuumba Binadamu kwa kutumia wingi" Nukuu: Na TULIMUUMBA MTU"
Endele hapa tena
ALLAH ANAUMBA MAJINI KWA KUTUMIA WINGI:
Suratul Hijr 27. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
Allah anaendelea kutumia wingi katika uumbaji. Sasa anasema kuwa "TULIWAUMBA MAJINI" Allah anaendelea kutumia wingi katika uumbaji.
KARIBU TUONE,
QURAN 39:2 " KWA YAKINI, SISI TUMEKUTEREMSHIA KITABU HIKI KWA HAKI, BASI MUABUDU MWENYEZI MUNGU KWA KUMFANYA MOLA YEYE TU"
hapo tunaona, hao wanaotumia WINGI (sisi) WAKISEMA, ndio wameteremsha Quran, na wanamwambia mtume amuabudu mwenyezi Mungu tu!
Hebu tujiulize Je! Hawa Wanaosema hivyo ni kina nani hasa?