Ukweli ni kwamba katika damu ya Yesu Kristo kunapatikana zaidi
ya mambo manne nitakayokushirikisha humu; lakini kwa sasa naona nianze na haya
manne:-
1. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kuondoa dhambi. Imeandikwa katika kitabu
cha 1Yohana 1:9 kuwa; “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki
hata ATUONDOLEE dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”.
2. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kupatanisha. Imeandikwa katika kitabu
cha Waefeso 2:13-16 kuwa; “Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa
mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye
amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa
kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili
wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa
mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. AKAWAPATANISHA wote wawili
na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui
kwa huo msalaba”
3. Uzima wa Milele katika Damu ya Yesu Kristo. Imeandikwa katika kitabu cha
Yohana 6:53-54 kuwa; “Basi Yesu akawaambia Amini, amini, nawaambieni, msipoula
mwili wake mwana wa Adamu nakuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye
mwili wangu na kuinywa damu yangu anao UZIMA WA MILELE…..”
4. Uwezo wa Damu ya Yesu Kristo katika kutulinda. Imeandikwa katika kitabu cha
ufunuo wa Yohana 12:11a kuwa; “Nao wakamshinda (shetani) kwa damu ya
mwana-Kondoo….” Mtihani mkubwa sana kwetu sisi wakristo ni kuyaweka katika
matendo yale tunayofahamu katika Biblia. Nakushauri kwa Jina la Yesu Kristo
kuwa uwe mtendaji wa neno, na usiwe msomaji tu. Ni maombi yangu kwa Bwana ya
kuwa Roho wa ufahamu wa Bwana atakuwa juu yako unaposoma na ketenda neno lake.
Imeletwa kwenu na
Max Shimba
No comments:
Post a Comment