Tuesday, May 6, 2014

JE, NI HAKI KWA MKRISTO KUSALI(KUOMBA) JUMAPILI?

JE, KUNA USHAIDI WOWOTE ULE NDANI YA BIBLIA UNAO MRUHUSU MKRISTO KUSALI(KUOMBA) JUMAPILI?

Tafadhali ungama nami katika somo hili fupi ambalo lina leta utata mwingi sana kwa waaminio katika Kristo na hata wale wanao mfuta Allah.
Sasa rejea na soma hii aya hapa chini:
WALIKUTANA SIKU YA KWANZA YA JUMA:
Matendo 20: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Siku ya kwanza ya Wiki ni Jumapili na hii ni siku ambayo walio mwamini Yesu walikusanyika na kuabudu. Huu ni ushaidi wa kuonekana kwa macho ambao Wakristo wanaabudu Jumapili hivi leo na walifanya hivyo katika Karne ya kwanza.
1 Wakorintho Mlango 16 1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo. 2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
Katika Wakorintho hapo juu tunasoma kuwa Watakatifu walikutana siku ya kwanza ya Juma ambayo ni Jumapili.
Ingawa kutokana na Warumi 14:1-12, tumewekwa huru kutokana na laana ya Sheria, hivyo basi, kusali si lazima iwe Jumamosi au Jumapili. Mungu hana utegemezi wa siku tena bali unaweza kusali siku yeyote ile na Mungu akakusikia na si lazima uwe kwenye Jengo ambalo tunaliita "Kanisa".
Biblia inaendelea kusema kuwa, tupo huru katika Kristo Warumi 6:14. Ndio maana tuanenda Kanisani katikati ya wiki na tunasali Mungu.
Zaidi ya hapo, kutokana na kuesabu masaa kwa kutumia kalenda ya Warumi, Siku huwa inaanza saa 6 za usiku, ndio maana Mwaka huwa unaanza Saa hiyohiyo ya 6 usiku. Hivyo basi kutokana na ushaidi wa aya hizi (Luka 11:5; Matendo ya Mitume 16:25; 20:7; 27:27) ni ushaidi tosha kuwa, Wakristo wa Kwanza walisali Jumapili na wali hesabu siku kuanzia saa 6 Usiku.
Katika agano la Kale tunasoma: Nehemia 8: 2 Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.
Hapo tumesoma kuwa Kuhani alisoma Torati meble ya mkusanyiko katika Siku ya Kwanza.
SIKU ZOKE NI SAWA NA UNA HAKI YA KUABUDU:
Sasa soma aya hizi hapa chini kwa ufasaha:
Warumi 14.5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
Nduguzangu, kutokana na Warumi 14, tumewekwa huru kuchagua siku ya kuabudu, na nini tule au tusile, hivyo hivyo ni kuadhimisha kwa Bwana. Hivyo basi, hakuna kosa lolote lile mtu anapo sali Jumamosi au Jumapili au Jumatatu, au siku yeyote ile ya wiki. Mungu wetu yupo kila siku na siku zote alizumba yeye.
WALIKUTANA KILA SIKU HEKALUNI NA KUSALI:
Matendo ya Mitume 2: 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,
Unaona hiyo aya hapo juu inavyo sema? Je, Jumatatu imekosekana kwenye hiyo aya, vipi kuhusu Jumanne? Ndio maana nilisema sisi tumewekwa huru kutokana laana ya sheria na sasa tupo huru kuabudu Mungu siku yeyote ile. Mungu si wa Jumamosi tu au Jumapili tu au Ijumaa tu. Mungu ni wa kila siku.
KWANINI UNAPENDA MAFUNZO AMBAYO NI DHAIFU?:
Wagalatia 4:8 Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si miungu. 9 Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? 10 Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.
Mtume Paulo anatukumbusha kuwa, mafunzo ambao tulikuwa tunayafuata kabla ya kukombolewa na Yesu yalikuwa dhaifu. Sasa tumejazwa na Roho Mtakatifu ambaye ndie Mwalimu wetu Mkuu.Basi tushikamane naye na tujifunze kutoka kwake.
Ni mategemeo yangu kuwa, somo hili litatufungua macho na tunasoma Biblia zaidi na kumwomba Roho wa Mtakatifu atufundishe yote.
Katika huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
1633 Broadway, 30th Floor, New York, NY 10019

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW