Biblia inatuambia, "Kwa maana katika kiyama hawaoi wal hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni"(Mathayo 22:30). Hili lilikuwa ni jibu la Yesu alipokuwa akijibu swali la kuhusu mwanamke ambaye alikuwa ameolewa mara nyingi katika maisha, yeye ataolewa na nani mbinguni (Mathayo 22:23-28)? Ni wazi kwamba, hakutakuwa na kama ndoa mbinguni. Hii haimaanishi kwamba mume na mke hawatambuana mbinguni. Hii pia haina maana kwamba mume na mke hataweza kuwa na uhusiano wa karibu mbinguni. Chenye inatuonyesha ni kuwa mume na mke hawataoana tena mbinguni.
kuna uwezekano mkubwa zaidi, hakutakuwa na ndoa mbinguni kwa sababu hatutajitaji ndoa. Wakati Mungu alianzisha ndoa, alifanya hivyo kutimiza mahitaji fulani. Kwanza, aliona kwamba Adamu alikuwa na haja ya mwaharusi. "Mungu Bwana akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye" (Mwanzo 2:18). Hawa alikuwa suluhizo kwa tatizo la upweke wa Adamu, kama vile haja ya kuwa na "msaidizi," mtu ambaye atakaa pamoja naye kama rafiki na kutembea naye katika maisha. Mbinguni, hata hivyo, hakutakuwa na upweke, wala hitaji lolote la wasaidizi. Tutazungukwa na wingu la umati wa waumini na malaika (Ufunuo 7:9), na mahitaji yetu yote yatatimizwa, ikiwa ni pamoja na haja ya urafiki.
Pili, Mungu aliumba ndoa kama njia ya uzazi na kujaza dunia na binadamu. Mbinguni, hata hivyo, mbinguni haitajazwa na uzazi. Wanaoenda mbinguni hufika huko kwa imani katika Bwana Yesu Kristo; hawataumbwa huko kwa njia ya uzazi. Kwa hiyo, hakuna kusudi kwa ndoa mbinguni kwa vile hakuna uzazi au upweke.
No comments:
Post a Comment