Saturday, January 12, 2019

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA

Image may contain: text
Tangu mapema kabisa Mungu wetu anatufundisha kwamba, mbingu na nchi za sasa zitachakaa na kuharibika, na kama mavazi, Mungu atazibadilisha
Zaburi 102:25 Hapo mwanzo uliutia msingi wa nchi, Na mbingu ni kazi ya mikono yako. 26 Hizi zitaharibika, bali Wewe utadumu Naam, hizi zitachakaa kama nguo; Na kama mavazi utazibadilisha, Nazo zitabadilika.
Nchi ya sasa yaani dunia hii au ulimwengu, umechosha na kuchakaa mno Baaya ya kukaliwa na mamilioni ya wenye dhambi wanaofanya machukizo mbele za Mungu. Dunia hii imechakazwa kwa gharika wakati wa Nuhu na vita vya kila namna mpaka vita ile ya mwisho “GOGU NA MAGOGU”.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwepo na bahari tena.
Watu wengi wako na dhana potovu juu ya mbinguni itakuwa kama nini. Ufunuo mlango wa 21-22 yatupa kiupana picha kamili ya mbingu mpya na nchi mpya. Baada ya matukio ya nyakati za mwisho, mbingu ya sasa na nchi ya sasa zitatolewa na zibadilishwe na mbingu mpya na nchi mpya. Mahali pa kukaa milele pa Wakristo patakuwa katika nchi mpya. Nchi mpya ni “mbinguni” mahali ambapo tutakaa milele yote. Ni katika nchi mpya Yerusalemu mpya, mji mkuu wa mbinguni utakuwa. Utakuwa katika nchi mpya ambapo milango yake na njia zake zitakuwa sha dhahabu
Mbingu- na nchi mpya- ni mahali panapoonekana, ambapo tutaishi na miili ya utukufu (1 Wakorintho 15:35-58). Hoja kwamba mbinguni itakuwa katika “mawingu” ni jambo lisilo la kibibilia. Dhana kuwa tutakuwa “roho zinazo elea mbinguni” pia sio la kibibilia. Mbingu ambayo watakatifu wataiona itakuwa sayari mpya na kamilifu ambapo tutaishi. Nchi mpya haitakuwa na dhambi, uovu, magonjwa, mateso na kifo. Itakuwa sawa na nchi hii ya sasa, au pengine nchi iumbwe upya lakini isiwe na laana yoyote au dhambi.
MBINGU MPYA
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.'' ( Ufunuo 21:1-4 )
Ni muhimu kukumbuka kwamba wazo la kale, “mbinguni” ilimaanisha mawinguni ya juu kabisa ambapo Mungu anakaa. Kwa hivyo wakati Ufunuo 21:1 yazungumzia mbingu mpya, kuna uwezekano kuwa inamaanisha kuwa sayari mpya itaumbwa- nchi mpya, mawingu mapya, na sayari ya juu kabisa mpya. Inaonekana kana kwamba mbingu ya Mungu itaumbwa upya pia, kukipa kila kitu ulimwenguni “mwanzo mpya,” hata kama ni mwili au kiroho. Je! Tutapata ruhusa ya kuingia mbingu mpya milele yote? Labda, lakini tutangoja tuone. Tafadhali wote tuliruhusu neno la Mungu lichonge uelefu wetu wa mbinguni.
Tazama atayafanya yote kuwa mapya ( Isaya 66:22; Isaya 65:17; 2 Petro 3:13; Ufunuo 21:1-7 ). Mbingu hizi na nchi mpya zitakuwa ni nzuri mno, hakuna mfano wake uliowahi kuwako au utakaokuwako. Ufundi wote wa uumbaji wa Mungu utaishia hapa. Hapa ni mahali watakapoishi wateule wake Mungu milele na milele. Wala walio ndani ya Kristo Yesu ni viumbe vipya na hivyo wanastahili kukaa katika MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW