Saturday, June 11, 2022

JE, KUMIMINWA NI KUFIRWA KAMA WANAVYO DAI WAISLAM?


Waislamu wamekuwa ni mahodari sana katika kufanya jitihada za kumkashifu Mtume PAULO, kwa kudai kuwa alikuwa Gay (Shoga) Pale aliposema kuwa alimiminwa, katika maandiko haya yafuatayo:-

Wafilipi 2: 17 Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
18 Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.

2 Timotheo 4:6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

Kitu ambacho kinawafanya Waislamu wanatafsiri vibaya maandiko haya ya Paulo, ni ukosefu wao wa Elimu, maana hata kabla ya wao kuanza KUYAPOTOSHA MAANDIKONHAYO, tayari tulishaarifiwa juu ya upotoshwaji wa maandiko yamuhusuyo PAULO.

2 Petro 3:15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.

Katika nyaraka za Paulo yapo mambo amabayo ni vigumu kuyaelewa, na mambo hayo watu wasio na Elimu huyapotosha kama vile wapotoshavyo na maandiko mengine, na hivi ndivyo wanavyofanya Waislamu kwa kudai Neno kumiminwa lina maana ya Kufirwa, wakati Neno hili halina mana hiyo kabisa.

KUMIMINWA KUNA MAANA GANI?

Unapozungumza habari ya kumiminwa, ina maana ya kuhamishwa sehemu fulani na kwenda sehemu nyingine, mfano: unapoyamimina maziwa, au maji, ina maana unayatoa sehemu moja kuyapeleka sehemu nyingine hii haina maaana mbaya kabisa,

Yeremia 48:11 Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.

Kwa hivyo kumiminwa ni kutoka sehemu kwenda sehemu nyingine, Maana hata Pendo la Mungu lilimiminwa mioyoni mwetu, yaani lilitoka sehemu (kwa Mungu) na kuja kwetu sisi.

Warumi 5:5 na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.

AYUBU KUZALIWA KWAKE ALIKUFAFANISHA NA KUMIMINWA, YAANI KUTOKA KWA BABA KUJA TUMBONI MWA MAMA, BABA, YAANI YEYE AYUBU KAWA MMIMINWA NA MUNGU, YAANI ALITOLEWA SEHEMU MOJA KWENDA SEHEMU NYINGINE. UUMBWAJI WAKE NA MUNGU KATIKA TUMBO LA MAMA YAKE, AMEKUITA NI KUMIMINWA.

Ayubu 10:8 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga; Nawe utageuka na kuniangamiza?
9 Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10 Je! Wewe hukunimimina kama maziwa, Na kunigandisha mfano wa jibini?
11 Umenivika ngozi na nyama, Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.
12 Umenijazi uhai na upendeleo, Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.

Sasa kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kusema kuwa eti Mungu anapomuumba (Anapommimina) mtu anamfira kwa kuwa limetumika neno kumiminwa, hii ni akili ya kidhalili kabisa ambayo hata Hayawani hawawezi kuwa nayo, Maana neno kumiminwa limetumika sana hata wakati wa wana wa Israeli, walimimina mafuta juu ya Kuhani, lakini haimanishi Kuhani huyo aliye miminwa, yani kumiminiwa mafuta alikuwa Shoga.

Walawi 21:10 Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;

DAUDI ALIMSIFIA MASIHI AJAE KWA JINA LA BWANA YA KUWA NEEMA IMEMIMINWA KINYWANI MWAKE

Zaburi 45:1 Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.
2 Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.

Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kusema eti Neema kumiminwa kinywani, kuna maana ya kufirwa, La hasha, NENO KUMIMINWA HALINA MAANA YA USHOGA kabisa, ni tafsiri ambovu tu za wanadamu ambao hawapendi kukaa chini na kujifunza wakapata kuelewa kama alivyo tahadharisha Mtume Petro katika Andiko ambalo nimelinukuu yaani 2 Petro 3:15-18, Narudia tena neno kumiminwa halina maana mbaya kama wengi wanavyo dhani.

Kutoka 30:32 Hayatamiminwa katika kiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine mfano wa haya kama yalivyoungwa kwa viungo vyake; ni matakatifu, na kwenu ninyi yatakuwa matakatifu.

PAULO ALIPOSEMA KUWAN YEYE ANAMIMINWA, ALIKUWA ANAMAANISHA JUU YA KIFO CHAKE, YAANI DAMU YAKE ITAMWAGIKA, ITAMIMINIKA, YAANI WATAMMIMINA.

Wafilipi 2: 17 Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote.
18 Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami.

Pulo hakukiogopa kifo kabisa, ndiyo maana alisema hata akimiminwa yeye anafurahi, Maana alikichukulia kifo chake cha kuchinjwa na damu yake kumiminika, ni Faida,

Wafilipi 1:21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.

PAULO alifurahia kumiminwa kwake kwa kuwa kazi alisha imaliza Imani ameilinda, hana shaka tena na safari yake amekwisha hakikishiwa, ya kuwa taji lipo tayari kwa ajili yake.

2 Timotheo 4:6 Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
8 baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

TAFSIRI MBOVU ZA KUPINDUA HAZINA MAANA KABISA, MAANA SISI WAKRISTO TUNAWEZA KUWEKA TAFSIRI NYINGINE JUU YA MUHAMMAD, NA KUIFANANISHA NA USHOGA, KWENYE HABARI HIII

”Sababu ya kusilimu Hamza ni kuwa alimuona Aboujahal akimwingilia Mtume” (Kitabu cha Historia ya Mtume Muhammd, uk. 19)

Hapo tunaambiwa kuwa ABOUJAHAL alimwingilia mtume, na neno kuingilia kwa wengi lina fahamika ni tendo la kufanya mapenzi, kama ambavyo Ibrahimu alimwingilia Hajiri na kumpa mimba.

Mwanzo 16:4 Basi akamwingilia Hajiri, naye akapata mimba. Naye alipoona ya kwamba amepata mimba, bibi yake alikuwa duni machoni pake.
5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.

JE! SISI NASI WAKRISTO TUKIFASIRI NENO HILO KAMA WAISLAMU WANAVYOFASIRI NENO KUMIMINWA KUWA NI KUFIRWA, NASI TUKASEMA MUHAMMAD ALIFIRWA NA ABOUJAHAL, MAANA ALIINGILIWA, JE! ITAKUWA NI SAHIHI TAFSIRI HIYO?

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW