Wednesday, December 31, 2014

FREEMASONS NA ILLUMINANT


images


Hiki ni kitabu chenye siri nzito za Freemasons na Illuminanti.
Utangulizi.
Ni mpango wa Shetani kuangamiza sheria ya Mungu tangu mwanzo. Shetani amekuwa
akifanya vita dhidi ya amri 10 za Mungu ambazo ndicho kipimo pekee cha utii kwa
Mungu. Katika vita hiyo, Shetani amekuwa akitumia mawakala wa aina mbalimbali kiasi
cha kufanikiwa kuwadanganya mamilioni ya watu duniani nao wakaiacha sheria ya
Mungu na kufuata mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Shetani ameanzisha kanisa
lake na kuweka amri 11 kinyume cha amri 10 za Mungu. Mbeleni tutaona jinsi waumini
wa Shetani kwa dini la Freemasons na Illuminati wanavyotumia namba na ishara katika
kazi zao duniani kiasi cha kuwapofusha watu huku wakidhani kwamba wanamuabudu
Mungu wa mbinguni kumbe wanamuabudu Shetani mwenyewe.
Tunaishi katika nyakati za hatari. Majanga yameenea kila mahali. Machafuko ya kila
aina yameenea ulimwenguni kote. Ubakaji, matetemeko ya ardhi, moto usiowezekana
kuzimwa, mafuriko wakati wa kiangazi, migomo ya wafanyakazi, maporomoko ya ardhi,
kuyumba kwa uchumi, milipuko ya Volkano na mengine mengi yanazidi kutokea kila
kukicha, tena katika mataifa makubwa yaliyoendelea na hata kuitwa ‘mataifa ya
ulimwengu wa kwanza’.
Kuongezeka kwa machafuko haya ya asili na kisiasa yanawafanya wanadamu wawe na
hofu kuhusu maisha yao ya baadae. Inaonekana kana kwamba tupo katika ncha ya
mwisho mbele yetu kukiwa na shimo kubwa tayari kuangukia shimoni. Yote haya ni
dalili za mwisho wa wakati kwa wale walio na masikio ya kusikia na macho ya kuona,
kwamba ulimwengu hautaendelea kwa muda mrefu ukiwa katika hali hii. Mioyo ya watu
inajawa na hofu kwa haya yanayotokea (Luka 21:26). Na watu wanajiuliza maswali:
“kwa nini haya yanatokea?” “Je, Shetani ametawala kikamilifu?”
Hapana, Mungu hajawaacha watu wake waaminifu, lakini maswali hayo yote
yanaonyesha kwamba kuna kitu nyuma ya matukio haya kuliko wengi wanavyoweza
kuelewa.
Kuna vita kali inayoendelea kati ya nguvu za nuru na nguvu za giza —-vita kali kati
ya Yesu na Shetani—-na matokeo yake ndiyo yanayoonekana kwa wanadamu ikiwa ni
matukio hayo. Hata hivyo Mungu wa mbinguni amewaambia watu wake kwamba “muda
ubakio si mwingi.” Na anaendelea kusema “Tukijua ya kwamba saa ya kuamka katika
usingizi imewadia, kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza
kuamini. Usiku umeenda sana, mchana umekaribia, basi, na tuyavue matendo ya giza, na
kuzivaa silaha za nuru.” 1 Wakor 7:29; Warumi 13:11-13.
Paulo anatueleza kwamba “Tuvae silaha za Mungu,” ndipo tutakapoweza kusimama
dhidi ya madanganyo ya Mwovu (Waefeso 6:11).
Nilipokuwa nasoma unabii wa Danieli, Ezekieli, Ufunuo nk sikujua jinsi unabii huu
utakavyotimia na kwamba kumbe kundi linalofanya kazi zake kwa siri kubwa ndilo
linalotimiza unabii huu kwa kiasi kikubwa sana.
Wengi hawana habari na madanganyo haya ya Shetani na Mungu ametuagiza
kwamba tusiwe wajinga kiasi cha kutotambua mbinu za Shetani na hivyo “Shetani
akapata kutushinda” 2 Wakorintho 2:11.
Mafanikio makubwa ya Shetani katika udanganyifu yamepatikana kwa njia ya
kuwafanya watu wawe wajinga wa mbinu anazotumia katika kazi yake. Wakati
tunapokuwa wajinga au kuchanganyikiwa, ndipo Shetani anapotushinda na amefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kuwashinda wanaume na wanawake wengi ulimwenguni. Hivyo
hatupaswi kulala usingizi na kushindwa kutambua kile kinachoendelea katika ulimwengu
wa giza. Kwa nini? Kwasababu “Mshitaki wenu, kama simba angurumaye, huzunguka
zunguka, akitafuta mtu ammeze.” 1 Petro 5:8; Ufunuo 12:12.
Mwovu anajua kwamba muda wake ni mchache na hivyo halali akiwa anafanya kazi
ya kuuongoza ulimwengu kuelekea katika uangamivu wa mwisho. Watu wa Mungu
karibu watajaribiwa. Wale wasioshinda kwa damu ya mwana kondoo watapata hofu ya
majaribu na hivyo kushindwa.
Lakini ni kwa njia gani Shetani anafanya kazi yake? Anafanya kazi kupitia mawakala
gani? Jibu linatolewa na Mungu. kwa upendo mwingi Mungu anatufunulia wahusika
wakuu katika mchakato huu wa vita ya mwisho kati ya Kristo na Shetani. Wahusika
hawa ndio wanaostahili kulaumiwa kutokana na matokeo tunayoyaona katika ulimwengu
wote kama yalivyotajwa hapo juu.
Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anatufunuliwa wahusika au mawakala watano
ambao ni:
1—Mnyama mwekundu wa Ufunuo 12—Shetani mwenyewe
2—Mnyama mfano wa chui wa Ufunuo 13—Rumi ya kidini
3—Mnyama mfano wa mwana kondoo wa Ufunuo 13:11—Taifa la Marekani
4—Sanamu ya Mnyama Ufunuo 13—Umoja wa makanisa —WCC
5—Mnyama wa rangi nyekundu sana na mwanamke wa Ufunuo 17—-Illuminati,
freemason wakiwa wameungana na kanisa la Rumi..

Wengi hawakuwa wanatofautisha wanyama hao lakini utakapojifunza kwa undani
zaidi utagundua kwamba mnyama wa Ufunuo 17 ambaye ni mwekundu sana mwenye
pembe kumi na vichwa saba ambaye amembeba mwanamke inamaanisha muungano wa
Illuminati wakiwa wameunda majimbo kumi katika dunia nzima pamoja na kanisa la
Rumi likiwa na watawala saba tangu kuanza kazi yake baada ya kupata jeraha la mauti.
Biblia inapotumia neno mwanamke kiunabii humaanisha kanisa (Ufunuo 21:2) na neno
‘kichwa’ humaanisha kiongozi wa kanisa ambapo kwa kanisa la Mungu, kichwa ni Kristo
lakini kwa kanisa la uongo, kichwa ni mwanadamu aliyechukua nafasi ya Yesu duniani,
(Wakolosai 1:18; 2Wathesalonike 2:4). Biblia kamwe haijawahi kutumia neno ‘kichwa’
kumaanisha kiongozi wa kiserikali ila hutumia neno ‘watawala au wafalme’. Ndio maana
vichwa saba inamaanisha vipindi saba vya viongozi saba wa kanisa.
Ufunuo 17:8 anasema kwamba mnyama huyo yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na
katika Ufunuo 9:11 tunasoma kwamba “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa
kuzimu…”. Mafungu yote hayo yanamaanisha umizimu (spiritualism) ambayo ni imani
ya Illuminati. Imani hii inamfanya muumini aamini kwamba hakuna kifo na mtu
anapokufa anakuwa amebadilisha mahali kwa kuhama duniani na kwenda mahali pengine
akiendelea kuishi na kwamba hiyo ndiyo mbingu yake maana hawaamini kama kuna
ufufuo. Chanzo cha fundisho hili ni Shetani alipomfundisha Hawa kwamba “Hakika
hamtakufa” Mwanzo 3:4. Hivyo tutajifunza na kuona ukweli huu wa Illuminati kwa
kujiunga na kanisa ili kutimiza malengo yao.
Je, kuna watu au kitu kinachoitwa Illuminati? Inaweza kuwa katika kizazi chetu hiki?
Baadhi wamekuwa wakidhihaki kuhusu swala zima la Illuminati. Hata hivyo katika
kitabu hiki unaweza kupata ufahamu wa kina kuhusu Illuminati na Freemason ndani ya
jamii tunayoishi. Je, maneno kama Illuminati au Freemason ni mapya kwako? Hilo
linawezekana maana maneno hayo hayafahamiki kwa watu wengi, hata kwa wasomi
wakubwa wa elimu ya duniani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wahusika wa maneno
hayo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa siri kubwa kiasi cha kuwafanya watu
mamilioni wasielewe kinachoendelea na hivyo maneno hayo kuendelea kuwa siri kubwa.
“The great strength of our order lies in its concealment,” yaani “nguvu kubwa ya
utaratibu wetu iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa” ni maneno ya
Adam Weishaupt, mwanzilishi wa Illuminati mwaka 1776. Akaendelea kusema, “Let it
never appear in any place in its own name, but always covered by another name and
another occupation” yaani “Hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima
ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine.” (Kutoka kwa Robin’s Proofs of a
Conspiracy, p. 195.)
Kazi hizi za Illuminati zimekuwa zikifanyika duniani kote kwa karne nyingi kiasi
kwamba watu wengi hawajui hata kuwepo kwa watu kama hao. Njama hizi za siri
zinaweza kuwa na msingi wake tangu wakati wa Nimrodi, mtu yule muovu aliyeanza
kazi zake za uasi huko Mesopotamia. Wakati kila mwalimu wa dini anajua kuhusu mnara
wa Babeli, ni wachache wanaojua kwamba kanuni za mchakato huo wa zamani wa
kujenga mnara wa Babeli ndizo zinazofanya kazi hadi leo katika nyanja za Siasa na Dini.
Kitabu hiki kiitwacho ‘Illuminati na Freemason katika mnyama wa namba 666’,
kitakupa ukweli wa leo na wa ajabu na ukiondoa Biblia, ni vitabu vichache vinavyoweza
kukupatia habari za uhakika na muhimu kwa ajili ya wokovu wa maisha yako. Sio lengo
la mwandishi wa kitabu hiki kushabikia dini fulani au kuanzisha kanisa na kupata
waumini kama wafanyavyo walio wengi, bali lengo ni kutoa bila woga wala upendeleo
ukweli halisi kama ulivyotolewa na Mungu mwenyewe. Hivyo kama utakutana na habari
zinazopingana na imani yako ni vema basi kutulia na usikasirike maana hasira ya
mwanadamu haitendi haki ya Mungu (Yakobo 1:20), ni vema kumuuliza Mungu kwa
unyenyekevu ili akuhakikishie kama habari hizi zinatoka kwake na uwe tayari kupokea
lolote atakalokujibu. Mungu ni mwaminifu na hakika atakujibu kama utamwendea kwa
nia ya kutaka kufuata ukweli wake. Lengo la mwandishi wa kitabu hiki ni kuwapeleka
wasomaji kwa Mungu mwenyewe na sio kuwapeleka kwa mwandishi. Kabla ya kuanza
kujifunza kwa undani, hebu tuone vyanzo vya habari hizi nzito. Ninatoa shukrani kubwa
kwa ajili ya vitabu hata vile ambavyo hatuvikubali, maana vinatuonyesha mawazo ya
waandishi wengine. Vipo vitabu vingi ambavyo vimetumika katika kuandaa kitabu hiki,
vitabu hivyo baadhi ni pamoja na “The Illuminati 666” cha ndugu Roy Allan Anderson;
“The broken Cross” cha Padre Peirs Compton wa kanisa katoliki; “The Two
Babylonians” cha ndugu Alexander Hislop, “Freemasonry encyclopedia”, “Morals and
Dogma” cha Dr. Albert Pike; “To be God of One World” cha Robert Sessler; “The Keys
of this Blood” cha Padre Malachi Martin wa kanisa katoliki, “The Secrets of The
Illuminati” cha ndugu Mac Marquis aliyewahi kuwa freemason na akajitoa, mtandao wa
Wikipedia na mitandao mingine mingi ikiwa ni pamoja na vyanzo vya kuaminika kutoka
kwa Illuminati na Freemason wenyewe; pamoja na vitabu vingine vingi utakavyoviona
kama rejea ya kila nukuu utakayoisoma. Hata hivyo kitabu ambacho tumekitegemea sana
katika kuandika kitabu hiki, ni kitabu cha vitabu vyote, kitabu ambacho ni zaidi ya vitabu
vyote, kitabu ambacho ni tofauti na vitabu vingine vyote duniani kilichoandikwa na zaidi
ya watu 30 walioishi wakati na mahali tofauti tena kwa tofauti ya maelfu ya miaka, wengi
wao bila kukutana wala kufahamiana huku muasisi akiwa ni Mungu Mwenyewe, kitabu
hicho ni “Biblia Takatifu” ambayo pamoja na kuandikwa na watu zaidi ya 30,
hawakutofautina hata katika neno moja. Wakati tumetumia nukuu kutoka katika vitabu
vingine, lakini bado tumechukulia kwamba neno la Mungu ndani ya Biblia ndilo lenye
nuru na ukweli wa mwisho na hivyo limetumika hata kupima maandishi ya vitabu
vingine. Kwa muda wa miaka zaidi ya kumi na mbili sasa tangu nianze kufanya
uchunguzi kuhusu vyama vya siri, kamwe sijawahi kufundisha bila kupima mafundisho
ya vyama hivi kwa kutumia Biblia. Kila mipango na matukio yanayofanywa na Illuminati
nimekuwa nikiyapima kwa Biblia katika unabii ili niwe na uhakika kama mipango yao
iko sawa na unabii alioutoa Mungu kupitia Biblia.
Tunaweza kusoma katika Ufunuo 17:17 nabii Yohana anasema: “Maana Mungu
ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja na kumpa yule
mnyama ufalme wao, hata maneno ya Mungu yatimie” ikiwa na maana kwamba Mungu
ametia shauri lake mioyoni mwa Illuminati ili wapange mipango yao ya kumpa ufalme
wao mnyama wa namba 666 kusudi maneno ya Mungu—yaani unabii wa Mungu utimie.
Hapa tunaweza kutambua kwamba mipango ya Illuminati inakwenda sawa na unabii wa
Mungu. Kitabu hiki kitakupa habari za uhakika jinsi mipango ya Illuminati ilivyowekwa
kwa ajili ya kumpa utawala wao na nguvu zao mnyama wa namba 666 ili apate kutawala
dunia kama Mungu alivyotufunulia katika unabii wa Biblia. Mipango hiyo ni ya siri
ikiwa ni pamoja na kuweka ratiba ya vita kuu tatu (3) za dunia ambapo tayari vita kuu
mbili za dunia zimeshatekelezwa wakati vita kuu ya tatu ya dunia itatekelezwa muda si
mrefu.
Katika agano la kale na agano jipya ndani ya Biblia ndipo tumeweza kupata mwanga
wa kuelezea siri hizi za Illuminati na Freemason, ambalo ndilo kusudi la kitabu hiki ili
watu wajue ukweli na kisha wawe huru kutoka utumwani mwa shetani. Mtume Paulo
katika barua zake kwa kanisa ameelezea kuhusu “Siri ya Mungu” ambayo katika neno la
Mungu ni “Mungu kufunuliwa katika mwili,” na “Kristo ndani yetu, tumaini la utukufu
wetu” (1Timotheo 3:16; Wakolosai 1:26,27). Katika barua yake ya pili kwa
Wathesalonike anaelezea kuhusu “Siri ya kuasi” ambayo anaiita “Mtu wa dhambi,”
maana yake mnyama wa namba 666, anayejifanya kuwa ni Mungu akitaka aabudiwe
kama Mungu (2Wathesalonike 2:7; 3 na 4). Mtume anasema kwamba siri hiyo ilikuwa
inatenda kazi tangu wakati wake lakini akaelezea kwamba siri hiyo itafanya kazi kubwa
zaidi wakati wa mwisho kwa kutumia ishara na maajabu mengi. Hivyo tunakuta aina
mbili za siri, yaani “Siri ya Mungu” na Siri ya kuasi”. Siri ya kuasi inatokana na uasi wa
Shetani na kisha kuendelea kufanya kazi zake kwa siri kubwa ili kuwafanya watu
wasielewe kinachoendelea katika ulimwengu wa siasa, uchumi, elimu na dini na hivyo
watu wengi wanakuwa watumwa wa freemason bila wao kujua kama ni watumwa.
Kwa nini nimehusisha mnyama wa namba 666, Illuminati, freemason na maswala ya
ibada na imani? Ukweli ni kwamba unapoongelea Illuminati, Freemason na mnyama wa
namba 666 unaongelea kuhusu mambo ya imani, ibada na utawala kama anavyosema
mmoja wa Illuminati mwenye digrii 33 Bw. Albert Pike, namnukuu: “Every Masonic
Lodge is a temple of religion, and its teachings are instruction in religion” (Albert Pike,
Morals and Dogma, P. 213.) Kwamba “kila Loji (Jumba au kituo) ya Freemason ni
hekalu la mambo ya dini, na mafundisho yake ni maagizo katika dini.” Bw. Albert
anaendelea kusema kwamba: “Freemasonry is a search for Light. That search leads us
directly back, as you see, to the Kabalah.” [Albert Pike, Morals and Dogma, p. 741]
Kwamba “Freemason ni kutafuta nuru. Na kutafuta huko kunatufanya, kama unavyoona,
tujielekeze Kabalah.” Kama Freemason wana kazi ya kutafuta nuru, ambayo kwa kweli
siyo nuru ya kweli, basi watu wanaotafuta wokovu wanapaswa kutafuta nuru ya kweli.
Yesu alisema, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” Mathayo 5:14 Hivyo tutakuwa
tukichunguza mambo ya imani, ibada na utawala ambavyo ni vitu muhimu zaidi kuliko
kitu kingine katika maisha ya mwanadamu maana ndivyo vitakavyotoa taswira ya hatima
ya kila mmoja wetu, ama ni uzima wa milele au kupotea milele.
Mibaraka ya kujifunza neno la Mungu ni kwamba unapoona dalili fulani zikitokea,
hazikustui wala kukutia hofu. Dalili hizo badala yake zinakufanya usonge mbele katika
kufanya kile ambacho Mungu amekiagiza ili kushiriki na wengine mibaraka hiyo ya
ukweli kadri wengi wanavyoweza kuwa na masikio na kusikia. Lakini pia kushiriki huku
kwa mibaraka na wengine si kwa lengo la kuwafanya wawe na hofu, bali kuwafanya
wajiandae kutokana na kile kitakachoupata ulimwengu kadri tunavyoishi. Kwa kufanya
hivyo mara kwa mara huwafanya wasikilizaji na wasomaji watafute kutembea na Mungu
kwa ukaribu zaidi ili kwamba wawe tayari kwa lolote atakalowaambia kulifanya katika
siku hizi za mwisho. “Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo
yatakayotendeka; wala hakuna jambo jipya chini ya jua.” Mhubiri 1:9.
Kujifunza unabii kunaweza kuwa ni jambo muhimu na zuri ambalo kamwe haliwezi
kushindwa katika kuamsha roho ya kumtafuta Mungu. Kila siku mtu anapojifunza ukweli
wa leo kutoka kwa Mungu, ndipo anapoanza kuona zaidi na zaidi unabii unavyotimia
mbele yake. Wakati watu wengi wanashindwa kuona hatari inayowakabili, msomaji wa
neno la Mungu anapata mbaraka wa kujua maonyo na hivyo kuweza kujiandaa yeye na
nyumba yake kwa ajili ya kurudi kwa Yesu mara ya pili. Na hii ndio sababu kwamba
Yesu hatakuja kama mwivi kwa yeye aaminiye, maana anaweza kujua unabii na
kujiweka tayari kwa ujio wa Yesu. Ndio maana Paulo anasema, “Bali ninyi ndugu,
hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.” 1 Wathesalonike 5:4.
Mara nyingi wahubiri huhubiri kuhusu mafungu mawili yanayofuatia katika nukuu
hiyo ya Paulo na kisha wanasimamia hapo tu. sababu ni kwamba, kama watalihubiri
fungu hilo hapo juu, kondoo wao watahitaji kufahamu ni jinsi gani Wakristo baadhi
watakutwa hawako tayari au wako gizani wakati Yesu anarudi. Lakini mhubiri huyo kwa
vile hajifunzi unabii na wala hajui unabii vya kutosha ili aweze kuwasaidia wasikilizaji
wake, hivyo anakwepa kusoma fungu hilo ili kuepuka maswali atakayoulizwa kutokana
na fungu hilo.
Kuna matukio mengi ya kiunabii ambayo yameshatimia katika siku zetu hizi kiasi
kwamba sina nafasi ya kuyaelezea maana kila mtu anaona hali ilivyo. Moja ya unabii
muhimu sana katika siku hizi za mwisho ni ule wa mnyama wa namba mia sita sitini na
sita. Baadhi ya matukio ya kiunabii hayaonekani kuwa ni unabii na watu wengi
wamechukulia kuwa ni hali ya kawaida ya asili kutokea. Wakati tunaamini kwamba Yesu
aliahidi kwamba atarudi tena kuwachukua walio wake, baadhi wameifanya hiyo ahadi
kuwa mzaha na hilo lilielezwa na mtume Petro, akasema,“…..Mkijua kwanza neno hili ya
kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao
tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana tangu
hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa
kuumbwa.” “Watayakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe
watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao
watajiepusha wasisikie yaliyo ya kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” 2 Petro 3:3,4; 2
Timotheo 4:3,4. Hili nalo ni tukio la kiunabii maana limetimia. Utakuta ukimwambia mtu
akusubiri utarudi muda si mrefu, anakuambia “Umekuwa Yesu?” Akimaanisha kwamba
Yesu alisema atarudi lakini hajarudi na hatarudi hivi karibuni. Bahati mbaya wengi wa
watu hawa, wenye dhihaka, ni wale wanaodai kuamini mamlaka kuu ya Biblia.
Wanaamini kwamba Yesu atarudi lakini sio sasa ila ni miaka mamia ijayo. Sasa hapa
Mungu anatupatia unabii wa siku za mwisho kuhusu mnyama wa ajabu ambaye
anatambulika kwa hesabu ya kibinadamu. Wakati Mungu anatumia wanadamu kama
wakala wake katika kupeleka nuru ulimwenguni, Shetani naye anatumia wanadamu kama
wakala wake wa kueneza dini ya Shetani. Mungu anawaita mawakala wake kuwa ni
Wachungaji, Wainjilisti, Mitume, Manabii na watu mmoja mmoja kama washiriki wa
upande wa Mungu. Shetani amekuwa akiwaita mawakala wake kuwa ni Illuminati na
Freemason ambao hata hivyo hujigeuza na kujiita kama wachungaji, Wainjilisti, Mitume
Manabii kumbe kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. Nitapaje kuwatambua Freemason na
Illuminati hata kama wanajiita majina ya wakala wa Mungu? kitabu hiki kitatoa majibu
mengi ya maswali yako. Napenda pia kuomba radhi mapema kwa kutokutafsiri baadhi ya
maneno yaliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza; hii ni kutokana na umuhimu wa maneno
hayo kuwa katika lugha iliyotumika kuyaandika na pia kubana nafasi ili kitabu kisiwe
kikubwa. Naamini kwa wale wasiojua lugha ya Kingereza watapata watu wa kuwasaidia
kujua maana ya maandishi hayo kwa kuwa ni ya muhimu pia.
Baada ya kujifunza yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki utaweza kutambua yafuatayo:
1. Malengo na matukio ya Mpango Mpya wa Ulimwengu—-New World Order.
2. Madhara yatokanayo na mpango huo kwa kila mtu duniani.
3. Jinsi mpango huo unavyoathiri hata sasa kila mtu, kila familia na kila dini hata
kabla ya hitimisho la mpango huo.
Ukiwa umeshapata ujuzi na ukweli huu utaweza kujua jinsi ya:
1. Kujilinda wewe mwenyewe dhidi ya mpango huu, kuwalinda watoto wako,
kuilinda familia yako na wote uwapendao.
2. Kuishi maisha ya Kikristo huku ukiwa ni mshindi ndani ya ulimwengu huu wa
giza kuu la kiroho kwa sababu utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru.
Tutaanza kuona katika sura ya kwanza jinsi Shetani anavyofanya kazi kwa siri
kubwa chini ya utambulisho wa namba 666 na katika sura zitakazofuatia za kitabu
hiki tutaona msingi wa uasi mkuu na matokeo yake, tutaona pia baadhi ya matukio
ndani ya jamaii, kiuchumi, kiutamaduni na kidini yaliyo na muhuri wa Illuminati, na
hatimaye tutapata wito kutoka mbinguni ili kama tutaitikia wito huo tuweze kurejea
katika kanisa la mitume kama lilivyokuwa kabla ya ukengeufu kisha Yesu
atakaporudi hivi punde, atukute tuko tayari kumlaki mawinguni.
Kwa nini ni muhimu kumjua Mnyama wa namba
666?
Umoja wa mataifa na namba 666
Katika picha hapo juu unaweza kuona umuhimu wa kujua asili ya namba 666 na kwa nini
namba hiyo inatumiwa na viongozi wakuu wa umoja wa mataifa. Kwa kifupi kwenye
picha hiyo wapo watu 6 wakiongoza mkutano wa umoja wa mataifa na nyuma yao kuna
kitambaa kilichoandikwa ‘United Nations 666’ kumaanisha kwamba umoja wa mataifa
unaandaa njia ya utawala wa mnyama wa namba 666.
Je, asili ya namba 666 ni nini? Namba 666 inatoka wapi? Wengi wanasoma Biblia au
kusikia kutoka kwenye Biblia watu wakitaja namba 666 lakini ni wachache sana
wanafahamu kwamba namba 666 ilitoka wapi au kwa nini kitabu cha Ufunuo
kinazungumzia kuhusu namba hiyo na kwamba iko kinyume na Mungu. Lakini pia nini
maana ya namba 666? Watu wengi wanafikiri kwamba namba hiyo ni ya shetani, Je ni
kweli? Hebu tuangalie kwa ufupi historia ya namba hii kwamba ilitoka wapi.
Namba 666 inatokana na ibada zilizokuwa zikifanywa na watu wa Babeli wakati wa
kipindi cha nabii Ibrahimu na nabii Danieli. Babeli ni mji na mnara uliojengwa na
Nimrodi mara baada ya gharika akiwa na makusudi makubwa mawili. Kusudi la kwanza
ilikuwa ni kuwalinda watu wa Babeli na gharika kwa kutumia mnara uliokusudiwa kufika
mbinguni kwenye miungu wa angani. Kusudi la pili lilikuwa ni kuwakusanya watu wote
wakae mahali pamoja na kuwa na serikali na dini moja kinyume na mpango wa Mungu
wa kuijaza nchi. Mungu aliingilia kati na kukwamisha ujenzi wa mnara wa Babeli ingawa
Nimrodi alifanikiwa kufika mbinguni kimawazo na kupata miungu 36 ambazo ni sayari
na nyota. Makusudi hayo mawili yameendelea kufanya kazi hadi leo na hivi karibuni
ulimwengu wote utashuhudia serikali na dini moja ikimuabudu mungu jua ambaye
alikuwa ni mungu baba wa Wababeli. Watu wa Babeli waliabudu miungu iliyotokana na
utafiti wa nyota—yaani unajimu (astrology). Hivyo watu wa Babeli wakawa na miungu
ambayo ni jua, mwezi, sayari zinazoonekana pamoja na nyota walizozigundua wakati wa
utafiti wa nyota. Watu wa Babeli ndio chimbuko la mwanzo wa unajimu wa nyota
ambapo hata leo tunaona wanajimu wakitabiri kwa kutumia nyota. Wababeli walitumia
hesabu pia katika shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na ibada zao.
Kulikuwa na jumla ya miungu 36 na mungu aliyekuwa mkuu alikuwa ni mungu jua
kwa sababu alichukuliwa kuwa ndiye baba wa mimgu wote. Wapagani wa Babeli
walikuwa wakiwaabudu miungu hao kwa sababu mbalimbali kama vile kupiga ramuli,
kuomba kinga na hata kutoa utabiri wa wakati ujao kwa sababu waliamini kwamba wote
walikuwa ni waovu hivyo waliwaogopa miungu wao.
Watu wa Babeli waliamini kwamba namba zina nguvu kwa miungu waliokuwa
wanaabudiwa. Kila mungu kati ya miungu 36 alipewa namba yake iliyotumika
kumuwalisha mungu na mahali pake (Rejea Murl Vance, Trail of the Serpent, uk. 26,
27, 72). Namba aliyopewa mungu iliwakilisha nguvu aliyonayo mungu huyo. Kwa hiyo
namba husika kwa mungu iliwakilisha ukuu wake ikimaanisha kwamba mungu
aliyepewa namba za awali alikuwa na nguvu kubwa kuliko aliyepewa namba za mbele.
Kwa nini kulikuwa na miungu 36? Je, namba 36 ilitokana na nini? Wababeli walipata
idadi ya miungu wao kuwa 36 kwa sababu kila mungu alitakiwa kuheshimiwa au
kutawala kwa mzunguko wa nyuzi 10 au digrii 10 kwa mwaka na kwa vile mwaka una
siku 360 waligawa kwa 10 na kisha ikawa sababu ya kwanza kupata idadi ya miungu wao
36. Lakini pia wanajimu au watafiti wa sayari na nyota waligundua jumla ya sayari na
nyota 36 na kwa vile walikuwa wakiziabudu wakazifanya kuwa miungu wao. Ni
kutokana na miungu hao 36 Wababeli walifanya hesabu na kupata namba 666
ikimaanisha mamlaka, nguvu na ukuu wa miungu wote 36.
Watu wa Babeli walihesabu miungu wao kuanzia namba 1 hadi 36 na kisha
kujumlisha. Mungu wa kwanza alipewa namba 1 na mungu wa pili alipewa namba 2 na
kuendelea. Mungu wa namba 1 alikuwa ni mungu jua na mungu namba 2 alikuwa ni
mungu mwezi. Miungu kuanzia namba 3 hadi 36 walikuwa ni watoto wa mungu jua
ambao walikuwa ni sayari na nyota zilizogunduliwa na wanajimu wa Babeli. Ndipo
wakajumlisha namba 1 hadi 36 na kupata namba 666. tazama hesabu hii kuhusu asili ya
namba 666:
1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7 + 8 + 9 + 10 + 11 + 1
2
+ 13 + 14 + 15 + 16 + 17 + 18 + 19 + 20 + 21 + 2
2
+ 23 + 24 + 25 + 26 + 27 + 28 + 29 + 30 + 31 + 3
2
+ 33 + 34 + 35 + 36 = 666
Umuhimu wa namba 36 kwa Wababeli ulisababishwa na mgawanyo wa ishara 12
zinazoitwa ‘12 Zodiac signs’ sawa na miezi 12 kwa mwaka na ishara hizo zilitokana na
unajimu wa nyota na waligawa namba 36 katika mafungu matatu ya 12 Zodiac signs—12
x 3 = 36. Wababeli waliamini kwamba mtu anapokufa anakwenda kwa mungu wake.
Miungu hawa 36 waliitwa kwa jina la ‘Decans’ kwa pamoja kwa sababu kila mmoja
alitakiwa kufanya kazi kwa digrii 10 katika mzunguko wa Zodiac kwa siku 10 katika siku
360 za mwaka. Kila mtu alipewa kundi lake katika ishara 12 kutegemeana na mwezi
aliozaliwa na huo ukawa mwanzo wa utabiri wa maisha ya mtu kwa kutumia nyota
zilizokuwa katika mafungu matatu (3) ya miezi 12 katika jumla ya miungu 36.
Sayari 7 au joka lenye vichwa 7 ndilo lililotawala miungu hawa wote 36 walioitwa
Decans na kati ya miungu hao aliyekuwa mtawala wa wote alikuwa ni mungu jua. Jumla
ya namba 1 hadi 36 sawa na 666 iliitwa “The Grand Number of the Sun” yaani jumla kuu
ya hesabu ya jua.
Kila mungu aliwakilishwa kwa alama na wakati wa ibada kila muumini alitakiwa
kuvaa hirizi inayomuwakilisha mungu wake kati ya miungu 36. Hivyo kulikuwa na aina
36 za hirizi zilizowakilisha miungu 36. Hirizi hizo zilitengenezwa kwa mfumo wa hesabu uitwao
‘6×6 Matrix’ na mtu ambaye alikataa kuvaa hirizi iliaminiwa kuwa angepata majanga ya ugonjwa, njaa,
mateso na kisha kifo.
Wapagani wa Babeli walitakiwa kuvaa hirizi yenye namba na alama ya mungu
mhusika. Wakristo wachukua desturi hii kwa kuendelea kuvaa msalaba shingoni
ukiwakilisha alama ya mungu Ishtar. Unaweza kuangalia picha hii mwanamke akiwa amevaa sura
ya simba kichwani kumaanisha utawala wa Babeli uliowakilishwa na simba (Danieli 7:4) na amevaa hirizi
shingoni yenye namba tofauti pamoja na mduara wenye jicho kifuani mwake uliowakilisha mungu jua
aonaye kila mahali.
Hirizi na alama ya mungu mhusika
Hirizi hizo zilitengenezwa kwa mfumo wa hesabu uitwao ‘6×6 Matrix’ (rejea jedwali la hesabu za Illuminati)
na mtu ambaye alikataa kuvaa hirizi na alama ya mungu wake iliaminiwa kuwa angepata majanga ya
ugonjwa, njaa, mateso na kisha kifo. Je, mtu alipata kujua vipi kwamba mungu fulani ni mungu wake? Watu
wote waliwekwa kwenye mafungu matatu (3) ya ’12 Zodiac Signs’ kufuata mwezi aliozaliwa mtu husika na
hivyo kulikuwa na makundi matatu (3) yaani kundi la kwanza watu wote waliozaliwa mwezi wa kwanza hadi
wa nne, kundi la pili waliozaliwa mwezi wa tano hadi wa nane, la tatu mwezi wa tisa hadi wa kumi na mbili.
Kila kundi likiwa na miezi mitatu lilileta namba 6, yaani 1+2+3 =6 na wakaweka makundi yote matatu pamoja
na kupata 666 ikimaanisha namba iliyowahusu watu wote kutokana na kuzaliwa kwao ndani ya miezi 12 ya
mwaka. Unaweza kuchunguza alama zinazotumika kwenye utabiri wa nyota utaziona zikiwakilisha ng`ombe,
nge, samaki na kadhalika. Elimu hiyo ilitokana na miungu wa Babeli waliowakilishwa kwa alama na namba.
Sayari 7 au joka lenye vichwa 7 ndilo lililotawala miungu hawa wote 36 walioitwa
‘Decans’ na kati ya miungu hao aliyekuwa mtawala wa wote alikuwa ni mungu jua. Kwa
mfano kama mtu alivaa hirizi yenye namba 2 ilimaanisha kuwa mungu wake ni mungu mwezi na hivyo
alitakiwa awe na alama ya mungu mwezi akiwa amevaa shingoni mwake pamoja na hirizi na kama mtu
alivaa hirizi namba 1 alitakiwa kuvaa alama ya mduara iliyowakilisha mungu jua huku aliyevaa hiziri namba
6 alivaa pamoja na alama ya msalaba ikiwakilisha mungu Ishtar.
Kwa kutumia hesabu, Wababeli walifanikiwa kutengeneza jedwali lenye namba 1 hadi 36 ambapo namba
hizo zikijumlishwa kwa pamoja katika kila msitari wowote unapata jumla ya 111 na kwa vile jedwali lina
misitari 6 walizidisha 111 x 6 = 666.
Namba iliyoandikwa kwenye hirizi ilimpa nguvu mvaaji zilizotoka kwa mungu aliyepewa namba hiyo.
Nguvu ya mungu iliweza kuongezeka kwa kujumlisha namba ya mungu huyo na namba zingine katika
msitari na kupata namba 111 na mungu alizidi kupata nguvu zaidi kwa kuzidisha 111 x 6. Namba 666
ilikuwa ni alama ya mamlaka ya miungu wote hivyo ilimaanisha kwamba ilikuwa na nguvu kwa miungu wote.
Hapa chini ni jedwali lenye namba za miungu 36 wa Babeli.
Kumbuka kwamba Wababeli walikuwa ni waabudu sanamu na hawakumuabudu Mungu wa kweli. Hata
hivyo leo pia kuna ibada nyingi ambazo chimbuko lake ni ibada za sanamu kutoka Babeli.
Jedwali la miungu 36 wa Babeli.
6 32 3 34 35 1
7 11 27 28 8 30
19 14 16 15 23 24
18 20 22 21 17 13
25 29 10 9 26 12
36 5 33 4 2 31
Zingatia kwamba namba 666 haiwezi kusimama peke yake bila kuhesabu miungu
maana bila kuhesabu huwezi kupata jumla ya namba 666. Hivyo unapotaka kuielezea
namba 666 lazima ufanye hesabu na kisha upate jumla yake iwe 666. Hata hivyo
haimzuii mtu kutumia njia nyingine ili kupata jumla ya 666, ila jambo muhimu ni
kwamba unatakiwa ujue asili ya namba 666 na kwamba ilipatikana kwa kujumlisha
miungu wa Babeli na ndio maana Mungu wa Mbinguni anaihusisha namba 666 na Babeli
maana chimbuko lake ni Babeli. Kwa watu wa Babeli, mungu aliyehitimisha hesabu na
kufanya jumla iwe namba 666 ndiye aliyekuwa na nguvu hata kumshinda mungu jua
ambaye alikuwa ni baba wa miungu wote. Wakati Biblia inapotuambia kwamba mnyama
ana namba 666 inatuambia kwamba namba 666 ilipatikana kwa kuhesabu na kujumlisha
miungu na haimaanishi kwamba namba 666 inasimama peke yake. Kama hakuna miungu
itakayohesabiwa, isingewezekana kupata jumla ya namba 666. Biblia inatuambia pia
kwamba hesabu inaanzia kwa mungu wa kwanza na kujumlisha namba ya miungu
wanaofuatia na mungu ambaye angehitimisha hesabu kwa kufanya jumla iwe 666 mungu
huyo angeweza kuwa na nguvu zaidi hata ya mungu wa kwanza maana yeye angetumia
namba 666 yenye nguvu za miungu wote.
Wababeli pia walikuwa na miungu saba (7—sayari 7) wa kwanza ambao ndio
walikuwa maarufu na ndio waliotumia majina ya siku kwa wiki kama ifuatavyo:
JEDWALI LA SAYARI 7 SAWA NA MIUNGU 7 YA BABELI.
Miungu Sayari/vichwa vya Joka/majina ya siku katika wiki
Jina la Sayari Jina la mungu wa Babeli Jina la siku kwa leo
Jua Shamash—namba 1 Sunday – jumapili
Mwezi Sin—namba 2 Monday- jumatatu
Mars Nergal—namba3 Tuesday- jumanne
Mercury Nabu—namba 4 Wednesday- jumatano
Jupiter Marduk—namba 5 Thursday- alihamisi
Venus Ishtar—namba 6 Friday- ijumaa
Saturn Ninib—namba 7 Saturday- jumamosi
Unaweza kuona jinsi miungu hawa wa Babeli walivyoendelea kuabudiwa hata wakati
wa Ukristo maana baada ya karne nyingi kupita, wakati mtume Paulo na Barnaba
walipotembelea Listra, walifanya muujiza wa kumponya mtu aliyekuwa kiwete. Watu wa
mji huo walikuwa waabudu miungu wa Babeli na mara baada ya kufanyika kwa muujiza
huo, watu “wakapaza sauti zao wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa
mfano wa wanadamu. Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye
aliyekuwa mnenaji”. Matendo 14:12. Unaposoma Biblia ya King James, jina Zeu ni sawa
na Jupiter, na Herme ni sawa na Mercury. Leo sayari au madini ya Mercury yanatumiwa
sana kwa ajili ya mawasiliano na ndio maana wapagani hao walimuita Paulo jina la
Mercury kwa sababu yeye ndiye alikuwa mnenaji. Ni kwa njia hiyo hata leo ibada za
miungu wa Babeli zinatawala ndani ya dini nyingi na waumini wengi hawajui kwamba
wanaabudu wasichokijua kama Yesu alivyomwambia yule mwanamke msamaria
(Yohana 4:19-24). Sasa, utakapofahamu kweli hii, tafadhali itikia wito wa Mungu
anaposema, “Umeanguka, umeanguka Babeli….Tokeni kati yake enyi watu wangu”.
Ufunuo 18:4.
Unaweza kuangalia jinsi joka mwenye vichwa saba alivyoaminiwa na Wababeli kuwa
ni miungu saba, kitu ambacho ni kweli ukilinganisha na Ufunuo 13na Ufunuo 17.
Wababeli waliendelea na hesabu, wakajumlisha namba 1 hadi 3 yaani 1+2+3 = 6 na
kuhitimisha kwamba namba 6 inawakilisha nguvu ya mungu baba (jua), mungu mama
(mwezi) na mungu mwana (sayari ya mars). Kisha wakatumia namba 11 kujumlisha
miungu namba 1 hadi 11 yaani 1+2+3+4…..+11 = 66 wakamaanisha kwamba namba 66
ina nguvu za miungu 11 wa kuanzia namba 1 hadi 11 na kisha wakajumlisha namba 1
hadi 36 wakapata namba 666 ikimaanisha mamlaka na nguvu za miungu wote. Hapa
walichukua namba 3, 11 na 36 na kuzifanya kuwa namba muhimu kwao. Biblia
inatuambia kuhusu mfalme Nebukadneza wa Babeli kwamba “alifanya sanamu ya
dhahabu ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa 60 na upana wake dhiraa 6…” Danieli
3:1. Nebukadneza alitumia hesanu za miungu wa Babeli ili kutengeneza sanamu
ikimaanisha kwamba alichukua miungu watatu yaani 1+2+3 = 6 kwa upana wa sanamu
hiyo na kisha akazidisha kwa nyuzi 10 ya kila mungu katika mzunguko wa Zodiac signs
na kisha kupata 6×10 = 60 kwa vipimo vya urefu wa sanamu hiyo.
Kwa kifupi hiyo ndiyo asili ya namba 666 ikiwa inatokana na jumla ya miungu wa
Wababeli ambao walikuwa miungu 36 na ukijulisha namba zote kuanzia 1 hadi 36 = 666.
Kazi iliyopo sasa ni kutumia kanuni ya Wababeli ili tuweze kumjua mnyama
anayewakilishwa na namba 666 kwa leo maana hatimaye ulimwengu wote utamsujudia
mnyama huyo badala ya kumuabudu Mungu. Tutaanza kwa kujifunza katika kitabu cha
Ufunuo na Danieli ili kuona ujumla wa jinsi ya kumtambua mnyama huyo.
Tunasoma kwamba “Na watu wote wakaao juu ya nchi wakamsujudu, kila ambaye
jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo aliyechinjwa tangu
kuwekwa misingi ya dunia. Mtu akiwa na sikio na asikie. Hapa ndipo penye hekima. Yeye
aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu.
Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufunuo 13: 8,9; 18. Jambo muhimu ni
kwamba heasabu ya mnyama huyu inapatikana kwa kuhesabu, yaani 1, 2, 3, …na
kadhalika na kwamba mnyama huyu ataabudiwa, lakini watakaomwabudu ni wale ambao
majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo, kwa maana nyingine ni
wale ambao hawatakwenda mbinguni, wale ambao hawakukubali kafara ya Mwanakondoo.
Watu wengi leo wanaridhika kuandikwa majina yao kwenye vitabu vya
makanisa yao badala ya kujitahidi ili majina yao yaandikwe kwenye kitabu cha uzima
cha Mwana-kondoo.
Sasa ni jukumu na muhimu kwa kila mmoja wetu anayetaka jina lake liandikwe katika
kitabu cha Mwana-kondoo kutambua kwamba jina lake litaandikwa kweny kitabu hicho
kwa masharti ya kutokumsujudia mnyama wa namba 666. Tunapaswa kujiuliza swali
moja muhimu, kwamba, nitawezaje kutokumsujudia mnyama huyo kama mimi
mwenyewe sijamfahamu jinsi anavyofanana, jinsi anavyofanya kazi yake na hata
kufahamu mahali alipo? Jibu ni kwamba ni lazima umtambue huyo mnyama na kutambua
kazi zake ndipo utafanikiwa kutokumsujudia na hivyo jina lako kuandikwa kwenye
kitabu cha Mwana-kondoo.
Lakini pia “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea
chapa katika kipaji cha uso wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya
Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake;
naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele ya Mwanakondoo.”
Ufunuo 14:9,10. Je, ni muhimu kweyu kujifunza ili tumtambue huyu mnyama
mwenye namba 666? Kwa wale wanaotaka majina yao yaandikwe kwenye kitabu cha
Mwana-kondoo wataona umuhimu huo.
Shetani amekuwa akitumia namba sita kuonyesha utawala wake maana katika viumbe
vyote vilivyoumbwa na Mungu hapa duniani, ni Adamu peke yake ndiye aliyeasi sheria
ya Mungu na Adamu huyo aliumbwa katika siku ya sita. Hivyo Shetani akapata utawala
wa dunia hii kupitia kiumbe aliyeumbwa siku ya sita (Mwanzo 2:26-31). Tangu
alipofukuzwa kutoka mbinguni Shetani amekuwa akimtumia mwanadamu kama wakala
wake wa kufanya kazi ya kupotosha kazi ya Mungu. Wakati wa utawala wa Babeli
Shetani alimtumia mfalme wa Babeli kama wakala wake na akamuagiza atengeneze
sanamu yenye vipimo vya namba sita: “Nebukadreza, mfalme, alifanya sanamu ya
dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita,
akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli.” Danieli 3:1. Baada ya
kutengeneza sanamu hiyo, iliamuriwa kwamba watu wote waisujudu na kuiabudu
sanamu hiyo atakayekataa sharti auwawe. Lakini walikuwepo vijana watatu ambao
walikubali kufa kuliko kuisujudu sanamu hiyo. Vijana hao walikataa kwa sababu majina
yao yalikuwa yameandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo. Ndivyo itakavyokuwa
hivi karibuni watu wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha Mwanakondoo
watamsujudia mnyama wa namba 666, na kwa kweli wengi wanamsujudia
mnyama huyo, wengine wakiwa wanajua na wengine wakiwa hawajui. Hata hivyo uwe
unajua au hujui kitu muhimu ni kwamba wote wanaomsujudu huyo mnyama majina yao
hayakuandikwa kwenye kitabu cha Mwana-kondoo.
Hivyo basi limekuwa kusudi la Shetani kuuangamiza ulimwengu kupitia mnyama wa
namba 666 na ni jambo muhimu kwetu kumfahamu mnyama huyo maana bila
kumfahamu tutaangamizwa na Shetani kama Mungu anavyosema “Watu wangu
wanaangamizwa kwa kukosa maarifa…..” Hosea 4:6. Haya si maarifa mengine bali yale
ya kuweza kuihesabu hesabu ya mnyama, yaani mia sita sitini na sita maana Yohana
anatuambia pia kwamba, “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu
hesabu ya mnyama huyo…”
Napenda tuelewe kwamba tunapojifunza habari za mnyama huyu tunajifunza habari za
ibada ya kweli na ibada ya uongo maana mnyama huyu anaabudiwa pia. Hebu tuiruhusu
sasa Biblia iweze kutuelezea habari zaidi za mnyama huyu. Tutaanza kwa kuchunguza
mambo yanayokwenda sambamba na mnyama huyu kisha tutahakikisha kama tuko sawa
kwa kuihesabu hesabu ya mnyama. Biblia inasema:
“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na
juu ya vichwa vyake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. 2.
Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama
miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake
na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. 3. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana
kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote
ikamstajabia mnyama yule. 4. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama
uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama
huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? 5. Naye akapewa kinywa cha kunena
maneno makuu ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na
miwili. 6. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani
yake, nao wakaao mbinguni. 7. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda,
akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. 8. Na watu wote wakaao
juu ya nchi wakamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima
cha mwanakondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia” Ufunuo 13: 1-8.
a) Maelezo hayo yamejaa mafumbo au alama, je nitafahamuje
mafumbo na alama hizo?
Tunahitaji kuiruhusu Biblia itafsiri mafumbo na alama ilizozisema. Tungetegemea
kwamba, Mungu, kwa faida yetu, alifunua ndani ya Biblia maana ya mafumbo na alama
hizi. Kwa hiyo, kile tunachohitaji ni usomaji makini ili tupate tafsiri ndani ya Biblia. Kwa
njia hiyo, tunaepuka kukisia na ubahatishaji wa kibinadamu.
Kwa hakika, Biblia inabatilisha kukisia na ubahatishaji wa kibinadamu kwa sababu
“hakuna unabii …….upatao kutafsiriwa kama apendavyo mtu fulani tu” 2Petro 1:20.
Biblia inajitafsiri yenyewe. Kwa mfano, kitabu cha Ufunuo kina jumla ya mafungu 404.
Kati ya hayo, mafungu 278 yanapatikana neno kwa neno katika vitabu vingine vya
Biblia, ambapo maana yake inajieleza wazi zaidi.
Kwa hiyo, tunakutia moyo kufanya kile Biblia inachotaka ufanye unapojifunza
(Angalia Matendo17:10,11 watu wa Thesalonike “…walilipokea neno kwa usikivu,
wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo”), na
weka kila fundisho lipimwe na maandiko. Kwa vile, kila atakayejifunza Biblia kwa
kuomba, akitamani kufahamu kweli, ili aitii kweli hiyo, atafahamu maandiko. “Mtu
akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa
Mungu, au mimi nanena kwa nafsi yangu tu” Yohana 7:17
b) Ni alama (au mafumbo) gani tunazohitaji kuzifunua?
Kuna alama nyingi kwa ajili ya mnyama, hata hivyo, tutajikita zaidi kwenye zile ambazo
ni muhimu kwa ajili ya fundisho hili ili kumtambua mnyama, sanamu ya mnyama na
alama ya mnyama.
Alama hizi ni ‘mnyama’, ‘joka’, ‘bahari’, ‘miezi 42’, na ‘makufuru’.
Mnyama: Katika unabii wa Biblia, mnyama ni alama ya mfalme au ufalme. “wanyama
hao wakubwa, walio wanne, ni wafalme wanne….mnyama wa nne atakuwa ufalme wa
nne…”:
Dan. 7:17,23.
Kuhusu mnyama huyu, tunajifunza mnyama wa pekee kwa sababu siyo tu nguvu ya
kisiasa, bali pia ni mnyama mwenye dini, maana watu “walimsujudu huyo mnyama”.
Ufunuo 13:4.
Joka: Katika unabii wa Biblia, Joka ni jina jingine la shetani, baba wa uongo na
machafuko. “yule joka akatupwa, yule mkubwa,….aitwaye ibilisi na shetani,
audanganyae ulimwengu wote.” Hii ingemaanisha kwamba wakati shetani alipotoa
“nguvu zake, kiti chake cha enzi, na uwezo mwingi” kwa mnyama, tunaweza kumtarajia
mnyama akiwa na tabia ile ile ya shetani au joka, ya udanganyifu. Hivyo basi,
udanganyifu mkubwa utaonekana katika tabia ya mnyama. Ufunuo 12:9; 13:2.
Bahari: Katika unabii wa Biblia, bahari ni alama au kielelezo cha wingi wa watu tofauti
au wingi wa watu mbalimbali. “….Maji ni jamaa, na makutano, na mataifa, na lugha”
Ufunuo 17:15. Vilevile, ufalme huu wa pekee uliinuka kutoka baharini, ikimaanisha
kwamba ulitoka katika eneo la dunia ambalo lilikuwa na watu wengi wa mataifa
mbalimbali.
Miezi Arobaini na miwili: Kipindi hiki ni sawa sawa na miaka mitatu na nusu (42
gawanya kwa miezi 12). Na Biblia iliandikwa kwa mujibu wa kalenda ya Kiyahudi
ambapo kila mwaka wa kiyahudi una siku 360 (yaani siku 30 kwa kila mwezi). Kwa
hiyo, miaka mitatu na nusu na miezi arobaini na miwili vyote ni sawa na siku 1260.
Sababu inayotufanya tubadili miezi kwenda sambamba na siku zake ni kwamba, wakati
Mungu alipotoa unabii, mara nyingi Amekuwa akilinganisha siku moja kwa mwaka
mmoja. “….yaani, siku arobaini, kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu
yenu, ndiyo miaka arobaini…..” “…..siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja,
nimekuagizia.” Hesabu14:34, Ezekieli 4:6.
Kwa hiyo, miezi arobaini na miwili ya kiunabii inamaanisha miaka 1260 ambayo
mnyama alipewa “kinywa kunena maneno makuu, ya makufuru” na atafanya “vita na
watakatifu na kuwashinda: na akapewa uwezo kwa kila kabila, na jamaa, na lugha, na
taifa.” Ufunuo 13:5,7… Ikimaanisha kwamba katika kipindi hiki cha miaka 1260,
mnyama atakufuru, atatesa wakristo, na atakuwa na uwezo mkuu.
Makufuru: Katika Biblia, makufuru yameelezewa katika namna mbili, ya kwanza ni
pale mtu anapodai kuwa yeye ni Mungu au muwakilishi wake. “…kwa ajili ya kazi
njema, hatukupigi mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu
wajifanya mwenyewe u Mungu.” Yohana 10:33. Kwa hiyo, mnyama, ambaye ni mwenye
mamlaka ya kisiasa na kidini, anamkufuru Mungu kwa kujiweka mahali pa Mungu hapa
Duniani. Hata hivyo, wayahudi hawakumwelewa Yesu kuwa ndiye masihi, mwana wa
Mungu, sawa na Mungu, ambaye ni Mungu, tofauti na mwanadamu mwingine yeyote
asiye sawa na Mungu, na hivyo Yesu hakukufuru. Namna ya pili ya kukufuru, ni kujipa
uwezo wa kusamehe dhambi za watu. “Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani
awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?” Marko 2:7
Hata hivyo, Yesu alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi maana Yeye ni Mungu.
Mnyama huyu, mwenye nguvu za kisiasa na kidini, amemkufuru Mungu, sio tu kwa
kuchukua mahali pa Mungu hapa duniani, lakini pia kwa kudai kuwa na uwezo na haki
ya kusamehe dhambi. Hivyo si ajabu kuwa mnyama ana “majina ya makufuru” na
ananena “makufuru dhidi ya Mungu na jina lake” . Hii ni kwa sababu mnyama anadai
kuwa na nguvu ambayo ni haki ya pekee ya Mungu tu. Ufunuo 13:1,6.
Baada ya kuiruhusu Biblia ijitafsiri yenyewe, tunaweza sasa kuwa na funguo tisa
zitakazotusaidia kumtambua mnyama. Hata hivyo, hizi si funguo pekee za kumtambua
mnyama, zipo nyingi zaidi ndani ya Biblia. Tunatumaini muungano huu wa funguo za
utambuzi zitakuongoza kusoma na kujifunza zaidi Biblia ili uweze kupata funguo zaidi.
(1) Mnyama ana mamlaka ya kisiasa na kidini kwa wakati mmoja, “wakamsujudu yule
mnyama…..” Ufu. 13:4 (2) Mnyama alitoka kwenye eneo hapa duniani lenye watu
wengi wa mataifa “ …nikaona mnyama akitoka katika bahari.” Ufu.13:1 (3) Mnyama
alipata nguvu na mamlaka yake kutoka kwa shetani. “…yule joka akampa nguvu zake na
kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.” (4) Mnyama alitawala kwa mateso makali kwa
mda wa miaka 1260. “…akapewa kinywa kunena maneno ya makufuru. Akapewa uwezo
kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.” Ufu.13:5. (5) Mnyama aliwatesa
watakatifu kwa miaka 1260 na kuwashinda. Ufu. 13:7 (6) Mnyama atapona jeraha lake la
mauti “…na pigo lake la mauti likapona.” Ufu. 13:3 (7) Mnyama ana hesabu ya
kibinadamu 666 inayotambulisha ofisi yake. “…na aihesabu hesabu ya mnyama huyo. Na
hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufu.13:18 (8) Mnyama anakufuru kwa kudai
anasamehe dhambi na kuchukua nafasi ya Mungu hapa duniani. (9) Mnyama amefanya
makufuru mengine kwa vitendo vyake dhidi ya Mungu. “naye akapewa kinywa cha
kunena maneno makuu, ya makufuru.” Ufu.13:5. Hizo ndizo sifa za mnyama wa ajabu
mwenye namba 666. Sasa tunaweza kumtambua mnyama huyo kutokana na sifa zake
kwamba ni taifa ambalo lina utawala wa kisiasa na kidini pia. Haishangazi leo pia kuona
nchi nyingi zikitambuliwa kutokana na kuwakilishwa na wanyama. Kwa mfano Tanzania
inawakilishwa na mnyama aitwaye Twiga, Marekani inawakilishwa na ndege aitwaye
Tai, Urusi inawakilishwa na Dubu, China inawakilishwa na Joka (Dragon), Kenya
inawakilishwa na Jogoo nk.
Kwa nini mataifa huwakilishwa na wanyama? Maana yake ni nini? Tunasoma
kwamba “Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za
mbinguni zikavuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa wanne
wakatokea baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama Simba…wa
pili kama dubu, ….mwingine kama chui….mnyama wa nne mwenye kutisha.”Danieli
7:2-7. Pia tunasoma “Na yule mnyama niliyemuona alikuwa mfano wa chui, na miguu
yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha Simba….”
Ufunuo 13:2. Sababu ya kusoma mafungu hayo mawili ni kwamba katika Danieli
tunakuta wanyama wanne tofauti wakati katika Ufunuo tunakuta mnyama mmoja
mwenye alama za wanyama wanne wa Danieli. Huyu mnyama wa Ufunuo ni sawa na
mnyama wa nne katika Daniel ambaye anatamkwa kuwa ni mwenye kutisha, maana
yake ni kwa sababu alikuwa na tabia za wanyama watatu waliomtangulia kutokea.
Ukweli ni kwamba wanyama wa Danieli 7 ni falme nne kama inavyojitafsiri, yaani
Babeli, Uyunani au Greece, Umedi na Uajemi na Rumi au Roman Empire. Hizo ni
tawala zilizowahi kutawala dunia nzima. Baada ya Roman Empire alifuatia mnyama wa
ufunuo 13:1-10 ambao ni utawala wa Rumi ya kidini iliyotawala kwa miaka 1260
kuanzia mwaka 538-1798. Utawala huo ulikuwa na tabia ya tawala zilizoutangulia. i)
Simba: utawala unaowakilishwa na simba humaanisha kuwa na ujasiri mkubwa;
“Simba aliye hodari kupita wanyama wote; wala hajiepushi na aliye yote.” Mithali
30:30. ii) Dubu: Utawala unaowakilishwa na Dubu hufanana kwa kiasi fulani na
utawala unaowakilishwa na Simba; “Bwana aliyeniokoa katika makucha ya simba na
makucha ya dubu ataniokoa…” 1 Samweli 17:37. Pia soma Isaya 11:7. iii) Chui:
Utawala unaowakilishwa na mnyama chui humaanisha utawala wa kuvizia na
unaopenda vita kama vile simba na dubu; “Basi nimekuwa kama simba kwao; kama
chui nitavizia njiani; nitakuwa nao kama dubu aliyenyang`wanywa watoto wake; nami
nitararua nyama ya mioyo yao, na huko nitawala kama simba; huyo mnyama mkali
atawararua.” Hosea 13:7-8. Hizo ndizo zilikuwa tabia za falme nne zilizotawala dunia
yote. Sasa unaweza kuona kuwa Marekani kuwakilishwa na tai inamaanisha kuwa na
tabia ya tai; “Farasi zao ni wepesi kuliko chui, ni wakali kuliko mbwa-mwitu wa jioni;
na wapanda farasi wao hujitupa naam, wapanda farasi wao watoka mbali sana;
huruka kama tai afanyaye haraka.” Habakuki 1:8. Taifa la Marekani lilianzishwa
katika karne ya 18 wakati wa kipindi cha utawala wa mnyama wa 666 ambapo
tunasoma kwamba mnyama huyo (Marekani) alitokea katika nchi ikimaanisha kuwa
katika eneo ambalo halikuwa na watu. Wakati wa mateso ya mnyama wa 666 ndipo
watu walipokimbilia katika bara la Amerika wakitoka ulaya na mabara mengine na
mnamo July 4, 1776 Marekani ikapata uhuru chini ya Rais wa tatu aliyeitwa Thomas
Jafferson. Marekani kuwakilishwa na tai inamaanisha kwamba ni taifa linalofanya
haraka kuruka kama tai na kwenda mbali zaidi lengo likiwa ni kushambulia. Tai ni
ndege mkubwa anayekula nyama; hivyo ndio maana tunashuhudia tukiona taifa la
Marekani likivamia nchi yoyote duniani na hivi karibuni tutaona Marekani
ikiishambulia Iran baada ya kuipiga Iraq. Kumbuka kuwa utawala wa Umedi na Uajemi
ulikuwa katika maeneo ambayo leo kuna nchi za Iraq na Iran.
Tanzania kuwakilishwa na twiga; tunafahamu tabia ya twiga alivyo mpole, mnyama
asiyependa makuu tena anayependa kula majani ya juu kabisa ambayo hayajaguswa
tena yaliyo laini. Je, si kweli kwamba watanzania pia hawapendi ugomvi na ndio maana
kuna amani? Maana kila nchi inayowakilishwa na mnyama ina tabia ya huyo mnyama;
kwa mfano jirani zetu Kenya wanawakilishwa na jogoo, tunafahamu tabia ya jogoo
kwamba hapendi kushindwa na jogoo mwenzake, huoni chaguzi za Kenya hutawaliwa
na fujo na kutokukubali kushindwa(?). China inawakilishwa na dragon au joka. Joka
katika Biblia ni ibilisi na shetani; ukweli ni kwamba China ni nchi isiyotambua uwepo
wa Mungu, kumbuka enzi za Mao na siasa za Ukomunist, na ndiyo sababu iliyomfanya
Shetani afukuzwe mbinguni. Wachambuzi wa habari wanasema kuwa China na Asia
kwa ujumla ndiko wanakopatikana Freemason wengi kuliko maeneo mengine duniani,
haishangazi kuona uchumi wa China unakua kwa kasi maana kila anayemkubali
mnyama wa 666 atapata utajiri mkubwa. Tena inasemekana kuwa China ndiyo nchi
inayayoongoza katika ulimwengu kwa kunyonga raia wake – na hiyo kwa kifupi ni
tabia ya joka – ibilisi na Shetani. Hivyo nchi huwakilishwa na wanyama kutokana na
tabia ya wanyama hao na nchi husika huwa na tabia hiyo.
Sasa tutatumia kanuni asili kutoka kwa Wababeli jinsi ya kuipata namba 666 ili
tulinganishe na maelezo hapo juu tuone kama tuko sawa au la.
Biblia inasema “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu
ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini
na sita.” Ufunuo 13:18.
Nini Na ni Nani Illuminati?
Dr. Adam Weishaupt (1748 – 1830)
Baada ya kumuona mnyama anayetambulika kwa namba 666, sura hii inaanza kwa
kuwaelezea THE ILLUMINATI, kundi ambalo ni hatari zaidi katika mchakato mzima wa
kuharibu maadili na kuwafanya watu wamwabudu Lucifer – yaani Shetani aliye baba wa
uongo katika ulimwengu huu – Yohana 8:44.
Kuna wakati ambapo Mungu alimtoa mwokozi wa taifa la Israeli kwa kuwapa mtu
mwenye nguvu nyingi kuliko watu wote duniani. Mungu alimwambia mnadhiri wake
Samson kwamba asiseme na iwe siri kwake kuhusu asili ya nguvu zake. Ni kwa njia hiyo
hiyo ya kuficha asili ya nguvu zao, Illuminati wamefanikiwa kuutawala ulimwengu. Wao
wanasema kwamba:
“The great strength of our Order lies in its concealment; let it never appear in any
place in its own name, but always concealed by another name, and another occupation.
None is fitter than the lower degrees of Freemasonry; the public is accustomed to it,
expects little from it, and therefore takes little notice of it. Next to this, the form of a
learned or literary society is best suited to our purpose, and had Freemasonry not
existed, this cover wouldn’t have been employed; and it may be much more than a cover,
it may be a powerful engine in our hands… A Literary Society is the most proper form for
the introduction of our Order into any state where we are yet strangers.” (John
Robinson’s “Proofs of a Conspiracy” 1798, Boston, 1967, p. 112)
“Nguvu kubwa ya utaratibu wetu inapatikana kwa kuuficha utaratibu huo, hebu
isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima ifichwe kwa jina lingine, na kazi
nyingine. Hakuna anayefaa kama Freemason wa digrii za chini; jamii inafanya kazi
pamoja na hao, ina matarajio kidogo kutoka kwao, na kwa hiyo haina habari nao.
Wanaofuatia kwa hawa ni jamii ya watu waliosoma maana wanafaa kwa ajili ya
malengo yetu, na kama Freemason isingekuwepo, njia hii ya kujificha isingetumika; na
ingekuwa ni zaidi ya kujificha, ingekuwa ni injini yenye nguvu mikononi mwetu…jamii ya
wasomi ni njia inayofaa zaidi kwa kuelezea taratibu zetu katika taifa lolote mahali
ambapo sisi bado tu wageni.” (John Robinson’s “Proofs of a Conspiracy” 1798, Boston,
1967, p. 112)
Hivyo unaweza ukawa na jamii ya Illuminati na freemason wakiwa wanafanya kazi
kwa majina mengine na sio majina ya Illuminati na Freemason na hapo ndipo nguvu yao
ilipo. Watu wengi wameshindwa kuwatambua kwa sababu ya kujificha kwao. Kwa nini
wanajificha? Kwa sababu wanajua kwamba wanachokifanya si halali na wala hakitokani
na mapenzi ya Mungu. wanatumia jamii ya watu wasomi ili kufanikisha malengo yao.
Huwezi kuwazungumzia Illuminati bila kumfahamu Dr. Adam Weishaupt na huwezi
kuwazungumzia freemasons bila kumfahamu na kumtaja Dr. Albert Pike.
Unapofanya utafiti wa Illuminati na freemason katika mtazamo mzima wa ‘New World
Order ’, unapaswa kujua kanuni tatu ( 3) muhimu ambazo ndizo msingi wa
freemason/illuminati: 1)Thesis x Antithesis = Synthesis; 2) Hesabu na namba za
freemason; na 3)Alama na ishara za freemason. Huwezi kuelezea freemason kwa ufasaha
kama hutazingatia kanuni hizo tatu. ‘Thesis x Antithesis = Synthesis’ ndiyo kanuni
inayotawala kwa freemason na kutekelezeka kwake kunategemea hesabu na namba
pamoja na alama na ishara za freemason. Kwa nini wanatumia kanuni ya alama na
ishara? wanasema “By symbols…is a man guided and commanded… ” wakimaanisha
kuwa “watu huamrishwa na kuongozwa kwa kutumia alama”. Ndio maana hata waumini
wengi wanaongozwa kwa kutumia alama ama ya nyota ya pentagram, jua, mwezi au
msalaba. Kwa nini wanatumia kanuni ya namba? Kwa sababu “Occultists Worship
Numbers and numbers have power”. Hivyo kama umepungukiwa na moja ya kanuni hizo
ni wazi kwamba utafiti wako utapungua pia.
Dr. Adam Weishaupt alikuwa ni Profesor wa somo linaloitwa ‘cannon law’ katika
Chuo Kikuu cha Ingolstadt huko Bavari. Alipata elimu yake kutoka katika shirika
liitwalo ‘Jesuit Society’ na akawa Padre wa shirika hilo. Baadaye alitoka katika shirika
hilo na akajiunga na chama cha siri kiitwacho Rosicrucian na akajifunza uchawi wa
wayahudi uitwao Qabbala na ndipo alipoanzisha mpango wake uitwao ‘Order of the
Illuminati’ mnamo tarehe 01/05/1776 huko Bavaria. (Rejea, John Robison, A.M., Proofs
of a Conspiracy, p 63; Nesta H. Webster, The French Revolution, p 20).
Weishaupt alianzisha kikundi cha Illuminati kwa misingi ya utaratibu wa Jesuit (Jesuit
order). Illuminati ni chama cha siri na kina mpango wa kuangusha serikali na dini zote
ulimwengu kisha kuanzisha serikali na dini moja wanayoiita ‘New World Order’.
Weishaupt alianzisha chama cha Illuminati akiwa na wenzake wakiwa watano,
Weishaupt, Kollmer, Francis Dashwood, Alphonse Donatien DeSade na Meyer Amschel
Rothschild. Illuminati iliundwa kwa kusomea digrii tatu za awali ambazo ni Novice,
Minerval, na Illuminated Minerval; zikifuata utaratibu wa chama cha Jesuits na
freemasons. Wanachama wote walitakiwa kubadili majina yao na kutuma majina ya dini
yao ambapo Weishaupt aliitwa “Spartacus” msaidizi wake, Xavier von Zwack, aliitwa
“Cato”; Nicolai, akaitwa “Lucian”; Professor Westenreider akaitwa “Pythagoras”; Canon
Hertel akaitwa “Marius”; Marquis di Constanza akaitwa “Diomedes”; Massenhausen
akaitwa “Ajar”; Baron von Schroeckenstein akaitwa “Mohomed”; na Baron von
Mengenhofen “Sylla.” Makao makuu yalikuwa huko Munich, Ujerumani, yakijulikana
kama ‘the Grand Lodge of the Illuminati’ (au Lodge of the Grand Orient), na kupewa jina
la “Athens.” Vituo vingine vilikuwa huko Ingolstadt pakipewa jina la “Ephesus,”
Heidelberg jina la “Utica,” Bavaria kama “Achaia,” na Frankfurt pakajulikana kama
“Thebes.”
Ili kufanikisha lengo lao, waliweka mkakati ufuatao kama ilivyoandikwa na Nesta
Webster kwenye kitabu kiitwacho “World Revolution” uk. 22, wakiwa na malengo sita:
1. Kukomesha utawala wa kifalme
2. Kukomesha umiliki wa mtu binafsi
3. Kukomesha urithi
4. Kukomesha utawala na utumishi wa serikali za nchi
5. Kukomesha ndoa na familia kwa kuweka ndoa za mikataba na kuanzisha elimu ya
watoto kwa wote itakayosimamiwa na serikali moja.
6. Kukomesha dini na kuanzisha dini moja yenye mchanganyiko wa imani.
Ili kutekeleza mpango huu na kisha kutimiza malengo hayo, Weishaupt alitambua
kwamba anahitaji nguvu zisizo za kawaida ili kufanikiwa kuharibu ustaraabu wa nchi za
magharibi, ambapo nchi hizo zilikuwa na imani ya Kikristo. Hatua ya kwanza ilikuwa ni
kutengeneza alama ya utambulisho wa Illuminati na akabuni Piramidi likiwa na jicho na
kuweka maneno ya kilatini juu yake “Annuit Coeptus” yakimaanisha “kutangaza
kuzaliwa kwa” na chini ya Piramidi akaweka maneno “Novus Ordo Seclorum”
yakimaanisha “Mpango mpya wa Ulimwengu” (Rejea “The New World Order”, A. Ralph
Epperson, p. 108-112). Kisha akafanikiwa kuweka umbo hilo la Piramidi nyuma ya Dolla
moja ya Kimarekani.
Weishaupt alitambua kwamba ingekuwa vigumu kufanikisha mipango yake ikiwa
ulimwengu utaendelea kuwa na amani na hivyo akaamua kuanzisha utaratibu
utakaopingana na imani ya wakati huo kwa kanuni ya “Ordo ab chao” yaani “Order Out
of Chaos” ikimaanisha kuanzisha “machafuko yaliyopangiliwa”. Mataifa ya magharibi
wakati huo yalitawaliwa na serikali katika mfumo wa Thesis. Weishaupt aliamua
kuanzisha mfumo pinzani na Thesis ambao ni Antithesis. Mifumo hii miwili ilianza
kupingana (kupigana vita) na hili lilipelekea kuzaliwa kwa ya mfumo mpya (hybrid)
unaoitwa Synthesis ambalo ndilo lengo la Illuminati. Weishaupt akaweka kanuni ya
‘Order out of Chaos’.
Hebu tuangalie maana ya maneno hayo:
•  Thesis – Ni mfumo uliotawala Ulaya miaka ya 1700. Mfumo huu ulikuwa hivi:
Kiuchumi umiliki wa mali ulikuwa wa mtu au ubepari (economically Private
Enterprise), Kisiasa ulikuwa wa kifalme au demokrasia (politically either
Monarchy or Democracy), na kidini ulifuata Ukristo (religiously Judeo-Christian)
•  Anti-Thesis – Huu ni mfumo kinyume na Thesis na ndio unaopelekea kuzaliwa
kwa mfumo unaoitwa Synthesis kutokana na kupinga mfumo wa Thesis.
Kiuchumi ulitawaliwa na Ujamaa (Communism), Kisiasa ulitawaliwa na Udikteta
na kidini ulitawaliwa na kutokuamini uwepo wa Mungu (Ukomunist).
Mfumo wa Thesis ulikuwa na nguvu nchini Marekani na ndipo Illuminati waliona ni
vema kuanzisha taifa lenye mfumo wa Antithesis litakalokuwa na nguvu kubwa na
kupingana na taifa la Marekani. Ndipo taifa la Urusi likaanzishwa kwa kupewa nguvu
baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia na ya pili. Wakati Marekani ilifuata mfumo wa
Kibepari kiuchumi, Ukristo kidini na demokrasia kisiasa, Urusi ilifuata mfumo wa
Kijamaa kiuchumi, aethitic kidini na Udikteta kisiasa. Mwaka mmoja kabla ya
kumalizika vita kuu ya pili ya dunia ulifanyika mkutano wa viongozi wakuu watatu
mwaka 1944 huko Yalta. Viongozi hao waliunda pembe tatu (Piramidi) na walikuwa ni
rais wa Marekani Franklin Roosevelt, waziri mkuu wa Uingereza Winston Churchill na
Dikteta wa Kikomunist Josef Stalin wa Urusi. Viongozi hao walikutana ili kuweka
utaratibu wa utekelezwaji wa mipango ya ulimwengu kuhusu serikali na dini zote. Kila
mmoja anakumbuka vita baridi kati ya Marekani na Urusi ambapo hadi sasa vita hiyo
imemalizika kwa hesabu hii: Thesis x Antithesis = Synthesis.
Moja ya kanuni za ‘Order of the Illuminati’ inatokana na uchawi wa wa Simon Magus
uliochanganywa na Ukristo. Lakini pia kanuni hiyo ilitoka katika kundi moja liitwalo
‘Wanikolai’ ambao walikuwa wafuasi wa mmoja wa mashemasi saba aitwaye Nikolai wa
kanisa la awali la Kikristo (Ufunuo 2:14,15), [Rejea Grolier’s Encyclopedia, vol 9, p 374
(1944). The New Age Movement and the Illuminati–666, p 94-95, published by The
Institute of Religious Knowledge].
Illuminati wanapata wapi nuru yao? Wanapata nuru kutoka katika Filosofia ya
Ugiriki. Na je filosofia ya Ugiriki inapata wapi nuru hiyo? “The individual who became
spiritually or intellectually enlightened in the ancient Babylonian Mysteries was…called
an Illuminated.” [Institute, 666, p 92]
Kwamba mtu aliyepata ujuzi wa kiroho huko Babeli aliitwa “an Illuminated” yaani
aliyevuviwa nuru.
Neno Lucifer kwa Kilatin linamaanisha “Light –Bearer” yaani mwenye nuru; neno
Titan kwa Kigiriki lina maanisha “mungu Jua” na katika kitabu kiitwacho young`s
Concordance to the Bible” ukurasa wa 806, neno Lucifer limetafsiriwa kama
“Illuminated One” au “Shining One” yaani aliyevuviwa nuru. Hivyo Illuminati wanapata
nuru yao kutoka kwa shetani au mungu jua.
Weishaupt anakubaliana na hili ndio maana akaandika kwamba:
“This is the great object [uniting all the world into one] held out by this Association: and
the means of attaining it is Illumination, enlightening the understanding by the sun of
reason….The Flaming Star is the Torch of Reason. Those who possess this knowledge are
indeed Illuminati.” [Robison, Proofs, p 64, 93.]
Hebu tusitishe kwa muda mfupi kuwatazama Illuminati ili tupate nafasi ya kuliangalia
kundi la ‘Jesuit Society’ maana wao ndio waliomfundisha Adam Weishaupt ambaye ni
muasisi wa Illuminati.
Shirika la Jesuits lilianzishwa na Ignatius Loyola aliyezaliwa mwaka 1491 na
kufariki Julai 31, 1556. Sherehe ya Ignatius Loyola hufanyika kila ifikapo Julai 31 ya kila
mwaka, siku aliyokufa. Mkuu wa shirika la Jesuit anaitwa “Black Pope” yaani “Papa
Mweusi.” Hapa haimaanishi kuwa mkuu huyo anatakiwa awe wa rangi nyeusi yaani
mwafrika bali neno ‘black’ linamaanisha ‘asiyeonekana,’ na kwa maana hiyo Jesuit
Society wanafanya kazi za siri, zisizoonekana, tena za giza ambazo ni kinyume na nuru
ya neno la Mungu.
Shirika hili lilianzishwa ikiwa ni matokeo ya kanisa Katoliki kupiga vita uprotestant.
Kujitoa kwa Loyola katika kulitumika kanisa kunaweza kuonekana kwenye kanuni 13 za
shirika la Jesuits zinazolihusu kanisa; “Rules for thinking with the church” anaposema “I
will believe that the white that I see is black if the hierarchical Church so defines it”.
Kwamba “nitaamini rangi nyeupe ninayoina kuwa ni nyeusi kama mfumo wa uongozi wa
kanisa utatafsri hivyo.” Na ndivyo ilivyo katika shirika hili ya kwamba mtu anapaswa
kuamini na kufanyia kazi kile anachofundishwa na kanisa hata kama dhamira yake
inamwambia kuwa hicho si sahihi. Hebu soma nukuu hizi ili tuone chanzo cha chama cha
Jesuits:
“Kuinuka kwa dhama za giza kulitokana na kuruhusu Biblia ipatikane kwa urahisi hata
kwa watu wa kawaida na mafundisho ya waprotestant wanamatengenzo. Mafundisho
haya yalikuwa na msingi wa kutafsiri unabii kutokana na historia; yaani kuwakilisha siku
1260 za Danieli na Ufunuo kuwa miaka 1260. Viongozi wa matengenezo kama Luther,
Calvin, Huss, Wycliff, Knox, Latimer, Cranmer, Ridley, Hooker, Newton na wengine
waliamini hivyo na kufundisha.” Ibid p 7.
“Kwa kutumia mbinu hii ya kutafsiri unabii, kanisa la Roma lilionekana wazi kuhusika
na unabii huu wa pembe ndogo katika Daniel 7, na mnyama wa Ufunuo 13:1, mwanamke
wa Ufunuo 17, ikiwa ni pamoja na kichwa cha kanisa kuwakilisha Mtu wa Kuasi wa 2
Wathesalonike 2. Kadri mafundisho haya yalivyozidi, kanisa la Roma lililazimika
kujilinda dhidi ya kuongezeka kwa ushahidi wa unabii wa Biblia kulihusisha kanisa hilo.
Hivyo upapa ukaanza kuweka mipango ya kuwapinga waprotestant kwa kuanzisha
‘Jesuit society’ ili kisaidie kufundisha mafundisho ya kanisa na kuharibu mafundisho na
vitabu vyote vilivyokuwa kinyume na kanisa na kuanzisha “Holy Office of the
Inquisition” maalumu kwa ajili ya kuwatesa hata kuwaua wapinzani wa kanisa.” Ibid. pp
126, 127.
Kati ya mwaka 1524 na mwaka 1537 Loyola alisomea Theology huko Hispania na
Ufaransa. Mwaka 1534 alifika Ufaransa wakati wa kipindi cha mapambano dhidi ya
uprotestant, mapambano ambayo yalimfanya John Calvin akimbie kutoka Ufaransa.
Mwaka 1539, Loyola akiwa na wenzake walifanikiwa kuanzisha muungano na kuuita
‘Society of Jesus’. Mwaka uliofuata yaani 1540 chama hicho kikapewa baraka na Papa
Yohana III na ilipofika mwaka 1548 Papa huyo akatoa kibali kwa Society of Jesus ili
kiweze kushughulika na maswala ya kiroho. Loyola alikufa mnamo Julai 31, 1556 na
akabarikiwa na Papa Paul V mwaka Julai 27, 1609, akapewa hadhi ya utakatifu Machi
12, 1622 na Papa Gregory XV na akatangazwa kuwa kiongozi wa maswala la kiroho
mwaka 1922 na Papa Pius XI.
Jina kamili la Loyola lilikuwa ni Íñigo akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 13.
Baada ya kifo cha mama yake mwaka 1506 Íñigo alichukua jina la mwisho “de Loyola”
kutokana na jina la mji ulioitwa Loyola ambako alizaliwa. Akaamua kutumia jina la
“Ignatius of Loyola” yaani Ignatius anayetokea mji wa Loyola.
Mwaka 1534 aliwakusanya marafiki zake sita ambao alikutana nao chuo kikuu wakiwa
ni wanafunzi wenzake ambao ni Francis Xavier, Alfonso Salmeron, Diego Laynez na
Nicholas Bobadilla wote wakiwa ni Wahispania; Peter Faber akiwa ni Mfaransa; na
Simao Rodrigues aliyekuwa Mreno. Asubuhi ya tarehe 15 Agust 1534, katika kanisa la
Our Lady of the Martyrs huko Montmartre, Loyola akiwa na wenzake sita ambapo
mmoja wa marafiki hao alikuwa ni padre, waliapa kutumika maisha yao yote. Ignatius
akawa ndiye kiongozi mkuu (Superior General) wa chama cha Yesu – Society of Jesus.
Yeye ndiye aliyetunga katiba ya chama hicho mwaka 1540. Nukuu muhimu tunayoweza
kuichukua kutoka kwa Ignatius wa Loyola ni hii:
“That we may be altogether of the same mind and in conformity with the Church herself,
if she shall have defined anything to be black which appears to our eyes to be white, we
ought in like manner to pronounce it to be black. For we must undoubtingly believe, that
the Spirit of our Lord Jesus Christ, and the Spirit of the Orthodox Church His Spouse, by
which Spirit we are governed and directed to Salvation, is the same.” [Ignatius Loyola,
Spiritual Exercises, Rule 13 Henry Bettenson, ed., Documents of the Christian Church,
2nd ed. (London: Oxford University Press, 1963), p. 260.]
“Kwamba wote tuwe na nia moja na kukubaliana na kanisa, kama limetafsiri kitu
chochote kuwa ni cheusi wakati kinaonekana machoni mwetu kuwa ni cheupe, tunapaswa
kukitangaza kuwa ni cheusi. Maana bila shaka tunapaswa kuamini, kwamba roho wa
bwana wetu Yesu kristo, na roho wa kanisa la Orthodox ndugu yake, roho ambaye
anatuongoza katika wokovu, ni yule yule.” [Ignatius Loyola, Spiritual Exercises, Rule 13
Henry Bettenson, ed., Documents of the Christian Church, 2nd ed. (London: Oxford
University Press, 1963), p. 260.]
Kwa mujibu wa Ignatius Loyola, kanisa Katoliki na kanisa la Orthodox ni ndugu
mmoja na wote wanaongozwa na roho mmoja. Lakini pia tunaweza kujiuliza kwa nini
Loyola atumie rangi nyeusi hata kama ni nyeupe? Jibu ni kwamba alikuwa anaongelea
kiongozi mkuu wa chama hicho cha Jesuits ambaye anaitwa ‘black Pope’ yaani Papa
mweusi. Lakini pia Loyola aliweka kanuni 13 za kuongoza chama cha Jesuits. Katika
sura zitakazofuatia tutaona jinsi Illuminati wanavyoabudu namba ikiwepo namba 13 na
kuna uhusiano mkuwa sana kati ya Jesuits, Illuminati na Freemasons, wote wakiwa ni
watumishi wa mnyama wa namba 666.
Ni utaratibu gani unafanyika wakati mtu anapotaka kuwa mwanachama wa “Jesuit
Society?” Kama tutakavyoona, utaratibu wa kujiunga na chama cha Jesuits unafanana na
utaratibu wa kujiunga na freemason. Cha ajabu ni kwamba baadhi ya madhehebu na
makanisa yanafuata utaratibu huo wakati waumini, na hasa viongozi kama watawa,
wachugaji, maaskofu nk wanapopewa nafasi hizo kwa mara ya kwanza japo Biblia
inakataza wazi kutumia utaratibu kama huo.
Wakati mtu anapotaka kujiunga na chama cha Jesuits anatakiwa, pamoja na mambo
mengine, kutoa viapo vya utii katika chama hicho, kiongozi wa chama hicho na kiongozi
wa kanisa. Kabla ya kusoma viapo vya Jesuits, hebu tuiulize Biblia kuhusu viapo.
“Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana
nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana
ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuweka miguu
yake…wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa
mweupe au mweusi…..kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.” Mathayo
5:33-37. “Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape….msije mkaangukia hukumu.”
Yakobo 5:12.
Biblia inakataza kuapa kwa aina yoyote ile, hivyo kama Jesuits wanaapa wanafanya
hivyo kwa sababu wako kinyume na Biblia. Hata hivyo yapo madhehebu mengi yaliyo na
utaratibu wa kuapisha viongozi wao ikiwa ni wachungaji, maaskofu, mapadri kila
wanapowekwa wakfu kwa ajili ya kazi za kanisa husika. Chunguza ndani ya kanisa lako
huenda likawa moja ya wahusika wa viapo.
Sasa tuangalie viapo vya Jesuits. Naomba niweke maelezo haya katika lugha ya
Kingereza maana ndiyo iliyotumika kuandika viapo hivi, naamini kama hujui lugha hii
unaweza kupata mtu wa karibu akakupa tafsiri fasaha.
“When a Jesuit of the minor rank is to be elevated to command, he is conducted into
the Chapel of the Convent of the Order, where there are only three others present, the
principal or Superior standing in front of the altar. On either side stands a monk, one of
whom holds a banner of yellow and white, which are the Papal colors, and the other a
black banner with a dagger and red cross above a skull and crossbones, with the word
INRI, and below them the words IUSTUM, NECAR, REGES, IMPIOUS. The meaning of
which is: It is just to exterminate or annihilate impious or heretical Kings, Governments,
or Rulers. Upon the floor is a red cross at which the postulant or candidate kneels. The
Superior hands him a small black crucifix, which he takes in his left hand and presses to
his heart, and the Superior at the same time presents to him a dagger, which he grasps by
the blade and holds the point against his heart, the Superior still holding it by the hilt,
and thus addresses the postulant:”
Kabla ya viapo, maneno yafuatayo yatasemwa na kiongozi wa ngazi ya juu kwa Jesuits
anayeitwa “Superior”
Superior speaks:
“My son, heretofore you have been taught to act the dissembler: among Roman Catholics to be a
Roman Catholic, and to be a spy even among your own brethren; to believe no man, to trust no
man. Among the Reformers, to be a reformer; among the Huguenots, to be a Huguenot; among
the Calvinists, to be a Calvinist; among other Protestants, generally to be a Protestant, and
obtaining their confidence, to seek even to preach from their pulpits, and to denounce with all the
vehemence in your nature our Holy Religion and the Pope; and even to descend so low as to
become a Jew among Jews, that you might be enabled to gather together all information for the
benefit of your Order as a faithful soldier of the Pope.
Nimefupisha maelezo hayo na baada ya hapo ndipo viapo sasa vinaanza wakati muapaji
akiwa amelala chini kifudifudi:
The Extreme Oath of the Jesuits:
—-“I, _ now, in the presence of Almighty God, the Blessed Virgin Mary, the blessed Michael the
Archangel, the blessed St. John the Baptist, the holy Apostles St. Peter and St. Paul and all the
saints and sacred hosts of heaven, and to you, my ghostly father, the Superior General of the
Society of Jesus, founded by St. Ignatius Loyola in the Pontificate of Paul the Third, and
continued to the present, do by the womb of the virgin, the matrix of God, and the rod of Jesus
Christ, declare and swear, that his holiness the Pope is Christ’s Vice-regent and is the true and
only head of the Catholic or Universal Church throughout the earth; and that by virtue of the keys
of binding and loosing, given to his Holiness by my Savior, Jesus Christ, he hath power to depose
heretical kings, princes, states, commonwealths and governments, all being illegal without his
sacred confirmation and that they may safely be destroyed. Therefore, to the utmost of my power
I shall and will defend this doctrine of his Holiness’ right and custom against all usurpers of the
heretical or Protestant authority whatever, especially the Lutheran of Germany, Holland,
Denmark, Sweden, Norway, and the now pretended authority and churches of England and
Scotland, and branches of the same now established in Ireland and on the Continent of America
and elsewhere; and all adherents in regard that they be usurped and heretical, opposing the sacred
Mother Church of Rome. I do now renounce and disown any allegiance as due to any heretical
king, prince or state named Protestants or Liberals, or obedience to any of the laws, magistrates or
officers.
—–I do further promise and declare, that I will have no opinion or will of my own, or any mental
reservation whatever, even as a corpse or cadaver (perinde ac cadaver), but will unhesitatingly
obey each and every command that I may receive from my superiors in the Militia of the Pope
and of Jesus Christ.
—–That I may go to any part of the world withersoever I may be sent, to the frozen regions of
the North, the burning sands of the desert of Africa, or the jungles of India, to the centers of
civilization of Europe, or to the wild haunts of the barbarous savages of America, without
murmuring or repining, and will be submissive in all things whatsoever communicated to me.
—– I furthermore promise and declare that I will, when opportunity present, make and wage
relentless war, secretly or openly, against all heretics, Protestants and Liberals, as I am directed
to do, to extirpate and exterminate them from the face of the whole earth; and that I will spare
neither age, sex or condition; and that I will hang, waste, boil, flay, strangle and bury alive these
infamous heretics, rip up the stomachs and wombs of their women and crush their infants’ heads
against the walls, in order to annihilate forever their execrable race. That when the same cannot
be done openly, I will secretly use the poisoned cup, the strangulating cord, the steel of the
poniard or the leaden bullet, regardless of the honor, rank, dignity, or authority of the person or
persons, whatever may be their condition in life, either public or private, as I at any time may be
directed so to do by any agent of the Pope or Superior of the Brotherhood of the Holy Faith, of
the Society of Jesus.
Baada ya kumaliza viapo hivyo muapaji anatakiwa kuandika jina lake kwa kutumia kifaa
chakuandikia kilichochovywa damu yake iliyotolewa kifuani upande ulipo moyo wake.
Kisha Superior anauliza maswali yenye majibu kama ifuatavyo:
Question —From whither do you come? Answer — The Holy faith.
Q. —Whom do you serve? A. —The Holy Father at Rome, the Pope, and the Roman Catholic
Church Universal throughout the world.
Q. —Who commands you? A. —The Successor of St. Ignatius Loyola, the founder of the
Society of Jesus or the Soldiers of Jesus Christ.
Q. —Who received you? A. —A venerable man in white hair.
Q. —How? A. —With a naked dagger, I kneeling upon the cross beneath the banners of the Pope
and of our sacred order.
Q. —Did you take an oath? A. —I did, to destroy heretics and their governments and rulers, and
to spare neither age, sex nor condition. To be as a corpse without any opinion or will of my own,
but to implicitly obey my Superiors in all things without hesitation of murmuring.
Q. —Will you do that? A. —I will.
Q. —How do you travel? A. —In the bark of Peter the fisherman.
Q. —Whither do you travel? A. —To the four quarters of the globe.
Q. —For what purpose? A. —To obey the orders of my general and Superiors and execute the
will of the Pope and faithfully fulfill the conditions of my oaths.
Q. —Go ye, then, into all the world and take possession of all lands in the name of the Pope. He
who will not accept him as the Vicar of Jesus and his Vice-regent on earth, let him be accursed
and exterminated.”
The Jesuit Oath of Induction is also recorded in the Congressional Record of the U.S.A. (House
Bill 1523, Contested election case of Eugene C. Bonniwell, against Thos. S. Butler, Feb. 15,
1913, pp. 3215-3216) It can also be found in the book entitled, “Subterranean Rome” by Charles
Didier translated from the French and published in New York in 1843. Dr.
Hivyo ndivyo viapo kwa kifupi vya wanachama wa Jesuits na unaweza pia kuvipata
kwenye mtandao huu: http://www.zenit.org
Ukweli ni kwamba viapo hivyo vinamfanya muapaji awe tayari kuua ikiwa ni kwa siri
au kwa uwazi mtu yeyote atakayekuwa kinyume na kanisa. Tunajua kwamba ulimwengu
wote hatimaye utakuwa chini ya dini na serikali moja kama anavyosema Padre Malachi
Martin wa kanisa Katoliki katika kitabu chake kiitwacho “The Keys of this blood”,
anasema “He is as determined to be world ruler as was Constatine in his day.” p. 49.
Akimaanisha kwamba Papa wa kanisa Katoliki atakuwa kiongozi wa dunia nzima kama
alivyokuwa Constatine wakati wake. Hili pia linathibitishwa na Mungu kama
tunavyosoma kwamba “….akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na
taifa.” Ufunuo 13:7. Wale watakaokataa kutawaliwa na mnyama huyo watakabiliwa na
kifo maana tayari sheria imetungwa katika mahaka ya kimataifa inayoitwa “The Rome
statute of International Criminal Court.”
Hebu tumsikilize mkuu wa shirika la Jesuits anavyosema:
“See, sir, from this Chamber, I govern, not only to Paris, but to China; not only to China,
but to all the world, without anyone knowing how i do it.” (Tamburini, General of the
Jesuits.)
Yeye anasema kwamba “kutoka ndani ya ofisi hii, ninatawala, sio tu hata Paris, bali
hadi China, sio tu hadi China bali katika ulimwengu wote, bila mtu yeyote kujua jinsi
ninavyofanya.”
“In these last days God hath spoken to us by his son Ignatius, (Jesuit founder) whom he
hast appointed Heir of all thing, by whom also he made the world”. – Preached by F.
Doza J.S., “The Firey Jesuits,” p, 66
“Katika siku hizi za mwisho Mungu amezunguza nasi kupitia kwa mwanae Ignatius,
(mwanzilishi wa Jesuits) ambaye amemchakuwa kuwa mrithi wa vitu vyote, ambapo kwa
yeye aliumba ulimwengu”.
“The Grand Rule For an inferiro readily to declare his assent and consent to his
Superiror in active obediance when he says, the snow is black, or the crow is white…we
should always be ready to accept this principal: I will believe that the white that I see is
black, if the hierarchical Church defines it as such.” -The Spirit Exercies of St.
Ignatius, p. 141, -By Ignatius de Loyola.
Naye rais wa Marekani Abraham Lincoln akiwa anakifahamu chama cha Jesuits na
kazi zao alisema kwamba:
“This War (Civil war) would never have been possible without the sinister influence of
the Jesuits. We owe it to popery that we now see our land reddened with the blood of her
noblest sons”…. “The mormon and the Jesuit priests are equally the uncompromising
ENEMIES of our Constitution and our laws; but the more dangerous of the two is the
Jesuit- the romish priest, for he knows better how to conceal his hatred under the mask of
friendship and public deeds for the glory of God…. So many plots have already been
made against my life, that it is a real miracle that they have all failed, when we consider
that the great majority of them were in the hands of the skillful Roman Catholic
murderers, evidently trained by Jesuits. But Can we expect that God will make a
perpetual miracle to save my life? I believe not. ..My escape from their hands, since the
letter of the pope to Jeff Davis has sharpened a million of daggers to pierce my breast,
would be more than a miracle. But just as the Lord heard no murmur from the lips of
Moses when he told him that he had to die, before crossing the Jordan, for the sins of his
people; so i hope and pray that he will hear no murmur from me when i fall for my
nations sake. ..” (Abraham Lincoln)
“Vita hii isingewezekana kuwepo kama isingesababishwa na Jesuits. Tunamdai Papa
sasa kwa kuona ardhi yetu ikienea damu za watu wake…” “Watu jamii ya mormon na
makasisi wa shirika la Jesuit ni maadui wa katiba na sheria zetu; lakini kati ya hao
wawili Jesuits ndio kundi hatari zaidi – kasisi wa rumi, maana anajua vizuri jinsi ya
kuficha chuki yake katika mavazi ya urafiki na kufanya kazi za jamii kwa ajili ya utukufu
wa Mungu….hivyo njama nyingi zimewekwa dhidi ya maisha yangu, ambapo ni muujiza
kwamba wameshindwa, maana tunajua kwamba wengi wao walikuwa miongoni mwa
wauaji wa Roman Catholic waliotumia akili nyingi, bila shaka wakiwa wamefundishwa
na Majesuits. Lakini tutarajie kwamba Mungu ataendelea kufanya muujiza ili kuokoa
maisha yangu? Siamini hivyo…kutoka kwangu mikononi mwao, tangu barua ya papa
kwenda kwa Jeff Davis imenoa makali ya mamilioni ya watesaji ili kupasua kifua changu,
itakuwa zaidi ya muujiza nikitoka mikononi mwao. Lakini kama vile Bwana ambapo
hakusikiliza manung`uniko ya Musa wakati alipomuambia kwamba atakufa kabla ya
kuvuka mto Yordani, kutokana na dhambi za watu wake; ndivyo nilivyo na matumaini na
kuomba kwamba asisikie manung`uniko yangu nitakapoanguka kwa ajili ya taifa langu”.
(Abraham Lincoln)
Yapata mwaka 1865, Abraham Lincoln aliuawa baada ya kuonekana kuwa anapiga
vita vyama vya siri. Katika historia ya taifa la Marekani wapo marais wachache sana
ambao walipinga uwepo wa vyama vya siri mmoja wao alikuwa Abrahm Lincoln. Hata
hivyo wapinzani wa vyama hivi wamekuwa wakikutana na vikwazo na hata kuuawa.
Baada ya kugusia chama cha Jesuits sasa tuendelee na kuwaona Illuminati ambao
chimbuko lao ni Jesuit Society.
Ielewe kwamba unapozungumzia Illuminati, unazungumzia ibada na utawala katika
jamii, kama vile mnyama wa namba 666 anavyojishughulisha na ibada na utawala.
Mmoja wa waumini wa Illuminati mwenye digrii 33 ambaye aliwahi kuwa kiongozi
mkuu wa Illuminati nchini Marekani Dr. Albert Pike, anasema, namnukuu: “Every
Masonic Lodge is a temple of religion, and its teachings are instruction in religion”
(Albert Pike, Morals and Dogma, P. 213.) Kwamba “kila Loji (Jumba au kituo) ya
Freemason ni hekalu la mambo ya dini, na mafundisho yake ni maagizo katika dini.”
Unapoingia kwenye Loji za Freemason utakuta kuna Biblia ya toleo la King James ikiwa
imewekwa juu ya madhabahu (Altare) ya Loji hiyo. Bw. Albert anaendelea kusema
kwamba: “Freemasonry is a search for Light. That search leads us directly back, as you
see, to the Kabalah.” [Albert Pike, Morals and Dogma, p. 741] Kwamba “Kazi ya
Freemason ni kutafuta nuru. Na kutafuta huko kunatufanya, kama unavyoona, tujielekeze
Kabalah.” Katika dini ya Uislamu kuna kitu kinachoitwa الكعبة yaani al-Kabah huko
Mecca Saud Arabia. Illuminati nao wana kitu kinachoitwa Kabalah. Nitaelezea zaidi
katika sura zinazofuata.
Wakati Jesuits wanayaita majumba yao ya kufundishia kwa jina la ‘Convent’ na
wanaojiunga kuitwa ‘Novice’ Illuminati na freemason wanayaita majumba yao ‘Lodge’
na wanaojiunga katika digrii tatu za awali hutumia majengo yanayoitwa ‘Blue Lodge’.
Maana ya Illuminati ni “aliyepewa nuru” au kwa lugha ya kigeni “one who is
illuminated” au “the enlightened ones,” ikimaanisha “mtu aliyepokea nuru au ujuzi
mkubwa.” Umewahi kusikia watu wanaoitwa “Jesuits”? Kama umewahi kuwasikia,
tambua kwamba hao ndio waliomfundisha Adam Weishaupt, ambaye ndiye mwanzilishi
wa The Illuminati. Kwa maana nyingine, Illuminati ni mwanafunzi wa Jesuits.
Baada ya Adam Weishaupt kupata elimu yake kutoka kwa Jesuits, mwaka 1785
serikali ya Bavaria ikafunua mpango wa Weishaupt wa kuangamiza Ukristo na kutawala
serikali zote duniani. Mpango huo ulipingwa vikali na serikali ya Bavaria na kulifukuza
kundi la Illuminati nchini humo. Hata hivyo huu haukuwa mwisho wa Illuminati, kama
wanahistoria wengi walivyoandika. Mipango ya Weishaupt ilichukuliwa na
kushughulikiwa kama mapinduzi yaliyo hatari katika nchi ya Ujerumani (Bavaria) peke
yake. Lakini kuna mataifa mengi ambayo Illuminati walikuwa wanafanya kazi na hivyo
serikali za mataifa hayo hazikujali tahadhari ya serikali ya Bavaria kuhusu Illuminati.
Baada ya miaka michache mpango wa kuangamiza Ukristo na kisha kutawala serikali
zote ulionekana kwa mara ya kwanza wakati wa mapinduzi ya Ufaransa. Nguvu kama
hiyo ya mapinduzi ilionekana tena huko Ujerumani ikiitwa “The Legue of the Just”
kukiwa na matawi yake huko London, Brusses, Paris na Switzerland. Wakati Napoleon
alipoingia madarakani, hakuvumilia vitendo vya Jacobin Clubs vilivyokuwa chini ya
Illuminati hivyo akavifutilia mbali. Hata hivyo Illuminati waliendelea kufanya kazi kwa
jina lingine. Walifanya kazi kwa jina la “The Legue of the Just” ambapo “Karl Marx”
alikuwa mfuasi. Alipewa kazi ya kurudia kwa kuandika kwa kina kile kilichoandikwa na
Adam Weishaupt miaka sabini iliyopita.
Weishaupt alikufa mwaka 1830, lakini mipango yake ya mapinduzi iliendelezwa na
wafuasi wake ambao hadi leo wako kwenye hatua za mwisho za kukamilisha mipango
hiyo ya kuhakikisha kwamba dunia yote inarudia imani ya kipagani na kumuabudu
shetani.
Mwaka 1842 Karl Marx alianza kuandika propaganda za mapinduzi kwa ajili ya
“League of the Just”, akitumaini kusababisha machafuko. Mwaka 1844, akishirikiana na
Friedrich Engels, wakiwa chini ya usimamizi wa “The League of the Just”, Marx alianza
kuandika “Manifest der Kommunistichen Partei,” kinachojulikana kama “The Communist
Manifesto,” yaani “Ilani ya Ukomunist” iliyotolewa mwanzoni mwa mwaka 1848.
Baadaye, Illuminati wakiwa wanafanya kazi chini ya “The League of the Just,”
walibadilisha jina lao na kuitwa “The League of Communists”.
Wakomunist husherehekea May Mosi ikiwa ni kuzaliwa kwa harakati za mapinduzi
yao kwa sababu ilikuwa ni tarehe ya kuanzishwa kwa Illuminati iliyoanzishwa na Adam
Weishaupt. Wasomi wengi wanajua kwamba Ukomunist ni dhana ambayo haikubali
uwepo wa Mungu kama Biblia inavyoelezea. Vivyo hivyo Illuminati ni wapinzani
wakubwa wa Biblia maana wanatumiwa na Shetani ambaye ni adui wa Mungu na watu
wake. Na sio kwa kubahatisha kwamba Wakomunist wote hutumia umbo la pentagram
(umbo la nyota yenye pembe tano) kama moja ya nembo yao. Pia sio kwa kubahatisha
kwamba Wakomunist hutumia neno RED katika kuelezea harakati za mapinduzi yao.
Familia ya “The Rothschild international banking” ambayo kwa takribani miaka 200
imekuwa na mafanikio huko Ulaya katika nyanja za uchumi na siasa, ilianzishwa na
Mayer Amschel Rothschild mnamo Feb. 23, 1744 huko Frankfurt Ujerumani. Alikuwa na
watoto watano na jina la familia lilitokana na RED SHIELD.
Ni Adam Weishaupt pamoja na familia ya “the House of Rothschild” ndio
walioanzisha harakati hizi kwa sehemu zikiwa za kidini na kwa sehemu zikiwa ni za
kisiasa kama zilivyotabiriwa katika unabii wa Yohana kuwa ni mnyama mwekundu sana
atakayetoka katika shimo la kuzimu (yaani umizimu) Ufunuo 17:3,8.
Inaaminiwa kwamba Illuminati ni sehemu ya Freemason. Hawa Freemason, ambao ni
Illuminati, walichukua imani yao kutoka kwa “The Knights Templar”. “The Knights
Templar” kilikuwa ni kikosi cha kidini ambapo wafuasi wake walipata kuwa matajiri
wakubwa kutokana ka kupewa ardhi na zawadi kutoka kwa wafalme wa nchi za Ulaya.
Kufikia miaka ya 1300 kikosi hiki cha Templars kilijiita kuwa ndio wamiliki wa Benki
za Ulaya kutokana na utajiri mkubwa waliokuwa nao. Walikuwa na ndoto za kuwa
matajiri wakubwa kiasi cha kuununua ulimwengu. Mfalme wa Ufaransa na Papa
walianzisha msako wa kuwakamata The Knights Templar lakini Papa akawa na mashaka
kutokana na jinsi mfalme alivyokuwa anaendesha msako ndipo Papa akaendelea kufanya
msako bila kushirikiana na mfalme. Wakati wa msako huu kikosi hiki cha Templars
kikaungama kosa lao kwa Papa na kujifanya kuwa Templars sasa wamekuwa Wakristo
huku wafuasi wake wakificha imani yao ya kumuabudu Lucifa kama mungu wao.
Papa akawa amefanikiwa kukikomesha kikosi hiki lakini hakuwa amekikomesha kabisa
kwani hatimaye kiligeuka na kuwa Freemason huku jamii ikiwa inawaona Freemason
kuwa ni chama kizuri chenye malengo mazuri tu. ni kwa njia hii Adam Weishaupt
aliyekuwa mwanachama wa Freemason alifanikiwa kuanzisha imani ya chama cha siri
cha Illuminati ndani ya chama cha siri cha Freemason.
Freemason ni chama cha siri ambacho kipo hata leo kikiwa kinafanya kazi kwa kisingizio
cha kuleta usawa na amani kwa watu wote.
Kuna mtazamo mwingine kuhusu Illuminati, kwamba mwanzo wao unaanzia miaka
4000 iliyopita huko Mesopotamia, katika zama za kipindi cha Sumeria. Mfalme
aliyekuwa mtawala kipindi hicho aliitwa mfalme Uru-Nammu. Habari za Uru
zinapatikana pia ndani ya Biblia wakati wa utawala wa Babeli ikiwa ni Ur ya wakaldayo.
Lakini zaidi Freemason wakiwa ni waabudu Shetani, tunaweza kupata chimbuko lao
muda mrefu sana tangu wakati wa Habili na Kaini ambapo Kaini alimuasi Mungu.
Mafundisho ya Illuminati yana mchanganyiko wa siri za Mason (Masonic secrets)
yaani (Luciferian Doctrines), Islamic mysticism (Sufism), na Jesuit mental discipline
(Hatha Yoga). Nitaelezea zaidi kuhusu Freemason katika sura za mbele.
Luciferian wao wanaunda makundi ya Freemason maana wao wanakubali moja kwa
moja kwamba wanamwabudu Shetani. Islamic mysticism ni imani ambayo imo ndani ya
dini ya kiislamu, kihindu, budha, nk lakini ikiwa inatokana na imani ya Illuminati, hivyo
waislamu, wahindu na wabudha wengi wametekwa bila kujua na hivyo wanamwabudu
Lucifer pasipo kujua. Jesuit mental displine, yaani Hatha Yoga, ni mbinu ya Illuminati
inayotumiwa katika madhehebu ya Kikristo na kuwafanya waumini wao kumwabudu
shetani pasipo kujua, na hivyo wote wanajikuta wakiwa kinyume na Mungu wa
mbinguni. Kumbuka kwamba Shetani anatumia wakala anayeitwa Mnyama wa namba
666 maana mnyama huyo alipewa kiti cha enzi cha Shetani (Ufunuo 12:9; 13:2). Lakini
sasa tunaona pia mnyama huyo naye akitumia mawakala wake ambao wanaitwa
Illuminati. Tutaona pia kuwa Illuminati nao wanatumia mawakala wanaoitwa Freemason
na vyama vingine vya siri pamoja na taasisi kubwa zisizo za siri. Kwa ujumla, Illuminati
wanatumia mbinu ya “Divide and Rule” iliyotumiwa wakati wa ukoloni katika kulitawala
bara la Africa.
Kwa nje Illuminati wanajionyesha kuwa na nia ya kuifanya jamii iwe nzuri na safi
lakini kwa ndani lengo lao kubwa ni kujikweza na hatimaye kuweza kuitawala jamii yote
ya ulimwengu. Wafuasi wa Islamic mysticism (Sufism) wanaamini kwamba wao wako
kwenye safari ya kiroho kwenda kwa Mungu na kwamba inawezekana kuwa karibu sana
na Mungu wakati mtu akiwa hai – hapa kuwa karibu na Mungu wanamaanisha
kumsogelea Mungu kimwili na sio kimaadili – Katika imani ya Sufism, mtu akiwa katika
hali ya utambuzi – mawazo, hisia, mitazamo nk, wanaamini kwamba yote yanatoka kwa
mungu au ni zawadi kutoka kwa mungu. Rejea Septemba 11 kule World Trade Center,
waendesha ndege zilizogonga yale majengo marefu walikuwa na imani ya Sufism.
Sufis wanaamini kwamba wao wanajitahidi kuwa mungu na mungu anajitahidi kuwa
wao, yaani wanajitahidi kufanana na shetani na shetani anajitahidi kufanana na wao, na
hivyo siku moja watakutana na kufikia utimilifu wa kufanana wote. Lakini pia Illuminati
katika imani ya Jesuit mental displine (Hatha Yoga) wanajitahidi kuwafanya watu wa
imani ya Kikristo kuamini kwamba kwa juhudi zao wenyewe wanaweza kufikia
ukamilifu wa kufanana na Mungu. Hapa bwana J.D Buck, katika kitabu chake kiitwacho
Mystic Masonry anasema: “It is far more important that men should strive to become
Christs than that they should believe that Jesus was Christ…all men may reach the same
Divine perfection.” – J.D. Buck, Mystic Masonry.
“Ni muhimu kwamba watu wanapashwa kujitahidi kuwa Wakristo kuliko kuamini
kwamba Yesu alikuwa ni Kristo….watu wote wanaweza kufikia ukamilifu ule ule wa
kimbingu.” – J.D. Buck, Mystic Masonry. Ndio maana katika dini ya Waislamu utakutana
na mafundisho mengi sana yanayomshambulia Yesu na kumshusha hadhi aliyonayo –
hiyo inatokana na The Illuminati Doctrines katika imani ya Islamic mysticism (Sufism).
Hata hivyo Biblia inatuambia vizuri kwamba hiyo ilikuwa roho na nia ya Lucifer
aliposema kwamba: “…Nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti changu juu kuliko
nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za
Kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye Juu.” Isaya
14:13. Lucifer aliapa kukiweka kiti chake juu na hatimaye kufanana na Aliye juu – yaani
Mungu. Maana ya mlima wa mkutano ni kanisa la Mungu. Kama umo ndani ya kanisa
linalojiita kuwa ni kanisa la Mungu – najua kwamba makanisa yote yanajiita kuwa ni
makanisa ya Mungu – sasa muelewe kwamba Lucifer aliapa kuketi juu ya mlima wa
mkutano. Kuhusu Pande za Kaskazini katika unabii Kaskazini ni upande wa mlima
Sayuni – yaani upande wa kanisa la Mungu; Soma Zaburi 48:2 “Kuinuka kwake ni mzuri
sana, Ni furaha ya dunia yote, Mlima Sayuni pande za Kaskazini, Mji wa Mfalme Mkuu.”
Hivyo shetani amefanikiwa kuuteka ulimwengu wa kiroho kwa kutumia mnyama wa
namba 666 na Illuminati katika Islamic mysticism, na Jesuit mental displine – yaani
Hatha Yoga.
Illuminati na taifa la Marekani:
Tutaanza kuangalia muhuri wa taifa la Marekani na alama zilizotumika kutengeneza
muhuri huo unaoonekana kwenye noti ya dola moja ya Marekani. Unapotazama dola
moja ya marekani utakuta kuna alama ya Piramidi upande mmoja na alama ya tai upande
wa pili. Kama hujawahi kuona noti hiyo unaweza kuangalia kwenye picha hapa chini.
“Our beautiful seal is an expression of Freemasonry, an expression of occult ideas.”
(Wyckoff, H. S. The Great American Seal. The Mystic Light, the Rosicrucian Magazine,
p.56).
Maelezo hayo yanajitosheleza kutuonyesha kwamba alama zilizotumika kubuni
muhuri huo wa marekani zinatokana na Freemason.
Noti ya Dola Moja ya Marekani.
Piramidi likiwa na jicho. Tai akiwa amevalishwa bendera ya Marekani
Hapa ndipo penye nguvu ya Illuminati. Katika dola moja ya Marekani ndipo tunakuta
kile kinachoitwa “Great Seal of The United States of America”. Kuna vitu vingi
vinavyoelezea jinsi Illuminati walivyohusika katika ubunifu wa muhuri huo wa taifa
lenye nguvu kubwa duniani. Ubunifu huo wal iupata kutoka kwa mungu
wanayemwabudu. Mungu huyo anaitwa GAOTU – Great Architect Of The Universe.
Yeye ndiye mwenye jicho katika Piramidi lililoko kwenye muhuri huo na kwenye dola
moja ya Marekani. Wabunifu wa muhuri huu walikuwa ni watu sita ikiwa ni ishara ya
kwamba walikuwa chini ya utawala wa Shetani maana namba sita kama tulivyoona
hutumiwa na Shetani ikimaanisha utawala wa Shetani. Watu hao walikuwa kama
ifuatavyo: 1) Benjamin Frankline, 2) John Adams, 3) Tomas Jeffeson, 4) Francis
Hopkinson, 5) Charles Thomson ambaye alibuni pia bendera ya Marekani, na 6)William
Burton. Kwa maelezo zaidi soma kitabu kiitwachwo “Illuminati 666” Uk. 232-234.
Hebu tuchunguze kwa makini kila tunachoweza kukiona kwenye muhuri huo. Tuanze
na Piramidi………
Katika Piramidi iliyopo kwenye dola moja ya Marekani chini kabisa utakuta maneno
haya: MDCCLXXVI na kisha kuanza kozi za tofali hadi kozi 33 ikimaanisha degree ya
juu kabisa ya Illuminati. Kwa nini ziwepo degree 33? Swali hili litajibiwa kwa undani
katika sura zinazofuata mbele.
Wengi wamekuwa wakitafsiri maneno MDCCLXXVI kuwa ni mwaka 1776 ambapo
Marekani ilipata uhuru wake, lakini ukweli ni kwamba yana maana ya May 1, 1776,
tarehe ya kuanzishwa kwa Illuminati. Pia kwenye Piramidi lililoko kwenye dola moja ya
kimarekani kuna maneno “Annuit Coeptis” juu ya piramidi yakimaanisha “Our enterprise
(conspiracy) has been crowned with success” yaani “njama zetu zimepata mafanikio”. Na
chini kabisa ya piramidi kuna maneno “Novus Ordo Seclorum” yakielezea asili na lengo
la njama hizo “new order of the ages” yaani “mpango mpya wa vizazi”. Sasa ukiyaweka
pamoja maneno hayo yanamaanisha kwamba Illuminati “wanatangaza Kuzaliwa kwa
mpango mpya wa kipagani”. Kwa mujibu wa kitengo cha hazina cha serikali ya Marekani
tamko lililotolewa August 15, 1953, ambapo kulitolewa maana halisi ya alama
zilizowekwa nyuma ya dola moja: “Jicho na umbo la pembe tatu lilimaanisha mungu
aonaye yote. Piramidi ni alama ya kuwa na nguvu na uwezo na kwa vile piramidi hilo
linaonekana kutokukamilika, ina maana kwamba kuna kazi bado ya kufanywa.” “Mungu
aliyetajwa hapo ni mungu wa Misri na anaitwa Horus ambaye jicho lake kamwe
halifumbwi wala halisinzii.”
Kwa upande mwingine tunamkuta Tai akiwa ameshikilia vitu miguuni mwake. Kwenye
mguu wa kulia (Right Talon) Tai huyo amebeba tawi lenye majani kumi na tatu (13)
yenye matunda ya mizeituni (Berries) kumi na tatu (13). Maana ya namba 13
inawakilisha familia kumi na tatu za Illuminati (Illuminati bloodline) na maana ya
matunda ni jinsi taifa la Marekani linavyotoa misaada ya hali na mali duniani, maana ya
majani ni jinsi Marekani inavyojishughulisha na kutafuta kile kinachoitwa amani duniani.
Inadaiwa kwamba Marekani ndiyo inayoongoza katika kutoa misaada kwa wakimbizi
kwenye shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa – UNHCR. Inashangaza kwamba hata
nembo ya UN na UNHCR ina tawi lenye majani kumi na tatu kama lile aliloshikilia Tai
anayewakilisha Marekani. Juu ya kichwa cha Tai kuna nyota kumi na tatu (13) ambazo
zinatengeneza umbo lenye pembe sita (6) ‘hexagon’. Hapa namba 6 inawakilisha alama
ya utawala wa Illuminati na mnyama wa namba 666 ikiwa ni idadi ya waliohusika kubuni
muhuri huo wa Marekani. Katika mguu wa kushoto Tai huyo amebeba mishale kumi na
tatu (13). Mishale kumi na tatu maana yake ni kwamba familia hizo kumi na tatu za
Illuminati ambazo ndizo zinazotawala Marekani ziko tayari kufanya vita na taifa lolote
lile linalotishia amani (majani 13) duniani. Taifa hilo litakuwa tayari kufanya vita kwa
jinsi ya Tai arukaye na kushambulia popote duniani.
Kwa hatua hii, inatupasa kuchunguza njama zinazotumika katika matukio duniani.
Ukweli ni kwamba watu wengi wanadhihaki juu ya matukio kama hayo. Hata hivyo
napenda niwakumbushe wasomaji ukweli huu:
I) Biblia inaelezea wazi kwamba Shetani amekuwa mpinzani wa Mungu tangu mwanzo
wa historia ya ulimwengu huu akijaribu kuutawala ulimwengu kutoka mikononi mwa
Mungu. Wote wawili, Shetani na Mungu hutenda kazi kwa kutumia mawakala ambao ni
binadamu ili watawale dunia hii. Tunaona hali kama hii katika kitabu cha Danieli 10
wakati Danieli alipokuwa akiomba kwa muda wa siku ishirini na moja katika ombi
lililopata majibu. Wakati malaika wa Mungu alipomwendea Danieli, alimwambia Danieli
kwamba Mungu alikuwa amesikia ombi lake na kujibu tangu siku ya kwanza alipoanza
kuomba na alimtuma malaika huyo ili aende kumpa jibu. Hata hivyo, malaika huyo
alicheleweshwa na mapepo wa shetani ambao walikuwa wanapigana na malaika wa
Mungu. Vita hiyo ilikuwa kwa ajili ya nini? Ilikuwa ni kwa ajili ya kuona ni nani haswa
anayewatawala wafalme wa dunia hii, maana wao ndio wanaofanya maamuzi kila siku
ambayo yataadhiri historia ya mwanadamu. Biblia inafundisha juu ya njama za Shetani
na wafuasi wake hapa duniani dhidi ya Mungu na watakatifu Wake.
2) Mwanahistoria aitwaye Edward Gibbons aliandika katika kitabu chake kiitwacho “The
History of the Decline and Fall of the Roman Empire”, kwamba sababu kubwa
iliyosababisha kuanguka kwa dola ya Rumi iliyotawala takribani miaka 1200 ilikuwa ni
njama za siri ndani ya serikali yenyewe. Wakati huo huo waliofanya njama hizo
walikuwa wakifanya kazi ya kujiangamiza wao wenyewe, walifanikiwa kuwadanganya
wakazi katika Dola hiyo. Mtu yeyote asiyejifunza historia yuko tayari kuirudia, kwa hiyo
tunapaswa kuamka na kuwa na tahadhari ya njama zinazotukabili za mpango mpya wa
ulimwengu (NWO) kutoka kwa Illuminati.
Illuminati na Freemason walifanikiwa kubuni ramani ya jiji la Washington DC huko
marekani katika maumbo ya Freemason. Hapa chini ni picha ya ramani ya jiji la
Washington DC ikiwa na umbo la Pentagram linalotumiwa na waabudu wa Shetani ikiwa
ni sharti ya kupata nguvu kutoka kwa Shetani..
JIJI la Washington DC Jiji la Washington DC.
Ramani ya jiji la Washington ambayo ni makao makuu ya Marekani ikiwa imebuniwa
katika mtindo wa umbo la Pentagram ambalo ni umbo la kishetani pamoja na umbo la
Piramidi. Maeneo muhimu ya jiji la Washington, kama White House, US Capitol,
sanamu za makumbusho ya marais wa Marekani yalibuniwa na Freemasons na kujengwa
katika mitindo ya Freemason. Utakumbuka pia kwamba makao makuu ya wizara ya
ulinzi yamejengwa katika muundo wa pembe tano (Pentagon) ikiwa ni kwa ajili ya
matumizi ya namba tano katika Freemason. Je, nini maana ya umbo hilo? Jibu
litapatikana kwenye sura inayofuata katika kipengele cha ishara za vidole viwili na vidole
vitatu.
Malengo ya Illuminati ni yapi?
Katika kitabu chake kiitwacho “The broken Cross” Bw. Peirs Compton ambaye ni
kasisi wa kanisa Katoliki na aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la “The Universe” la kanisa
Katoliki, anasema kwamba: “The Illuminati had …a plan …they decided on a most
ambitious line of conduct. It would form and control public opinion. It would
amalgamate religions by dissolving all the differences of belief and ritual that had kept
them apart; and it would take over the Papacy and place an agent of its own in the
Chair of Peter.” (“The Broken Cross”, by Peirs Compton, 1981. p. 7-8)
Lengo kubwa la Illuminati ni kuhakikisha kwamba wanafutilia mbali imani za dini
zote, kutawala mawazo ya watu, na kisha wanakalia kiti cha Petro huko St. Peters
Vatican. Mipango hiyo iliandaliwa tangu mwaka 1776 wakati mwanzilishi wa Illuminati
Adam Weishaupt alipopata ufadhili wa fedha kutoka taasisi za kifedha zinazotawaliwa na
familia ya Kifreemason ya Rothschilds.
Baadae mtu mmoja ambaye alikuwa muumini wa Illuminati bw. Nubius, mwaka 1818
aliandika akiwa anaelezea malengo ya Illuminati kwamba ni kuhakikisha wanatawala
katika dini zote ulimwenguni. Hata hivyo Biblia inatuambia kwamba hilo limekuwa ni
lengo la Shetani tangu mwanzo maana alisema kwamba, “…Nitapanda mpaka mbinguni,
nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa
mkutano, Katika pande za mwisho za Kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana na yeye Aliye Juu.” Isaya 14:13. Compton anamnukuu Nubius akisema
kwamba:
“The Papacy has been for seventeen hundred years interwoven with the history of
Italy. Italy can neither breathe nor move without the leave of the Supreme Pontiff…It is
necessary to seek a remedy. Very well, a remedy is at hand. The Pope…will never enter
into a secret society. It therefore becomes the duty of the secret societies to make the first
advance to the Church and the Pope, with the object of conquering both.” Peirs
Compton, The Broken Cross p. 13.)
Illuminati walijua kwamba watakapofanikiwa kutawala katika kanisa la Roma itawawia
rahisi kutawala katika dini zote wakiwa wanatokea Vatican. Lakini pia Illuminati walijua
kwamba Papa hawezi kujiingiza kwenye vyama vya siri na hivyo wakawa na lengo la
wao kuingia kwenye kanisa na kwa Papa wakikusudia kuwatawala wote, kanisa na Papa.
Ni kwa jinsi gani Weishaupt alifanikiwa kupata fedha kutoka kwa Benki iliyo chini ya
Rothschilds (House of Rothchilds)? Compton anaelezea kwamba “He (Weishaupt) was
backed financially,…by a group of bankers under the House of Rothschild. It was under
their direction that the long-range and worldwide plans of the Illuminati were drawn
up…” p. 8-9.
Hivyo ikaandaliwa mipango ya muda mrefu (long term and worldwide plans) kwa ajili
ya kufanikisha malengo ya Illuminati katika kile kinachoitwa ‘New World Order’.
Katika kutekeleza mipango yao, Illuminati walibuni matumizi ya namba, ishara na
maumbo katika kutoa amri zao. Ishara hizo zinatokana na nguvu za Shetani. Bwana
Compton anasema:
“By symbols…is a man guided and commanded…The Illuminati made use of … a
pyramid, or triangle, which has been long known to initiates as a sign of mystic or solar
faith. At the top of that pyramid, or sometimes at its base, was, and in fact, still is, the
image of a separate human Eye, which has been variously referred to as the open eye of
Lucifer…or the eternal watcher of the world and the human scene.”
“The pyramid was one of the symbols that represented the unknown and nameless deity in
pre-Christian cults. Centuries later, it was resurrected as a symbol of the destruction of
the Catholic Church; and when the first phase of that destruction had been brought
about…by those who had infiltrated and since occupied some of the highest places in the
Church, they reproduced it as a sign of their success.”
Kisha Compton anatustua kwa kutufunulia siri hii:
“It (this All-Seeing Eye) overlooked the crowds who gathered for the Philadelphia
Eucharistic Congress in 1976. It was taken up by the Jesuits who edited the Society’s
year book; and it appeared on a series of Vatican stamps issued in 1978.” (p. 10-11).
Compton more specifically identifies the true meaning of this All-Seeing Eye:
“The Eye, which can be traced back to the Babylonian moon worshippers, or astrologers,
came to represent the [Pagan] Egyptian Trinity of Osiris, the sun; Isis, the moon
goddess; and their child, Horus…” (p. 11-12).
Compton anaelezea kwamba Illuminati hutumia ishara na alama katika kuamrisha
watu, na ndio maana walianzisha matumizi ya Piramidi au pembe tatu ambapo juu ya
Piramidi hilo kuna jicho lenye maana ya utatu wa miungu wa Misri wanaoitwa Osiris
(mungu jua baba), Isis (mungu mwezi mama) na Hurus (mungu mwana). Kumbuka
kwamba Shetani huigiza kutoka kwa Mungu na kisha kupotosha maana halisi
iliyokusudiwa na Mungu. Shetani hana uwezo wa kuumba wala kutengeneza kitu kipya
tofauti na alichoumba Mungu. Katika kuhakikisha kwamba Illuminati wanatawala dini
zote, walifanikiwa kuingiza matumizi ya maumbo na namba ndani ya dini mbalimbali
ikiwa ni pamoja na matumizi ya alama ya jua, alama ya nusu mwezi, alama za ndimi za
moto nk. Nitaelezea kwa undani zaidi dini ambazo zimeathiriwa na Illuminati katika
matumizi ya maumbo.
Compton anasema kwamba “By mid-1800’s, the State of Italy had been taken over by the
Illuminati” (Compton, The Broken Cross, p. 17). But, still, the religious office of the
Papacy was outside their control.
Kwamba “kufikia miaka ya katikati ya 1800, taifa la Italia lilikuwa tayari limetekwa na
Illuminati” (Compton, The Broken Cross, p. 17). Hata hivyo ofisi ya Papa ilikuwa nje ya
utawala wao.
Compton anasema kwamba “by 1960s the liberals or progressives, secure in having
brought the designs of the secret societies to a successful conclusion, were exultant…The
entire world of religion was now permeated by its influence…” (Compton, The Broken
Cross, p. 62)
Kwamba kufikia miaka ya 1960 tayari Illuminati walikuwa wamejiingiza katika dini zote
ulimwenguni. Hili linathibitishwa na ziara ya Papa Paul VI kwenye umoja wa mataifa
(UN) Oktoba 4, 1965 alipohutubia mbele ya viongozi wa dini kubwa sita ulimwenguni
ambazo ni Buddhism, Hinduism, Islam, Judaism, Confucianism, na Wakristo. Compton
anasema kwamba hotuba hiyo ilifanyika ndani ya chumba maalumu kwa ajili ya ibada za
Illuminati kwenye jengo la Umoja wa mataifa, namnukuu: “This [meditation] room was
a centre of the Illuminati, given over to the Cult of the All-Seeing Eye that under a
system of allegories and veiled secrets…was dedicated to the service of pagan cults, and
the obliteration of Christian in favour of humanistic beliefs.” (Compton, The Broken
Cross, p.68-69).
Je, Compton anakubalika kwa kipimo cha unabii wa Biblia? Ndio, katika kitabu cha
Ufunuo 17 tunasoma kuhusu mnyama ambaye yu tayari kupanda kutoka kuzimu akiwa
amembeba mwanamke. Jambo muhimu ni kwamba wakati Yohana anaonyeshwa njozi
hii alipelekwa jangwani ndipo akamuona mnyama huyu. Jangwani ni mahali pa shida
ikimaanisha kipindi kigumu. Historia inatuambia kwamba kanisa la Roma limekuwa
jangwani tangu mwaka 1798 wakati Papa Pius VI alipokamatwa na jenerali Bethier wa
Ufaransa na kisha kufia huko na kuonekana kana kwamba mwisho wa kanisa hilo
ulikuwa umefika. Sasa mwaka 1929 ndipo kanisa likarudishiwa tena utawala wake wa
kikanisa na hivyo kuanza kuwa na vichwa, yaani viongozi na hadi sasa wamefika mapapa
saba tangu mwaka 1929. Tumekwisha kuonyesha kwamba mnyam huyo ni utawala wa
Illuminati na kwa kuwa Yohana alimuona mnyama huyo akiwa amembeba mwanamke
(kanisa)—ikimaanisha muungano wa Illuminati na kanisa, Yohana anatudhihirishia
kwamba tangu mwaka 1929 tayari Illuminati walikuwa wameungana na kanisa. Hivyo
Compton kwa kusema kwamba kufikia miaka ya 1960 tayari Illuminati walikuwa
wameuteka ulimwengu wa dini, ni wazi kwamba Compton yuko sahihi kwa kipimo cha
Biblia.
Huo ukawa mwanzo wa ujenzi wa hekalu linaloitwa “Temple of Understanding”
lililojengwa kwenye hekari 50 huko Potomac Washington. Malengo ya ujenzi wa hekalu
hilo yalionekana kuwa ni ibada za Illuminati kutokana na idadi ya madhehebu
yaliyohudhuria kwenye mkutano huo. Idadi ya madhehebu hayo ilikuwa ni sita ambayo
ni Buddhism, Hinduism, Islam, Judaism, Confucianism na Wakristo. Kumbuka kwamba
namba sita hutumiwa na Illuminati kuwakilisha utawala wao. Nitaelezea kwa kina
kuhusu matumizi ya namba na maana zake.
Uzinduzi huo uliofanywa na Papa Paulo VI ukawa ni tangazo rasmi la kuanzishwa kwa
dini moja kutokana na mipango ya Illuminati iliyoanzishwa mwaka 1776 kwa jina la
New World Order. Hivyo basi kile tunachokiona leo katika ulimwengu wa dini, siasa,
uchumi, utamaduni nk ni matokeo ya mipango ya Illuminati ya kutaka kutawala
ulimwengu wote.
Siku chache baada ya Papa Paul VI kurudi Vatican kutoka Marekani kwenye Umoja wa
Mataifa, askofu Mendes Arceo wa Cuernavaca alisema kwamba itikadi za Carl Max ni za
muhimu kwa ajili ya ufalme wa Mungu, wakati huo Papa Paul VI akasema kwamba
Roma ilikuwa tayari kuweka msimamo mpya kuhusu vyama vya siri. Compton anasema:
“Within a few days of Paul’s return to Rome, the Bishop of Cuernavaca, Mendes Arceo,
was declaring that ‘Marxism is necessary in order to realize God’s kingdom at the
present time'; while Pope Paul let it be known that Rome…was ready to take a new look
at secret societies.” (Peirs Compton, The Broken Cross, p.72)
Katika harakati za mipango ya Illuminati ya kutawala dunia, chama hicho cha siri
kilianzisha taasisi nyingi ambazo hadi leo zinafanya kazi duniani kote. Lifuatalo ni
jedwali la utawala wa Illuminati likiwa na nguzo sita. Namba sita hutumiwa na Illuminati
kuashiria utawala wao.
Ili kufanikiwa katika malengo yao ya kuitawala dunia kupitia Dini, uchumi, siasa na
Ajira/kazi, Illuminati walifanikiwa kuanzisha taasisi za Kidini, kiuchumi, kisiasa na kazi
na ajira, zote hizo zikiwa zinafanya kazi kwa mwongozo wa Illuminati. Katika taasisi za
kidini tunakuta Baraza la Umoja wa makanisa ulimwenguni (World Council of Churches)
ambalo lilianzishwa na Illuminati kwa makusudi ya kuunganisha dini zote za Kikristo na
kutengeneza “Mnara wa Babeli” wa kiroho. Tayari kuna makanisa mengi ambayo
yamejiunga kwenye umoja huo. Wengi hawajui kama umoja huo uko chini ya chama cha
siri cha Illuminati ambacho kina siri kubwa sana katika kutawala dini na dunia kwa
ujumla. Ukitaka kujua kama kanisa lako ni mwanachama wa Baraza hilo unaweza
kutembelea mtandao wa Baraza hilo kwenye http//www.wcc-coe.org/.
Ieleweke kwamba WCC ina vitengo kama Christian World Communion, Global
Christian Forum, nk. ambapo kanisa linaweza lisiwe member wa WCC moja kwa moja
ila likawa member wa vitengo vilivyo chini ya WCC.
Siri ambazo Illuminati/Freemason hawataki zifahamike kwa watu
Kuna siri muhimu ambazo Freemason na Illuminati hawataki zifahamike kwa watu. Siri
hizo ni:
– Viongozi wa dini wamefanikiwa kuwatawala mamilioni ya wanaume na
wanawake, ambao wamekuwa wakifundishwa tangu utoto wao, kwamba viongozi
hao ni wajumbe kutoka kwa Mungu.
– Leo viongozi hao wamezungukwa na mamia ya alama na mavazi ya Freemason
kama vile pete, kofia nk kiasi kwamba watu wengi hawajui hilo.
– Illuminati wanaamini kwamba kuna zaidi ya Mwokozi mmoja aliyesulubiwa.
Kwamba wapo zaidi ya ishirini.
– Illuminati wanaamini kwamba Yesu alifundishwa na waalimu kutoka Misri.
– Kisha Yesu akawa “jua” na wale wanafunzi wake kumi na wawili wakawa ndio
ishara kumi na mbili zinazotumiwa na Freemason zinazozojulikana kama Zodiac
– Mbingu zinasemekana kuwa ziko “juu” hata hivyo kutokana na mzunguko wa
dunia (rotation of the Earth) juu na chini hubadilishana mahali pake.
– Wanaoingia kwenye vyama hivi vya siri huanza kupanda ngazi (uti wa mgongo)
hadi juu kwenye kilele cha mlima (ubongo), wakiwa wanapitia kwenye shimo
lililoko sakafuni. Mahali hapo ndipo palipo na hekima (wisdom).
– Utatu (trinity au triune) katika mwanadamu ni moyo, ubongo, na viungo vya siri –
kila kimoja kimepewa kiwakilishi cha alama katika degree tatu za kwanza za
Freemason. Moyo na ubongo huitwa Kaini na Habili. Vyote viwili vinawajibika
kuleta usawa kamili (total equilibrium).
– Mti uitwao Pine wenye majani yenye ncha kama sindano ni sawa na mkia wa
nyoka wenye kitu kama kidole kinachoitwa mkuki mtakatifu. Hiki ndicho
kinachounganisha mambo ya zamani na yaliyopo (old and present)
– Uti wa mgongo ni sawa na nguzo yenye ngazi 33 ambazo wakati mwingine
huitwa nyoka au wachawi. Hii ndio fimbo ya Her-me ikiwa imezungukwa na
nyoka wawili, mmoja mweusi mwingine mweupe. Na ndio maana ya degree 33 za
Freemason.
– Kiungo kati ya ubongo na viungo vya siri mwilini kinatokana na uti wa mgongo
ambao ndicho kiungo chao – yaani ubongo na viungo vya siri huunganishwa na
uti wa mgongo wenye ngazi 33.
– Freemason wanafundisha kwamba mtawala wao ambaye wanamwita mungu
anajulikana kwa watu wote kama “Mimi niko”
– Freemason wa kiwango cha juu kabisa wanaamini kwamba watu wengi ni wazito
kama mawe, wakiwa wanafaa kutumiwa kwenye ujenzi kama matofali, uzito wao
unatokana na ugumu wao wa kuamini kwamba maana halisi ya maisha ni kuwa
na nguvu za kutoa uhai ulimwengunin (giving life in the world).
– Ini (Liver) ndio ufunguo wa damu mwilini. Jina Lucifa ni jina lenye moto,
lisilofanya kazi, sawa na damu isiyo na kazi. Mtu akiwa na ini ni sawa na kusema
kwamba anaishi (To have a liver is to live). Neno “Live” ukiligeuza nyuma
linakuwa “Evil” yaani uovu na neno “Lived” ukiligeuza linakuwa “Devil” yaani
Mwovu. Red (Roth) yaani rangi nyekundu ni rangi ya vita. Yellow (Gold) yaani
rangi ya njano au ya dhahabu ni ishara ya kupata nguvu, wakati Blue ni rangi
waliyopewa watawala. Green (Yellow+Blue) yaani rangi ya kijani ambayo ni
mchanganyiko wa rangi ya Blue na njano ni rangi waliyopewa wanaojiunga
kwenye chama cha Freemason (Greenland). Rangi nyeupe (White) humaanisha
silaha, wakati rangi nyeusi ni ishara ya uchawi wa watu weusi (Black Magic)
– Bahari (Meru-Mara-Mary) alikuwa ni bikira mama. Uhai wa kwanza (ndani ya
bahari) ulitoka kwenye mdomo wa 1) samaki na kisha kutokea kwenye ardhi
kupitia 2)chura. baadae uhai ukapatikana kutoka kwa 3)nguruwe pori dume, kisha
4)simba na hatimaye 5)nyani. Kisha uhai ukabadilika na kuonekana kuwa 6)mtu
(hatua ya sita). Tumbo lililoleta mabadiliko haya ya uzazi ni Bustani ya Edeni na
huwakilishwa na herufi “O”. Kisha mtu akavumbua moto (Lumerian # 7) huko
Ethiopia wakiwa ni watu wafugaji. Walivumbua pia bahari ya Atlantic (The
Atlanteans # 8) wakati wakifuatilia jua lilipokuwa linazama upande wa
magharibi. Mwisho, watu walioitwa (Aryans # 9) walionekana kwa mara ya
kwanza huko Georgia kwenye milima ya Caucuses. Hivyo Freemason wakaamini
kwamba uumbaji haukukamilika na wao wakawa “miungu.”
– Watu hawa waitwao Aryans wanapatikana kwenye kitabu cha Mwanzo sura ya 2
katika Biblia. Wakiwa wanatumia genes zenye umbo la pembe tatu walianza kazi
ya “New World Order”, wakiwafanya watu wazaliane kama nyuki kwenye
mzinga, wakati nyuki wa kiume hugeuka na kisha kuanza kuzaa bila msaada wa
nyuki wa kike. (Adamu alitolewa ubavu na mahali pake pakawekwa yai
lililotolewa kwenye test – tube. Baada ya miezi tisa, akazaliwa mtoto
mwanamume aitwaye Tubal Cain, na hatimaye akapelekwa huko Babeli. Hivyo
Freemason wakaanzisha mapango wao na kuuona wenye mafanikio kama ya
nyuki.
– Freemason wanasema kwamba mtu mpya hazaliwi mara moja. Wanasema
kwamba mtu huzaliwa kwa degree. Wakati wa miezi tisa mtu huzaliwa akiwa njiti
(pre-mature). Mtu huyo anahitaji kutengenezwa zaidi. Freemason wanasema
kwamba utambuzi wa kiroho “Spritual consciousness” ni “mimi niko” wa kweli,
ambaye hupatikana baada ya mwaka wa ishirini na moja wakati mawazo huanza
kutoka katika viungo wa siri (kukomaa kwa balehe). Hata hivyo kwa Freemason
maisha huanza mtu anapofikisha umri wa miaka arobaini, baada ya miaka ishirini
ya kujitoa kwake, na kuwa mtumishi mwaminifu.
– Wanawake, hamuoni kwamba mnapaswa kuamka na kuwatuma freemason wa
kike kweny vikao. Mkiendelea kukubali kunyanyaswa kiakili, kimwili na kiroho
nguvu zetu zitakwisha. Msikubali kuendelea kunyanyaswa. Jiteteeni katika
maisha yenu na taratibu ulimwengu wote utafadhaika.
– Kwamba kanisa au dhehebu lazima liwe chini ya uongozi wa watu katika mfumo
wa umbo la pembe tatu (Piramidi) na kwamba mtu hawezi kuokolewa asipokuwa
ndani ya kanisa au dhehebu hilo.
– Baada ya miaka elfu kumi ya Freemason, je huu sio wakati wa wanaume na
wanawake kujichukulia madaraka ya kisiasa, kidini na kiuchumi na kuunda
paradiso ambayo ilikuwa imepotea hapa duniani?
Hizo ndizo baadhi ya siri muhimu ambazo Freemason hawataki zijulikane kwa watu.
Ukichunguza kwa makini siri hizo utagundua mambo mengi ikiwa ni pamoja na maana
ya degree 33. Lakini pia utagundua kwamba katika somo la Historia kuna topic
inayosema “Evolution of man” Yaani uibukaji wa mwanadamu. Kwamba mtu
hakuumbwa kama Biblia inavyosema ila alitokana na mabadiliko ya viumbe kutoka hatua
ya kwanza hadi ya 9. Sasa ieleweke kwamba chanzo cha topic hiyo ni Freemason. Jambo
lingine ni kwamba siku za hivi karibuni wanasayansi wamekuwa wakifanya utafiti wa
kuzalisha watoto kupitia chupa (Test Tube). Hiyo pia ni imani ya Freemason ambao
wanaamini kwamba Adamu alipotolewa ubavu, kama Biblia inavyosema, wanadai
aliwekewa yai kupitia kwenye chupa (test tube) na kisha akazaliwa Tubal Cain bila
msaada wa mwanamke. Wao wanasema bahari ndio mwanamke na tutaona katika sura za
mbeleni kwenye kitabu hiki jinsi freemason wanavyopata nguvu kutoka kwa jinni
liitwalo LILITH ili kuwaweka wanawake mahali ambapo hawakuwekwa na Mungu.
Ndio maana tunaona harakati za kuwanyanyua wanawake ili washike majukumu ya
wanaume, hata hivyo Freemason wanajua kwamba hilo litakapofanikiwa, ulimwengu
wote utafadhaika! Lakini pia Freemason wanasema kwamba watu wana mioyo mizito
kwa sababu hawawaamini na hivyo wamekuwa wazito kama mawe ambayo yanafaa
kutumiwa katika ujenzi. Hivyo wanawatumia watu kujenga babeli yao bila watu kujua.
Kwa mfano watu wengi wamekuwa wakiiga mitindo ya kidunia iliyoanzishwa na
Freemason, madhehebu mengi yamekuwa yakifuata mafundisho yaliyo maagizo ya
wanadamu (Mathayo 15:9), madhehebu mengi yamefuata mfumo wa Piramidi, na kwa
kweli wengi wamekuwa ni mawe mazito yanayotumiwa na Freemason kujengea.
3
Freemason na Kazi zao.
Sasa tunaingia katika hatua muhimu kabisa ya kujua kazi za vyama hivi vya siri
maana tayari vimo ndani ya jamii bila jamii yenyewe kujua. Tumeona mnyama wa
namba 666 na Illuminati, ambao malengo yao ni mamoja, ya kuitawala dunia, kisiasa,
kiuchumi, kidini nk. Nimegusia pia kundi la Freemason katika sura iliyopita. Ukweli ni
kwamba huwezi kutenganisha Illuminati na Freemason kama tulivyoona kwenye sura
ya pili. Lakini pia huwezi kuwazungumzia freemason bila kumfahamu na kumtaja Dr.
Albert Pike.
Dr. Albert Pike alizaliwa Disemba 29, 1809 akiwa ndiye mtoto mkubwa kwenye
familia ya watoto sita ya Benjamin na Sarah Andrews Pike. Pike alizaliwa na kukulia
kwenye familia ya Kikristo kwenye dhehebu la Episcopal. Akiwa na umri wa miaka 15
alifanya mtihani wa Harvard College na akafaulu lakini hakuweza kusoma chuoni hapo
kwa sababu ya kukosa fedha. Baada ya kusafiri hadi kufika mahali panapoitwa Santa,
aliendelea na safari yake hadi Arkansas ambapo aliajiriwa kuwa mhariri wa gazeti kabla
ya kufanya kazi bar. Akiwa Arkansas, alikutana na Mary Ann Hamilton na akamuoa
Novemba 28, 1834. Aliweza kuzaa watoto 11 pamoja na mkewe. Alipofikisha umri wa
miaka 41 aliomba kujiunga na freemason kwenye Loji inayoitwa Western Star Lodge No.
2 huko Little Rock, Ark ikiwa ni mwaka 1850. Alipata Digrii zake 10 za York Rite
kuanzia mwaka 1850 hadi 1853. Alipata digrii ya 29 ya Scottish Rite mwezi Machi 1853
akiwa Loji ya Albert Gallatin Mackey huko Charleston.
Kwa mujibu wa maandishi ya mwanzo kabisa kuhusu Freemasons, maandishi hayo
yanasema kwamba chanzo cha freemasons ni Adam anayesemekana kuwa ndiye Mason
wa kwanza kabisa. Kitambaa kinachoitwa ‘apron’ wanachokivaa Masons wakati wa
ibada zao wanadai kuwa ni sawa na ngozi aliyoivaa Adamu na Hawa katika bustani ya
Eden. Ujuzi wa kujua mema na mabaya alioupata Adamu baada ya kula tunda
walilokatazwa ulichukuliwa hadi kwa mtoto wa Adam aitwaye Seth, na kisha kwa
Nimrod ambaye ndiye mwanzilishi wa ujenzi wa mnara wa Babeli, yeye akiwa ni kitukuu
wa Nuhu. Dr. Albert Mackey (mwenye digrii 33 na mwandishi wa Freemasonry
Encyclopedia) anarejea kwenye maandishi ya mwaka 1560 yakielezea kwamba chanzo
cha freemasons ni kwenye mnara wa Babeli na kwamba Nimrodi aliwafundisha wajenzi
wa mnara huo imani ya freemasons. Baada ya Mungu kuchafua lugha yao, siri zote za
freemasons inasemekana kuwa zilipotea.
Wakati mfalme Sulemani (Solomon) alipokuwa anajenga hekalu, freemasons
wanaamini kwamba imani yao ilianzishwa tena. Mackey anasema kwamba Sulemani
(Solomon) ndiye aliyekuwa Grand Master wao mkuu na Loji (Lodges) zote zilianzishwa
na Sulemani. Hata hivyo Martin L. Wagner ambaye ni muumini wa freemason
anafundisha kwamba jina ‘Solomon’ sio jina la kabila ya Israeli kwa sababu maana ya
jina hilo yaani Sol-om-on humaanisha jua katika lugha ya kilatini ‘Sol’, katika lugha ya
kihindi ‘om’ na katika lugha ya Misri ‘on’ hivyo kumaanisha kwamba Solomon ndiye
mungu jua na mkuu wa Freemasons baada ya Nimrod.
Wakati wa utawala wa Uyunani (Greece) kulikuwa na vikundi vilivyoitwa ‘guilds’ sawa
na vyama au ‘unions’ kwa wakati wetu huu. Vikundi kama hivyo viliitwa “Dionysiacs,”
huko Roma na ndivyo vilivyohusika na ujenzi wa viwanja vya michezo (stadiums).
Baadae vikundi hivi ndivyo vilivyohusika na ujenzi wa makanisa (cathedrals) na majengo
makubwa na baadaye vikapewa majina kama Carpenta, builders, draftsmen, craftsmen
katika fani ya ujenzi. Watu hao kulingana na fani zao walikaa kwenye vikundi pamoja na
mahali hapo pakaitwa Loji au Lodge. Ndio chanzo cha majengo ya kuabudu ya
freemasons kuitwa ‘Lodges’. Wale wote waliokuwa na fani ya ujenzi wa majengo
waliitwa ‘Masons’ lakini iwapo mtu asiye na ujuzi wa ujenzi wa majengo huku akitaka
kujiunga na chama hicho aliitwa ‘Accepted Mason’. Baadae Dr. Albert Pike aliandika
kitabu kinachoitwa ‘Morals and Dogma of the Ancient and Accepted Scottish Rite of
Masonry’ alichokiandika mwaka 1871. Kitabu hicho ndicho chenye mafundisho na
mwongozo wa imani ya freemasons.
Ndani ya kitabu hicho kuna jumla ya digrii 33 za freemason na walitumia mahesabu
katika kutoa digrii zao 33, unadhani waliamua tu? hapana! Walipata digrii 33 kutokana
na kinachoaminiwa “human trinity” yaani ‘utatu wa kibinadamu’ kwamba ni moyo,
ubongo na viungo vya siri. Wakasema kwamba viungo vya siri na ubongo
vinaunganishwa na ngazi 33 za vipingili vya viungo vya uti wa mgongo (joints).
Kwamba uti wa mgongo una ngazi 33 kutoka unapoanzia kwenye viungo vya siri hadi
kichwani kwenye ubongo. Hapa inabidi tuwaulize madaktari watupe ukweli kuhusu hizo
ngazi 33 za uti wa mgongo. Mtu anapobalehe ndipo anapoanza kupanda ngazi na
anapofikia umri wa kuwa na akili (ubongo) timamu iliyotulia huwa amefikia ngazi ya
juu kabisa katika ubongo, sawa na kumaliza ngazi zote 33 za uti wa ubongo.
Digrii hizo 33 ni kama ifuatavyo: The Blue Lodge (Symbolic Lodge of Hatimaye
imani ya freemasonry ilisambaa taratibu katika maeneo mengi duniania: Ufaransa (1718-
25) , Ireland (1725-26), Hispania (1726-27), Uholanzi (1731), Ujerumani (1730-33),
Africa (1735), Scotland (1736), Ureno (1736), Switzerland (1737), Italia (1733-37),
Russia (1731-40), Canada (1745), Sweden (1735-48), Prussia (1738-40), Austria (1742),
Poland (1784), na Mexico (1825).
Ili kujiunga na imani hii lazima mtu awe na umri wa miaka 21 (3×7) na kama ni mtoto wa
freemason anaweza kujiunga akiwa na umri wa miaka 18 (9+9). Zipo Loji kuu (Grand
Lodges) 150 duniani na kuna wanachama wasiopungua 6,000,000 duniani kote.
Kila digrii ina mafundisho yake ambapo kadri freemason anavyopanda ngazi kutoka
digrii ya chini kwenda digrii ya juu anafunuliwa siri zaidi kuhusu malengo, ibada na
utaratibu mzima wa freemason na Illuminati. Albert Pike anasema: “The Blue Degrees
(the Blue Lodge degrees) are but the outer court or portico of the Temple. Part of the
symbols are displayed there to the Initiate, but he is intentionally mislead by false
interpretations. It is not intended that he shall understand them; but it is intended that he
shall imagine he understand them”.
[Albert Pike, Morals and Dogma, p. 819; Emphasis added]. Akimaanisha kwamba
freemason wa digrii za chini hawapaswi kujua siri na maana halisi ya alama za freemason
ila huwa anadanganywa ili afikiri kwamba anazijua.
Unaweza kuona aina za digrii hizo; kwa mfano digrii ya 18 inayoitwa ‘Knight of Rose
Croix’ hushughulika na elimu ya aina za misalaba na jinsi ya kufanisha kuziingiza ndani
ya taasisi na madhehebu mbalimbali kwa imani ya Illuminati na freemason na kwa kweli
freemason wa digrii hiyo wamefanikiwa kwa kiwango cha juu kabisa kuingiza aina
nyingizi za misalaba ndani ya makanisa na taasisi bila ya waumini kujua maana ya
misalaba hiyo. Tutaona kwenye sura za mbele katika kitabu hiki.
Yapata Januari 22, 1870 Pike alipata maono ya nuru “illuminated” kutoka kwa
GAOTU—Shetani—kuhusu mpango maalumu wa jinsi ya kutimiza malengo ya New
World Order yaliyowekwa na Adam Weishaupt, miaka 94=9+4=13 au 9×4=36 iliyopita,
tangu Mei Mosi, 1776, Malengo hayo yalipangwa yakamilike ifikapo Millenia ya 7.
Ndipo akaanza kwa kuandika kitabu mashuhuri kwa freemason kinachoitwa “Morals
and Dogma” ambacho kilichapwa kwa mara ya kwanza mwaka 1871, mwaka mmoja tu
baada ya kupokea njozi ya kutekeleza mpango mpya wa dunia. Unaweza kujiuliza
kwamba hivi mpango wa zamani wa dunia ulikuwa ni upi hadi waweke mpango mpya wa
dunia? Freemason wanauita Ukristo kuwa ni “Mpango wa Zamani wa dunia” na hivyo
walidhamiria kuharibu Ukristo na hivyo kuanzisha mpango mpya wa dunia (New World
Order) ambao ni Upagani. Tayari viongozi wakuu wa mataifa ya dunia (UN) wamekuwa
wakikutana mjini New York ili kuangalia malengo ya Millenia yamefikia wapi, na kwa
uwazi wamekuwa wakisema kwamba kuna umuhimu wa kuharakisha New World Order
kwa visingizio vya umaskini, maradhi na ujinga.
Ni njozi gani aliyoipata Pike mwaka 1870? Pike alivuviwa kwamba lazima kuwepo na
vita kuu 3 za dunia na zilipangiliwa kwa kutumia namba na hesabu za Illuminati na
freemason. Ilipofika mwaka 1914, miaka 44 kupita tangu njozi ya Pike, ndipo vita ya
kwanza ya dunia ikaanza kama ilivyopangwa kwa namba za Illuminati na freemason.
Hapo kuna hesabu za illuminati zilizotumika kupanga vita hizi tatu. Njozi ilikuwa Januari
22, namba 22 = 11 x 2. Kisha ilipita miaka 44 = 11 x 4, ndipo vita ya kwanza ikaanza.
Lakini pia vita kuu ya pili ilianza mwaka 1939 ikiwa ni miaka 69 = 3 x 23 kupita tangu
njozi ya Pike mwaka 1870, hata hivyo namba 6 na 9 zote huabudiwa na Illuminati.
Lakini pia ilikuwa imepita miaka 21 = 3 x 7 tangu kumalizika kwa vita kuu ya kwanza na
kuanza vita kuu ya pili. Namba zilizotumika kuandaa vita kuu mbili za dunia ni namba 3,
6, 9 na 11. Ifikapo mwaka 2011 itakuwa imepita miaka 66 tangu kumalizika kwa vita kuu
ya pili. Mpangilio wa namba 6, 66, na 666 huwa na nguvu zaidi kwa freemason na ni
kutokana na miaka 66 kupita tangu vita ya pili illuminati wamepanga kuanzisha vita ya
tatu ya dunia. Tutaona kwenye sura mbeleni.
Pike alifariki manamo Aprili 2, 1892 huko Washington DC. Tutarudi kuchunguza njozi
ya Pike na mpango wa vita kuu tatu (3) za dunia zilivyopangwa kwa namba na hesabu za
Illuminati.
Yesu aliahidi kwamba “……. hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala
lililofichwa ambalo halitajulikana. Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru;
na msikialo kwa siri lihubirini juu ya nyumba.” Mathayo 10:26-28 na sasa siri
zilizopangwa na Illuminati zinafichuka na si muda mrefu ulimwengu utashuhudia vita
kuu ya 3 na ya mwisho ya dunia itakayotumiwa kama sababu ya kuundwa kwa serikali na
dini moja ya dunia. Unajua nini kilitokea mara baada ya vita kuu ya kwanza na ya pili za
dunia? Je, vita kuu ya tatu itaanza lini? itakuwaje? Umejiandaaje na vita hiyo? Malengo
ya New World Order hatimaye yatakamilika lini? Kumbuka kuwa vita ya kwanza na ya
pili za dunia zilipangwa kwa makusudi yenye malengo ya kutekeleza mipango ya
Illuminati na hawawezi kutumia namba 2 maana hiyo siyo namba yao hivyo lazima
waanzishe tena vita kuu ya 3 ya dunia ndipo wafanikiwe kuanzisha serikali na dini moja.
Hilo tutaliona mbeleni.
Kwanza kabisa nini maana ya Freemason? Katika dictionary au kamusi wanasema
kwamba Freemason is a member of a certain secret society. Yaani Freemason ni
mwanachama wa chama cha siri au jamii ya siri. Hata hivyo neno Freemason linatokana
na maneno mawili, Free na Mason. Maana ya Free ni huru na maana ya Mason ni mtu
mjenzi wa majengo katika fani ya uwashi. Tunajua kuna wajenzi wanaoitwa kapenta, ila
Masons ni wajenzi uwashi. Kwa mafundi ujenzi wa uwashi wanafahamu kwamba wakati
wanajenga hasa kwa kutumia matofali, kila mstari wanaoujenga huitwa kozi, kwa
Kingereza course. Hivyo pia Freemason wanapojenga wanajenga kwa kozi wanazoziita
degree. Je, Freemason wanatumia nini kwenye ujenzi wao? kama tulivyoona kwenye siri
za Freemason, wanajenga kwa kutumia mawe, ambayo ni watu wasiojua kama
wanatumiwa kujenga. Freemason wanajenga nini? Wanajenga ulimwengu mzima wa
dini, siasa, uchumi na kazi/kilimo/ajira. Katika kitabu cha Ufunuo 7:1 Biblia inataja
‘pepo nne za dunia’ ambazo zinazuiliwa na malaika wanne ili kazi ya kuwapiga muhuri
watu wa Mungu ikamilike. Pepo nne za dunia huwakilisha 1)machafuko ya kidini,
2)machafuko ya kisiasa na utawala, 3) machafuko ya uchumi na biashara na 4)
machafuko ya wafanyakazi na wakulima. Tutaona kwamba freemason nao wamejigawa
katika makundi manne ili kuhakikisha wanafanikisha mpango mpya wa dunia
ulioanzishwa na Weishaupt mwaka 1776 na hivyo kumaanisha pepo nne za dunia kama
zilivyoelezewa na Mungu kwenye kitabu cha Ufunuo 7:1. Tumeona kwamba
Illuminati/freemason wameungana na mnyama wa namba 666 na hili linathibitishwa na
Padre wa kanisa Katoliki Martin Malachi kwa kusema kwamba “He is protected by four
governments” “people of the world seem to him ready for strong worldwide moral
government with control.” (The keys of this Blood pp. 120, 160), akimaanisha kwamba
Papa na Vatican inalindwa na serikali nne na hatimaye ulimwengu wote utatawaliwa na
Vatican. Je, serikali hizo nne ni zipi? Ni makundi manne ya freemason.
Kuna degree 33 za Freemason. Mtu anapoanza katika hatua ya kwanza atatakiwa
kusoma degree ya kwanza inayoitwa Entered Apprentice degree; kisha atpanda na kufika
Degree ya pili inayoitwa Fellow Craft Degree na Degree ya tatu inaitwa The Master
Mason degree hadi kufikia degree ya 33 ambayo ndiyo ya juu kabisa. Kama tulivyoona
utaratibu wa kujiunga na Jesuits ni pamoja na viapo vikali, hapa pia tunaona kwamba
unapoingia katika Freemason utatakiwa kuapa katika kila ngazi unayopanda, hapa
nitaweka viapo katika kila ngazi tatu za awali, nitaweka katika lugha ya Kingereza bila
kutoa tafsiri ya moja kwa moja, nitaelezea kwa ujumla wake maana ya viapo hivyo; kama
hujui lugha ya Kingereza, tafadhali naomba umhusishe aliye karibu nawe ili akufafanulie;
kabla ya kuapa, atasomewa maneno yafuatayo:
“Mr. _______, before you can proceed further in Freemasonry, it will be necessary for
you to take an Obligation appertaining to this degree. It becomes my duty as well as
pleasure to inform you that there is nothing contained in the Obligation that conflicts
with the duties you owe to God, your country, your neighbor, your family, or yourself.
With this assurance on my part, are you willing to take the Obligation?” (Nevada ritual,
circa 1984)
Maneno hayo yanamaanisha kwamba unapoingia Feemason utaendelea kuwa na
mahusiano na Mungu wako, na nchi yako, na jirani zako, na familia yako kama
kawaida. Lakini Freemason wanamwabudu mungu yupi? Wao wanamwabudu mungu
anayeitwa GAOTU – Great Architect Of The Universe – yaani ‘Mbunifu mkuu wa
ulimwengu.’ Freemason hawamwabudu Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Sala
zao zote huelekezwa kwa GAOTU. Architect ni mtu anayebuni ramani za majengo,
majengo unayoyaona katika nchi mbalimbali yakiwemo yale yaliyomo ndani ya miji ya
nchi yetu, yanatokana na ubunifu wa watu wanaoitwa Architects. Ni watu wenye elimu
kubwa sana kuhusu mambo ya ubunifu na ujenzi wa majengo. Freemason nao ni
wajenzi wa maadili wanayoyataka wao na pia wanaye Architect (mbunifu) wao mkuu
ambaye ndiye wanayemwabudu, jina la Architect wao ni GAOTU. Huyo ndiye mbunifu
mkuu wa shughuli za Freemason katika ujenzi wa ulimwengu, wengine ni watekelezaji
tu.
Wapo watu pia wanaoelekeza sala zao kwa viumbe badala ya kuelekeza kwa
Muumbaji. Wao pia hawatofautiani na Freemason maana wote wanakwenda kinyume
na Mungu, na ukweli ni kwamba wanafanya hivyo kutokana na ubunifu wa GAOTU
maana kazi yake ni kubuni mbinu mbalimbali za kuwafanya watu wawe mbali na
Mungu. Yesu anasema kwamba tunapotaka kusali tusali hivi, “Baba yetu uliye
mbinguni……” Mathayo 6:9-13, ikimaanisha kwamba sala zetu zote tuzielekeze kwa
Mungu aliye mbinguni tena kwa Jina la Yesu. GAOTU anajua kwamba Mungu alisema,
“mtu akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote” Yakobo 2:10, ndio maana
anajitahidi kuwafanya watu wamkosee Mungu hata katika kitu kidogo, na watakuwa
wamemkosea juu ya yote. Hivyo unaweza ukawa mlokole, msabato, mkatoliki,
muislamu, mbudha, myahudi nk. lakini ukimkosea Mungu katika jambo moja tu
umemkosea juu ya yote. Ndio maana leo hii katika dunia nzima kuna utitiri wa
madhehebu na dini za kila aina. Wataalamu wanasema kuna dini zaidi ya elfu tatu! Je,
wote watakwenda Paradiso? Biblia inasema, “Je! Hamjui ya kuwa wale washindanao
kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja?” 1 Wakorintho
9:24. Hivyo pamoja na kuwa na dini nyingi kiasi hicho na dini zote zikiwa zinadai
kupiga mbio ili kupata tuzo ya uzima wa milele, ni wale tu wanaotii kila moja ya amri
za Mungu ndio wanaopiga mbio vizuri na ndio watakaopata tuzo, nao watatoka katika
dhehebu moja tu.
Kwa nini watu huingia Freemason? Ni kwa sababu ya kutaka utajiri wa dunia hii.
Wakati shetani anamjaribu Yesu, alimwonyesha utajiri, “Kisha ibilisi akamchukua
mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.” Mathayo 4:8, 9. Baada ya
ibilisi kushindwa kumnasa Yesu, sasa aliendelea kutumia njia hiyo hiyo kwa kumtumia
mnyama ili awape watu utajiri kupitia Freemason, tunasoma kwamba, “Lakini katika
mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua
atamheshimu, kwa dhahabu na fedha, na vito vya thamani na vitu vipendezavyo…..na
yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye
ataigawa nchi kwa rushwa.” Danieli 11:38,39. Ndio maana watu wengi wanaingia
kwenye vyama vya siri kama Freemason na kila anayeingia humo hufanywa apate
kumiliki vitu vingi na kuwa tajiri mkubwa, tena hao ndio chanzo cha rushwa nchini na
hata kusababisha ufisadi wa hali ya juu katika nchi mbali mbali.
Unapokubaliana na swali katika maneno ya awali hapo juu, utatakiwa kuapa kwa
kuzingatia ngazi unayotaka kupanda katika Freemason. Viapo hivyo ni kama ifuatavyo:
Entered Apprentice Degree: “….my throat cut across, my tongue torn out, and with my
body buried in the sands of the sea at low-water mark, where the tide ebbs and flows
twice in twenty-four hours, should I ever knowingly or willfully violate this, my solemn
Obligation of an Entered Apprentice.”
Fellow Craft Degree: “….my left breast torn open, my heart and vitals taken thence,
and with my body given as a prey to the vultures of the air, should I ever knowingly, or
willfully, violate this, my solemn Obligation of a Fellow Craft.”;
Master Mason Degree: “….my body severed in twain, my bowels taken thence, and with
my body burned to ashes, and the ashes thereof scattered to the four winds of Heaven,
that there might remain neither track, trace nor remembrance among man or Masons of
so vile and perjured a wretch as I should be, should I ever knowingly or willfully
violate this, my solemn Obligation of a Master Mason.” (Nevada ritual, circa 1984)
Viapo hivyo tumevifupisha ili kuonyesha nini kitakachotokea endapo mtu ataamua
kuwasaliti Freemason kama amejiunga nao. Mwanachama anapokiuka viapo hivyo
hupotea kimuujiza. Wapo wanaoamini kwamba mtu anapokuwa freemason hawezi
kutoka kwenye chama hicho, wanasema “Once a mason always a mason” lakini hilo si
kweli maana wapo wengi walioingia kwenye vyama vya siri bila kujua kwa undani
kuhusu vyama hivyo ikiwa ni pamoja na freemason na walipofahamu kwa undani
walitoka, watu hao wamekuwa msaada mkubwa kutoa siri za vyama hivyo. Katika
miaka ya 1800 kapteni William Morgan aliachana na chama hicho cha Freemason na
alikuwa amejiandaa kutoa siri zao ndipo akakamatwa huko Niagra, New York
Marekani na kuuawa, mwili wake haukuonekana hadi hivi leo. Lakini wengi wametoka
na hadi leo wapo wakiendelea kutoa siri za vyama hivyo. Ndugu msomaji kama
unaweza kuchunguza zaidi utagundua kuwa kuna viapo ambavyo watumishi wa
madhehebu kadhaa hutakiwa kuvifanya wanapoingia katika utumishi wao. Freemason
huapa kwamba watamtii GAOTU lakini pia hata watumishi wa madhehebu kadhaa
huapa kutoa utii wao sio kwa Mungu bali kwa kiongozi mkuu wa kanisa husika na kwa
kanisa lenyewe. Tafadhali chunguza katika dhehebu lako pengine ni wachungaji,
maaskofu, mitume na manabii wa siku hizi au makasisi, nk. Cha ajabu kuna madhehebu
ambayo huwaapisha watu wanapotaka kwenda kubatizwa baada ya kukubali imani yao.
Hata hivyo madhehebu hayo kwa kuwaapisha wachungaji, maaskofu au makasisi, na
hata waumini wao wanapokwenda kubatizwa, wanaonyesha kuwa wametekwa na
Freemason kutokana na ubunifu wa GAOTU kwa sababu Biblia inasema kwamba:
“Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana
nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana
ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuweka miguu
yake…wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa
mweupe au mweusi…..kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.” Mathayo
5:33-37. “Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape….msije mkaangukia hukumu.”
Yakobo 5:12.
Je, viapo vya watumishi wa makanisa na waumini wao vinatoka wapi kama sio kwa
Freemason ambao nao huapa pia? Tena vinatoka kwa GAOTU – mbunifu mkuu wa
ujenzi wa maadili yaliyo kinyume na Mungu. Mbona Biblia iko wazi kuhusu kuapa
maana Mungu amekataza kuapa na hasa kwenye mambo ya dini.
Freemason ni wajenzi walio huru, ambao wanafanya kitu chochote kwa uhuru bila
kupingwa. Kwa vile Freemason walianza kuwepo tangu karne ya 18, sio rahisi kwa sasa
kuweza kupinga malengo yao maana wao ndio wanaoshikilia uchumi wa dunia, jambo
muhimu kwetu ni kujisalimisha kwa Yesu. Sehemu wanapopata mafunzo yao panaitwa
Lodge, sawa sawa na chuo mahali wanafunzi wanapopata elimu yao. Lodge pia ni
sehemu za ibada za Freemason.
Freemason walianza mnamo karne ya 18 wakiwa ni moja ya kikosi cha mnyama wa
666 katika kutimiza malengo yake. Wakati wa miaka 1260 (Ufunuo 13:1-8) ya mateso
ya watu wa Mungu iliyoanza mwaka 538AD na kuishia mwaka 1798 kwa papa Pius VI
alipokamatwa na kuifia huko Ufaransa, kulitokea mkakati wa kutaka kuendeleza
utawala wa Rumi ya kidini na hivyo kuanzishwa kwa vikosi mbalimbali kwa ajili ya
kutimiza malengo hayo ambapo muda si mrefu tutashuhudia lengo lao kuu likitimia.
Moja ya vikosi hivyo ni Freemason ambao nao wamegawanyika katika vikosi kadhaa.
Vikosi hivyo ni pamoja na “The Knight of Malta”, ambapo kazi yake ni kushugulika
na makanisa ya Kiprotestant ili yageuzwe yafanane na Rumi na kwa kiasi kikubwa
kikosi hiki kimefanikiwa sana maana kimeweza kuunda umoja wa makanisa ambapo
unatawaliwa na Rumi na hivyo kuwa chini ya Rumi. Hata hivyo Mungu anasema, “Na
kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope,
watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama
vile chuma kisivyoshikamana na udongo.” Danieli 2:43. Hivyo katika muungano huo
wa makanisa kuna chuma na udongo vimechangamana, chuma yakiwa ni madhehebu
makubwa na yenye nguvu wakati udongo madhehebu madogomadogo katika muungano
huo. Kumbuka kwamba unabii hujirudia (Mhubiri 1:9). Yohana anatuambia kwamba
muungano huo utavunjika wakati pigo la saba litakapopigwa, “Na mji ule mkuu
ukagawanyika mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli mkuu
ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghazabu ya hasira
yake.” Ufunuo 16:19. Hata hivyo watakuwa wamechelewa maana mda wa kutubu
utakuwa umepita. Kuhusu ufafanuzi wa kugawanyika mafungu hayo matatu katika
Ufunuo 16:19, nitayaelezea kwa kina mafungu hayo matatu katika sura zitakazofuata.
Pia katika kudhoofisha maadili na kuwafanya watu wasipate muda wa kusoma neno
la Mungu, kikosi hiki ndicho kinachoshughulika sana na kuvumbua michezo
mbalimbali na hasa mpira wa miguu ambao duniani kote una mashabiki wengi sana.
Wengi hupenda kuangalia ligi kuu hasa ya Uingereza yenye alama ya Simba, je
umewahi kujiuliza pesa nyingi zinazotumika kudhamini mpira, kununua wachezaji na
mishahara ya wachezaji nk zinatoka wapi? Je umewahi kujiuliza kuwa unatumia masaa
mangapi katika kushabikia michezo ukilinganisha na masaa unayotumia katika kutafuta
uhusiano wako na Mungu? je, huoni kwamba hatimaye utajikuta unashindwa kuwa na
mahusiano mazuri na Mungu? hivi karibuni kutakuwa na kombe la dunia, hivi
litafanyikia wapi safari hii? Nadhani kila mtu anajua! Lakini ukimuuliza akutajie mstari
wa Biblia unaompa matumaini ya kuingia Paradiso, Mmmh! Kikosi hiki pia
kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuingiza nadharia za kibinadamu katika mambo ya
kiroho. Hao ndio wanaoshinikiza wawepo maaskofu mashoga, lakini pia wameweza
kuweka hata maaskofu na wachungaji wanawake. Katika Biblia hakuna mchungaji wala
askofu mwanamke, Biblia inasema kwamba, “Ni neno la kuaminiwa, mtu akitaka kazi
ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa
mke mmoja…” 1 Timotheo 3:1-7. Hapo hakuna mke wa mume mmoja, au nimesoma
vibaya? Kikosi kingine cha Freemason kinaitwa “The knight of Columbus” kikiwa na
kazi ya kushughulika na Siasa na Tawala za serikali zote duniani. Kazi kubwa
wanayoifanya ni kuhakikisha katiba za nchi mbalimbali zinabadilishwa ili kukidhi haja
zao. Moja ya mafanikio makubwa ambayo kikosi hiki kimefanikiwa ni pamoja na
kufanikiwa kuzishawishi nchi mbalimbali ili iwepo sheria ya haki sawa kwa kina mama
na watoto ili wawe sawa na wanaume. Ni kweli kwamba Mungu anapenda watu wote
wawe na haki sawa, ila ni haki katika mahitaji kama vile hewa, chakula, matibabu, na
mambo kama hayo yanayohusu uhai wa mwanadamu lakini sio usawa katika uongozi
au utawala. Utasikia viongozi wakisisitiza kwamba watoto wasipigwe viboko –
nyumbani wala shuleni, na hata sasa watoto wamewashitaki wazazi wao eti kwa sababu
wamechapwa viboko walipofanya makosa; lakini Biblia inasema kwamba, “Usimnyime
mtoto wako mapigo, maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, na
kumuokoa nafsi yake na kuzimu.” Mithali 23: 13,14. Maana nyingine ni kwamba
Mungu anatuambia kama tunataka watoto wetu tuwaokoe na kuzimu hatuna budi
kuwachapa fimbo pale wanapofanya makosa. Pia utaona wanawake nao wakishika
nyazifa za utawala na kuongoza wanawake, Biblia inakataza hilo kwa kusema,
“Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa
utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.”
Mwanzo 3:16. Mtawala kwa mujibu wa neno la Mungu ni mwanamume. Kikosi cha
tatu kinaitwa “The knight Templars”, kikosi hiki kinashughulika na shughuli zote za
uchumi na biashara. Hawa wamefaulu kwa kiasi kikubwa kufanikisha biashara huria
(free trade) maana kila kitu wanataka kifanyike huru, lengo la biashara huru au soko
huria ni kuweza kuweka sheria moja kwa urahisi itakayosimamia shughuli zote za
kibiashara, maana kama kila nchi itakuwa na sheria zake za biashara, itakuwa vigumu
kukataza watu wasiuze wala kununua, kwa vile katika Biblia tunasoma “Tena kwamba
mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la
mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:17. Hivyo tunaona tena uhusiano kati
ya Freemason na mnyama wa 666. Kazi wanayoifanya Freemason ni kazi ya mnyama
wa 666 ndio maana watashinikiza watu wawe na chapa au hesabu ya mnyama ndipo
waweze kufanya biashara. Umewahi kusikia juu ya cashless business? Ni biashara
ambayo watu watakuwa wakitumia kadi ya electronics na sio fedha katika biashara zao.
Ndio maana tunaona nchi mbalimbali zikijiunga na kutumia sarafu moja, ila lengo ni
kutumia sarafu moja kwa dunia nzima. Hatimaye kikosi hiki kitahakikisha kwamba
hakuna mfanyabiashara wala mnunuzi atakayefanya biashara au kununua isipokuwa
amemkubali mnyama wa 666. The knite Templers ndio wamiliki wa Benki kuu ya
dunia na IMF. Benki ya Dunia pamoja na IMF zinamilikiwa na familia mbili za
Freemason wa The knite Templers ambazo ni The Rothschilds ya Uingereza, japo wako
Marekani ila chimbuko lao ni Uingereza na ni wayahudi wa kuzaliwa, familia ya pili ni
The Warbugs ya Ujerumani. Kila moja ya familia hizo ina watoto watano ambao kwa
kila wakati wamekuwa wakitawala katika taasisi hizo kubwa za fedha duniani. Hakuna
mtu asiyejua kwamba taasisi hizi ndizo zinazotoa mikopo kwa nchi mbalimbali na
hutoza riba kubwa kiasi kwamba nchi husika hushindwa kulipa madeni hayo na
hatimaye kulazimika kufuata masharti yao ili wapewe msamaha wa madeni yao na
kupewa mikopo tena zaidi. Kwa taarifa zaidi nenda na fungua mtandao wa google kisha
search the rothschilds au the Warburg. Hebu sasa tumsikilize ndugu Baron M.A
Rothschild, yeye anasema kwamba,
“Give me control over a nations currency, and I care not who makes its laws.” ~Baron
M.A. Rothschild,
Yeye anasema kwamba “Nipe utawala wa fedha za mataifa yote, sijali ni nani
anayetunga sheria zake.” Zaidi unaweza kwenda kwenye mtandao ambapo utapata
kujua sababu za kuanzishwa kwa Benki ya dunia zikitajwa na Rais wa tatu wa
Marekani Thomas Jefferson kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya kuwawezesha
Freemason watawale dunia. wwww.crownempire.org/index.php/illuminati/1621-theilluminati-
today/. Hivi karibuni tulishuhudia kile kinachoitwa Kuyumba kwa uchumi
duniani, hata nchi yetu ikatangaza mpango wa kunusuru uchumi wa nchi. Tatizo hili
lilianzia Marekani kisha kufuatia nchi za Asia na Ulaya. Huo ni mwanzo wa
kushinikiza nchi zote kukubaliana na kile kinachoitwa Global Economic Reform
ambapo hatima yake ni kukatazwa kuuza wala kununua kama huna chapa au hesabu ya
mnyama wa 666.
Kikosi cha nne cha Freemason kinaitwa “Scotish Templars”, hiki kinahusika zaidi
na maswala ya kazi na kilimo. Hawa wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa kushawishi
vyama vya wafanyakazi na wakulima ili walete migogoro katika nchi husika, lengo
likiwa kudhoofisha serikali husika ili kwamba wapate nafasi kubwa ya kuweza
kufanikisha malengo yao. Ni juzi tu kulikuwa na migomo ya waendesha ndege za
mashirika makubwa ya ndege duniani wakizishinikiza serikali zao zitekeleze matakwa
yao ambayo hatimaye serikali zitadhoofika na kujisalimisha kwenye mpango wa The
New World Order. Vikosi vyote hivyo hushirikiana katika kusaidia kutimiza malengo
ya kila kikosi na hatimaye kumuwezesha mnyama wa 666 kutimiza mipango yake.
Vikosi hivyo ndizo pepo za nne za duniani alizoziona nabii Yohana akiwa katika kisiwa
cha patmo. Hadi sasa malakika wanne wanaendelea kushikilia au kuzuia pepo hizo nne
hadi kazi ya kupigwa muhuri kwa watu wa Mungu itakapokamilika. Hata hivyo kadri
muda unavyokwenda ndivyo malaika hawa wanne wanaachilia taratibu pepo hizo nne
na ndio maana tunaona dini na madhehebu ya kila aina yakiibuka na mafundisho ya
mashetani, tunashuhudia migomo mikubwa ya wafanyakazi, tunashuhudia kuanguka
kwa uchumi wa dunia na hata tunashuhudia nguvu za asili zikitikisa dunia kama vile
mafuriko, moto, matetemeko na matukio mengine mengi. Unaweza kurejea jedwali la
utawala wa Illuminati na kujifunza katika jedwali hilo utaona vikosi vinne vya
freemason.
Imeandikwa na GIDEON M.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW