Tuesday, December 2, 2014

Somo: MAPEPO NI NINI? [SEHEMU YA TATU]


Sehemu ya Tatu.

Somo: MAPEPO
Mada ndogo: “Mtu anawezaje kupata mapepo”
Lengo kuu: kuzijua mbinu zamapepo na kujilinda nazo
Lengo mahsusi: kudumu katika maombi ya vita kuzipinga roho za kipepo.
Ksms tulivyokwisha kuona kuwa pepo ni roho wachafu wasio na mwili wala umbo wenye uwezo wa kuingia ndani ya kiumbe hai na kuchukua umbo na sura ya kiumbe huyo,pamoja na namna mwanadamu anavyoweza kujikuta katika uhusiano na pepo kupitia ibada9 za sanamu, sadaka, kuyafuga n.k. hapa tutaendelea kujifunza juu ya habari hizi ambazo kila mtu ni vema akizijua.
Wakati mwingine, mtu huweza kujikuta katika hali ya kuvamiwa bila yeye kujua. Ndugu yangu mpendwa, kuvamiwa na pepo si mpaka uugue au ujisikie kuwa dhaifu, pepo huweza kuharibu vitu vyako pole pole, mtu aliyevamiwa na pepo, anaweza kumvuruga awe na hasira tu, asifanikiwe katika shughuli zake tofauti kama vile biashara,masomo, kazi ya ajira, ufugaji,kilimo n.k.
Mtu aliyefungwa kwa namna hii, huambiwa kuwa nyota yake imechukuliwa, na hapa ndipo waganaga wa kienyeji na waaguzi husema kuwa umetupiwa mikosi au mizimu imekasirika na kupaswa kutaaswa kwa kuogeshwa dawa,kuchanjwa au kunyweshwa; hatua hii ni hatari sana, kwa humfanya mwanadamu aingie mikataba mingine na mapepo, na hii huwa ni njia ya moja kwa moja, baada ya kipindi fulani, ile hali ya zamani hujirudia na kulazimika kwenda kwa mganga tena ili kukupatia dawa kali zaidi, bila kujiujua unakuwa unafanya mikataba migumu zaidi na kuzidi kuangamia; utakuta mtu anapewa miiko mikubwa mikubwa ambayo haitekelezeki na mwisho wake mtu huyu anakuwa mtumwa na miiko ya kipepo na anapoivunja basi humwangamiza kabisa.
Mpendwa, dawa iko kwa Yesu, jislaimishe leo uwe huru. Yeye pekee ndiye anayeweza kukuweka huru, ndiye anayeweza kuisafisha nyota yako, ndiye anayeweza kukuinua, njoo kwake leo, usikubali kudanganywa,Yesu ndiye yote ndani ya yote. Haleluya.
Zifuatazo ni njia kuu tano za mtu kupatwa na mapepo;-
(a) Kuabudu miungu- hizi ni ibada zinazofanywa katika madabahu ya shetani. Ibada juu ya mizimu, wafu, kuyaomba mali majini,kutaka ushirika na shetani ili kufanikiwa na ibada zote za namna hii. Kwa kufanya ibada hizi, hujitenga na MUNGU hivo kuwa na ushirika na shetani (1Wakorintho 10:20-22)
(b) Kwa matendo maovu ya mwili- mtu aliyetawaliwa na nguvu za mwili/ hisia, hawezi kuwa na ushirikana MUNGU kwa kuwa, mwili siku zote hupambana na roho. Mtu aliyetawaliwa na matdndo ya wili (Wagalatia 5:19-21) hawezi kumpendeza MUNGU kwa kuwe yeye huongozwa na tamaa za mwili wake wala hayuko tayali kuongozwa na ROHO wa Mungu. Hii ni pamoja na uzinzi,uchawi,ulevi,ulafi na ibada zote za sanamu.
NB; Matendo ya mwili- ni matendo maovu yote yaliyo kinyume na sheria ya MUNGU, ambayo watu ambao hawajakombolewa, hutawaliwa nayo kama dhambi ya asili. Ni lazima kuitubu ili uwe salama. Kumbuka, watu waliozoea kufanya dhambi, huweza kupagawa na pepo (Yohana 5:14)
(c) Kwa kuzifuata DINI za Uongo- hizi ni dini za kiudanganyifu, imani zisizoieleza kweli ya MUNGU. Imani zilizokinyume na wokovu kamili kupitia YESU KRISTO. Ni muhimu kujiepusha na imani/dini hizi ili uwe salama. Dini zakiudanganyifu zipo nyingi na zimekwishashika hatamu (Ufunuo12:9, 1Wathesalonike 3:5). Ni vema kuitafuta iliyo imani ya kweli na kuifuata, usiseme mimi nimekulia katika dini fulani, hivyo hii ndiyo dini yangu, hapana, dini haitakupeleka popote, kikubwa ni wokovu kamili ili ufike mbinguni.
(d) Kutokusamehe- hii ni hali ya kutokuachilia, hali ya kulipiza kisasi. Mpendwa, mtu wa kisasi, hawezi kuurithi ufalme wa Mungu, kwa maana mtu ambaye hayuko tayali, hatasamehewa pia dhambi zake. Mtu aliyefungwa na roho ya kutokusamehe, adui humpandikizia watesaji (Mathayo 18:34&35) hizi ni roho za kumkumbusha maovu yote aliyotendewa ili ahisi uchungu rohoni mwake, ashindwe kusamehe.
(e) Mtu asiye na neno- kukaa bila kusoma neno la Mungu na maombi pia, humpelekea mtu kuwa mtupu, hivyo kufanyika masikani ya adui/ibilisi au makao ya pepo (Mathayo 12:44).

Ni vema kudumu katika sala na kuomba na kusoma neno ili usiwe mtu, bali Roho wa Mungu afanye makaondani yako. Mtu wa Mungu kamwe si mtupu, huongozwa na kujazwa kwa Roho wa Mungu siku zote.
Ndugu yangu mpendwa, jitahidi sana kuweka utaratibu wa kuwa na muda wa kwenda mbele za Mungu kwa sala na maombi kila siku. Hii itakusaidia kuwa karibu na Mungu zaidi. Kumbuka, unavyomkaribia Mungu, ndivyo unavyozidi kuwa mbali zaidi na shetani.(Yakobo 4:8).

Natumai unaendelea kubarikiwa na mafundisho ya neno la Mungu, je, mtu alivamiwa na mapepo yuko je? Endelea kufuatana nami toleo lijilo.......
Somo: MAPEPO NI NINI [SEHEMU YA NNE]
Mungu akubariki.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW