Ukweli hakuna Andiko lolote lenye pumzi ya Mungu mahali popote
linasomeka kuwakumbuka marehemu, iwe kwa dakika moja au kwa dakika mbili.
Lakini lipo Andiko linasomeka, "wafu hawana Ijara tena katika nchi ya
walio hai". Kwa hiyo kwa mujibu wa andiko hilo, hata misa za wafu
HAZIRUHUSIWI, ikimaanisha arobaini za marehemu wote hazina nafasi ndani ya Neno
la Mungu.
WAFU/MFU NI NANI?
Utangulizi:-Neno wafu ndani ya Biblia limetumika likiwa na Maana
zaidi ya moja, Linaweza kutumika kama
i.
Ni
hali ya Roho kutengana na mwili yaani Kifo cha mwili.(Luka 8:55, Muhubiri 9:5)
ii.
Ni
hali ya Mtu kutengana na Mungu au kuvunja uhusiano mwema na Mungu (Kutenda
dhambi) yaani Kifo cha Kiroho (Ayubu 21:25)
Kifo cha kiroho. Kuna aina tatu ya wafu katika eneo hili ambayo
mtu anaweza kufa kiroho lakini bado anaendelea kuwa hai kimwili. Huyu anaweza
akatubu na kufufuka katika wafu akawa hai tena .Pia mtu anaweza kufa kiroho na
kimwili maana yake Roho imekufa na mwili umekufa hana nafasi ya kutubu tena. (Ufunuo
20:5). Kifo hiki ni kibaya zaidi na kinatisha. Ambacho Bwana Yesu alisema
msiwaogope wawezao kuuwa mwili bali Mungu mwenye uwezo wa kuuwa mwili na Roho,
(Soma Matayo 10:28). Kifo cha tatu ni Mtu kufa kimwili lakini bado anaendelea
kuishi Kiroho. Hapa Yesu alisema mtu akiniamini mimi na kutimiza neno langu
ataishi hata kama akifa.
MAOMBI KWA AJILI YA WAFU
Viongozi wengi hufundisha kwamba hakuna kuokoka duniani na hao
hao mtu akifa wanamwombea kwamba alazwe pema peponi kana kwamba kuna wokovu baada
ya kufa. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu.(Waebrania 9:27).
Kanisa au Mchungaji au Padri, au Mtume haliwezi kuomba mfu
kupumzika kwa amani pema peponi, Ndugu zangu wakati wa wokovu ni sasa hivyo
baada ya kufa ni hukumu (Waebrania 9:27). Watakie kupumzika kwa amani wafu ila
tambua kwamba huwezi kuwabadilishia makao yao ya milele, kama ni mbinguni ni
mbinguni tu na kama ni motoni ni motoni tu.
Kuombea wafu huwafanya wenye dhambi kuendelea kutenda dhambi
wakiamini kwamba baada ya kufa kanisa litaomba ili wao waingie mbinguni. Ndugu
nakuambia tena WOKOVU NI SASA. Katika Luka 16:26…Na zaidi ya hayo, kati yetu
sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu
wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'' Biblia inatuonyesha watu
waliokufa wengine wako pema peponi na
wengine wako kuzimu,’’ ’’ MUNGU humpokea
mwenye dhambi ambaye hutubu kwa woyo na kujitakasa kwa msingi wa imani peke
yake katika damu ya YESU KRISTO. Hivyo humpa uzima wa milele. 2 WaKorintho
6:2’’(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu
nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni
sasa)‘’ Wakati wa wokovu ni sasa Wakati wa kuokolewa/kuokoka ni sasa Wakati huu
ndio unatakiwa kuokolewa sio baada ya kufa.
Ndugu zanguni, ningependa kuwakumbusha kuwa, wakati wa Wokovu ni
sasa na sio utakapo kufa. Mafundisho ya kuombea wafu hayapo kwenye Biblia na
hatuoni Yesu akiombea wafu bali akifufua wafu. (Yohana 11:43-44; Luka 7:11 -15;
Marko 5:35).
Mungu awabariki sana
Max Shimba Ministries Org.
No comments:
Post a Comment