Wednesday, July 1, 2015

A’isha: Mke wa Muhammad Mwenye Miaka Tisa

Watu wengi wamesema kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na mke wake mwenye umri mdogo zaidi, A’isha, binti wa Abu Bakr, alipokuwa na miaka karibu 53 na [A’isha] alikuwa na miaka tisa. Baadhi ya Waislam wanakataa maneno haya. Kama mtu atadai kuwa Muhammad na A’isha walijamiiana wakati A’isha alipokuwa na umri wa miaka tisa, na walifanya makosa, jambo hili litakuwa ni kashfa kubwa sana kwa Muhammad. Kwa upande mwingine, kama ilikuwa kweli, jambo hili litaonyesha sura tofauti kabisa ya Muhammad itakayo washtua watu wengi. Kwa hiyo basi, madai haya dhidi ya Muhammad ni ya kweli au uongo? 
 
Andiko hili litaanza kwa kutoa ushahidi wa A’isha kuwa na miaka tisa wakati ndoa yake ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba, kisha litatoa vipingamizi 11 dhidi ya jambo hili, na mwishoni, litauliza itakuwa vipi endapo kila wazo lilikuwa sahihi.
 
Jambo hili ni la muhimu kwa desturi iliyotumika sehemu nyingi sana lakini ambayo imepuuzwa sana siku za leo: mabibi arusi watoto kwenye nchi za Kiislam waliotokana na mfano wa Muhammad.
Huko Iran, hadi kufikia Juni 2002 iliruhusiwa kisheria kwa msichana wa miaka 9 kuolewa kwa ruhusa ya wazazi. Voices Behind the Veil (Sauti Ttokea Nyuma ya Mtando) uk.136-137.
Huko Ivory Coast kitabu hiki pia kinatuambia kuhusu msichana wa miaka 12 ambaye alikuwa anaondoka nyumbani asubuhi kwa masaa mengi kabla ya kurudi nyumbani. Baada ya baba yake kumfunga, alimuunguza kwa kipande cha chuma, alimfungia kwa muda wa siku tatu bila chakula, hatimaye almwoza kwa mwanaume wa miaka 40. Hakuwahi kumpeleka shule kwa sababu alisema kuwa jambo hilo litawaondoa kwenye desturi zao, (mabinti) wataanza kuuliza maswali, na kutokupenda kuolewa mpaka wafikishe umri wa maka 19 au 20. 
Wataliban
 walizishawishi familia zao kuoza mabinti wao wakiwa na umri mdogo hata miaka nane. Voices Behind the Veil uk.110.
Gazeti la Dallas Morning News 9/28/03 uk.1,10S lilikuwa na habari ya kusikitisha kuhusu tabu ya wasichana wa Kiislam wa Nigeria ambao waliolewa wakiwa na umri mdogo sana, walipata ujauzito na walipopata uchungu wa uzazi miili yao midogo ilikuwa bado haijawa tayari. Kwa kiasi kikubwa habari hii ilikuwa mbaya, kimsingi wengi wa wasichana hao walihitaji kuzaa kwa upasuaji (C-section) lakini hawakuweza kupata huduma hiyo. Wengi wao walinusurika, lakini hawakuweza kupata watoto tena kwa sababu ya kuharibiwa kwa miji ya mimba.
 
Ili kuelewa asili ya mamlaka ya mfano wa Muhammad, ni muhimu tufahamu jambo moja kuhusu Hadithi za Kiislam. Hadithi zina nafasi ya juu sana katika madhehebu ya Suni kuliko mapokeo yalivyo na nafasi kwenye makanisa ya Katoliki na Orthodox. Waislam wa madhehebu ya Suni wanaamini kuwa mikusanyiko sita ya Hadithi ndiyo yenye mamlaka kubwa zaidi kwenye Uislam baada ya Kurani. Sehemu iliyobaki ya andiko hili inaonyesha kuwa dai hili ni la kweli kabisa, kwa mujibu wa vyanzo vingi vya awali vya Kiislam vyenye kuunga mkono. Pamoja na nukuu hizi toka kwenye Hadithi sita zinazoaminika ni nukuu toka kwa wana historia wa zamani wa Kiislam wanaoheshimika sana ibn Ishaq na al-Tabari.
 
1. Sahih al-Bukhari 810-870 BK, 256 BH
1a. "Alisimulia baba wa Hisham: Khadija alkufa miaka mitatu kabla ya Nabii kuondoka Madina. Alikaa huko miaka miwili au zaidi kisha akamuoa ‘Aisha alipokuwa msichana mwenye umri wa miaka sita, na Muhammad aliikamilisha ndoa yao kwa tendo la unyumba wakati ‘Aisha alipokuwa na umri wa miaka tisa." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 43 na.236, uk.153.
  

1b. Habari hizo zipo pia kwenye Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 43 na.234, uk.152.
  

1c. "Alisimulia ‘Urwa: Nabii aliandika (mkataba wa ndoa) na ‘Aisha wakati msichana alipokuwa na umri wa miaka sita na aliikamilisha ndoa yake nay eye kwa tendo la unyumba wakati akiwa na miaka tisa na ‘Aisha aliendelea kuwa naye kwa miaka tisa (yaani mpaka kifo cha Nabii). Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 sura ya 60 na.88, uk.65.
  

1d. Alisimulia ‘Aisha: Nabii alikuwa akinisitiri kwa Rida (vazi lenye kukinga sehemu ya juu ya mwili) yake nilipokuwa nawaangalia Waethiopia waliokuwa wanacheza kwenye ua wa nyuma wa msikiti. (Niliendelea kuangalia) hadi nilipotosheka. Hivyo unaweza kuelewa ni jinsi gani binti mdogo (ambaye hajafikia umri wa kuvunja ungo) ambaye ana hamu ya kufurahia burudani alivyofanyiwa mambo ya namna hii. Bukhari juzuu ya7 kitabu cha 62 sura ya 115 na.163, uk.119.
  

1e. "Alisimulia ‘Aisha: (mke wa Nabii) sikumbuki kama wazazi wangu waliamini dini yoyote ile isipokuwa dini ya kweli (yaani Uislam), na (sikumbuki) siku yoyote iliyopita bila sisi kutembelewa na Mtume wa Allah asubuhi na jioni." Bukharijuzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 4 na.245, uk.158. Kwa hiyo, ‘Aisha ama hakuwa mkubwa ama hakuwa amezaliwa kabisa wakati wazazi wake walipo badili dini na kuwa Waislam. Jambo hili linaendana na yeye kuwa mtoto wakati ndoa yake na Muhammad ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba.
 
2. Sahih Muslim 817-875 BK, 261 BH
Mkusanyiko huu unachukuliwa kuwa wa pili wenye kuaminika zaidi miongoni mwa Hadithi.
  

2a. "(3309) A’isha (Allah na apendezwe naye) aliripoti: Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka sita, na niliingizwa nyumbani mwake nikiwa na miaka tisa. (A’isha) Aliendelea kusema: Tulikwenda Madina na nilishikwa na homa kwa muda wa mwezi mmoja, na nywele zangu zilianguka hadi kwenye ndewe (masikioni). Umm Ruman (mama yangu) alikuja kwangu na wakati huo nilikuwa kwenye bembea pamoja na wenzangu ninaocheza nao. Mama aliniita kwa sauti na nilikwenda kwake na sikujua kwa nini aliniita. Alinishika mkono na kunipeleka mlangoni, na nilikuwa ninasema: Ha, ha (kana kwamba nilikuwa natweta kwa mshangao), mpaka msukosuko wa moyo ulipomalizika. Alinipeleka kwenye nyumba ambako walikuwa wamekusanyika wanawake wa the Ansar. Walinibariki na kunitakia bahati njema na kusema: Uwe na sehemu katika mambo mazuri. Mama alinikabidhi kwao. Waliniosha kichwa changu na kuniremba na hapakuwa na kitu kilichonitisha. Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) alikuja pale asubuhi, na nilikabidhiwa kwake." Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 sura ya 548 na.3309, uk.715-716.
  

2b. "(3310) A’isha (Allah na apendezwe naye) aliripoti: Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka sita, na niliingizwa kwenye nyumba yake nilipokuwa na miaka tisa."
(3311) A’isha (Allah na apendezwe naye) aliripoti kuwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alimuoa alipokuwa na miaka saba, na alipelekwa kwenye nyumba yake (Mtume) kama bibi arusi alipokuwa na miaka tisa, na hapa midoli (wanasesere) yalikuwa pamoja naye: na (Nabii Mtakatifu) alipokufa ‘Aisha alikuwa na miaka kumi na nane." Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 sura ya 548 na.3310, 3311, uk.716.
  

2c. "(5981) A’isha aliripoti kuwa alizoea kuchezea midoli mbele ya Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) na wenzake aliokuwa akicheza nao walipokuja (nyumbani) kwake waliondoka kwa sababu walimwonea aibu Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake), lakini Mjumbe wa Allah (amani na iwe juu yake) aliwatuma kwake (A’isha).
 
2d. (5982) Hadithi hii imesimuliwa kwa mamlaka ya Hisham ikiwa na mlolongo ule ule wa waenezaji huku ikiwa na utofauti kidogo wa maneno." Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 29 sura ya 1005 na.5981-5982, uk.1299.
 

3. Sunan Abu Dawud 817-888/9 BK, 275 BH
3a. "(2116) A’isha alisema: Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka saba. Msimuliaji Sulaiman alisema: Au miaks sita. Mtume alifanya nami tendo la unyumba nilipokuwa na miaka tisa." Sunan Abu Dawudjuzuu ya 2 kitabu cha 5 sura ya 700 na.2116, uk.569.
  

3b. "(4913) A’isha alisema: Nilizoea kuchzea midoli. Nyakati zingine Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) aliniingilia wakati wasichana walikuwa pamoja nami. Alipoingia (ndani ya nyumba) walitoka nje, na alipotoka nje waliingia ndani."Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1769 na.4913, uk.1373.
  

Angalia kwa ungalifu. Hii haimaanishi kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na A’isha wakati wenzake aliokuwa akicheza nao wakiangalia. Badala yake inamaanisha kuwa wenzake walicheza naye, na walienda nje wakati Muhammad alipokuja, na walirudi baada ya Muhammad kuondoka.
 
3c. "(4915) A’isha alisema: Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) alinioa nilipokuwa na miaka saba au sita. Tulipokuja Madina, baadhi ya wanawake walikuja. Kwa mujibu wa maelezo ya Bishr: Umm Ruman alikuja kwangu nilipokuwa nabembea. Walinichukua, walinitayarisha na kunipamba. Baada ya hapo nilipelekwa kwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake), na alinichukua na kuanza kuishi nami kinyumba nilipokuwa na miaka tisa. (Umm) alinivutia mlangoni na niliangua kicheko.
Abu Dawud alisema: Hii ndio kusema: Nilipata siku za mwezi, na nililetwa kwenye nyumba, na kulikuwa na wanawake kadhaa wa Ansari (Wasaidizi) ndani yake. Walisema: Kwa bahati nzuri na baraka. Masimulizi ya baadhi yao yamejumuishwa na mengine. Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4915, uk.1374.
  

3d. (5916) [kosa la uchapaji, namba sahihi ni 4916]. Masimulizi yaliyotajwa hapo juu yalienezwa pia na Abu Usamah kwa namna kama hii hii kupitia mlolongo wa wasimulizi tofauti. Maelezo haya yanasema: ‘Kwa bahati nzuri.’ (Umm Ruman) alinikabidhi kwao. Waliniosha kichwa changu na kunivisha upya. Hakuna mtu aliyekuja kwangu mara moja isipokuwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) mchana wa kabla ya saa sita. Hivyo walinikabidhi kwake. Sunan Abu Dawudjuzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4916, uk.1374.
  

3e. (4917) A’isha alisema: Tulipokuja Madina, wanawake walikuja kwangu wakati nilipokuwa nacheza kwenye bembea, na nywele zangu zilifika kwenye masikio. Waliniletea, wakaniandaa na kunipamba. Kisha wakanipeleka kwa Mtume wa Allah (amani na iwe juu yake) na alinichukua na kuishi nami kinyumba, nilipokuwa na umri wa miaka tisa. Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4917, uk.1374.
  

3f. (4918) Masimulizi yaliyoelezwa hapo juu yalienezwa pia na Hisham b. ‘Urwah kupitia kwenye mlolongo wa asimlizi tofauti. Maelezo haya yanasema pia: Nilikuwa nabembea na nilikuwa na marafiki zangu. Walinichukua na kunipeleka kwenye nyumba; kulikuwa na wanawake kadhaa wa Ansar (Wasaidizi). Walisema: Kwa bahati njema na baraka. Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4918, uk.1374.
  

3g. (4919) A’isha alisema: Tulifika Madina na kuishi na Banu al-Harith b. al-Khazraj. Alisema: Naapa kwa Allah, nilikuwa nabembea kati ya mitende miwili. Kisha mama yangu alikuja, na aliniambia nishuke chini; na nywele zangu zilifika kwenye masikio. Kisha muenezaji anasmulia masimulizi yaliyobaki." Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1770 na.4915-4919, uk.1374.
  

Hitimisho kuhusu Abu Dawud: nukuu na nukuu znazopinga nukuu 7 zinathibitisha kuwa A’isha alikuwa na miaka tisa.
 
4. Tirmidhi 825-892 BK, 209-279 BH
Siwezi kusema kitu chochote kuhusu umri wa A’isha kwenye Tirmidhi kwani siwezi kuipata Jami ya Tirmidhi. Hata hivyo Shamaa-il ya Tirmidhi haina kitu chochote kinachohusiana na jambo hili.
 
5. Sunan Nas’ai 830-915 BK, 215-303 BH
Sunan Nas’ai yenyewe haiongelei jambo hili.
 
Hata hivyo, tafsiri ya Kiingereza inasema, "Wakati Hadrat A’isha alipopitisha miaka tisa ya ndoa, Nabii Mtakatifu Muhammad (amani na Baraka za Allah na ziwe juu yake) alipata maradhi yanayosababisha kifo. Tarehe 9 au 12 ya mwezi wa Rabi-ul-Awwal 11 BH, aliondoka kwenye ulimwengu huu wenye kudumu hadi kifo …Hadrat A’isha alikuwa na miaka kumi na nane wakati Nabii Mtakatifu Muhammad (amani na Baraka za Allah na ziwe juu yake) alipokufa na aliendelea kuwa mjane kwa miaka arobaini na nane hadi wakati alipokufa akiwa na miaka sitini na saba." Sunan Nasa’i juzuu ya 1 #18, uk.108-109 (Maelezo ya Kiingereza yanatangulia)
  

Kumbuka kuwa (A’isha) alikuwa na miaka tisa ya ndoa na Muhammad, na kwa kuwa alikuwa na miaka kumi na nane Muhammad alipofariki, alikuwa na miaka tisa alipoanza maisha ya ndoa yake na Muhammad. 
 
 
6. Ibn-i-Majah 824-886/887 BK, 273 BH
6a. A’isha aliolewa alipokuwa na miaka sita, na tisa alipokwenda kwenye nyumba ya Muhammad. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 kitabu cha 9 sura ya 13 na.1876, uk.133.
  

6b. A’isha aliolewa akiwa na miaka saba, alikwenda kwenye nyumba ya Muhammad akiwa na miaka tisa, na alikuwa na miaka 18 wakati Muhammad alipokufa. Kwa mujibu wa al-Zawa’id, isnad zake ni sahihi kwa mujibu wa Bukhari. Hata hivyo Abu ‘Ubaida hakusikia kwa baba yake, kwa hiyo ni munqata (ina pengo) Ibn-i-Majah juzuu ya 3 kitabu 9 sura ya 13 na.1877, uk.134. 
 
7. Mwana Historia ibn Ishaq – aliyefariki mwaka 767/773 BK, 145/151 BH
7a. "Yahya b. Abbad b. Abdullah b. al-Zubayr kutoka kwa baba yake aliniambia kuwa alimsikia Aisha akisema: "Mtume alifia kifuani pangu wakati wa zamu yangu: Sijamkosea mtu yoyote yule kuhusiana naye. Ilikuwa ni kwa sababu ya kutokujua kwangu na udogo uliozidi kiasi hata Mtume akanifia mikononi mwangu."
(Guillaume, A., The Life of Muhammad, tafsiri ya Ibn Ishaq's Sirat Rasul Allah, Oxford University Press, Karachi, Pakistan, uk. 682). A’isha alisema kuwa alikuwa kijana sana wakati Muhammad anakufa.
 
8. Mwana Historia al-Tabari – aliyefariki mwaka 923 BK
8a. ‘Aisha alikuwa na miaka 6 (au 7) alipoolewa, na ndoa ilikamilishwa kwa tendo la unyumba alipokuwa na umri wa miaka tisa. al-Tabari juzuu ya 9 uk.129-131. Muhammad b. ‘Amr ni mmoja wa waenezaji.
 
8b. ‘Aisha alikuwa na miaka 6-7 alipoolewa, na ndoa ilikamilishwa kwa tendo la unyumba alipokuwa na miaka 9-10, miezi mitatu baada ya kuja Maka al-Tabari juzuu ya7 uk.7. Mlolongo wa ueeneaji wa masimulizi haya unamhusisha mtu mmoja ambaye jina lake halijatajwa kutoka Quraysh. 
  

8c. Aisha alikufa mwezi June-July 678 BK (58 BH) akiwa na miaka 66. Jambo hilo linamfanya awe amezaliwa mwaka 610 BK. Inasemekana kuwa alikamilisha ndoa yake na Nabii kwa tendo la unyumba alipokuwa na miaka tisa. al-Tabarijuzuu ya 39 uk.171, 173. (al-Tabari aliandika juzuu 38 za historia, pamoja na juzuu ya 39 inayoitwa Biographies of the Prophet’s Companions and Their Successors.)
 
X 8c. Kwa upande mwingine, al-Tabari pia aliandika kuwa "Watoto wake [Abu Bakr] wote wanne walizaliwa na wake zake wawili – majina yake ambayo tumeisha yaelezea – wakati wa kipindi cha kabla ya Uislam." (Tarikh’l-umam wa’l-mamlu’kAl-Tabari, juzuu ya 4, uk.50, Kiarabu, Dara’l-fikr, Beirut, 1979. al-Tabari juzuu ya 11 uk.141 pia inaelezea jambo hili, huku rejeo la 766 chini ya ukurasa likiwa linasema al-Tabari alikuwa na mgogoro hapa. Rejeo chini ya ukurasa pia linasema kuwa al-Baladhuri Ansab I, uk.409-411; Ibn Hajar Isabah IV, uk.359-360 inaafiki kuolewa kwake akiwa na miaka 9.
 
Maelezo ya Waiislam Walio Wengi
Kuna aina kuu mbili za majibu ambayo Waislam wanatoa kuhusiana na jambo hili: walio wengi wanakubaliana kuwa Hadithi hizi zinaaminika hapa, na wachache hawakubaliani.
 
Mitazamo mingi inathibitisha uhakika wa Hadithi hizi. Kama Hadithi na wana historia wanapaswa kuaminika, basi Muhammad, akiwa na miaka karibu 53, alifanya tendo la ndoa na msichana wa miaka tisa. Kama Muislam mmoja alivyoniambia "… na nadhani A’isha alikuwa msichana mwenye miaka tisa aliyekuwa na furaha kubwa sana ulimwenguni".
 
Tovuti hii ifuatayo inasema kuwa, na pia inawashutumu Waislam wenye mawazo mapana na huru kwa kutoa mtazamo wa ki-magharibi kuhusu mwenendo na kuukana ukweli. http://admin.muslimsonline.com/~islamawe/Polemics/aishah.html
 
Rejeo la 1958 kwenye uk.715 linasema kwa sehemu kuwa: "Kwa mujibu wa Imam Shafi’i, ndoa katika umri mdogo si kitu cha kukubalika sana. Ilikuwa katika mazingira fulani ya pekee sana hata Hadrat A’isha aliolewa na Nabii (amani na iwe juu yake). Jambo la pili la kulizingatia ni kwamba Uislam haujaweka mpaka wa umri wa kubarehe/kuvunja ungo kwani jambo hili linatofautiana kati ya nchi moja na nyingine, rangi ya ngozi tokana na hali ya hewa, urithi, na hali za mwili na ya kijamii. Watu wanaoishi kwenye maeneo yenye baridi hubarehe wakiwa na miaka mingi zaidi kuliko wale wanaoishi kwenye maeneo yenye joto ambako wavulana na wasichana hubarehe/huvunja ungo wakiwa na umri mdogo. "Joto la wastani la nchi au jimbo,’ wanasema watunzi wa kitabu kinachofahamika sana Woman, "linachukuliwa kuwa kigezo kikubwa zaidi hapa, si tu kuhusiana na kupata siku za mwezi bali pia kuhusu suala zima la maendeleo ya kijinsia wakati wa kuvunja ungo. … Kwa namna hiyo hiyo, mtunzi wa Kinsey Report anaeleza: ‘Kutokea kwa vitendo vya ngono vya katika miaka maalum kabla ya kubarehe (kuanza kivitendo) kunaonekana kuwa kwingi zaidi kwa makundi ya umri mdogo. Kiasi cha asilimia nane ya wanawake waliohojiwa walisema kuwa walifanya vitendo vya ngono kabla ya kubarehe wakiwa na miaka mitano hadi saba" (Alfred C. Kinsey na wengineo, Sexual Behaviour in the Human Female, p.110)" – Taarifa hizi zote zilinukuliwa kutoka Sahih Muslim juzuu ya 2 rejeo la 1958, uk.715.
 
Mfasiri wa Sahih Muslim juzuu ya 2 anatoa maelezo kwenye rejeo la 1960 kwenye uk.716. "Ndoa ya Nabii Mtakatifu (amani na iwe juu yake) na A’isha imekosolewa na wakosoaji wa Magharibi. Ni ajabu, hata hivyo, kwamba wakosoaji wa wakati Muhammad (amani na iwe juu yake) waliotoa kila aina ya shutuma dhidi yake hawakusema, hata kwa uchache, kuhusu ndoa hii. Ni muhimu ieleweke kuwa kama yalivyo matendo yote ya Nabii Mtakatifu (amani na iwe juu yake), hata hii ndoa ilikuwa na lengo la Kiingu ndani yake. Hadrat A’isha alikuwa msichana aliyekomaa na alikuwa anakua kiakili na kimwili kwa uharaka wa ajabu walionao watu wachache sana. Alipelekwa kwenye nyumba ya Nabii Mtakatifu (amani na iwe juu yake) muda mfupi kabla ya kubarehe kwake, kipindi ambacho ni rahisi zaidi kujengeka na kuathirika katika maisha yake. … Hata kwa kuangalia jinsia na maumbo ndoa hii ilikuwa ni yenye furaha kama inavyoonyeshwa kwenye rekodi za Hadithi. ‘Wakati tofauti (ya umri),’ anasema Von De Velde, Mkurugenzi wa Zahanati ya Magonjwa ya Wananawake (Gynaeological) ya Harlem [New York?], ‘ni kubwa, mf. inazidi miaka kumi na tano hado ishirini, matokeo yanaweza kuwa furaha zaidi. Ndoa ya mzee (anayekongoloka) – madamu asiwe mzee (aliye na madhaifu na maradhi ya uzee) – na binti mdogo sana, mara nyingi huwa ni yenye mafanikio na amani sana. Bibi arusi hufahamishwa na huzoezwa mara moja mahusiano ya kimwili yenye kiasi" (Ideal Marriage, Its Psychology and Technique, London, 1962 uk.243)." Sahih Muslim juzuu ya 2, uk.716.
 
Matukio ya Maisha ya Muhammad na A’isha
Tukio (miaka +/- 2)BK.BH
Muhammad anazaliwa570-53
Kuhamia Ethiopia617-5
A’isha anaolewa akiwa na miaka 6-76220
Kuhamia Madina6231
Ndoa inakamilishwa kwa tendo la unyumba alipokuwa na miaka 8-96231
Vita ya Badr and Uhud6253
Muhammad anafariki akiwa na miaka 63 na A’isha miaka 1963311
A’isha ampinga ‘Ali65635

 
Tazama tafsiri na maelezo ya wanazuoni rasmi wa Hadithi, katika kujaribu kueleza uhalali wa umri wake mdogo wakati ndoa ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba, yanathibitisha umri mdogo. 
  

Rejeo la 2728 chini ya ukurasa huo huo linasema kwa sehemu: "Kwa hiyo ndoa ya Nabii (amani na iwe juu yake) na A’isha katika umri ambapo alikuwa karibu na kuvunja ungo ulikuwa umuhimu sana, kwani ilikuwa kupitia kwake mafundisho yangeweza kupitishwa kwa mafanikio kwa wanawake wadogo ambao ndio kwanza wameingia kwenye kundi la Uislam. Pia ndoa hii imepingana na nadharia potofu ambayo imeshamiri kwenye mawazo ya watu kuwa ilikuwa kinyume na miiko ya kidini mtu kuoa binti ya mtu mwingine ambaye amemwita kuwa kaka yake." [Abu Bakr na Muhammad walikuwa mtu na kaka yake kidini, lakini si kwa kuzaliwa.]
  
Waislam wamesema kuwa ama watu walioa/olewa wakiwa na umri mdogo wakati ule na/ama wasichana kwenye nchi zenye joto wanayo kawaida ya kupevuka mapema zaidi. Hata hivyo, umri wa kuanza ndoa si jambo la msingi, kwani hata wakati watoto wanaoa/olewa wakati wote wana umri chini ya mwaka mmoja, hawaanzi kuishi pamoja kama mume na mke hadi mke anapofikisha umri wa kutosha kuweza kupata watoto. Matokeo ya mfano wa Muhammad, kama ilivyoelezwa huko nyuma, wasichana wa Kiislam wa Nigeria wamekuwa wakiolewa mapema sana, na kuwa wajawazito kabla miili yao haijawa na uwezo wa kupata watoto. Wasichana hawa wa Kinigeria nao walilelewa kwenye sehemu yenye joto.
 
Vipingamizi 11 Vinavyowezekana
Wazo linaloungwa mkono na watu wachache linakataa kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na msichana mwenye miaka tisa, mara nyingi wanadai kuwa A’isha alikuwa na umri wa miaka 17 hadi 19. Zifuatazo ni sababu zinazotolewa, na maitikio yake.
 
 
Pingamizi la 1: Mashaka juu ya Watatu wa Waenezaji
1.1 Mtu mmoja kutoka Quraysh ambaye jina lake halifahamiki ni mwenezaji kwenye al-Tabari juzuu ya 7, uk.7, ambayo ni kumbukumbu dhaifu.
1.2 Hisham ibn ‘Urwah ni mwenezaji kwenye nukuu nyingi. Kama alikosea sawa na watu wote wanao mnukuu kiusahihi nao watakuwa na taarifa isiyokuwa sahihi. Mizanu'l-ai`tidal, kitabu chenye kuelezea [madokezo ya maisha ya] waenezaji wa simulizi za Nabii (amani na iwe juu yake) anaripoti kuwa alipokuwa mzee, kumbukumbu ya Hisham iliharibika vibaya sana (juzuu ya 4, uk.301-302). 
Tehzibu’l-tehzib
, moja ya vitabu vinavyofahamika sana kuhusu maisha na kuaminika kwa wenye kusimulia simulizi za Nabii (amani na iwe juu yake) kinaripoti kuwa kwa mujibu wa Yaqub ibn Shaibah: "masimulizi ya Hisham yanaaminika isipokuwa yale yaliyoripotiwa kupitia watu wa Iraq." Kinaendelea kusema kuwa Malik ibn Anas alizipinga simulizi za Hisham ambazo ziliripotiwa kupitia watu wa (juzuu ya 11, uk. 48 - 51).
1.3 Muhammad ibn Amr anaitwa dhaifu na Ibn Abu Hatim kwenye Al-Jarah wa al-Ta’deel: Yahya alisema, "yuko miongoni mwa watu ambao ungependa [kuripoti kupitia kwao]." Abu Hatim alimuuliza Malik ambaye alisema kitu kama hicho, na Yahya bin Mu’een alisema "Watu wanajiepusha kuzikubali simulizi zake"
Al-Dhahabiy kwenye "Siyar Aa`laam al-Nubalaa", anasema kuwa Juzyanniy alisema kuwa Muhammad ibn Amr hana nguvu [ya kuaminika]. Al-Dhabahiy pia anasema Yahya ibn Qataan alisema Muhammad ibn Amr hakuwa mwangalifu sana katika kuripoti masimulizi.
‘Uqailiy pia alisema Muhammad ibn Amr alikuwa msimuliaji dhaifu [asiyeaminika sana] kwenye al-Du`afaa al-`uqailiy, juzuu ya 4, uk.109. 
  

Itikio la pingamizi la 1: Hata kwa kudhania Hisham, ibn Amr, na mtu ambaye jina lake halijatajwa ni waenezaji dhaifu, kuwa wadhaifu haimaanishi kuwa si sahihi. Vipi pia kuhusu wengine wengi zaidi ambao si dhaifu? Lifuatalo ni jedwali la kurekodia matokeo:
 
Jedwali la Kurekodia Kumbukumbu 
 
MsimuliajiKumbukumbu Zenye NguvuKumbukumbu DhaifuKumbukumbu Zenye Kupinga
Al-Bukhari41-
Sahih Muslim31-
Abu Dawud61-
Tirmidhi---
Nasa’i---
Ibn-i-Majah11-
Ibn Ishaq1--
al-Tabari031
JUMLA1571

Kumbukumbu 7 dhaifu hazizibatilishi kumbukumbu zenye nguvu; badala yake zinaziongezea kuaminika kwake. 

 
 
Pingamizi la 2: Hakuna waenezaji wengine wa Madina
Hisham ibn ‘Urwah aliishi Madina miaka 70 kisha akahamia Iraq. Inakuwaje hakuna mtu mwingine yoyote kutoka Madina anayesimulia kuwa A’isha alikuwa na miaka nane au tisa? Pia wasimuliaji wengine wote wanatokea Iraq.
 
Itikio la pingamizi la 2: Hili ni dai linalotegemea ukimya: watu wengi hawakuripoti kitu chochote kuhusu umri aliokuwa nao A’isha wakati ndoa yake ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba. Pai Iraq ingeweza kuwa chanzo kizuri, kwa sababu kufikia wakati wa ‘Uthman wengi wa wandani wa A’isha walihamia Iraq. Hakika tunaweza kudhani kuwa A’isha alikumbuka muda alioolewa na aliwaambia watu wengine.
 
Pingamizi la 3: Je Waarabu walikuwa na ndoa za watoto?
Hakuna sehemu [inadaiwa] inayoongelea ndoa za watoto katika historia ya Waarabu, kwa hiyo kama Muhammad alifanya jambo hili, ingetegemewa kuwa jambo hili lisilokuwa la kawaida lilipotiwe na idadi kubwa ya watu. Hakuna mtu ambaye angeibishia ndoa hii ya umri mdogo kama ingekuwa haijawahi kutokea.
 
Itikio la pingamizi la 3: Ingawa jambo hili liliripotiwa na watu kadhaa, kuna angalau ndoa moja (na ukamilisho wake kwa tendo la unyumba) ya watoto inayoongelewa na watu wa Muhammad. Mwanamke mmoja [inadhaniwa kuwa aliolewa] alipata mjukuu akiwa na umri wa miaka 21 kwa mujibu wa Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 48 sura ya18 na.831, uk.514. Mwisho, kwa kuwa hakuna mtu aliyepinga taarifa ya ndoa hii ya watoto, hata wengi wa wanazuoni wa Kiislam wanaoamini kuwa ilitokea.
 
 
Pingamizi la 4: Msichana mdogo wakati Sura 54:46 ilipoandikwa
A’isha alisema alikuwa msichana mdogo wakati Sura 54:46 [al-Qamar inayohusu kugawanyika kwa mwezi] ilipoandikwa, ambayo [inadaiwa] ilitokea karibu miaka 9 kabla ya Hija. Hakusema kuwa mtoto mchanga [sibyah], bali msichana mdogo [jariya]. (imechukuliwa kutoka http://www.understanding-islam.com/ri/mi-004.htm)
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Bukhari, kitabu'l-tafsir, Arabic, Bab Qaulihi Bal al-sa`atu Maw`iduhum wa'l-sa`atu adha' wa amarr.
 
Itikio la pingamizi la 4: Kuna sehemu tatu za jibu hili.
1a (matumizi ya neno): Wazo hili limesimamia kwenye hoja inayodhaniwa kuwa neno jariya ambalo ni neno la kawaida kwa msichana mwenye miaka chini ya kumi halikuweza kutumika. Hata hivyo masimulizi mengi yanasema kwamba A’isha alikuwa bado anachezea midoli wakati alipokuwa anaolewa na Muhammad.
1b (sura isiyokuwa sahihi): Ni rahisi kwa wasimuliaji wachache kusahau sura sahihi kuliko wasimuliaji wengi kusahau kuwa alikuwa mke mwenye umri mdogo.
1c (muda usiokuwa sahihi wa Sura): Inawezakuwa ni sura sahihi, lakini hatuna uhakika lini Sura 54:46 iliandikwa. Ibn Hajar kwenye Fath al-Baariy na Maudid wanasema ilikuwa karibu miaka 5 kabla ya Hija, sio miaka 9 kabla.
 
 
Pingamizi la 5: Aisha akiwa Badr na Uhud
Baadhi ya simulizi zinasema kuwa A’isha alikuwa pamoja na jeshi kwenye vita vya Badr na ‘Uhud (vyote hivyo mwaka 3 BH). Hadithi hizi pia zinaonyesha kuwa wavulana wenye umri wa chini ya miaka 15 waliruhusiwa kushiriki kwenye Vita vya ‘Uhud. al-Tabari juzuu ya 12, uk.75 inasema mvulana alishiriki kwenye Vita vya al-Qadisiyyah mara tu baada ya kufikisha umri wa kubarehe. Masimulizi yanayomtaja A’isha akiwa ‘Uhud ni: BukhariKitabu'l-jihad wa'l-siyar, vya Kiarabu,Bab Ghazwi'l-nisa' wa   qitalihinna ma`a'lrijal. Vitabu vyenye kuonyesha kuwa wavulana wenye umri wa chini ya miaka 15 hawakuruhusiwa kushiriki ni: Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 48 sura ya 18 na.832, uk.514, Kitabu'l-maghaziBab ghazwati'l-khandaq wa hiya'l-ahza'b.
 
Itikio la pingamizi la 5: A’isha, akiwa msichana, hakuwahi kupigana vita yoyote ile. Umri wa miaka 15 "ni ukomo kati ya utoto na ukubwa". Kwa hiyo msichana angekuwepo kwa ajili ya nini?
Msichana wa miaka 10/11, licha ya kuwa pamoja na Muhammad usiku, alikuwa na vitu vingi sana ambavyo angeweza kufanya. Wanawake na watoto wadogo walikwenda kwenye uwanja wa vita baada ya vita na kuwapa maji Waislam waliojeruhiwa na waliwamalizia maadui waliojeruhiwa. al-Tabari juzuu ya 12 uk.127, 146. Wakati wa siku za vita, wanawake na watoto walikuwa wanachimba makaburi ya watu waliokufa. al-Tabari juzuu ya 12, uk.107.
Mwisho, msichana mdogo A’isha alichukuliwa kuwa mtu mzima, kwa sababu Waislam walimwita msichana mtu mzima mara alipoanza siku zake za mwezi kwa mujibu wa maelezo ya mtafsiri wa Kiingereza kwenye Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 48 sura ya 18 kabla ya na.832, uk.513.
 
 
Pingamizi la 6: Dada yake A’isha aliyemzidi miaka kumi alikufa mwaka 73 BH akiwa na umri wa miaka 100. 
Taqri’bu’l-tehzi’b
 na Al-bidayah wa’l-nihayah wanasema kuwa ‘Asma alikufa mwaka 73 BH wakati akiwa na miaka 100. Kwa kuwa Asm’a atakuwa alikuwa na miaka karibu 26/27 mwaka 1 BH, A’isha atakuwa na miaka 16/17 mwaka 1 BH, sio miaka 8-9. (Umri wa Asm’a wakti alipokuwa anakufa umeongelewa na: ibn Hajar al-Asqalani kwenye Taqri'bu'l-tehzi'b uk.654 na ibn Kathir kwenye Al-bidayah wa'l-nihayah juzuu ya 8 uk.372, Kiarabu. Kwamba ‘Asma alikuwa na miaka kumi zaidi imeongelewa kwenye: Abda'l-Rahman ibn abi zanna'dSiyar A`la'ma'l-nubala'Al-Zahabi, juzuu ya 2, uk.289, Kiarabu, Mu'assasatu'l-risalah, Beirut, 1992, ibn Kathir kwenye Al-Bidayah wa'l-nihayahIbn Kathir, juzuu ya 8, uk. 371, Kiarabu, Dar al-fikr al-`arabiAl-jizah, 1933).
 
Itikio la pingamizi la 6: Kwa kuchukulia kuwa vitabu hivi viko sahihi katika jambo hili, watu wanaweza kuuripoti kwa makosa umri wa watu wengine baadaye ya kufa kwao.
Kwa mfano, kama unamwamini ibn Hajar kwenye upande wa awali kuhusu wakati ‘Asma alipokufa, utatakiwa pia kumwamini ibn Hajar kwenye Isabah IV, uk.359-360 anapomwonyesha A’isha kuwa aliolewa alipokuwa na umri wa miaka 9. (imeelezewa chini ya ukurasa kwenye al-Tabari juzuu ya 11, uk.141 rejeo la 766 chini ya ukurasa). 
Vipi kuhusu midoli? Kinyume na Pingamizi la 6, mwandishi aliripoti kuwa vyanzo vingi vya Kiislam vinamwelezea A’isha kuwa alikuwa bado akichezea midolo alipoolewa. (Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 8 sura ya 548 na.3310, 3311, uk.716; Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 29 sura ya 1005 na.5981-5982, uk.1299; Sunan Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1769 na.4913, uk.1373, ibn Hanbal.
 
  

Pingamizi la 7: al-Tabari alisema Abu Bakr alikuwa na watoto wanne kabla ya kipindi cha Uislam.
Kwa kuwa A’isha alikuwa mmoja wa watoto hao, atakuwa alikuwa na umri wa miaka angalau 13 au 14 wakati ndoa yake ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba.
 
Itikio la pingamizi la 7: al-Tabari juzuu ya 11, uk.141 rejeo la 766 chini ya ukurasa linasema kuwa al-Tabari anapingana hapa. Pia alisema kuwa A’isha alikwa na miaka 8-9 wakati ndoa ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba. Tabari aliripoti idadi kubwa ya vitu, na yeye au vyanzo vyake vilikuwa na makosa kwenye vitu kadhaa. Hata hivyo, mtu angeweza kukumbuka kitu muhimu zaidi kuliko kitu ambacho sio muhimu. Al-Tabari ana sehemu tatu zenye kusema kuwa A’isha alikuwa na miaka 8-10 wakati ndoa ilipokamilishwa kwa tendo la unyumba, na ni sehemu moja tu inayoweza kumonyesha kuwa na umri mkubwa zaidi.
 
 
Pingamizi la 8: A’isha aliukubali Uislam kabla ya ‘Umar bin Khattab kwa mujibu wa Ibn Hisham kwenye Sirah al-Nabawiyyah juzuu ya 1, uk.227-24 (Kiarabu). Alikuwa mtu mwenye umri wa miaka 20/21 wakati ambapo ‘Umar alikuwa na miaka 41 (sehemu hiyohiyo juzuu ya 1, uk.295). Kwa hiyo Muislam mmoja anadai kuwa jambo hili linathibitisha kuwa A’isha alilazimika kuukubali Uislam katika mwaka wa kwanza (karibu mwaka 610 BK).
 
Itikio la pingamizi la 8: Kuna sehemu tatu za jibu.
1. Hakuna mtu leo hii anayeujua mfuatano halisi. Kwa ujumla kuna kutofautiana kwa kiasi kikubwa kuhusiana na mfuatano wa watu walioupokea Uislam, kama al-Tabari juzuu ya 5, uk.80-87; juzuu ya 12, uk.38 zinavyoelezea. Kama hawawezi kuafikiana juu ya watu watano wa kwanza, ni kwa vipi wataweza kuafikiana juu ya mtu wa 21?
 
2. A’isha hakuwa amebadilika na kuwa Muislam, kwa sababu hakuwahi kukumbuka muda ambao Muhammad hakwenda kwa wazazi wake mara mbili kwa siku na wazazi wake hawakuwa Waislam. Jambo hili lilitokea kabla ya kuhamia Ethiopia kwa mara ya kwanza (617 BK) (Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 sura ya 44 na.245, uk.158).
3. ‘Umar alikuja kuwa Muislam mara baada ya kuhamia Ethiopia (617 BK) kwa mujibu wa Ibn Ishaq uk.155, 156. Kwa hiyo kitu ambacho Ibn Hisham anakihesabu kuwa ni kubadilika kwa A’isha kuwa Muislam kunaweza kutokea kati kuzaliwa na umri wa miaka mitatu.
 
Pingamizi la 9: Kwa mujibu wa al-Tabari, miaka nane kabla ya Hija, wakati Abu Bakr alipopanga kuhamia Habshah, A’isha alikuwa ameposwa na Mut’am. Abu Bakr alimuomba Mut’am kumchukua Aisha aende nyumbani kwake, lakini Mut’am alikataa kwa sababu Abu Bakr amekuwa Muislam. Kwa hiyo A’isha atakuwa alikuwa na umri mkubwa wa kutosha kuwa mke miaka nane kabla ya Hija. Kumbukumbu nyingine ni Tehqiq e umar e Siddiqah e Ka'inatHabib ur Rahman Kandhalwi, Urdu, uk.38, Anjuman Uswa e hasanah, Karachi, Pakistan
 
Itikio la pingamizi la 9: Hata kama maelezo haya ni sahihi, Waarabu wa wakati ule hata leo mara nyingi wanawaposa wasichana mara wanapokuwa wamezaliwa. Abu Bakr alikuwa na mabinti wengine kwa hiyo inawezekana kuwa alikuwa mmoja wa hao.
 
 
Pingamizi la 10: Kwa mujibu wa mtaalamu wa sheria wa Kiislam Ahmad ibn Hanbal, kabla A’isha hajaolewa, alikuwa anaitwa Kiarabu Bikr, ambayo maana yake ni bikira au mwanamke ambaye bado hajaolewa. (Musnad Ahmad ibn Hanbal, juzuu ya 6, uk. 210, Kiarabu, Dar Ihya al-turath al-`arabi, Beirut. 
  

Itikio la pingamizi la 10: Neno bikr linamaanisha bikira na halina umri maalum. Kama alikuwa tayari mwanamke mkubwa, kwa nini Muhammad alingoja kwa miaka mitatu baada ya kumuoa kabla ya kukamilisha ndoa kwa tendo la unyumba? Pia, maelezo ya mtafsiri wa Kiingereza kwenye Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 48 sura ya 18 kabla ya na.832, uk.513 yanasema kuwa walimwita msichana mtu mzima wakati alipoanza siku zake kwa mara ya kwanza.
 
 
Pingamizi la 11: Ibn Hajar aliripoti kuwa Fatima, binti wa Muhammad, alizaliwa wakati Muhammad alipokuwa na umri wa miaka 35, kitu ambacho kitamfanya awe na miaka mitano zaidi ya A’isha. Jambo hilo litamfanya A’isha awe na miaka 15/16 wakati walipokamilisha ndoa yao kwa tendo la unyumba. (Al-isabah fi tamyizi'l-sahabahIbn Hajar al-Asqalani, juzuu ya 4, uk.377, Kiarabu, Maktabatu'l-Riyadh al-hadithaal-Riyadh, 1978).
  
Itikio kwa pingamizi la 11: Sunan Nasa’i juzuu ya 1 #29, uk.115-116 (Maneno ya Kiingereza kwa mbele)
 kwa kweli inasema kuwa Fatima alikuwa na umri wa miaka 29 alipokufa (miezi sita baada ya Muhammad), jambo ambalo linamfanya awe na miaka kumi zaidi ya A’isha. Kwa hiyo ama Ibn Hajar, au vinginievyo watu wengine wote wanafanya makosa. Hadithi zenye kuaminika zingeaminiwa na wengi wa Waislam kwa Kisuni kuliko Ibn Hajar, hata kama A’isha alikuwa na umri mdogo.
Vipi Kama Muhammad Hakufanya Hivyo Kabisa?
Hebu tudhanie kwa muda mfupi, kuwa baadhi ya Waislam waliochukua fikra za Kimagharibi wako sahihi katika jambo hili; vyanzo vyote vya Hadithi na mengi ya maelezo ya al-Tabari yanayohusiana na jambo hili si sahihi, na kwamba A’isha hakuwa na miaka 8 au 9 bali msichana wa miaka kumi na (teenager) wakati Muhammad alipokamilisha ndoa yake naye. Kama Hadithi zote hizi nyingi si sahihi basi kuna maswali manne ya kuwauliza Waislam.
1. Nini maana ya "Suni" kama siyo mapokeo ya Kiislam ya Hadithi?
Ni kitu gani kinachofautisha Muislam wa madhehebu ya Suni? Ni mtu ambaye:
a) kisiasa anafikiri kuwa Abu Bakr, 'Umar, na 'Uthman walikuwa makhalifa sahihi
b) kidini anaamini Sunnah, au mapokeo kwenye Hadithi yanaaminika mara nyingi, na angalau kwamba Allah hakutoa Hadithi ili kuwaongoza watu kufanya vitu vibaya ambavyo Allah asingeviunga mkono.
 
2. Ni kwa nini Allah aliruhusu Hadithi ziibadilishe jamii ya Kiislam kwa zaidi ya miaka 1,200?

Fikiria kuenea kwa mabibi arusi wadogo leo kulikoelezewa Nigeria na maeneo mengine ya Kiislam, na masumbufu ya kiafya ya wasichana ambao ndio kwanza wameanza kupata siku zao za mwezi lakini bado wadogo sana kiasi cha kuweza kuzaa Hata kama baadhi ya Waislam wenye fikra za kisasa wako sahihi au sehemu kubwa ya wasomi wa Kiislam itakuwa sahihi, kila mtu anakubali kuwa Hadithi zenye kuaminiwa za Waislam wa madhehebu ya Suni zimetoa mfano wa Muhammad kukamilisha ndoa yake na A’isha kwa tendo la unyumba wakati binit akiwa na miaka 8/9 na akichezea midoli.

Kama Hadithi zote hizi zisingekuwa sahihi, unadhani kuwa zinatoa mfano mbaya, na kuunga mkono vitendo hivi vya kikatili?
 
"Allah ni mwenye njama/mwongo." Sura 3:54. Je uongo huu ulikuwa ni moja ya njama za Allah, njama za Shetani, au tendo la ndoa na msichana wa miaka tisa halikuwa njama?
 
3. Kwa mujibu wa Uislam, kitu gani kitatokea endapo utalifuata dhehebu lisilokuwa sahihi?
Kwa mujibu wa Hadithi hizo hizo, Waislam watagawanywa kwenye madhehebu 72 au 73, na watasema wazi kabisa kwamba madhehebu yote yatakwenda Jehanamu isipokuwa moja. (Abu Dawud juzuu ya 3 na.4579-4580, uk.1290-1291; Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 36 sura ya 17 na.3992, uk.312). Kurani pia inawakemea watu wote wanaojitenga na kuwa dhehebu kwenye Sura 30:32. Kama Hadithi si sahihi kuhusiana na jambo hili, na zinafanya uovu kuunga vitendo hivi vibaya, kama wewe ni Muislam wa madhehebu ya Kisuni, upo kwenye dhehebu lisilokuwa sahihi. "U-Suni" wenyewe
a) umewapotosha watu vibaya sana
b) umewahukumu Waislam ambao wapo kwenye dhehebu lenye kupotosha. Kama watu wamejikuta wako kwenye "dhehebu lisilokuwa sahihi", je endapo wanataka kumpendeza Mungu, haitawapasa kubadilika na kuliacha dhehebu hilo?
 
4. Je njia sahihi yaweza kuwa kitu ambacho hukukitegemea?
Kama Waislam wa madhehebu ya Suni hawangekuwa dhehebu sahihi na madhara ya kufuata mifano mibaya ni makubwa, je inawezekana kuwa njia sahihi haiwezi kuwa inaitwa Islam?
 
Maswali Manne kwa Waislam wa Kawaida tu
Kila mmoja anatakiwa kukubali kuwa Hadithi na wengi wa wanazuoni wa Kiislam wa zamani na hata siku hizi wanafundisha kuwa Muhammad alifanya tendo la ndoa na msichana mwenye umri wa miaka nane au tisa.
 
Yafuatayo ni maswali manne, lakini maswali haya ni kwa Waislam tu wanaofundisha kuwa Hadithi hizi zinaaminika.
 
1. Kwa nini Waislam wengi wanaamini kuwa sheria za Kiislam (Sharia) ni nzuri, lakini wanaficha sehemu mojawapo?
 
2. Je unaposema kuwa Muhamad hakuwahi kufanya dhambi, unamaanisha kuwa kitu chochote alichokifanya na kukiunga mkono hautasema kuwa si sahihi? Kama si hivyo, kuna aina yoyote ya ubakaji au kitendo chochote cha kujamiiana ambacho utakihukumu, hata kama Muhammad alikiruhusu au kukitenda?
 
3. Kwa nini Waislam wengi sana wenye fikra za ki-magharibi wanashindwa kuyafuata mafundisho ya Hadithi? Ni kitu gani wanachokiona ambacho labda wewe hukioni?
 
4. Kama unawaambia watu kuzifuata Hadithi, na unazo picha za watu za kawaida na zenye kutembea nyumbani mwako (ikiwemo TV), au unavaa nguo yenye rangi ya njao na wewe ni mwanaume, je umesoma vitu mbalimbali ambavyo Kurani na Hadithi zinasema kuhusu wanafiki?
 
Kuzuiliwa kwa picha zote za watu au wanyama (ikiwa ni pamoja na picha za kawaida na TV) kumeelezwa kwenye: 
Bukhari
 juzuu ya 3 kitabu cha 34 sura ya 41 na.318, uk.180-181; juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 45-46 na.447-450, uk.297-299; juzuu ya 8 kitabu cha 73 sura ya 75 na.130, uk.82-83; juzuu ya 9 kitabu cha 93 sura ya 56 na.646, uk.487. 
Sahih Muslim
 juzuu ya 3 kitabu cha 22 sura ya 5382 na.5246-5252, uk.1157-1158; juzuu ya 3 rejeo la 2519-2520 chini ya uk.1160-1161. 
Abu Dawud
 juzuu ya1 kitabu cha 1 sura ya 92 na.227, uk.55-56; juzuu ya 3 kitabu cha 36 sura ya 1769 na.4913-4914 rejeo la 4288, uk.1373. 
Sunan Nasa’i
 juzuu ya1 kitabu cha 1 sura ya 169 na.264, uk.240; juzuu ya 1 kitabu cha 9 sura ya 454 na.764, uk.471. 
Ibn-i-Majah
 juzuu ya 4 kitabu cha 29 sura ya 56 na.3359, uk.481; juzuu ya 5 kitabu cha 32 csura ya 44 na.3649-3651, uk.108-109. (na.3652 pia inaelezea jambo hili, lakini 3652 inafahamika kuwa Hadithi dhaifu (daif). 

 
Katika miaka ya mwishoni mwa 1960, kulikuwa na vitendo vya ukatili huko Saudi Arabia wakati pich za watu zilipoonyeshwa kwenye TV.
 
Hitimisho: Usimsikilize mtu anayeshika mapokeo, isipokuwa pale unapompata mshika mapokeo asiyekuwa na kigeugeu. Kama huwezi kumpata mshika mapokeo ambayo hana kigeugeu, basi …
 
 
Hitimisho kwa Usuni lakin Sio Waislam wa Madhehbu ya Kisuni
Kwa Waislam wa kisasa wenye fikra za ki-magharibi ambao wanazikataa Hadithi, hapa tena kuna maswali manne:
 
1. Je neno "Suni" linamaanisha nini?
 
2. Je Allah amewadanganya wafuasi wake kwa karne nyingi?
 
3. Je Uislam unasemaje kuhusu watu wanaoyafuata madhehebu yasiyokuwa sahihi?
 
4. Je njia sahihi yaweza kuwa ni ile ambayo haujaizingatia?
 
Hitimisho: Nyakati nyingine hata wana historia wenye ufahamu mkubwa huwa wanafanya makosa madogo madogo, lakini jambo hili si kosa dogo. Endapo wana historia wa Kiislam walisema jambo hil baya kuhusu Muhammad, unawezaje kumwamini Muhammad mwenyewe anayeelezewa kwenye historia ya Uislam? Hata kama Kurani inaruhusu tendo la ndoa na mtu ambaye mkono wako wa kuume unammiliki…
 
Badala Yake: Mfuate Mungu wa Kweli
Achana na mapokeo mabaya. Kwa ujumla, usiweke upendo na utiifu wako kwenye mapokeo yoyote yale. Mtafute Mungu tu. Hata Waislam wanaiheshimu Torati na Biblia, ingawa ni wachache tu ndio waliozisoma. Kwa nini usizisome Injili na kuona jinsi mafundisho ya Yesu yalivyokuwa tofauti?
 
Kiambatanisho: Tamaduni Nyingine
Tertullian, akiandika mwaka 200-240 BK, anasema kuwa hata washenzi "hawakuwapeleka kwenye biashara zao" wasichana hadi walipofikisha miaka 12, na wavulana hadi walipokuwa na miaka 14. Mandhari hapa ni uchumba katika ndoa, hata kama mtu anaweza kubisha kuwa hii ni kukamilisha ndoa kwa tendo la unyumba. On the Veiling of Virgins sura ya 11 uk.34. Sasa mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mbili na wako tofauti na Muhammad aliyeikamilisha ndoa yake na A’isha kwa tendo la unyumba akiwa na umri mdogo zaidi kuliko ule wa washenzi.
Marejeo
www.AnsweringIslam.org ni tovuti pana sana yenye kuwashilisha na kujadili mambo mengi ya Uislam.
 
Arbery, A.J. The Koran Interpreted Macmillian Publishing Co. 1955.
 
Ali, Maulawi Shr. The Holy Qur’an : Arabic Text and English Translation. Islam International Publications Limited. 1997 (Imechapishwa kwa msaada wa Waislam wa KiaAhmadiyya)
 
Awde, Nicholas mfasiri na mhariri. Women in Islam : An Anthology from the Qur’an and Hadiths. St. Martin’s Press 2000 (kurasa 207). Ananukuu kutoka Bukhari tu, na bila umakini wowote anaisadiki bila ushahidi kuwa Bukhari ina kila kitu kilichomo kwenye vitabu vingine.
 
Badawi, Jamal, Ph.D. Gender Equity in Islam : Basic Principles. American Trust Publications. 1995.
 
Caner, Ergun Mehmet. Voices Behind the Veil. Kregel Publications. 2003 (kurasa 218)
 
Hasan, Prof. Ahmad. Sunan Abu Dawud : English Translation with Explanatory Notes. Sh. Muhammad Ashraf Publishers, Booksellers & Exporters 1984 (juzuu tata)
  
The History of al-Tabari
. Ihsan Abbas na wengineo. Bodi ya uhariri. Juzuu 1-11. SUNY Press.
  
The Holy Qur-an : English translation of the meanings and Commentary
. Imetafsiriwa na ‘Abdullah Yusuf ‘Ali. Imerekebishwa na kuhaririwa na Presidency of Islamic Researches, IFTA, Call and Guidance. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Tarehe haijaonyeshwa)
 
Khan, Dr. Muhammad Muhsin (mfasiri) The Translation of the Meanings of Sahih Al-Bukhari Arabic-English. Islamic University, Al-Medina Al-Munawwara AL MAKTABAT AL SALAFIAT AL MADINATO AL MONAWART. Hakuna tarehe, hakuna hati miliki.
 
Malik, Muhammad Farooq-i-Azam. English Translation of the Meaning of AL-QUR’AN : The Guidance for Mankind. Institute of Islamic Knowledge. 1997.
  
Sahih Muslim
 by Imam Muslim. Rendered into English by ‘Abdul Hamid Siddiqi. International Islamic Publishing House. (tarehe haijaonyeshwa)
  
Sunan Ibn-i-Majah
 by Imam Abu Abdullah Muhammad b. Yazid ibn-i-Majah al-Qazwini. Translated by Muhammad Tufail Ansari. Kazi Publications 121-Zutgarnain Chambers, Ganpat Road, Lahore, Pakistan. Worldwide Copyright 1993 Zaki Publications Lahore Pakistan.
  
Sunan Nasa’i
 imetafsiriwa na Muhammad Iqbal Siddiqi. 1994 Kazi Publications.
  
The NIV Study Bible : New International Version
 Zondervan Bible Publishers. 1985. 

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW