Wednesday, April 13, 2016

MWANAMKE WA KIISLAM HANA HAKI MBELE YA MUMEWE

Leo nitawapa hadith kadhaa kuhusu Wanawake wa Kiislam na jinsi wanavyo onewa na Mtume Muhammad.
NGONO NI LAZIMA HATA KAMA MWANAMKE ANAUMWAKutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mume atakapomwita mkewe kwenye kitanda chake [kwa tendo la ndoa] na yule mke akakataa kumuitika, Malaika humlaani mpaka kupambazuke”[Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa atakapolala mwanamke hali ya kuwa amekihama kitanda cha mumewe. Hadiyth namba 4821 na namba 4822; Muslim, kitabu cha Nikaah, mlango uharamu wa mwanamke kujizuilia [kujitenga] na kitanda cha mumewe, Hadiyth namba 2602 na Hadiyth namba 2603 na 2604.]
MWANAMKE KABLA YA KUFUNGA LAZIMA APEWE RUHUSA NA MUMEWE. HUU NI MSIBA
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asifunge mwanamke [Swawm ya Sunnah] na huku mumewe yuko pamoja nae isipokuwa kwa idhini yake huyo mume na wala asimruhusu mtu katika nyumba ikiwa mumewe yuko isipokuwa kwa idhini yake huyo mume” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa Swamw ya Sunnah ya mwanamke kwa idhini ya mumewe, Hadiyth namba 4820; na katika Kitabu cha Tafsiri Qur aan, Suuratul Qul A’uwdhu birabbil Falaq, Hadiyth namba 4823; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa atachotoa mtumishi katika mali ya tajiri wake, Hadiyth namba 1710].
MWANAMKE WA KIISLAM HARUHUSIWI KUSAIDIA NDUGU ZAKE
Imepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Asitoe mwanamke kitu chochote kutoka katika nyumba ya mumewe isipokuwa kwa idhini ya mumewe.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha Nikaah, mlango wa Swawm ya Sunnah ya mwanamke kwa idhini ya mumewe, Hadiyth namba 4823; na Muslim, katika Kitabu cha Zakaah, mlango wa atachotoa mtumishi katika mali ya tajiri wake, Hadiyth namba 1710].
MWANAMKE WA KIISLAM KAZI YAKE NI KUMFURAISHA MUMEWE NA NGONO TU.
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu) amesema kwamba aliulizwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wanawake gani bora? Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Ambae humfurahisha [humpendezesha]anapomtazama, na humtii anapomwamrisha, mke humhifadhi katika nafsi yake na mali ya mumewe” [Imepokelewa na Ahmad, katika Musnad ya Kumi waliobashiriwa Jannah, Musnad waliobakia katika Mukthiriyna katika Swahaabah (Radhiya Allahu ‘anhum), Musnad Abi Hurayrah (Radhiya Allahu ‘anhu), Hadiyth namba 7245 na 9377 na 9445].
MWANAMKE WA KIISLAM HARUHUSIWI KUOMBA TALAKA
Katazo La Kudai Talaka Bila Ya Sababu Inayokubalika
Ndoa ni katika mambo Aliyoyaamrishwa Allaah na kuyahimizaMjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ndoa ni mafungamano ya kishari’ah baina ya mwanamme na mwanamke yenye mipaka, nidhamu, vidhibiti na kanuni maalumu; na inaathiri mengi; ima kujenga na kusimamisha familia ya Kiislamu yenye kuongozwa na kuongoka kwa uongofu wa Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwa miongoni mwa tofali la kuijenga jamiirabbaaniy [yenye kumuabudu Allaah pekee Mola wa viumbe vyote na yenye kufundisha Kitabu, kukisoma na kukifuata]; na ima kuvunja na kubomoa familia kwa kuivuruga vuruga na kuisambaratisha na kusababisha athari mbaya kwa jamii na watoto kwa kuachana kwa mume na mke.
Na katika yaliyokatazwa ambayo yameenea na kuzagaa kwa wenye kupenda dunia na kuiweka kando Aakhirah ni kwa mwanamke kumtaka au kumghilibu mumewe; iwe kwa kumhadaa au vinginevyo kwa kumshurutisha amuache mkewe ili apate kuolewa yeye au abakie yeye pekee yake [kama ni mke mwenza] hili limekatazwa kama ilivyothibiti katika Hadiythi kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mwanamke asitake (katika Riwayah: Si halali kwa mwanamke kudai kuachwa ukhti wake [mwanamke mwenzake] ili aichukue nafasi yake na kuolewa yeye; kwani hatopata isipokuwa yale aliyoandikiwa.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, kitabu cha tafsiyr ya Qur-aan, Surat Qul A’uwdhu Birabbil Falaq, Hadiyth namba 6141 na 4782; na Muslim, katika Kitabu cha ndoa, mlango wa Uharamu wa kuwakusanya mwanamke na Shangazi yake, Hadiyth namba 2527; na Abu Daawuud, katika Kitabu cha atw-Twalaaq, mlango katika mwanamke anamtaka mumewe talaka ya mke wake, Hadiyth namba1865].
Max Shimba Ministries Org

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW