Thursday, February 21, 2019

JE, YUKO WAPI MUNGU BABA KWENYE AGANO LA KALE?

Image may contain: sky, cloud, text and outdoor
Ukweli unaoshangaza ni kwamba watu walioishi ziku za Agano la Kale walikuwa na uelewa mdogo sana juu ya Mungu Baba. Bali yeye alikuwepo na kwa kweli ametajwa mara-kadhaa.
Moja ya sababu zilizomfanya Kristo aje duniani kama mwanadamu ilikuwa ni kumdhihirisha Baba (Yohana 1:18; 5:37; 8:19; 14:7; Luka 10:22). Asingeweza kumdhihirisha iwapo kama Mungu wa Agano la kale ambaye ndiye Waisraeli walimjua, alikuwa ni Baba.
Tena basi kisababisho cha kwanza cha kuwepo kwa Mtu ambaye hatimaye alikuwa ndiye Baba kinapatikana kwenye sura ya kwanza kabisa ya ya Biblia. “Mungu akasema, Na tumfanye [sio mimi] mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;....” (Mwanzo 1:26). Hii haiashirii “uwingi wa mwenyezi” kama wasomi na wanazuoni wengine wanavyofikiri).
Kwenye aya ya 2 tumepewa jina linguine la “Bwana [YHVH] Mungu”” kama mshiriki mlengwa wa matendo na maneno wa hii “sisi.” Kumbe huyu –Wamilele (ambayo naiyo maana ya neno YHVH)—ndye kila mara ndiye anayeshughulika na wanadamu kama ujumbe wa Biblia unavyosema. Kwenye Mwanzo 14:18, tunamkuta Mtu huyu akiwa kama “mfalme wa amani na haki” (Melkizedeki kwenye Waebrania), “mfalme wa Salemu” (amani). Thibitisho? Usemi unaotumika hapa ni wa kumuelezea Melkizedeki huyu “kumeshuhudiwa kuwa anaishi”—kuwa ni wamilele (Waebrania 7:8). Kwa uthibitisho zaidi wa mwonekano huu wa Melkizedeki, msomaji anakaribishwa kuagizia jarida letu linalotolewa bure linaloitwa “Usiri kuhu Melkizedeki Umetatuliwa”.
Jambo la kuliangalia hata hivyo ni kwamba, Melkizedeki, YHVH, ndiye ambaye hatimaye alikuwa ni Yesu Kristo, aliyefanyika kuwa Mungu Mwana, ambaye kwa wakati ule alikuwa ni Kuhani (linganisha na Waebrania 7:1 na aya nyingine zinazofuatia na Waebrania 8:1), wa “Mungu Aliye Juu Sana”.(Mwanzo 14:18-22). Sasa, ni nani huyu basi aliyejulikana kama Mungu Aliye Juu Sana, mtu ambaye alikuwa ni kuhani? Basi Yesu mwenyewe na ajibu: “…Baba ni MKUU kuliko mimi. (Yohana 14:28).
Ni kweli,
Lakini hebu na tupate uhakika. Je, alikuwa ni Yesu Kristo gani mwana wa “na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli;” malaika alimwambia Mariamu kabla hata Yesu mimba yake haijatungwa kwamba “kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu … Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu,” (Luka 1:35,32).
Luka 8:28 na Marko 5:7 zinathibitisha kuwa Yesu ni “Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana” na Mwana wa Mungu Aishie Juu Sana”. Baba ametajwa mara mbili zaidi kwa jina hili kwenye Agano Jipya—Matendo 7:48 na 16:17.
Ni nani basi Yesu anayetuambia tumuombe dua zetu? Ni Baba (Mathayo 6:9). Na ni nani ambaye Daudi alikuwa anamuomba? “Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.” (Zaburi 57:2). Na tena “Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu” (Zaburi 7:17).
Ndiyo, inawezekana kuwa kwa hakika Daudi alimjua Yule ambaye hatimaye atakuwa Baba (kumbuka, asingeweza kumuitwa Baba na huku akiwa bado hajawahi kuwa na Mwana. Melkizedeki, YHVH alikuwa hajawa Mwana bado). “Neno la Bwana [YHVH] kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako” Zaburi 110:1; Waebrania 1:13
Daudi aliimba, “Bwana alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake” (IISamweli 22:14).
Je, Musa pia alilijua hilo? “Aliweka mipaka ya watu Kwa kadiri ya hesabu…” Kumbukumbu la Torati 32:8).
Nebukadneza mpagani kwa hakika asingeona ni vigumu kuwaamini washiriki wawili walio mbalimbali lakini pamoja kwenye familia ya Mungu. Wababelonia waliabudu miungu mingi sana ya uwongo. Baada ya Nebukadneza kusababisha watu watatu wafungwe na watupwe kwenye tanuru la moto, hatimaye alichungulia ndani na kuwaona “Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.” (Danieli 3:25-26).
Nabii Danieli aliona kinabii kurudi kwa ufufuo na kupaa mbinguni kwa Kristo na kwenda mbinguni kwa Baba ili akaupokee Ufalme (pia soma Luka 19:11,12,15): “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa” (Danieli 7:13-14). Huyu “Mzee wa Siku” anayetajwa hapa anamaanisha ni Baba ingawaje kwenye aya ya 9 inaonyesha kuwa Mwana anaweza pia kuitwa “Mzee wa Siku” sawa tu na anavyoweza kuitwa Wamilele [YHVH].
Huenda hata manabii wanaweza kuwa na fununu kidogo zinazoonyesha kuwa Mungu alijulikana kama familia: “Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?” (Mithali 30:4).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW