*Karama ni nini?*
Karama (kutoka Kiarabu الكرامة) ni zawadi yoyote inayotokana na ukarimu wa Mungu kwa viumbe wake.
*Kipawa ni nini?*
Vipawa/kipawa ni uwezo, nguvu, zawadi ya tofauti iliyo zaidi ya wengine anayopewa mtu ili amtumikie MUNGU.
Kipawa ni kipaji anachopewa mtu na MUNGU ili amtumikie MUNGU.
*Kipawa na karama wakati mwingine ni kitu kimoja maana karama ni zawadi za Neema ambazo ROHO MTAKATIFU humpa mtu anayeokolewa na YESU KRISTO.*
Kuna vipawa vya asili yaani alivyozaliwa navyo mtu, kwa jina lingine vinaitwa vipaji, lakini pia kuna vipawa huja tu baada ya kuokolewa na YESU KRISTO.
Hivyo karama na vipawa wakati mwingine vinaweza kufanana.
Wapo watu hutumia vipawa vyao vizuri na wengine hutumia vipawa vyao vibaya.
Sijui wewe unatumiaje kipawa chako ulichopewa na MUNGU ili umtumikie katika kazi yake.
Kanisani kumejawa vipawa vingi lakini sio wote wenye vipawa wanavitumia kwa kazi ya MUNGU.
Kuna watu wana vipawa vya kuongea sana lakini wanavitumia kwa umbea, uongo na majungu na sio kutumia kipawa hicho kupeleka injili ya KRISTO.
Wengine wana vipawa vya kuhubiri lakini akihubiri saa moja yeye amejitaja jina Mara 20 huku yeye ambaye ndiye mwenye injili akimtaja Mara 1 tena katika mfano dhaifu, hiyo ni hatari sana.
Mwingine ana kipawa cha kuimba na katika albamu yake ya nyimbo za injili 9 hajamtaja YESU kwenye wimbo hata mmoja, hiyo ni hatari sana maana mtu anajiita mwimbaji wa nyimbo za injili harafu hamjui mwenye injili kwamba ni YESU KRISTO.
Najua wapo wanaotumia vizuri sana vipawa vyao lakini hata wanaotumia vibaya vipawa vyao nao ni wengi sana.
Ndugu, wewe unayesoma ujumbe huu na umepewa kipawa na Bwana YESU basi tumia kipawa chako kwa utukufu wa MUNGU na sio wewe kutafuta utukufu.
Usitumie kipawa chako kama utavyo wewe bali tumia kipawa chako kama atakavyo MUNGU.
Warumi 12:6-9 "Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema."
*Talanta ni Nini?*
Talanta ni fedha ya mtaji inayohitajika kuzalishwa ili kuongezeka.
*✓✓Kibiblia talanta ni karama au Huduma unayotakiwa kuifanyia kazi ili kumletea faida MUNGU.*
✓✓Talanta ni Huduma aliyoweka MUNGU ndani yako kwa lengo la kumzalia matunda.
Mathayo 25:14-18 " Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja TALANTA TANO, na mmoja TALANTA MBILI, na mmoja TALANTA MOJA; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule ALIYEPOKEA TALANTA TANO akaenda, akafanya biashara nazo, AKACHUMA FAIDA talanta nyingine tano.
Vile vile na yule MWENYE MBILI, yeye NAYE AKACHUMA nyingine mbili FAIDA.
Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake."
Ufalme wa MUNGU unakuhitaji ushughulike na unakuhitaji kuzitumia karama zako alizokupa ROHO MTAKATIFU baada ya wewe kuokoka.
Warumi 12:6-8 " Basi kwa kuwa TUNA KARAMA ZILIZO MBALIMBALI, kwa kadiri ya neema mliyopewa; IKIWA UNABII, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; IKIWA HUDUMA, tuwemo katika huduma yetu; MWENYE KUFUNDISHA, katika kufundisha kwake; MWENYE KUONYA, katika kuonya kwake; MWENYE KUKIRIMU, kwa moyo mweupe; MWENYE KUSIMAMIA kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha."
✓✓Nguvu uliyonayo mteule ni talanta ambayo unatakiwa uitumie kuwaleta watu kwa YESU KRISTO.
*Je unaitumiaje talanta yako?*
✓✓Mali zako au fedha zako ni talanta unayotakiwa kuitumia kuipeleka injili ya KRISTO mbele.
*Je unaitumiaje talanta yako?*
✓✓Karama na Huduma uliyopewa na ROHO MTAKATIFU ni talanta unayotakiwa kuitumia vyema ili kumzalia KRISTO matunda.
Wewe una Mali za MUNGU na hizo Mali MUNGU anataka faida itakayotokana na kuzalisha kwako kutoka katika Mali hiyo aliyokupa MUNGU.
*✓✓Mali za MUNGU kwako ni karama, vipawa, Huduma, utumishi, muda, fedha na vyote alivyokubariki.*
Ndugu hakikisha unamletea MUNGU faida inayotokana na uhai aliokupa, kutoka katika talanta ambayo MUNGU amekupa.
Shalom
Max Shimba Ministries
No comments:
Post a Comment