Saturday, October 23, 2021

MUISLAM WA KWANZA NI MWANAMKE BI KHADIJA BINTI KHUWEYLID

 


Ni Nani aliyekuja na dini ya kiislamu? 


Tunaposoma katika ufafanuzi wa aya ya 19-20 kati ka suratul Yusuf ulio ndani ya Qurani juzuu ya 12 chapa ya tatu ya Kiswahili ukurasa wa 311 kuna maneno ambayo yanaelezea mtu aliyekuja na dini ya kiislamu hapa duniani na maneno yenyewe ni haya… Unaona kwanza kulikuwako zaidi ya miaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo Nabii Muhammad khalafu wakausingizia Uislamu kuwa ndio ulikuja na kuuza watu. Kadiri ya ufafanuzi huu uliomo ndani ya qurani, na ushahidi wa vitabu maarufu vya hadithi za muhammad katika Sahih Al-Bukhari na Sahih muslim. Na vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na masheikh wa dini ya kiislamu, inathihirika waziwazi kuwa dini ya uislamu imeletwa na kuanzishwa na Muhammad (s.a.w.) mfano mzuri wa mwanzo wa dini ya uislamu tunauona katika kitabu kiitwacho maisha ya nabii muhammad (s.a.w.)


kilichotungwa na aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar na baadaye nchi ya Kenya marehemu Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy. Katika ukursa wa 18 kuna maneno yanayo husu mke wa Muhammad aliyeitwa Khadija binti Khuweylid nayo yanatuhadithia hivi… Akarejea kwa mkewe bibi Khadija, akamsimulia habari hii. Palepale bibi huyu akamwamini, akawa ndiye mtu wa awali kabisa kushehedusha shahada ya uislamu. Basi mwislamu wa mwanzo kabisa ni mwanamke.


Katika kitabu hicho hicho cha maisha ya nabii Muhammad ukurasa wa 18 kifungu c. wametajwa waislamu wa awali kabisa nao ni hawa… 


(i) Mwislamu wa kwanza Bibi Khadija bint Khuweylid Mtume aliamrishwa kufundisha dini siku ya jumatatu na bibi huyu alisilimu siku hiyo hiyo akafanya ibada na mtume usiku ule ule kabla ya mtu yeyote ulimwenguni huyu ndiye aliyefuzu kwelikweli.


(ii) Mwislamu wa pili Sayyidina Ali bin Abi Talib bin Abdul Muttalib Alipomwana mtume na bibi Khadija usiku ule wanafanya mpya aliwauliza, “hii ni ibada gani?” Mtume alimfahamisha na akamtaka awe pamoja nao lakini yeye alikataa kwanza akasema mpaka niende nikamshauri baba yangu”. Mtume akamkataza kuitoa siri ile nje. Mara asubuhi ya usiku ule ule, kijana huyu akaja kwa mtume akampa habari kuwa yeye yu pamoja nao. Akawa ndiye islamu wa pili duniani. Aliposilimu alikuwa kijana wa miaka 10 hivi. 


(iii) Mwislamu wa tatu na wa nne. Zayd bin Haritha Al Ka’bi na Bibi Aymana. Huru wa mtume na mwanawe wa kupanga alikuwa akikaa pamoja na mtume na akasilimu kama sayyidina Ali mchana wa jumane. Alisilimu yeye na mkewe, bibi ummu Aymana yaya wa mtume. Hawa wote ndio waislamu wa awali kabisa ambao walisilimu mara baada ya muhammad s.a.w. kuleta dini ya uislamu ambayo alianzisha rasmi hapa duniani jumatatu ya siku ya 17 ya mwezi wa ramadhani sawa sawa na 27 th December ya mwaka wa 610 baada ya Kristo. Kabla ya Muhammad dini ya kiislamu haikuwepo kabisa duniani.


Swali 

Nani wakwanza kuwaa mwislamu kati ya Muhammad na Bi Khadija?


Je, huoni kwamba Uislam unajichanga kwa Maandiko yake yenyewe?


Tafakari 


Chukua Hatua


Max Shimba Ministries

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW