Allah na Muhammad Wamemkopia Mtume Paulo: Uchanganuzi wa Kitaaluma
Na: Dr. Maxwell Shimba
Utangulizi
Mijadala kuhusu uhusiano kati ya Qur’an na Biblia imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika uwanja wa theolojia na falsafa ya dini. Swali kuu ni: Je, Qur’an ni ufunuo mpya kutoka kwa Allah, au ni mkusanyiko wa masimulizi yaliyotokana na maandiko ya Biblia? Kwa uchunguzi wa kitaaluma, ni wazi kwamba sehemu kubwa ya Qur’an inajengwa juu ya simulizi na mafundisho yaliyokuwepo katika Biblia maelfu ya miaka kabla ya Muhammad. Hoja hii inaleta hitimisho kwamba Muhammad na Allah waliegemea sana mafundisho ya Biblia na kwa namna fulani kumkopia Mtume Paulo, ambaye alieneza Injili ya Yesu Kristo kwa mataifa.
1. Qur’an na Urejeleo wa Biblia
Qur’an imejaa marejeo ya moja kwa moja ya simulizi za kibiblia, zikiwemo:
-
Yusufu (Sura ya 12 – Surat Yusuf), simulizi lililokuwapo katika Biblia takriban miaka 3500 kabla ya Qur’an.
-
Imran na familia yake (Sura ya 3 – Surat Al Imran), iliyoelezwa Biblia miaka 3000 kabla ya Muhammad.
-
Yona mwana wa Mittai (Sura ya 10 – Surat Yunus), simulizi lililojulikana tayari katika Agano la Kale.
-
Ibrahimu (Sura ya 14 – Surat Ibrahim), Baba wa Imani, ambaye simulizi zake ziliandikwa Biblia karne nyingi kabla.
-
Maria mama wa Yesu (Sura ya 19 – Surat Maryam), simulizi la kibiblia lililotangulia sana Qur’an.
Aidha majina na habari za manabii wakubwa kama Musa, Haruni, Daudi, Sulemani, Yakobo, Isa, na Yohana Mbatizaji, yamechukuliwa moja kwa moja kutoka Biblia. Qur’an hata hivyo haijawahi kutoa simulizi mpya, bali imetoa muhtasari usio na kina wa habari zilizokwishajulikana kwa Wayahudi na Wakristo.
2. Ushahidi wa Qur’an Kuhusu Chanzo cha Habari
Qur’an yenyewe inakiri kuwa Muhammad alisimuliwa habari za manabii na hakupewa ufunuo mpya kuhusu wao:
-
Qur’an 4:164 – “...na mitume wengine hatukukuhadithia habari zao, na Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.”
-
Qur’an 40:78 – “...miongoni mwao tumekusimulia, na miongoni mwao hatukukusimulia.”
Aya hizi zinathibitisha kuwa Muhammad alitegemea masimulizi yaliyokuwepo, badala ya kupokea ufunuo wa kipekee. Hii inapingana na madai ya Wahyi mpya, na inathibitisha urejeleo wa maandiko ya Biblia.
3. Qur’an Inavyowaamuru Waislamu Kurudi Kwenye Biblia
Qur’an mara kadhaa inawaelekeza wafuasi wake warejee katika vitabu vya awali (Torati na Injili):
-
Al-An’aam 6:154–155 – Musa alipewa Kitabu kilicho na maelezo ya kila kitu, na watu wakaamrishwa wakifuate.
-
An-Nisaa 4:136 – Waislamu wanahimizwa waamini vitabu vilivyoteremshwa kabla ya Muhammad.
-
Al-Maaida 5:46 – Injili ni nuru na uwongofu; yeyote aikataye hana nuru.
-
Yunus 10:94 – Muhammad mwenyewe aliambiwa akipata shaka, aulize kwa wale wanaosoma Maandiko yaliyokuwa kabla yake.
Kwa hiyo, hoja ya Waislamu kuwa Biblia imechakachuliwa inapingana moja kwa moja na Qur’an. Ikiwa Biblia ingekuwa imepotoshwa, basi Allah asingewaelekeza wafuasi wake warejee humo.
4. Hoja Dhidi ya Waislamu Wapinga Biblia
-
Kudai Biblia ni ya Paulo – Ikiwa kweli ni ya Paulo, kwa nini simulizi zake zimo katika Qur’an? Hii inamaanisha Allah na Muhammad walimkopa Paulo, na kwa mantiki hiyo Paulo anakuwa “akbar” (mkubwa) mbele ya Allah na Muhammad.
-
Kudai Biblia imechakachuliwa – Ikiwa imechakachuliwa, kwa nini Qur’an imejaa marejeo yake na kwa nini Allah aliwaamuru warejee humo?
5. Hitimisho
Kwa uchambuzi wa kitaaluma, ni dhahiri kwamba:
-
Qur’an imejengwa juu ya simulizi za Biblia.
-
Muhammad hakupokea ufunuo mpya, bali alisimuliwa habari zilizokuwa tayari katika Biblia.
-
Qur’an yenyewe inakiri na kuthibitisha uhalali wa Maandiko ya awali, ikiwemo Torati na Injili.
-
Hoja za Waislamu dhidi ya Biblia zinapingana na ushahidi wa Qur’an.
Kwa hiyo, hoja inabaki kuwa: Allah na Muhammad walimkopia Mtume Paulo na Biblia nzima. Paulo, kwa maana hiyo, anakuwa mkubwa mbele ya Muhammad na Allah, kwani maandiko yake yamekuwa msingi wa masimulizi ya Qur’an.
Mwisho, wito unabaki pale pale: Njoo kwa Yesu Kristo, Mungu Mkuu, aliyefunuliwa katika Biblia, ambaye ndiye nuru na wokovu wa ulimwengu wote.
No comments:
Post a Comment