Friday, May 13, 2016

WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI? (SEHEMU YA TATU)

Rafiki zetu wameanza kuweka majibu yao kwa kujaribu kutoa maelezo kuhusu swala la Allah kumtaka Muhammad asilimu kwa kusema kuwa sio kila unapotamka shahada maana yake unasilimu kwa maana ya kufanyika Muislamu, lakini pia wanasisitisa kuwa Muhammad mwana wa Abdallah na Amina ni muislamu tangu kuzaliwa kwa mujibu wa aya ya 30:30.
Lakini tukimakinika vyema utagundua hakuna jipya analotuelezea rafiki yetu, kwani kwa Mujibu wa aya nilizotangulia kuzitoa na naomba kurejea aya ya 6:14
" 14. Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. "
http://www.iium.edu.my/deed/quran/swahili/without/6.htm
Katika aya hii Muhammad hajapewa amri ya kutamka shahada , la, bali ametakiwa asilimu na katu asiwe miongoni mwa WASHIRIKINA; Hapa pia inabidi kuwakumbusheni swali nililotangulia kuuliza; Hivi je kabla ya amri hii alikuwa Muhammad miongoni mwa MAKAFIRI, WASHIRIKINA? Lakini pia aya hii ni Amri wala kamwe hatujaonyeshwa wapi alipotii amri hii mwana wa Amina.
Tukumbuke pia mazingira alolelewa ndani, yalikuwa mazingira ya kishirikina, kwa maana nimetoa ushahidi kuwa Babu yale, na hata Ami yake walikuwa Makafiri , washirikina na ndio waliomlea. hawa walezi wake walikufa katika hali hii ya ujahiliya.
Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu kama Ibrahimu, watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?
Tunasoma hivi:
Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said:Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).
عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَجُلا قَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ ، أَيْنَ أَبِي ؟ قَالَ: ((فِي النَّارِ)) فَلَمَّا قَفَّى دَعَاهُ ، فَقَالَ: ((إِنَّ أَبِي وَأَبَاكَ فِي النَّار)) مسلم
Yaani:
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.

Sio hayo tu, lakina pia hata Bi Amina mamake na Muhammad kafa kafiri. tunasoma
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((اسْتَأْذَنْتُ رَبِّي أَنْ أَسْتَغْفِرَ لأُمِّي فَلَمْ يَأْذَنْ لِي ، وَاسْتَأْذَنْتُهُ أَنْ أَزُورَ قَبْرَهَا فَأَذِنَ لِي )) مسلم
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Niliomba ruhusa kutoka kwa Allaah kumuombea msamaha mamangu, lakini Hakunipa ruhusa. Nikamuomba idhini nilizuru kaburi lake (mamangu), Naye Akanipatia ruhusa)) [Muslim]
Inaelezwa katika Kitabu cha ‘Awn al-Ma’abuud:
“Kauli yake (Muhammad) ((lakini Hakunipa ruhusa)) ina maana kuwa (mama yake) alikuwa kafiri na hairuhusiwi kumuombea maghfirah kafiri.”
Na swali ambalo tungependa tujiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mja wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu; Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia; Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Kuhusiana na Ibrahimu, hilo ni jambo ambalo Wakristo tunawaachia Waislamu wenyewe maana sisi wengine tunaamini na hata ushahidi wa kihistoria na kimaandiko unaonyesha wazi kwamba Ibrahimu hajawahi kamwe kukanyaga mguu wake Uarabuni.
Kwa mfano, ufuatao ni ushahidi mmojawapo juu ya jambo hili. Tunasoma kwamba:
Narrated Abu Dhaar: I said, "O Allah's Apostle! Which mosque was built first?" He replied, "Al-Masjid-ul-Haram." I asked, "Which (was built) next?" He replied, "Al-Masjid-ul-Aqs-a." I asked, "What was the period in between them?” He replied, “Forty years.” (Sahih Bukhari 4:55:636).
Yaani:
Imesimuliwa na Abu Dhaar: Nilisema, “Ewe Mtume wa Allah! Ni msikiti upi ulikuwa wa kwanza kujengwa?” Akajibu, "Al-Masjid-ul-Haram." Nikauliza, “Ni upi ulifuata?” Akajibu, “Al-Masjid-ul-Aqs-a.” Nikauliza, “Ulipita muda gani hapo katikati?” Akajibu, “Miaka arobaini.”
Muhammad naye ana mambo! Al-Masjid ul-Aqs-a ndiko hapo penye Ka’aba. Na Al-Masjid-ul-Haram ni hekalu la Mfalme Sulemani kule Uyahudi.
Sasa, hekalu la Yerusalemu lilijengwa na mfalme Sulemani kwenye takriban miaka ya 950 kabla ya Kristo (KK). Hii ni kusema kwamba, kama maneno ya Muhammad ni ya kweli – na ninaamini kwamba hakuna mwislamu ambaye anaweza kukiri kuwa Muhammad ni mwongo – basi, msikiti wa kwenye Ka’aba unatakiwa uwe ilijengwa kwenye 990 KK (ukiongeza hiyo tofauti ya miaka 40).
Hilo sio tatizo. Lakini shida inakuja unapomwingiza Ibrahimu. Ibrahimu aliishi takriban miaka 2000 kabla ya Kristo. Tazamahapa. Hii ni kusema, aliishi miaka takriban 1050 kabla ya kujengwa kwa hekalu la mfalme Sulemani. Sasa, kama Ibrahimu wa Muhammad aliyejenga Ka’aba aliijenga miaka 40 kabla ya hekalu la Sulemani, basi NI LAZIMA awe ni Ibrahimu mwingine na Ishmael mwingine tofauti kabisa na wale wa kwenye Biblia. Vyovyote iwavyo, hilo ni tatizo la Waislamu wenyewe kulitatua. Ni kazi kwao kujiridhisha na kujithibitishia wao wenyewe kwamba, kama wanataka imani yao itokane na Ibrahimu aliyeongea na Mungu wa Israeli, basi hali ndiyo hiyo!
Kutokana na ukweli huo hapo juu, tunabakia na uwezekano wa aina mbili: kwanza, kama Muhammad yuko sahihi juu ya hiyo miaka 40, basi Allah ndiye aliyekosea au aliongopa kusema kuwa Ibrahimu alijenga Ka’aba. Kama Allah yuko sahihi, basi Muhammad ndiye aliyekosea au kuongopa kwamba Ka’aba ilijengwa miaka 40 kabla ya hekalu la Sulemani. [Hata hivyo, kuna uwezekano kabisa huyu ni Ibrahimu mwingine kabisa. Hebu tutafakari yafuatayo:
Hata kama ka’aba ilijengwa na Ibrahimu (wa Biblia au mwingine tofauti), jambo moja ni dhahiri; kwamba wakati Muhammad anatokea na kuanzisha dini yake, ka’aba ilikuwa chini ya wapagani wa Uarabuni huku ndani na nje yake kukiwa na miungu zaidi ya mia tatu ili ndugu yetu amekubaliana nalo.
Ni mwaka 630 baada ya Kristo (BK), ndipo Muhammad na wafuasi wake walitwaa mamlaka ya mji wa Makka na kuifanya ka’aba kuwa sehemu ya kuabudia Mungu mmoja badala ya miungu zaidi ya mia tatu.
Ndugu zangu waislamu, ka’aba wala haina uhusiano na Mungu Mkuu aliyeumba mbingu na nchi. Ilikuwa ni madhabahu tu ya kipagani kwa ajili ya kuabudia miungu yao.
Hivi ndivyo tunavyoambiwa:
Narrated Abu Huraira: “In the year prior to the last Hajj of the Prophet when Allahs Apostle made Abu Bakr the leader of the pilgrims, the latter (Abu Bakr) sent me in the company of a group of people to make a public announcement: 'No pagan is allowed to perform Hajj after this year, and no naked person is allowed to perform Tawaf of the Ka’aba.'” (Bukhari V2, B26, #689 (V1, B8, No 365).
Yaani:
Imesimuliwa na Abu Huraira: “Kwenye mwaka kabla ya Hija ya mwisho ya Mtume pale Mtume wa Allah alipomfanya Abu Bakr kuwa kiongozi wa mahujaji, Abu Bakr alinituma pamoja na kundi la watu wengine ili kutoa tangazo: ‘Hakuna mpagani anayeruhusiwa kufanya Hija baada ya mwaka huu, na hakuna mtu aliye uchi anayeruhusiwa kufanya Tawaf ya Ka’aba.
Sijui ndugu msomaji kama unaiona maana ya maneno haya? Hiki ndicho tunachosoma humu:
1. Waislamu na wapagani walikuwa wakifanya hija pamoja kwenye ka’aba kwa miaka mingi hadi hapo Abu Bakr alipofanywa kiongozi.
2. Wakati wawapo kwenye hija, wapagani walikuwa wakifanya Tawaf (kuzunguka ka’aba) wakiwa uchi.
3. Wapagani walikuwa wakiabudu miungu yao ya kipagani kwenye ka’aba na waislamu wakimwabudu Allah.
Ili uone uzito wa jambo hili vizuri, hebu piga picha ya Hekalu la Sulemani alilojenga Yerusalemu kwa ajili ya Yehova. Yaani humo ndani ya hekalu wawe wanasali Wayahudi wanaomwamini Yehova na pia wapagani wanaoabudu jua, na mwezi na nyota; tena wakiwa uchi!!!!!!!
Kwa kuwa jambo hilo haliingii kamwe akilini; na haliwezekani, jibu ni moja tu: ni Muhammad ndiye aliyeenda kuingilia madhabahu ya wapagani na si kinyume chake!
Na ndiyo maana Muhammad alikuwa na ujasiri wa kutaka kuibomoa ka’aba. Hivi ndivyo tunavyosoma:
Narrated Aswad: Ibn Az-Zubair said to me, "Aisha used to tell you secretly a number of things. What did she tell you about the Ka'ba?" I replied, "She told me that once the Prophet said, 'O 'Aisha! Had not your people been still close to the pre-Islamic period of ignorance (infidelity)! I would have dismantled the Ka'ba and would have made two doors in it; one for entrance and the other for exit." (Sahih Bukhari 1:3:128).
Yaani:
Imesimuliwa na Aswad: Ibn Az-Zubaid aliniambia, “Aisha alikuwa akikusimulia kwa siri mambo kadha wa kadha. Je, alikuambia nini kuhusiana na ka’aba? Nikajibu, “Aliniambia kwamba, kuna wakati Mtume alisema, ‘Ewe Aisha! Kama watu wa kwenu wangekuwa bado hawako karibu na enzi ya ujinga ya kabla ya Uislamu (ukafiri), ningebomoa Ka’aba na ningejenga milango miwili; mmoja wa kuingilia na mwingine wa kutokea.’”
Hebu piga picha hapa pia; kwamba Musa aliambiwa na Yehova atengeneze hema ya kukutania. Akapewa maelekezo kwa undani sana ya namna kila kitu kinavyotakiwa kuwa, na akaambiwa afanye sawasawa na alivyoonyeshwa na Yehova. Halafu anakuja kutokea mtume au nabii miaka mia kadhaa inayofuata anasema, “Mimi naona katika nyumba hii Yehova alikosea kuweka mlango mmoja. Inatakiwa milango miwili hapa.” Hivi inawezekana kweli?
Sasa, kama kweli ni Allah ndiye alimwambia Ibrahimu na Ishmael wajenge ka’aba, inaingia kweli akilini Muhammad kuja kusema angeweza kuibomoa na kuijengea milango miwili?? Mwanadamu anaweza kumsahihisha Mungu?
Lakini hilo linawezekana tu kama nyumba yenyewe haina uhusiano wowote na Mungu; kama ambavyo ka’aba haina kamwe uhusiano wowote na Mungu wa mbinguni.
katika maelezo yake ndugu yetu katoa aya hii.2;285-286 . Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako. 286. Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. 286
Sasa hapa sijui hakika lengo la kutoa aya hii sijui, maana kama ni swala la Muhammad kuamini aliyoteremshiwa; basi miongoni mwa hayo aliyoteremshiwa ni aya ya 42:52; " 52. Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka."
Hapa Allah anamwambia ulikuwa kabla tukufunulie Qurani hii, ulikuwa ujui kitabu wala Imani; na ndio maana nikamwomba ndugu yetu atupe maelezo mwafaka haswa Ibada ya pangoni Muhammad kaifanya kwa utaratibu wa kitabu kipi , mwongozo upi, na Imani gani?
ndugu Ibrahimu pia amejaribu kusema neno Dhwa'lan hufasiri kutokana na mahala. .. lakini ajabu hakutupa ufafanusi wa aya ambazo yeye anapata ufafanusi mwingine wa neno Dhaallan kando na maana ya kupotea. mathalani mie nimetoa aya zingine kama vile, 4:136 " Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi huyo amekwisha potelea mbali. ..Faqad dhalla dhalallan baAAeedan.
6:77. Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea... Addhaallen
katika aya hizi bado neno Dhaallan bado linakuja kwa maana ile ile ya KUPOTEA; Hivyo Allah anavyomwambia, 93: 7. Na akakukuta umepotea akakuongoa? ; jamani hii sio tafsiri ya kwangu bali tafsiri za maulamaa waliosoma kutulikoni
lakini bila kutupa ushahidi rafiki yetu Ibrahimu anasema lengo la Muhammad kuamia pangoni ni kutokana na kuchukizwa na ibada za kishirikina walizokuwa wakifanya washirikina wa maka..
Na siku zote mitume wa Mwenyezi Mungu huepushwa na kufanya ibada ambazo mwenyezi mungu amezikataza...
kinyume na ili tunasoma; kutokana na Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:
'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."
Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.
Je ni ibada gani alizokuwa akizifanya mtume...
Kisha ndugu akadai Muhammad kabla ya utume wake kule pangoni alifanya ibada kwa utaratibu aliofundishwa na Mwenyezi Mungu ambao si wa kishirikina. Akatoa aya ya 40:55 Qur'ani. Imbayo inasema
"55. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi."
Sasa aya hii kipindi cha uteremsho wake na baada ya tukio la kuminywa pangoni; kisha aya hii Muhammad mbona anatakiwa kuomba msamaha kwa DHAMBI zake!!! ndio kule KUPOTEA, DHAALLAN, kumbe Allah anamtambua muhammad kuwa ni Mdhambi anayetakiwa kuomba msamaha kwa dhambi zake, kisa kumuhimidi jioni na Asubuhi.
Ama swala la kunilingania, nisikwende motoni nashukuru, sana japo hata mtume wako bado hana uhakika wa kuepuka huo mto na ndio maana mpaka leo Waislamu bado wanamswalia ili apate msamaha.
Ndugu yetu anahitimisha kwa kusema kuwa Muhammad hakuwa na haja ya kusilimu kwa sababu tangu kuzaliwa kwake alikuwa ni mwislamu. .aya ni ile ile niliyoitoa mimi 30: 30 Qur'ani.
Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.
فاقم وجهك للدين حنيفا فطرت الله التي فطر الناس عليها لا تبديل لخلق الله ذلك الدين القيم ولكن اكثر الناس لا يعلمون
Lakini aya hii kamwe haisemi kamwe kuwa Muhammad wala mimi nilizaliwa Muislamu baya zaidi nimekwisha kukuonyesheni ushahidi wa wazi kuwa Muhammad alikuwa miongoni mwa washirikina aliozaliwa ndani yao hadi kufikia hatua ya Allah kumupa amri ASIWE tena miongoni mwa washirikina.
Ni hitimishe tu kwa kusema bado hatuna ushahidi wa Uislamu wa Muhammad, ushahidi tulio nao unaonyesha wazi Khadija ndiye Muislamu wa kwanza Duniani wala hata huyu mzee Waraqa ambaye ndiye alimtaka ajibashirie utume, hatuoni pia akisilimu!
Fanya maamuzi; nafsi yako ni ya gharama Mpendwa.
NDIO MAANA BADO NAULIZA WAPI USHAHIDI KUWA MUHAMMAD KASILIMU AKAWA MUISLAMU? NA KAMA KASILIMU JE ALISILIMU LINI.
IKIWA kama KUNA MTU YEYOTE MWENYE USHAHID kuwa MUHAMMAD MWANA WA AMINA NA Bwana ABDALLAH ALIKUWA NI MUISLAMU? UWE NI USHAHIDI WA SURA, AU HADITH ALETE.
na Mwalimu Chaka
For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW