Saturday, May 7, 2016

MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO (YESU): MAX SHIMBA ANAJIBU MADA YA BERNARD NYANGASA



MTAWATAMBUA KWA MATUNDA YAO (YESU)
MAX SHIMBA ANAJIBU MADA YA BERNARD NYANGASA
"Bernard Nyangasa"
Ndugu msomaji,
Hii mada ni jibu kwa Bwana Bernard Nyangasa anaye jaribu kupindisha Neno la Mungu, kwa kumhusisha an au kuwaunganihsa Yahawe na Allah.
BERNARD NYANGASA ANASEMA:
Katika Matayo 7:15-24,Yesu anatutajia vigezo rasmi vya kuweza kuwagundua Wahubiri bandia, wanaofundisha mafundisho potofu.Kuwani "matunda" yao.Yaani kama mafundisho yao yanaafikiana na mafundisho ya Yesu.

MAX SHIMBA ANAJIBU:
***Jibu: Kwanza nitaanza kwa kuziweka aya ambazo Bwana Berbard Nyangasa amenukuu: Matayo 7: 15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
**** Jibu: Yesu alituonya kuwa “Wakristo wa uongo na manabii wa uongo” watakuja na kujaribu kuwadanganya hata wateule (Mathayo 24:23-27; angalia pia 2 Petero 3:3 na Yuda 17-18). Njia nzuri ya kujilinda na uongo na walimu wa uongo ni kuijua kweli. Ili ugundue pingamizi lichunguze pingamizi lenyewe. Muumuni yeyote ambaye, “analisoma Neno la ukweli” (2 Timotheo 2:15) na anafanyia uchunguzi Bibilia kwa makini anaweza kuitambua kanuni ya uongo. Kwa mfano, muumuni ambaye amesoma kazi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu katika Mathayo 3:16-17 papo hapo atashuku kanuni ambayo yakana utatu wa Mungu. Kwa hivyo, hatua ya kwanza ni kuisoma Bibilia na kuhukumu mafunzo yote kwa chenye maandiko yanasema.
***************************************************************************************************
BERNARD NYANGASA ANASEMA:

Aidha anatutahadharisha kuwa, Wahubiri hao bandia "watavaa ngozi ya kondoo".Kwa maana kuwa,watajifanya ni miongoni mwa wanaojiita wafuasi wa Yesu.Pia wapotoshaji hao watafanya miujizana maajabu makubwa (kuponyesha,kutoa mapepo nk) kwa kutumia jina la Yesu (aya 22-23). Tunasoma pia katika 2Yohana 9-11. "Kila apitaye cheo (kujitukuza),wala asidumu katika mafundisho ya Kristo,yeye hana Mungu.Yeye adumuye katika mafundisho hayo,huyo ana Baba na mwana pia.Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo,msimkaribishe nyumbani mwenu,wala msiimpe salamu.Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu".Angalia pia 1Timoth6:3-5.
LAKINI, Yesu anatupa njia rahisi ya kujua ukweli au uongo wa mafundisho.Anasema "Basi kila asikiaye hayo maneno yangu,na kuyafanya,atafananishwa na mtu mwenye AKILI,aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;mvua ikanyesha,mafuriko yakaja,pepo zikavuma,zikaipiga nyumba ile,isianguke;kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye,atafananishwa na mtu mpumbavu,aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;mvua ikanyesha,mafuriko yakaja,pepo zikavuma,zikaipiga nyumba ile,ikaanguka;nalo anguko lake likawa kuu" (Mathayo 7:24-27).YAANI; "Mvua,mafuriko,radi nk" ni maswali na hoja za kuhoji hayo mafundisho.Kama mafundisho ni sahihi,yanayowiana na maandiko,yatastahimili kujibu na kutoa ufafanuzi unaokubaliwa na akili.Lakini kama si sahihi,lazima yataumbuka tu.

MAX SHIMBA ANAJIBU:
****Jibu: Yesu alisema “kwa matunda yake mti hutambulikana” (Mathayo 12:33). Wakati unayatafuta “matunda” hapa kuna majaribio matatu hasa wastahili kuyatumia kutambua uangalifu wa mafunzo yake:
1) Huyu mwalimu anasema nini kuhusu Yesu? Katika Mathayo 16:15-16 Yesu anauliza, “Akawambia, Nyinyi mwaninena mini kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Katika 2 Yohana 9, tunasoma, “Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisno haya, huyo ana Baba na Mwana pia.” Kwa njia nyingine, Yesu Kristo ako hali moja na Mungu, yeyote ambaye anapuuza kifo cha Yesu kuwa kama dhabihu, na kukataa ubinadamu wa Yesu. Yohana wa kwanza 22: 22 yasema, “Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia.”
2) Je! Huyu mwalimu anaihubiri injili? Injili imefafanuliwa kuwa habari njema kuhusu kifo cha Yesu, kuzikwa kwa Yesu, na kufufuka kwa Yesu, kulingana na maandiko (1 Wakorintho 15:1-4). Jinsi yo yote ile yatakayo kuwa mazuri, kauli “Mungu anakupenda,” “Mungu anatutaka tuwalishe wenye njaa,” na “Mungu anataka uwe tajiri” sio ujumbe kamili wa injili. Vile Paulo anatuonya katika Wagalatia 1:7 “Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.” Hakuna mtu yeyote, hata mhubiri mkuu, ako na uhuru wa kuigeuza injili ambayo Mungu alitupa. “Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe” (Wagalatia 1:9).
3) Je! Huyo mwalimu anamiliki tabia ambazo zamtukuza Mungu? Kusungumzia walimu wa uongo, Yuda 11 yasema, “Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wemeangamia katika maasi ya Kora.” Kwa njia nyingine, mwalimu wa uongo anaweza kujulikana kwa kiburi chake (Kaini aliukataa mpango wa Mungu), tamaa (Balaamu anatabiri kwa ujira), na maasi (Kora anajinua zaidi ya Musa). Yesu alisema tuwe macho na watu kama hao na kwamba tutawajua kwa matunda yao (Mathayo 7:15-20).
************************************************************************************************
BERNARD NYANGASA ANASEMA:
WATU wanaochunguza maandiko,Biblia imewaita "Waungwana" .Inasema "Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya.Nao walipofika huko wakaingia katika Sinagogi la Wayahudi.Watu hawa walikuwa WAUNGWANA kuliko wale wa Thesalonike kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, WAKAYACHUNGUZA MAANDIKO KILA SIKU ,waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo" (Matendo 17:10-11).

MAX SHIMBA ANAJIBU:
****Jibu: Hapa sina tatizo napo kabisa maana Neno linasema kuwa watu hao wakayachunguza maandiko kila siku. Na hatusomi kuwa hao watu walitoa lawana au pinga maandika waliyo yachunguza kila siku bali kukubali kuwa Paulo na Sila walikuwa ni watumishi wa Mungu.
************************************************************************************************
BERNARD NYANGASA ANASEMA:
MAFUNDISHO yanayowekewa "kinga" ya "Fumbo la imani" ili yasihojiwe, HAYATOKANI na Mungu.Mwenyezi Mungu hana "aibu" ya kuficha.Ndio maana anatuhimiza tumtafute kwa akili na nguvu zetu zote.Anasema;"Mtafuteni BWANA, maadamu ANAPATIKANA, Mwiteni ,maadamu yu karibu" (Isaya 55:6). Anasema tena ;"Nanyi mtanitafuta na KUNIONA, Mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote" (Yeremia 29:13)

MAX SHIMBA ANAJIBU:
**** Jibu: Ni kweli kabisa ukimtafuta Bwana utampata na Zaidi ya hapo Utamwona. Kama ilivyo shahidiwa katika Yeremia 29: 13.
Je, huyu Bwana alionekanaje? Hakika Yesu ndie Bwana wa Mabwana na alionekana kwa macho. 14 Ufunuo 17: Watapigana na Mwanakondoo, lakini Mwanakondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.
LAKINI CHA AJABU, HAKUNA AYA HATA MOJA KWENYE QURAN ambayo inakiri haya kuwa Muhammad alimtafuta Mungu na akampata na Zaidi ya hapo Muhamamd aliweza kumuona Allah.
Hivyo basi, leo ndugu yetu Bernard Nyangasa amekiri bila ya kujua kuwa Muhammad hakuwa Mtume wa Mungu wa Mtumishi wa Mungu maana hakuwa kiri kuwa alimpata Mungu baada ya kumtafuta na ziaid ya hapo aliweza kumuoa Allah kama ilivyo thibitishwa na vitabu vilivyo tangulia kabla ya Quran.
Bwana Bernard Nyangasa, sasa nategemea umeanza kuelewa kwanini huwa napinga Utume wa Muhammad na Uungu wa Allah asiye onekana na aliye goma kuongea na Muhammad.
**********************************************************************************************
BERNARD NYANGASA ANASEMA:
KATIKA "kumtafuta" MUNGU (kutafuta imani sahihi),ushabiki,kufuata mkumbo,jazba nk,vinavuruga kabisa jitihada hiyo takatifu.KWANI mambo hayo yanazuia akili kufanya kazi yake ipasavyo.Ni vyema kuiachilia akili yenye jukumu na uwezo wa kuchuja mambo ifanye kazi yake kwa uhuru ili itoe tathmini sahihi.

MAX SHIMBA ANAJIBU:
****Jibu: Kunazo sauti nyingi zinazo shindania usikivu wetu, sasa kwa nini mtu afikirie kuhusu Yesu huko juu, sema Muhammad au Confucius (Mwana filosofia Fulani wa china), Buddha, au Charles Taze Russell, au Joseph Smith? Kwani hata hivyo si njia zote zinaelekea Mbinguni? Kwani si Dini zote ziko sawa? Ukweli ni kwamba Dini zote hazielekei Mbinguni kama jinsi ambavyo njia zote hazielekei Indiana.
Yesu pekee huzungumza kwa mamlaka ya Mungu kwasababu Yesu peke yake alishinda mauti. Muhammad,Confucius (Mwana filosofia Fulani wa china), na wengineo wanaendelea kubadilika kuwa mavumbi makaburini mwao mpaka leo hii, lakini Yesu, kwa nguvu zake, alitoka kaburini siku tatu baada ya kufa juu ya msalaba wa warumi uliojaa dhiki. Mtu yeyote mwenye uwezo juu ya mauti, ywastahili usikivu wetu. Mtu yeyote mwenye uwezo juu ya Mauti astahili kusikizwa.
******************************************************************************************
BERNARD NYANGASA ANASEMA:
FUNDISHO KUU; Kwa kuwa mafundisho ni mengi sana,hatuwezi kuhoji mafundisho yote.Njia fupi ni kuhoji kuhusu fundisho kuu la Mwenyezi Mungu ambalo halibadiliki kabisa tangu dunia kuumbwa.Fundisho hili ni kuamini "Upekee" wa Mwenyezi Mungu.Wayahudi wameliita "She'ma".Yesu akaliita "Uzima wa milele".Anasema ;"Na uzima wa milele ndio huu,wakujue wewe Mungu wa PEKEE,wa KWELI ,na Yesu Kristo uliyemtuma (Mtume)" (Yohana 17:3).
MAX SHIMBA ANAJIBU:
Na Yesu huyu asema hivi, “Njoni kwangu,ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo,nami nitawapumzisha’’ (Mathayo 11:28). Huu ni Ulimwengu mzito na maisha ni magumu. Wengi wetu tumefanyiwa madhambi, tumejeruhiwa, na tumetishika kivita. Ni kweli? Sasa, unataka nini? Uregesho ama dini tu? Mwokozi aishiye au Mmoja kati ya “Mitume’’ wengi waliokufa? Uhusiano wa maana au Kafara za utupu? Yesu si chaguo tu, Yeye ndiye chaguo!
Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta msamaha (Matendo 10:43). Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta uhusiano wa maana na Mungu (Yohana 10:10). Yesu ndiye “dini’’ ya kweli kama unatafuta uzima wa milele Mbinguni (Yohana 3:16). Weka imani yako kwa Yesu kama Mwokozi wako-hutajilaumu! Mwamini yeye kwa msamaha wa dhambi zako-hutaaibika.
***********************************************************************************************
BERNARD NYANGASA ANASEMA:
Uislam umeliita fundisho hili "kalimatut tawhiid" (kauli ya kumpwekesha M/Mungu).Quran inasema ;"Sema;hakika Mwenyezi Mungu ni mmoja".
KWAKUWA,HAKUNA maandiko yoyote Matakatifu yanayotaja Mungu mwenye "nafsi tatu" au "mbili",imani hiyo pamoja na za hapo juu, LAZIMA ipitishiwe "mvua,mafuriko,radi nk".Imani inakayohimili hoja na maswali magumu,ndio inastahili kuitwa "nyumba iliyojengwa kwenye mwamba" (imani sahihi).
TAFAKARI:CHUKUA HATUA
MAX SHIMBA ANAJIBU:
Utatu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu. Aya za biblia zifuatazo zitatumika kufafanua neno hili.
1) Kuna Mungu mmoja: kumbukumbu la torati 6:4; wakorintho wa kwanza 8:4; wagalatia 3:20; Timotheo wa kwanza 2:5.
2) utatu una nafsi tatu: mwanzo 1:1; 1:26; 3:22; 11:7 Isaya 6:8; 48:16; 61:1; Mathayo 3:16-17; Mathayo 28:19; wakorintho wa pili 13;14. Katika mwanzo 1:1 neno la wingi “Elohim” linatumika. Katika mwanzo 1:26; 3:22; 11:7 na Isaya 6:8, neno la wingi “sisi” limetumika. Kwa hivyo neno “Elohim’ na “sisi” kumaanisha zaidi ya mmoja halina pingamizi.
Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.
3) Nafsi hizi tatu zinatambulika katika maandiko. Katika agano la kale “ BWANA” linatofautishwa na “Bwana” (mwanzo 19:24; Hosea 1:4). “BWANA” ana “Mwana” (zaburi 2:7, 12; Methali 30:2-4). Roho anatofautishwa na “BWANA” (hesabu 27:18) na pia kutoka “Mungu” (zaburi 51:10-12). Mungu mwana atofautishwa na Mungu Baba (zaburi 45:6-7; waebrania1:8-9). Katika agano jipya, Yohana 14:16-17 ndipo Yesu anazungumza na Baba juu ya kuleta Msaidizi, Roho mtakatifu. Hii ina maana ya kuwa Yesu hakujichukulia yeye mwenyewe kuwa Baba wala Roho Mtakatifu. Katika kila mahali ndani ya agano jipya Yesu alipozungumza na Mungu Baba alikuwa akizungumza na nafsi moja wapo ya Utatu – Baba.
4) kila nafsi katika utatu huu ni Mungu: Baba ni Mungu: Yohana 6:27; warumi 1:7; petro wa kwanza 1:2. Mwana ni Mungu: Yohana 1:1, 14; warumi 9:5; wakolosai 2:9; waebrania 1:8; Yohana wa kwanza 5:20. Roho mtakatifu ni Mungu: Matendo ya mitume 5:3-4; wakorintho wa kwanza 3:16 (anayedumu ndani ni Roho mtakatifu –warumi 8:9; Yohana 14:16 –17; Matendo ya mitume 2:1—4).
5) Katika mpangilio ndani ya utatu huu: maandiko yanaonyesha kuwa Roho Mtakatifu humtumikia Baba na Mwana na Mwana humtumikia Baba. Huu ni uhusiano wa ushirika wao wala hupunguzi uungu wa nafsi yoyote ile. Kuhusu Mwana tazama: luka 22:42; Yohana 5:36; Yohana 20:21; Yohana wa kwanza 4:14. kuhusu Roho Mtakatifu tazama Yohana 14:16; 14:26; 15:26; 16:7 na hasa Yohana 16:13-14.
6) Majukumu ya kila nafsi katika utatu: Baba ndiye aliyesababisha kuwako kwa 1) ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Ufunuo wa Yohana 4:11), 2) ufunuo wa kimungu (Ufunuo wa Yohana 1:1) 3)wokovu (Yohana 3:16-17); Matendo ya kibinadamu ya Yesu ( Yohana 5:17; 14:10). Baba anaonekana kwanza katika haya yote.
Mwana ni wakala ambaye Baba humtumia kufanyia haya: 1) Kuumba na kustawisha ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Yohana 1:3; wakolosai 1:16-17); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 1:1; Mathayo 11:27; Yohana 16:12-15; Ufunuo wa Yohana 1:1); na 3) wokovu ( wakorintho wa pili 5:19; Mathayo 1:21; Yohana 4:42). Baba alifanya mambo haya yote kupitia Mwana anayetenda kazi kama mwakilishi wake.
Roho Mtakatifu ndiye anayetumiwa na Baba kufanya haya: 1) uumbaji na ustawishaji wa ulimwengu (mwanzo 1:2; Ayubu 26:13; zaburi 104: 30); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 16:12-15; waefeso 3:5; petro wa pili 1:21); 3) wokovu (Yohana 3:6; Tito 3:5; petro wa kwanza 1;2); na 4) matendo ya Yesu ( Isaya 61:1; Matendo ya mitume 10;38). Haya yote Baba ayatenda kupitia Roho Mtakatifu.
Baba, Mwana na Roho si vipande vya Mungu bali kila nafsi ni Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
May 7, 2016

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW