Saturday, December 17, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA KUMI NA MOJA)

Image may contain: 1 person
Ndoto ya Danieli Kuhusu Wanyama Wanne
I. Utangulizi:
A. Hii sura inaanza mabadiliko kubwa ya kitabu hiki.
1. Sura 1-6, Nyalaka za matukio ambapo nguvu za Mungu na utawala wake duniani unaonyeshwa katika viongozi wapagani kwa Yuda walipokuwa utumwani Babeli.
2. Sura ya 7-12 inahusu maono ya nguvu aliyoyapokea Danieli kuhusu maisha ya baadae ya Waebrania na kuanguka kwa milki ya Babeli.
B. Sura ya 7-12 ina muda wa utaratibu wake.
1. Matukio katika sura sita za kwanza zimetumia kipindi cha miaka 67, 606 - 539.
2. Maono katika sura ya 7-12 yamefunuliwa nyakati tofauti kati ya 549 na 536.
C. Maono manne katika 7-12, sura tatu za kwanza (sura 7,8, & 9) ni utabiri.
1. Neno “apocalyptic” linatokana na neno la Kiyunani “apokalyptein” lenye maana ya ‘kufungua; au kufunua jina la kitabu cha ufunuo katika Kiyunani ni Apokalupsis.
2. Maono ni kazi ya fasihi ambayo inaonyesha jinsi ambavyo Mungu anajibu ambapo anaangamiza nguvu zinazotawala za uovu na kubadilisha kwa haki.
3. Tabia ya maono ina maana ya:
a) Tarakimu za kialama/ishara - muunganiko wa namba fulani zikiwa na
eleza sifa za Mungu, mwanadamu au talatibu za mambo ya asili.
b) Sanaa ya maandishi: ni ya kuvumisha hata kubuni maneno picha yametumika
kuvutia na kusisitiza umuhimu na thamani ya misingi ya kanuni zake.
***===***
Daniel 7
Danieli aliota ndoto na maono ya Maana sana inayohusiana na siku za Mwisho.Biblia yasema,’’ Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo.Danielii akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.
Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali.Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.

Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.
Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Wanyama wale wanatoka Baharini ikiashiria kuwa wanatoka Katikati ya jamaa na makutano na mataifa na lugha[UFU17:15].
Upepo uvumao baharini ni Ishara ya vita[YER51:1].Wale wanyama wakubwa wanne,wanawakilisha falme kubwa Nne zitakazotokea Duniani[DAN7:17].
Yule simba Anawakilisha ufalme wa Babeli uliotawala Mwaka605BC-539BC.Mabawa ya simba huwakilisha wepesi wake wa kuvamia na kushinda.
Yule dubu anawakilisha ufalme wa Umedi na Uajemi ambao ulitawala tangu539BC-331BC.Mbavu tatu zinawakilisha nchi tatu ambazo Ufalme Huo uliufanyia Ukatili wakati wa Kuingia kwake.[ Babylon, Lydia, and Egypt,].
Yule Chui mwenye Mabawa Manne na Vichwa vinne Huwakilisha Ufalme wa Uyunani uliotawala tangu mwaka331BC-168BC.Mabawa Manne Huwakilisha wepesi wa ufalme huo kupigana vita na kushinda.Vichwa vinne Huwakilisha Ufalme Huo Utagawanyika katika Falme kuu nne[Cassander had Macedon and Greece in the west; Lysimachus had Thrace and the parts of Asia on the Hellespont and Bosphorus in the north; Ptolemy received Egypt, Lydia, Arabia,Palestine, and Coele Syria in the south; and Seleucus had Syria and all the rest of Alexander's dominions in the east. These divisions were denoted by the four heads of the leopard; B.C.308.].
Mnyama wa nne wa Kutisha Mwenye nguvu Mwenye Pembe Kumi,mwenye meno ya chuma anawakilisha Ufalme wa Rumi uliotawala tangu Mwaka168BC-176AD.Hebu tuuangalie kwa Makini Ufalme Huu Maana Unahusiana sana na Mambo ya siku za Mwisho.
SWALI: Danieli 7 ilitokea kabla ya Danieli 6. Kwa nini unadhani mfuatano uko hivi?
J: Sura zilizotangulia zinaongelea maisha ya Daniele. Haya ni maono ambayo hayana uhusiano na maisha ya Danieli. Maono haya yalitokea karibu mwaka 556-553 KK.
SWALI:
Kwenye Dan 7:2, je pepo za mbinguni zinawakilisha kitu gani? Kwa nini kuna pepo nne?
J: Pepo nne zinaweza kuwa roho zinazoathiri himaya nne.
The Expositors Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.85 inasema pepo nne zimedhibitiwa kwa namna fulani hadi wakati wa kuachiwa kwao, na malaika wanne kwenye Ufu 9:14. Hata hivyo, kuna ushahidi kidogo sana wa jambo hili.
SWALI: Kwenye Dan 7:2, bahari inawakilisha kitu gani?
J: Bahari inaweza kuwa inawakilisha umati wa watu. The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 7, uk.85 inasema hivyo hivyo.
SWALI:
Kwenye Dan 7:3-7, 17-19, je wanyama wanne ni wapi?
J: Dan 7:17 inasema hawa ni wafalme au falme nne. Falme hizi ni Babeli, Uajemi ya Umedi, Ugiriki/Makedonia, na Rumi. Hivi ndivyo zinavyoendana na picha hii:
Simba mwenye mabawa: Viumbe wanaoonekana kama simba wenye mabawa wakiwa wamelifunika lango lenye kuonekana vizuri sana la Ishtari huko Babeli. Pia, upande wa mbele wa chumba cha enzi ya Nebukadneza kwenye jumba la makumbusho la Verderasiatisches huko Berlin linaonyesha simba ambao awali walipakwa rangi za njano, nyeupe, bluu na nyekundu. Picha ya mchoro huu ipo kwenye kitabu kiitwacho Babylon kilichoandikwa na Joan Oates, uk.150.
Babeli iliitwa simba kwenye Yer 4:7. Farasi wa Babeli walikuwa wanakimbia haraka kuliko tai kwenye Yer 4:13. Babeli na Misri waliitwa tai kwenye Eze 17:3, 7. Baadaye, Wababeli waliwatenda mema Wayahudi, wakati Danieli alipokuwa kwenye makazi ya mfalme. Hab 1:8-9 haihusiki hapa, kwani farasi wa Wababeli wanalinganishwa na chui na mbwa mwitu na tai.
Dubu aliinuliwa upande mmoja: Himaya ya Uajemi ya Umedi ilikuwa na sehemu mbili, huku upande wa Kiajemi ukiwa na nguvu zaidi.
Chui mwenye mabawa manne na vichwa vinne: Ingawa chui ni mnyama mkubwa wan chi kavu mwenye kasi zaidi, anayefikia mwendo kasi wa km 97 (maili 60) kwa saa, chui mwenye mabawa manne atakuwa na mwendo kasi mkubwa zaidi. Alexander Mmakedonia aliishinda himaya yote ya Uajemi na hata sehemu za India katika miaka kumi na tatu ya kushangaza. Baada ya kifo chake, himaya iligawanywa miongoni mwa majemadari wake wanne. Ingawa chui wa Afrika hakuwa alama ya kawaida ya Wagiriki, hakuna mnyama mwingine muwindaji ambaye aliyeweza kuwakilisha mwendo kasi wa ushindi wa Alexander vizuri zaidi.
Mnyama mwenye meno ya chuma: Mnyama wanne alikuwa tofauti, alikuwa na mapembe, na alikuwa na kiburi. Wafalme wa Rumi walijiita miungu, na hata sadaka za kila mwaka zilitolewa kwao.
Isitoshe, watu wengi wanaona utimilifu wa pande mbili wa unabii huu, huku mpinga Kristo akiwa anakuja kutokea himaya iliyofufuliwa ya Rumi.
Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.610 kinadai kuwa chui alikuwa HImaya ya Uajemi, vichwa vyake vine vilikuwa wafalme wanne walikuwa wanajulikana na Danieli, na mnyama wanne alikuwa himaya ya Alexander. Asimov anasema hivi kwa sababu anajaribu kutenganisha Himaya ya Umedi na Himaya ya Uajemi. Hata hivyo, Wamedi, mbali na kuwasaidia Wababeli kuiangusha Ashuri, kupigana na Wasinthia, na kuungana na Waajemi, hawakuwa na mambo mengine yenye kuhusika na historia ya ulimwengu waliyoyafanya kama himaya uhuru.
SWALI:
Kwenye Dan 7:3-7, 17-19, badala ya Himaya ya Rumi, je mnyama wanne anaiwakilisha dola kamilifu ya Kiyahudi, kama kitabu cha mwenye kushuku Asimov’s Guide to the Bible, uk.610-611 kinavyosema kuwa jambo hili linauwezekano mkubwa zaidi wa kuwa hivyo?
J: Hapana. Isipokuwa Asimov anafikiri kuwa Wayahudi walikuwa na mawazo kuwa dola kamilifu ya Uyahudi ilikuwa ni kitu kibaya na kiovu, Asimov amechanganyikiwa sana hapa. Dan 7:7 inasema, ". . . na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi." Kwenye Dan 7:11 inasema, ". . . nalitazama hata mnyama yule [wa nne] akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa akateketezwa kwa moto." Mungu ndiye aliyemuua mnyama wanne, hivyo ni dhahiri kuwa mnyama huyu si dola yenye kumcha Mungu.
SWALI:
Kwenye Dan 7:5, je mbavu tatu zinawakilisha kitu gani?
J: Kuna maoni matatu tofauti:
Uajemi iliyotangulia ilikuwa na falme tatu: Misri, Ashuri na Babeli. Kwa mijubu wa vigezo vilivyopo, Uajemi haikuishinda Ashuri, kwa sababu Ashuri ilikuwa tayari imefanyika sehemu ya Himaya ya Babeli, ambayo Uajemi iliishinda.
Himaya zilizoshindwa na Uajemi zilikuwa tatu: Misri, Babeli, na Lidia. Himaya nyingizaidi hadi kufikia wakati huu ziliishinda himaya moja tu iliyotangulia. Hata hivyo, Uajemi ilzishinda tatu.
Pembe badala ya mbavu ndivyo toleo la Biblia la Kiingereza la NRSV linavyotafsiri maneno haya. Hata hivyo, majibu mawili yaliyotangulia yanaeza kutumika kwa pembe, kwa hiyo wazo hili ni lenye mjadala.
Hitimisho: Kwa kuwa mbavu zilikuwa kwenye mdomo wa dubu, zitakuwa ni falme tatu "zilizoliwa" na dubu. Hivyo, Misri, Babeli na Lidia ni tafsiri sahihi.
SWALI:
Kwenye Dan 7:7-9, 20, 24, je pembe kumi ni nini?
J: Dan 10:24 inatuambia kuwa hizi ni falme tatu. Mfalme wa mwisho huenda akawa ndiye Mpinga Kristo kwenye himaya iliyofufuliwa ya Rumi. Pembe kumi kwenye mnyama mwekundu zimeongelewa kwenye Ufu 17:3, 12-14.
SWALI:
Kwenye Dan 7:9, je Mzee wa Siku alipokuja, kwa nini viti vya enzi (wingi) viliwekwa?
J: Viti kadhaa vya enzi kwa ajili ya Baba, Mwana wa Adamu. Hata hivyo, "hukumu ikawekwa" kwenye Dan 7:10b, kwa hiyo inaweza kuwa ni wazee na huenda hata sisi pia, tunaowahukumu malaika.
SWALI:
Kwa nini Dan 7:13-14 ni aya nzuri kuwashirikisha Wayahudi na Mashahid wa Yehova?
J: Inamtaja Mzee wa Siku (Mungu Baba), na mmoja kama mwanadamu akija kwa Mzee wa Siku, kisha mamlaka ilipewa kwa mwanadamu, na watu wanaomwabudu kiusahihi. Maneno haya yanamuongelea Yesu Kristo.
SWALI:
Kwenye Dan 7:16 na 9:21, Gabrieli ni nani?
J: Gabrieli ni malaika mkuu aliyetumwa kupeleka ujumbe kwa Danieli, na baadaye kwa Maria Mama wa Kristo kwenye Luk 1:19, 26.
SWALI:
Kwenye Dan 7:25, je muda wa watakatifu kutiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili na nusu wakati?
J: Muda huu ni sawa na kipindi cha miaka tatu na nusu ya mateso kwenye Dan 9:27 na Ufu 11:3; 12:6,14.
USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA MBILI... Kwenye Daniel 8:8, kwa nini pembe nne zilikua kuelekea kwenye pepo nne za mbinguni?
Shalom
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW