Nabeel alizaliwa na kukulia kwenye familia na maisha ya kiislamu. Uislamu ulikuwa ni kila kitu kwake. Lakini wakati ulipofika wa yeye kujua jema na baya, alianza kujihoji kuhusu maisha yake, Mungu wake, na hatima yake ya milele. Hatimaye alimwomba Mungu amwonyeshe kweli. Je, nini kilitokea? Tafadhali fuatilia sehemu hii ya kwanza ya ushuhuda huu.
……………………………………
Nilipokuwa mdogo, wazazi wangi walikuwa wacha Mungu sana. Mimi nami nilikuwa mcha Mungu sana kwa sababu yao. Wazazi wangu walinifundisha kumwomba Allah kila wakati. Niliswali sala tano kwa siku ambazo ni za lazima. Lakini pia niliswali swala zaidi ya hizo. Swala ilikuwa ni sehemu muhimu kabisa ya maisha yangu. Kila nilipoamka asubihi niliomba mara tu nilipofungua macho yangu. Kisha nilipoenda bafuni, nilikuwa nikiomba swala ya wakati wa kuosha mikono yangu. Pia niliomba swala kabla ya kusoma Quran na mara baada ya kusoma Quran, ambayo niliisoma karibu kila siku.
Uislamu ulikuwa ndani yangu kabisa. Hivyo, wazazi wangu walikuwa wananifurahia sana maana nilikuwa ni aina ya mtoto wa Kiislamu ambaye walikuwa wanajivunia kumlea. Nilitokea kwenye familia ya kimisionari. Allah na mtume Muhammad walikuwa wanaheshimiwa sana. Allah alikuwa anaabudiwa muda wote.
Uislamu kwetu haukuwa tu ni dini, bali ulikuwa ni maisha yetu kabisa. Halikuwa ni jambo tulilofuata tu, bali zaidi sana hivyo ndivyo tulivyokuwa sisi wenyewe. Kwa hiyo, Uislamu ulikuwa ndiyo sehemu kabisa ya utu wangu.