Thursday, March 24, 2016

ALLAH KUPITIA MUHAMMAD AKIRI KUUMBA KWA SIKU SABA (7)

Ndugu msomaji,
Huu ni msiba mwingine kwa Waislam ambao kila kukicha Allah anawakoroga kwa kupitia Muhammad.
Bila ya kupotiza muda tuanze kwa kusoma sahihi hadith.
UTATA WA KWANZA:
ALLAH ALIUMBA DUNIA NA KILA KITU KWA SIKU SABA
Imetafsiriwa na Abu Hurairah; Nabii wa Allah alinishika Moono na akasema, Allah [Sifa zote na utukufu umwendee Allah] aliye umba dunia siku ya Jumamosi, na juu yake akaumba Milima siku ya Jumapili. Na akaumba Miti siku ya Jumatatu. Akaumba vitu mbalimbali siku ya Jumanne. Akumba Mwanga siku ya Jumatano. Akawajaza wanyama ndani yake siku ya Alhamisi na akamuumba ADAM, amani iwe juu yake baada ya alasir ya Ijumma, ikiwa ni uumbaji wake wa mwisho katika saa la mwisho la siku ya Injumaa, kati ya "Alasir na Usiku ulipoingia' (Muslim bin Hajjaj, as-Sahih, Hadith 7054 (27-2789)
Katika somo letu la leo, tutajifunza kuhusu uumbaji wa Dunia. Allah wa Uislam, anasema kuwa yeye ni Mungu na aliumba Dunia na vitu vyote vilivyo ndani yake. Hebu tuanze somo letu kwa kusoma aya za Quran.
UTATA WA PILI:
ALLAH ANAUMBA KWA SIKU SITA
Allah anasema katika Sura 7:54, 10:3, 11:7, na 25:59 kuwa, aliumba dunia kwa siku 6. Soma aya hizi hapa chini kwa ushaidi zaidi.
Quran 7:54. Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Surah 10: 3. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
Lakini Ndugu zanguni, nilipo endelea kuchunguza Quran nikagundua kuwa, kumbe Allah alidanganya pale alipo sema kuwa aliumba Dunia kwa siku sita. Sasa ungana nami katika uchunguzi wa uumbaji wa dunia kama ulivyo wekwa kiuwazi zaidi kupitia Quran iliyo shushwa na Jibril.
Sasa tutasoma Surah ya 41: 9-12. Katika hizi aya tutakazo zisoma, utangudua kuwa Allah hakuumba Dunia kwa Siku 6 kama alivyo dai hapo mwanzoni.

UTATA WA TATU:
HII AYA INASEMA ALLAH KAUMBA KWA SIKU MBILI (2)
Quran 41:9. Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.
+ (Jumlisha)
HAPA ALLAH ANAUNGANISHA MAWINGU NA ARDHI KWA SIKU NNE(4)
Quran 41:10. Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza 11. Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu.
+ (Jumlisha)
HAPA ALLAH ANAZITENGENEZA MBINGU KWA SIKU MBILI (2)
Quran 41:12. Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.
HIZI ZOTE KWA PAMOJA NI SIKU NANE (8)
Siku mbili kwa ajili ya viumbe wa dunia, basi siku nne kujaza ardhi na milima baraka, na chakula kwa ajili ya wakazi wake wote, na mwisho kwa siku mbili zaidi ili kujenga mbingu saba na kujenga nyota yao. Hii inaongeza hadi 2 + 4 + 2 = siku 8 kinyume na siku 6 zilizotajwa katika aya nyingine.
NGOJA NIWEKE KWA UFUPI
Muundo ni wazi sana: Haya ni Matabaka Matatu ambayo ni umbaji chini hadi juu:

A = SIKU MBILI:
Quran 41:9*** Mbingu [angani, "dari" juu ya dunia] katika siku 2
----------

B = SIKU NNE:
Quran 41:10*** BARAKA [kujaza dunia na kila kitu zinahitajika kwa ajili ya maisha] katika siku 4
---------

C = SIKU MBILI:
Quran 41:12***EARTH [msingi] kukamilika katika siku 2
SASA JUMLISHA HIZO SIKU:
A + B + C = 2 + 4 + 2 = 8
Ndugu zanguni, hivi Allah alishindwa mahesabu au ndio kutuhakikishia kuwa yeye hakuwa Muumbaji? Kwanini Allah afanye makosa makumbwa namna hii? Leo Allah kwa mara nyingine tena ametuhakikishia kuwa yeye si Muumbaji. Uchaguzi ni wako, kufuata Allah asiye fahamu aliumba Dunia kwa Siku Ngapi au Jehova ambaye alisema aliumba Dunia kwa siku 6.
Zaidi ya hapo, Allah anasema kupitia Muhammad (Muslim bin Hajjaj, as-Sahih, Hadith 7054 (27-2789) kuwa, aliumba kila kitu kwa siku SABA. Hapo sasa mimi sina la ziada, nawaachia wenyewe mjadili, JE ALLAH ALIUMBA AU NI LONGA LONGA TU?
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 24, 2016

1 comment:

Unknown said...

Kwani unavyosema mungu na unavyosa Allah unajua ni nini tofauti yake yani nasoma naona kabisa huyu anaeandika kidogo shake loose soma sana kaka/dada itakusaidia mambo ya Mwenyezi kamwe hayajadiliwi huyo ni shetani anakutawala huna budi kuachamana nayo wewe kupumua tu inatosha unajadili uumbaji wewe inakusadia nini na kusema Allah ni muongo kama nakosea kunukuu aliyekuumba wewe anaanzaje kuongopa shame upon you tumia akili angalia usije kuangamia na nna kuhisi tu ukiendelea na hiyo dini uloshikamana nayo kwa style hiyo hakika makazi yako yatakuwa ni moto labda tu ubadilike

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW