Monday, May 17, 2021

ALLAH KATEREMSHA BIBLIA

 SWALI LA WAISLAM KWA WAKRISTO: NANI KAPEWA BIBLIA?


Hili ndio swali la Waislam eti, Biblia sio Kitabu cha Mungu kwasababu hawajui nani kapewa.


Leo nawajibu kwa kutumia Quran yao. Kutokana na Quran aliyo pewa Muhammad inakiri kama ifuatavyo:


*Surat Al Ankabut 47* Na namna hivi tumekuteremshia Kitabu (cha Qur'ani). Basi *wale tulio *wapa* Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur'ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakao iamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipo kuwa makafiri. http://www.iium.edu.my/deed/quran/swahili/without/29.htm


*ALLAH ANASEMA KUWA BIBLIA KAITEREMSHA YEYE NA KAWAPA WATU WA KITABU.*


1. Allah anakiri kuwa Biblia kaiteremsha.

2. Allah anakiri kuwa Biblia kaWAPA watu wa Kitabu. Inamaanisha Biblia kapewa mtu zaidi ya mmoja.

3. Allah anasema kuwa watakao kataa Biblia hao ni Makafiri.

4. Kwasababu Biblia amepewa mtu zaidi ya mmoja, hiyo inamaanisha Biblia ni mkusanyiko wa vitabu.


SWALI:

*Ni nani hao walio pewa Biblia?*


Ndani ya Biblia kuna Torati, Zaburi na Injili vitabu wanavyo vikubali Waislam.


Katika Sura 3:3 yatuambia haya yafuatayo:

‘Amekuteremshia (hatua kwa hatua) Kitabu kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati (Sheria ya Musa) na Injili (ya Yesu) zamani – ziwe uongozi kwa watu, *Na akateremsha vitabu vingine* vya kupambanua (baina ya haki na batili).’


Je nani kapewa Torati?

Je nani kapewa Zaburi?

Je nani kapewa Injili?

Je vitabu vingine alivyo teremsha Allah ni vipi?


Waislam jibuni swali


Shalom


Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW