Uislam na Sayansi:
Mitazamo Iliyosahauliwa Imekumbukwa
Toleo la Juni 2006
Je, maneno kama aljebra, alkali, pombe, astrolabe, naphtha, na zircon kitu gani kinachoyapatanisha hasa? Maneno haya yote ni ya Kiingereza yaliyotoholewa kutoka katika Kiarabu na maneno ya Kiajemi yanayoturudisha nyuma kwenye miaka ya 700-1150 BK, wakati kituo cha kujifunza Sayansi bila shaka kilikuwa Mashariki ya Kati.
Watu wengi yawezekana wasijue mchango muhimu uliotolewa kwa sayansi na hesabu kutoka Mashariki ya Kati. Ifuatayo ni orodha fupi ya mafanikio ya mambo haya, na kisha hutafiti kauli za kisayansi zilizomo katika Korani. Lakini kuna maendeleo mengi makubwa ya kitabibu ambayo hayajatajwa hapa; huleta sifa kwa mjadala wake wenyewe.
Sayansi ya Mashariki ya Kati ya Zamani
Hata Wasumeria wa kwanza (3500-2000 KK) walikuwa na mchanganuo wa wanyama wote waliowajua. (Wadudu wakubwa kama vile nzige walijumuishwa pamoja na ndege, kama viumbe warukao.) Wamisri wa zamani na Wababeli walitumia nyota ili kuwasaidia kujua ni wakati gani wangeanza kupanda. Watu hao wa zamani walikuwa na maendeleo kadhaa katika kutengeneza meli, ufugaji wa wanyama, na upasuaji, hata upasuaji wa kichwa. Wamisri walitumia dawa ya meno tangu mwaka 2500 KK. Mitatu kati ya michango muhimu sana ya kisayansi ni kuandika, kulima pamoja na sayansi na teknolojia ya vitu yabisi kama vyuma.
Pengine mafanikio ya juu zaidi kielimu ya ulimwengu wa zamani yalikuwa maktaba ya mji wa Alexandria. Hapa kulitunzwa mamia ya maelfu ya juzuu za nakala asilia au nakala za fasihi nyingi za ulimwengu wa watu wa wakati ule.
Uhandisi na Uhandisi Majengo wa Zama za Kale
Wamisri walikuwa na gubeti tangu 2500 KK. Katika uhandisi majengo, kila mtu anajua mapiramidi ya kuvutia nchini Misri na mahekalu (Ziggurats) ya Sumeria na Babeli.
Kitu kisichojulikana sana ni kuwa Kaskazini-mashariki mwa Iran kulikuwa na bwawa kubwa, lililoibuka hasa katika mwaka 1800 KK, kushinikiza wahamiaji wengi katika nchi za India na Iran. Bwawa nchini Yemen liliufanya ufalme wa Sheba kuwa kituo maalum cha kilimo na biashara hadi hapo lilipovunjwa pia zaidi ya karne moja kabla ya Muhammad. Ujenzi wa mifereji, bustani zinazoning’inia, na miji yenye kuta nene ni mambo ya kuvutia hata leo. Na kwa hakika, kama ungeliweka Mji wa Ashuru, Ninawi kati ya Ufaransa na Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza, pasingekuwa na upande wowote ambao ungeweza kuuteka. Hatimaye ulitekwa, lakini ni kwa sababu tu mto wa Khosr ulipofurika na mafuriko yake yalivunja sehemu ya ukuta wa mji huo..
Mashariki ya Kati ya Kale na Hesabu
Haya majengo ya kiuhandisi yasingeweza kujengwa kama pasingekuwa na msaada wa hesabu. Wababeli wa zamani walikuwa na mfumo wa kuhesabu hadi 60. Walipendelea namba zinazoshabihiana; kwa mfano, wangegawa a/b kama *l/b. Wababeli wa zamani walikuwa wa kwanza kutumia aljebra kwa hesabu za mistari na hesabu za mchanganyiko wa namba na herufi (quadradic problems). Chati iitwayo Plimpton 322 ni chati ya namba za Pythagorean (a^2 + b^ + c^2). Wababeli walibuni vipimo vya namba za mraba kama uchoravyo mstatili na kisha kuhesabu ukubwa wa eneo. Kimahesabu, watu hawa hawakutumia kitu chochote zaidi ya vipimo vya mraba (squares). Wakati huo huo Wababeli walikuwa na thamani tofauti ya pai (pi), na iliyokuwa sahihi zaidi ilikuwa 3.125. Mwanamahesabu wa Kiarabu wa karne ya 10 Abu’l-Wafa’ alisema watu waliotoa elimu ya kimahesabu walikuwa mafundi sanaa (wanasanaa) na wasanii.
Hesabu za maumbo ya pembetatu za Wamisri zilikuwa bora kuliko za Wababeli, kwa sababu Wamisri walikuwa na ufahamu juu ya kona, na walikuwa na ile thamani ya pai ya 31/7 au 3.16. Hii si mbali na 3.14159. Na hii imo katika nyaraka za Rhind Paparas—paparas (mwaka wa 1650 KK) na Paparas ya Moscow iliyokuwapo wakati ule ule. Majengo mengi ya Kimisri yalikuwa na pande za 3 kwa 4, lakini hawakujua juu ya nadharia ya Pythagoras (Pythagorean theorem). Sayansi na hesabu nyakati za zamani zilikuwa za "kivitendo". Pengine hii ndiyo sababu, kwa shauku tu, hapakuwa na yeyote aliyekuwa na wazo la "sifuri" hadi ilipogunduliwa nchini India.
Aljebra Zilitoka Wapi?
Hesabu ya aljebra ya kwanza tunayoifahamu ilikuwa imehifadhiwa katika Paparas ya Rhind iliyotolewa nakala na mwandishi wa Kimisri aliyeitwa Ahmes (mwaka wa 1650 KK.). Huu ni muda mrefu sana kabla Musa hajazaliwa. Wakati huo huo Wayunani walikuwa wakipendelea zaidi hesabu za maumbo, Wachina walikuwa wakikokotoa hesabu za mchanganyiko wa namba na herufi kabla Kristo hajazaliwa, na Wahindu (kwenye miaka ya 628-1150 BK) walikokotoa na kupata majibu ya maswali tata zaidi ya hesabu. Huko Baghdadi Muhammad ibn Musa al-Khowarizmi/Khawarizmi (mwaka wa 825 BK), Abu Kamil (mwaka wa 900 BK) na al-Karkhi (mwaka wa1100 BK) waliziendeleza hesabu za aljebra zaidi. Kwa kiasi kikubwa sana ziliziambukiza hesabu za Ulaya wakati Robert wa Chester alipotafsiri kitabu cha al-Khowarizmi kwenye mwaka wa 1140 BK kiliitwa kwa Kilatini Liber Algorism, maana yake kwa ujumla ni "Kitabu cha al-Kowarizmi." Na neno algorism baadaye lilikuwa algorithm and aljebra [kwa lugha ya kimahesabu].
Hapa chini jedwali laorodhesha baadhi ya wanasayansi wa Mashariki ya kati na wale wa Kiarabu pamoja na wanamahesabu.
Avicenna (Ibn-Sina) 979/980-1037 BK | Licha ya kuwa tabibu muhimu sana kati ya enzi za Warumi na enzi ya leo, alikuwa mwanasayansi pia, mwanafalsafa, na mjenga hoja aliyeandika takriban kazi sanifu zipatazo 200. Albert Magnus wa England alijifunza mengi kutoka kwake |
Averroes (Abu al-Walid Muhammad bin Ahmad ibn Muhammad ibn Roshd) 1126-1198 BK | Alimsujudu [mwanafalsafa] Aristotle. Alisema mengi juu ya umaskini na masumbuko kutokana na jinsi Waislam walivyowachukulia |
Avempace (Ibn Gabirol) 1021-1058 BK | Mwanafalsafa wa Kiyahudi na Kihispania aliyemwuunga mkono Aristotle |
al-Karkhi miaka ya 1100 BK | Michango mbalimbali katika kwa hesabu za Aljebra |
Kemia/Alkemia na Fizikia
Makhalia wa Abbasid wa Baghdadi walikuwa na shulu ya Alkemia kwenye ya karne ya 9 au ya 10. Kazi za kwanza kabisa za Alkemia ya Kiarabu nusu ni za Kiarabu na nusu ni Kisiria. Khalid mwana wa Yezid (alikufa mwaka 708 BK) mwanafunzi wa mtawa wa Kisiria Marianus, alikuwa mwandishi wa kwanza wa Kiislam juu ya Alkemia, kufuatana na kitabu Kitab-al-Fihrist. Vipaji vya Wanaalkemia viliharibiwa kwa kujaribu kubadili madini ya "risasi" na vitu vingine kuwa dhahabu, lakini katika mchakato huo waligundua mambo mengi hii ni pamoja na Kemia pia. Wafuatao ni baadhi ya wanakemia maarufu wa Kiajemi na Kiarabu.
Geber (Jabir ibn-Hayyan) Kwenye miaka ya 760-815 | Mwanaalkemia wa Kiarabu aliyechuja chachu kitaalam na kutengeneza tindikali itokanayo na maji na naitrojeni. Alianza utafiti juu ya kubadili maumbo ya vitu yabisi (metals) na alivutiwa sana na kimiminika kiitwacho Zebadi (Mercury). Alikuwa mwenye sifa na maarufu kiasi kwamba kemia ikapewa jina la utani "Usanifu wa Jabir" |
Ibn al Haytham Alikufa mwaka 1039 BH [Baada ya Hija] | Alisomea mambo ya shinikizo, sumaku na sayansi ya mambo ya mwanga. Alisema kuwa huwa tunaona kwa kutumia mwanga unapoyaingia macho yetu, si miale ambayo jicho hutupa nje. |
Quth al-Din 1236 BK | Alielezea umbo la upinde wa mvua |
Rhazes (Al-Razi) kwenye miaka ya 850-925 | Mkemia wa kiajemi (na mwana anga) aliyetengeneza chokaa ya kuta za nyumba ya Paris na alijifunza madini ya shaba na kristole (crystalline) yaani antimony |
Abdul Salam of Pakistan. 1926-1996 BK | Alishiriki tuzo ya Nobel ya mwaka 1979 katika Fizikia. Alikuwa Qadiani ambaye Waislamu wengi humchukulia kama wenye mafundisho potofu wasio waislamu |
Geber (Jabir ibn-Hayyan) (alikufa mwaka 808 BK 193 BH [Baada ya Hija]) alikuwa Msufi mwenye imani ya kujikana mwenyewe kwa ajili ya mambo ya kiroho. Alikuwa na maabara huko Dameski. Vitabu vyake 200, vinane kati ya hivyo vilikuwa vya kemia, kujumlisha vitabu juu ya usindikaji, kutengeneza rangi, na uzito pamoja vipimo mbalimbali. Ama kwa hakika, wengine waiita kemia jina la utani "usanifu wa Jabir." Alitengeneza mezani iliyoweza kupima hadi uzito wa 1/6 ya gramu. Wakati watu wa Ulaya wa baadaye walidhani kuwa Phlogiston iliongezwa kwenye vitu vilipounguzwa, lakini Jabir alielewa kwa usahihi kwamba nguvu ya vitu vilivyoungua ilikuwa ikitoka, na kuacha mabaki ya majivu yasiyounguzika. Aligundua karatasi isiyounguzwa na moto, kizuia kutu, na kilichozuia maji kwenye nguo. Kwa uhalisia, alikuwa na wito wa karibu toka kwa watu japo alishauri kuwa maabara ya kikemia yalipaswa kuwa mbali na miji.