Ndugu msomaji;
Je, unamfahamu Roho Mtakatifu?
Je, Roho Mtakatifu ni nani kwako?
Katika kijarida hiki kifupi, ningependa
tumzungumzie Roho Mtakatifu kama alivyo semwa na kutajwa katika Biblia
Takatifu.
Kuna utatanishi mkubwa sana na maelezo
mengi sana kuhusu Roho Mtakatifu. Kuna imani zingine kama Mashahidi wa Yehova,
wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Nguvu Fulani na au ni uwezo wa Mungu katika
kufanya mambo. Wengine kama Waislamu, wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Malaika
Gabriel. Wengine husema kuwa Roho
Mtakatifu ni sehemu ya Nafsi ya Mungu. Lakini, Biblia inasema nini kuhusu Roho
Mtakatifu. Ni vyema tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu kwa kutumia aya za Biblia
na sio theologia na akili zetu.
ROHO MTAKATIFU NI MUNGU
Tuanze kwa ushaidi wa aya: Matendo ya Mitume
5:3-4. Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha
kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? 4 Kabla hujauza hilo
shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza, fedha ulizopata zilikuwa
zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Ujue
hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”
Katika aya hizo hapo juu, Petro anapambana na
anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na anasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali
Mungu. Kwa maana nyingine, Petro alikuwa anamwambia Anania kuwa, kumdanganya
Roho Mtakayifu ni sawa na kumdanganya Mungu. Huu ni uthibitisho wa kwanza kuwa,
kumbe Roho Mtakatifu ni Mungu.
ROHO
MTAKATIFU YUPO KILA MAHALI
Hebu tuangalie kama Roho Mtakatifu ana adhama za
Mungu aliye hai. Sifa, moja ya Mungu ni kuwa, yeye yupo kila Mahali. Je, Roho
Mtakatifu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali? Fungua Zaburi 139:7-8, “nitaenda
wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda
juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,”
Daudi anatuambia kwa kupitia Zaburi kuwa, huwezi
kumkimbia Mungu. Daudi anamtaja Mungu na au anamwita Mungu kuwa ni Roho. Hii
sifa ya kuwa kila mahali ni ya Mungu pekee, na katika Zaburi 139: 7-8, tumesoma
kuwa, Roho Mtakatifu yupo kila mahali.
Tuendele na ushahidi zaidi wa kuwa kila mahali; katika
Wakorintho wa Kwanza, hapa Mtume Paulo anasema yafuatayo 1 Wakorintho 2 aya ya
10 Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho
huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani
ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo
hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”
Kama Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu kilicho
ndani ya Binadamu, ambao wametapakaa Duniani kote, basi kitendo cha kuwa kila
mahali kwa wakati mmoja ni Mungu pekee ndie aliye na huo uwezo.
Tuendelee kwa Ushihidi mwingine katika aya hiyo
hiyo ya 10 ya Wakorintho wa kwanza Sura ya 2. Roho Mtakatifu ni Mungu kwasababu
ana akili, hisia, na mapenzi yake.
Katika Wakorintho wa kwanza 2:10 tumesoma kuwa
Roho Mtakatifu hufikiria na hujua siri iliyo ndani yako. Hii sifa ya kufikiria
na kujua, inavunja hoja ya Mashahidi wa Yehova kuwa Roho Mtakatifu ni “Nguvu”.
Nguvu haina uwezo wa kufikiria wala kufanya maamuzi.
ROHO
MTAKATIFU UHUZUNIKA