Monday, November 21, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA NNE)


Baada ya mfalme Nebukadneza kuuvamia Mji wa Yuda na kuushinda, aliwachukua wana wa Israeli hadi Babeli na kuwafanya watumwa. Mfalme Nebukadneza akaamuru watafutwe vijana wa kiizraeli ambao wanatoka katika uzao wa kifalme, na uzao wa kiungwana, vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa Hekima wenye elimu na maarifa ili wapate kusimama mbele zake. Mfalme akaagiza kuwa walishwe posho ya chakula cha mfalme na divai aliyokunywa kwa muda wa miaka mitatu ili kwamba waweze kusimama mbele zake wenye afya.
Basi Ashpenazi ambaye ndiye aliyekuwa mkuu wa matowashi wote akawapata akina Daniel ambaye aliitwa Belteshaza na Azaria ambaye aliitwa Abednego na mishaeli ambaye aliitwa Meshaki na anania ambaye aliitwa shedraka. Biblia yasema hivi;’-Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi. [Daniel1:8].
Danieli alifundishwa na Mama yake kuzitii sheria za Afya ambazo Mungu aliwaagiza wana wa izraeli kwamba wasile vyakula najisi ambavyo Mungu alivikataza ama kunywa divai ya mfalme. Hivyo Danieli alikataa kuzivunja kanuni hizi za afya. Hapa tunapata fundisho kubwa sana kwamba Afya ya miili yetu na uwezo wa akili na wa fahamu hutegemea ikiwa tutazitii kanuni za Mungu za Afya ambazo amezielekeza katika Neno lake na Mungu atatupatia afya ikiwa tutatii maelekezo yake.
Ndipo Danieli akamwomba yule msimamizi ambaye amewekwa na towashi mkuu kwamba awajaribu wa siku kumi kwa kuwapa chakula cha mtama na maji tu wanywe halafu baada ya siku hizo kumi awatazame nyuso zao na nyuso za wale wanaokula posho ya chakula cha mfalme ili kuona kama kitawapa afya ama la! Baada ya siku kumi Biblia yasema hivi;’-Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme. Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu. [Daniel 1:15-16].
Akina Daniel na wenzake walikula chakula cha nafaka na matunda ambacho Mungu alikiagiza katika Kitabu cha Mwanzo1;26-27, na matokeo yake walikuwa na afya kuliko hata wale waliokuwa wanakula nyama na chakula cha mfalme. Hapa tunapata fundisho. Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa chakula bora ambacho kama Mwanadamu akikitumia atakuwa na afya tele. Kuhusu akina Daniel Biblia inatoa ushuhuda huu;’-Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake. [Daniel 1:20].
Matunda, mbogamboga, na nafaka ni chakula bora kwa binadamu. Katika siku za Mwisho watu wa Mungu watakuwa wana matengenezo ya afya. Sharti wakatae kutumia vyakula vile vyenye kudhuru afya ya miili yao na kumtukuza Mungu kwa kutumia vyakula vile ambavyo vinauletea Miili yao afya njema na siha njema. Miili yetu ni hekalu ka Roho mtakatifu na imetupasa kumtumikia Mungu tukiwa na miili yenye afya, ndipo tunaweza kumtolea Mungu ibada yenye maana. Kuuharibu Mwili ambao ni Hekalu la Roho Mtakatifu kwa kula ama kutumia vyakula vinavyoharibu afya ni chukizo kwa Mungu.
MAJINA BELTESHAZA, SHADRAKA, MESHAKI NA ADENEGO MAANA YAKE NINI?

Kwenye Daniel 1:6, je majina haya yalimaanisha nini?
Hivi ndivyo yalivyomanisha kwa mujibu wa The Bible Knowledge Commentary: Old Testament, uk.1330.
Belteshaza:
lilikuwa neno la Kiakadi Belet-sar-usur lililomaanisha "Mwanamke, mlinde Mfalme."
Shadraka:
Yaelekea kilikuwa kitenzi cha Kiakadi Saduraku, kilichomaanisha "Ninamwogopa [mungu]". Kwa upande mwingine, huenda kilitoka Aku, mungu mwezi wa Kisumeria.
Meshaki:
Huenda kilikuwa kitenzi cha Kiakadi mesaku, kilichomaanisha "Nimedharau, enye kudharauliwa, nyenyekevu [mbele za mungu]."
Abednego:
Ilimaanisha mtumwa wa [mungu aliyeitwa] Nebo. Nebo alikuwa ni mungu wa Kibabeli wa kuandika na mimea. Alikuwa mtoto wa kiume wa Bel.
Majina haya yaelekea yalikuwa na lengo la kuwakumbusha kuwa walikuwa mateka, na kuitukuza miungu ya Babeli.
Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.600 kinatoa maana tofauti kabisa. Kinasema Belteshaza linamaanisha "Bel analinda maisha yake", Shadraki linamaanisha "Aku anaamuru", Meshaki lilikuwa neno lenye maana isiyokuwa na uhakika. Mtunzi anakubali kuwa Abednego linamaanisha "mtumwa wa Nebo."
SWALI:
Kwenye Daniel 1:7; 4:8, kwa nini Danieli na vijana wengine watatu wa Kiyahudi waliafiki majina yao kubadilishwa kuwa majina yaliyohusisha miungu ya kipagani?
Huenda hawakuwa na uhuru wa kuamua kuhusu jambo hili. Biblia haikatazi mtu kupewa jina la mungu sanamu, ingawa kwa kawaida muamini hatapenda kufanya hivyo.
SWALI:
Kwenye Daniel 1:8-20, Danieli na vijana wengine watatu wangeweza kusema, "kwa kuwa hatuna uhuru wa kuchagua" ni lazima tule chakula hiki. Upande mwingine, wangeweza kusema, "tuko radhi kufa kuliko kula chakula hiki." Je unadhani kitendo cha Danieli kilikuwa kizuri zaidi?
Kitendo cha Danieli kilihitaji kumtumaini Mungu. Aliamini kuwa Mungu atawafanya wawe na afya njema, ingawa hawakuwa wanakula nyama, au kunywa mvinyo (ambayo inaweza kupunguza madhara mabaya ya vyakula vilivyoathiriwa na bakteria).
SWALI:
Kwenye Daniel 1:10, kwa nini Danieli na rafiki zake hawakula chakula hiki?
Kwa kuwa vijana hawa wa Kiyahudi walizingatia amri za Agano la Kale zihusuzo chakula, kulikuwa na sababu zisizopungua tatu.
1. Moja ya sababu hizi hapana shaka ilihusu nyama ya nguruwe, samakigamba, huenda hata nyama ya ngamia, na wanyama wengine waliozuiliwa kuliwa. Isitoshe, hata wanyama wasafi huenda walipikwa kwenye vyombo vilevile vilivyopikia wanyama najisi.
2. Kwani hata wanyama safi, Wayahudi hawakuwa wanakula damu yake. Hatujasikia jamii za zamani zikitoa damu kabla ya kuwapika wanyama.
3. Huenda nyama ilitolewa kwa sanamu kwanza, na huenda hawakupenda kula nyama hiyo.
4. Kulikuwa na sheria nyingine, kama vile kutokumtokosa ndama katika maziwa ya mama yake.
John Chrysostom (kabla ya mwaka 407 BK) anaelezea kwa ushawishi mkubwa taabu yao kwenye makala yenye somo moja iitwayo None Can Harm Him Who Dot Not Injure Himself ch.15 (NPNF, juzuu ya 9), uk.281-282.
SWALI:
Kwenye Daniel 1:10-15, kwa nini vijana hawa wa Kiyahudi walionekana kuwa na afya bora kuliko wale wengine?
Ingawa Maandiko hayasemi, inaweza kuwa ni mchanganyiko wa sababu zisizopungua tano.
1. Huenda ulikuwa ni muujiza, mbali na hali ya kawaida.
2. Huenda chakula rahisi, kisichokuwa na nyama ya nguruwe na mapochopocho mengine, walichokula vijana wa Kiyahudi hakikuwa na vijidudu ambavyo vyakula vingine vilikuwa navyo.
3. Hapakuwa na viu vya kuhifadhi vyakula visioze, majokofu, na palikuwa na karafuu chache wakati ule. (Maradhi yanayosababishwa na bakteria na sumu nyingine zinazokuwa kwenye chakula huenda yalikuwa mengi sana wakati ule).
4. Huenda watu wengi kwenye jumba la mfalme walikunywa mvinyo kupita kiasi. Mbali ya kutokuwa nzuri kwa ini, mvinyo iliyozidi kiasi inaweza kumfanya mtu mwenye rangi nyeupe awe mwekundu usoni. Hii ni kwa sababu kapilari hupasuka na kuwa na rangi nyekundu.
5. Uwezekano mdogo sana ni kuwa kupungunguza kula vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi kunaweza kuounguza vipele usoni.
SWALI:
Kwenye Daniel 1:12-16, je Danieli hakuwa anakula nyama na kunywa mvinyo maisha yake yote?
Hapana, kwa sababu kwenye Daniel 10:2-4 wakati Danieli alikuwa anaomboleza kwa majuma kamili matatu, alibadilisha milo yake na hakula nyama wala kunywa mvinyo. Jambo hili linaonyesha kuwa hakuwa anakula vitu hivyo.
SWALI:
Kwenye Daniel 1:20, je waganga na wachawi walikuwa watu mashuhuri Babeli?
Ndiyo. Kuwa bayana, chimbuko la unajimu wa magharibi ni Babeli. Chanzo kingine cha unajimu kilikuwa Pergamumu, Asia Ndogo, lakini hii ilikuwa miaka 400 baadaye, na huu pia ulitokea Babeli.
SWALI:
Kwenye Daniel 1:21, je Danieli aliishi hadi mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi, au mwaka wa tatu kama Daniel 10:1 inavyosema?
Yote, kwa kuwa Danieli aliendelea hata baada ya mwaka wa tatu. Daniel 1:21 inasistiza kuwa Danieli alikuwa kiongozi si tu hadi mwisho wa Himaya ya Babeli, bali hata wakati wa Himaya ya Uajemi. Biblia haisemi kuwa Danieli alikufa au alistaafu mwaka wa kwanza wa Koreshi. Dan 10:1, ambayo inaweza kuwa iliandikwa baadaye kidogo, inasema hata mwaka wa tatu.
USIKOSE SEHEMU YA TANO Daniel 2, ndoto hii ilitokea lini? JE, ILIKUWA NDOTO IPI NA MAANA YAKE NINI?
USIKOSE SEHEMU YA TANO........ .
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW