Thursday, November 17, 2016

WAISLAM WENYE KUIMBA/KUSIKILIZA MUZIKI WATAGEUZWA KUWA NYANI NA NGURUWE.


HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAM WOTE DUNIANI WANAO SIKILIZA MUZIKI AU IMBA MUZIKI.
Muziki ni haraam kutokana na dalili dhahiri tulizopewa katika Qur-aan na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
وقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((ليكونن من أمتي أقوام يستحلون الحر و الحرير و الخمر و المعازف، و لينزلن أقوام إلى جنب علم، يروح عليهم بسارحة لهم، يأتيهم لحاجة، فيقولون: ارجع إلينا غدا، فيبيتهم الله، ويضع العلم، ويمسخ آخرين قردة وخنازير إلى يوم القيامة ((رواه البخاري
Na akasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na MUZIKI. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: “Rudi kesho”. Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah))[Al-Bukhaariy]
Imaam Abu Haniyfah amesema: “Kuimba (nyimbo, ngoma) ni katika madhambi makubwa ambayo inatakiwa Muislamu kujiepusha nayo haraka”
Khofu zaidi imuingie Muislamu kuwa anaweza kupata adhabu ya kugeuzwa nyani au nguruwe kwa maasi haya kama tulivyoonywa katika Hadiyth ifuatayo:
Na kasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watu katika Ummah wangu watakunywa pombe wakiipa jina jengine lisilokuwa hilo, MIZIKI itapigwa kwa ajili yao na watakuweko waimbaji wanawake. Allaah Atawadidimiza ardhini na Atawageuza wawe nyani na nguruwe)) [Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya Sahiyh]
GHADHABU ZA ALLAH KUWAANGAMIZA WAFANYAO MAASI HAYA
Vile vile ghadhabu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ni kali mno za kuangamizwa pindi maasi haya yatakapodhihirika.
عن عمر بن حصيل عن رسول الله صلى الله عليه وسلم انه قال: ((يكون فى امتى قذف ومسخ وخسف)): قيل يارسول الله ومتى ذلك قال: ((اذا ظهرت المعازف… )) اخرجه الترمذى وصححه العلامه الالبانى
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Kutatokea katika Ummah huu maafa ya kuteremshiwa mawe kutoka mbinguni, kugeuzwa maumbile ya binaadamu [kugeuzwa kufanywa nyani na nguruwe] na mididimizo [ya ardhi]. Ikaulizwa: Ewe Mjumbe wa Allaah, lini yatatokea hayo? Akasema: ((Itakapodhihirika muziki … )) [At-Trimidhy na ameipa daraja ya Sahiyh Shaykh Al-Albaaniy]
SAUTI ZA NYIMBO ZIMELAANIWA DUNIANI NA AKHERA
قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((صوتان ملعونان فى الدنيا والاخره مزمار عند نعمه ورنه عند مصيبه ((البزار و صححه العلامه الالبانى
Na kasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): ((Sauti mbili maluuni [zilizolaaniwa] duniani na Akhera; mizumari katika furaha na kuombeleza katika misiba)) [Al-Baazaar – na Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya Sahiyh]
Hivyo tumeona kuna umuhimu mkubwa wa kuwakumbusha ndugu zetu waepukane na haramu hii ili wajiokoe na ghadabu za Mola Mtukufu, ghadhabu kali ambazo zinafika kumgeuza mtu awe nyani au nguruwe kama tutakavyosoma katika hizi dalili za wazi wazi zenye uhakika.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ))
((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha)) [Luqmaan: 6]
Ibn Mas’uud (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema kuhusu Aayah hii “Naapa kwa Allaah hii inamaanisha ni kuimba” [At-Twabariy 20:127]
وعن ابن عباس قال عن آية: ((ومن الناس من يشتري لهو الحديث))، قال :الغناء وأشباهه إسناده صحيح – المحدث: الألباني
Na Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) pia amesema kuhusu Aayah: ((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi)) “Ni nyimbo na maneno ya yanayofanana (ya upuuzi)” [Isnaad Sahiyh kutoka kwa Shaykh Al-Albaaniy]
Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anamwambia Ibliys:
((وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُمْ بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الأَمْوَالِ وَالأَوْلادِ وَعِدْهُمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلاَّ غُرُورًا))
((Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na shaytwaan hawapi ahadi ila ya udanganyifu)) [Al-Israa: 64]
Hii inamaanisha ni nyimbo kama ilivyo rai ya Mujaahid katika Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]
Vile vile Hadiyth zifuatazo zimedhihirisha uharamu wa nyimbo, ngoma na kila aina ya muziki:
عبدالله بن عمرو بن العاص عن رسول الله صلى الله عليه وسلم انه قال: ((إن الله حرم الخمر والميسر والكوبه وكل مسكر حرام ((إسناده صحيح
و في رواية أحمد قال سفيان: قلت لعلي بن بذيمة: “ما الكوبة؟” قال: “الطبل”
Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amru ibnul ‘Aasw kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameharamisha pombe na kamari na kuubah na kila kilinacholewesha ni haram)) [Isnaad yake ni Sahiyh]

Na katika usimulizi mwingine kutoka kwa Imaam Ahmad, Sufyaan amesema: Nilimuliza ‘Aliy ibn Budhaymah: “Nini Kuubah?” Akasema: “Ngoma”.
INASHANGAZA SANA WAISLAM WA LEO WANAIMBA NYIMBO ZA BONGO FLEVA NA HUKU MASHEHE, USTAADH, IMAM WAO WAPO MSTARI WA MEBLE KUCHEZA NYIMBO ZA BONGO FLAVOR.
ALLAH AMESHA WAPIGA MUHURI NYOYONI MWAO NA WATAGEUZWA KUWA MANYANI NA MANGURUWE.
HAKIKA HAKUNA MUISLAM ATAYE WEZA HEPUKA GADHABU YA ALLAH YA KUWAGEUZA KUWA MANYANI NA MANGURUWE.
Ndio maana mimi sio Muislam, namfuata Yesu ambaye hana chuki na Nyimbo za Injili, Pambio, Tenzi za Rohono zinazo msifu Bwana.
Ni mimi MAX SHIMBA, mtumwa wa YESU KRISTO.
Shalom.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW