Friday, November 25, 2016

KITABU CHA DANIEL (SEHEMU YA SITA)


Falme zenye nguvu zilitokea na Kupita, na falme zenye nguvu zitatokea na Kupita lakini Mwisho wa Siku Mungu atausimamisha Utawala wake ambao hautapita kamwe nao utadumu milele hata Milele. Mungu ndiye Mfalme Mkuu naye amempa Kristo Mwana wake kuwa na Mamlaka yote ya Mbinguni na ya duniani.

Falme za duniani zina kiburi dhidi ya Mbingu na zinatawala kwa kiburi na kwa Kuiasi mamlaka ya Mungu zikifikiri kuwa zitadumu mulele, lakini zitapita. Yesu Kristo anakuja kukomesha falme zote za dunia na kusimika Ufalme wake ambao Utadumu hata milele na Milele. Ufalme wa Yesu ndio Lile Jiwe ambalo litakuja kuipondaponda ile sanamu na kuisagasaga na kisha kuwa mlima Mkubwa na kuijaza dunia yote.

Biblia yasema hivi;’-Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti. [Daniel 2:44-45]
Hata sasa Mungu ndiye atawalaye mataifa yote na amewawekea Muda wa kutubu na kumrudia yeye. Mkono wake ndio unaotawala siasa zote na mwenendo wote wa kimataifa. Yeye ndiye anayewashusha wafalme na kuwapa wale awapendao ufalme. Mataifa makuu yanatenda dhambi na kumpuuza Mungu walakini Biblia yasema kuwa Kristo atakuja kuuadhibu ulimwengu na kuwaokoa wenye haki na kusimika ufalme wake wa haki na wa milele.
Biblia yasema hivi;’-Dunia hii itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana Bwana amenena neno hilo. Dunia inaomboleza, inazimia; ulimwengu unadhoofika, unazimia; watu wakuu wa dunia wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele. [Isaya 24:3-5].
Kristo atakuja ili aitetemeshe mno dunia walakini watu wa Mungu wataokolewa na kupewa Ufalme na kutawala Milele hata milele pamoja na Kristo. Biblia yasema hivi;’-Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia. Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo; ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia. [Isaya 2:19-21].
Walakini kuhusu watakatifu Biblia yasema hivi;’-Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. [Daniel 7:27]
SWALI:
Kwa nini Daniel 2:4b-7:28 iliandikwa Kiarami wakati Daniel 8:1-12:13 iliandikwa Kiebrania?
Danieli au katibu wake mmoja au zaidi aliweza kuandika kwa lugha yeyote aliyoona nzuri zaidi; hakuna kitu chochote kitakatifu zaidi katika lugha ya Kiebrania. Hatufahami sababu ya waandishi wanadamu kuchagua kuandika namna hii. Sababu mojawapo inaweza kuwa kwamba sura za kwanza zilihusu mataifa yaliyopo Mashariki ya Kati, wakati sura za mwisho ziliwahusu Wayahudi.
Ezra 4:8-6:18 na 7:12-26 pia zimeandikwa Kiarami. Pia zingatia kuwa Danieli sura za 1-6 zimeandikwa kwa kutumia nafsi ya tatu, wakati Daniel 7:2 inaanza na nafsi ya kwanza.
Sehemu iliyoandikwa Kiarami inaanza mara moja baada ya "kumjibu mfalme kwa Kiarami." Kitabu hakirudi kwenye Kiebrania hadi Daniel 8:1.
SWALI: 

Kwenye Daniel 2:4b-7:28, kitu gani zaidi tunachokijua kuhusu Kiarami?
Kiarami ilikuwa ni lugha iliyodumu kwa muda mrefu sana, iliyofanana sana na Kiebrania. Ilitumiwa na Labani na watu wa Shamu wakati wa uhai wa Abraham (Mwanzo 31:47); ilitumiwa hapa, na wakati wa Yesu, na ilitumiwa kwa karne chache zaidi na Wanestori na Wakristo wengine Shamu na upande wa mashariki. The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.247 inasema uchunguzi huu wa isimu (sayansi ya lugha) umeonyesha kuwa kulikuwa na makundi makubwa manne ya Kiarami: Kiarami cha zamani, Kiarami rasmi, Kiarami cha Levanti (sehemu ya mashariki ya Bahari ya Mediteramia pamoja na visiwa na nchi jirani), Kiarami cha mashariki. Waashuri kutoka karibu mwaka 1100-605 KK waliongea Kiarami rasmi.
Nje ya Biblia, "Waarami", wakiwemo wale waliome kwenye Kitabu cha Danieli, wameonekana kwenye maandiko ya Ugariti wakati wa kipindi cha Amarna, karibu mwaka 1400 KK. The Expositor’s Bible Commentary pia inasema Kiarami cha kwenye Danieli kilitumika kutoka karne ya 7 na kuendelea, na kilitumiwa kwenye karne ya 5 na Wayahudi kwenye makaratasi ya mafunjo huko Yebu (Elephantine), Misri na kwenye Kitabu cha Ezra. The Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 1, uk.403 inasema kuwa Kiarami hiki kinachukuliwa kuwa tofauti na Kiarami kilichoandikwa Qumran karibu na wakati wa Yesu.
Tazama The New International Dictionary of the Bible, uk.74-75 kuona picha ya Kiarami kilichoandikwa kwenye chombo cha ufinyanzi kilichomwongelea Eliashibu, mtu ambaye anawekuwa alikuwa kamanda wa ngome ya Aradi. Wycliffe Bible Dictionary, uk.123 inasema kuwa mifano mingi imeonekana ya Wababeli (mwaka 605-538 KK) na Waajemi walikuwa wakitumia Kiarami rasmi katika barua zao za kikazi. Mkusanyiko wa Borchardt una barua 13 za Kiajemi, zilizoandikwa Kiarami, kutoka Misri.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:6, je neno hili "heshima" linadokeza nini?
"Thawabu" ni neno la umoja (siyo wingi), na linamaanisha zaidi zawadi kuliko malipo.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:18, Danieli aliwezaje kuwekwa pamoja na "wenye hekima", kwani walikuwa wanafunzwa uchawi?
Vijana wa Kiyahudi walifunzwa lugha na maandiko ya Wababeli. Haimaanishi kuwa walifunzwa mambo ya dini au uchawi, na hata kama ilikuwa kinyume cha nia yao, hapakuwa na ushahidi wowote kuwa walifanya mambo hayo. Tazama kwenye Dan 2:2 kuwa Nebukadneza alipowaita wachawi, wafanya mazingaombwe na wanajimu, Danieli hakuwa miongoni mwao. Danieli alikuja kusikia kuhusu jambo hili baadaye.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:20-23 kuna sababu gani zisizopungua nne za Danieli kuchukua muda mrefu kiasi hicho kumsifu Mungu baada ya Mungu kumfunulia maana?
Hii ni sara nzuri sana, ambayo imeundwa vizuri sana. Huenda kukawa na sababu hizi nne.
1. Kama Nebukadneza angewaua watu wote wenye hekima, Dan 2:18 inaonyesha kuwa Danieli naye pia angeuawa. Danieli alijawa na shukrani kwa sababu ya usalama wake, rafiki zake, na watu wengine.
2. Hata bila ya hatari iliyopita, Danieli alishukuru bayana kuwa Mungu alimfunulia mafumbo yake kwake. Tunapaswa kuwa na shukrani Mungu anapotufunulia vitu mbalimbali kupitia neno lake.
3. Kwa ujumla, Danieli alikuwa mtu wa shukurani na mwenye mazoea ya kumwomba Mungu, mara tatu kwa siku kwenye Dan 6:10. Danieli alikuwa na mazoea ya kushukuru na kuomba kwa Mungu.
4. Ombi hili huenda lilikuwa "ulinzi" kwa Danieli. Ilikuwa dhahiri kuwa hakuna binadamu ambaye angeweza kulifanya jambo hili, bila msaada wa Mungu. Danieli anaweza kuwa alifikiria kukusanya vitu alivyokuwa navyo kukabiliana na hali iliyokuwepo wakati huo, au kuwa alistahili kwa ajili ya uhusiano wake wa karibu na Mungu. Ombi hili lilikuwa ni ukiri wa Danieli kuwa ni Mungu tu, na hakufanya kitu chochote zaidi ya kile ambacho Mungu alimfunulia.
SWALI: Kwenye 2:24, kwa nini Danieli hakuwaacha watu wenye hekima wa Babeli waliokuwa wapagani wauawe?
Danieli hakuwa na chuki au nia mbaya dhidi yao. Yeyote miongoni mwa watu waliochaguliwa na Mungu aliyeshiriki kwenye vitendo vya uchawi alipata adhabu ya kifo kwenye Agano la Kale. Hata hivyo, si watu wenye hekima wa Babeli waliokuwa wachawi, na hata wale waliokuwa wachawi hawakujua kuwa Biblia ilikataza.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:24-25, kwa nini Arioko alisema kuwa amempata Danieli, badala ya kusema Danieli alikuja kwake?
Huenda Arioko alitaka kupata sifa njema kwa kitu ambacho hakukifanya. Kwa bahati mbaya, wakati mwingine wafanya biashara siku hizi nao hupenda kupata sifa njema kwa vitu ambavyo hawajavifanya.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:28-3:1, je Nebukadneza alimwamini Mungu baada ya hapo?
Nebukadneza walau alimini kuwa Mungu wa Danieli alistahili kuheshimiwa, hasa kwa kuwa alikuwaa na uwezo wa kusimamisha na kuondoa falme. Hata hivyo, baada ya hapo, kwenye Dan 3:1 Nebukadneza alisimamisha sanamu ambayo watu wote walitakiwa kuinama mbele yake na kuisujudia.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:30, kwa nini Danielie alikuwa makini kuhakikisha watu wanafahamu kuwa hekima haikutoka kwake, bali kwa Mungu?
Kwenye jamii ambayo watu na sanamu zisizokuwa na uhai ziliabudiwa kwa sababu yeyote ile, Danieli alitaka kuhakikisha kuwa anawafahamisha watu kuwa ni Mungu tu aliyetakiwa kuabudiwa hapa, na si Danieli.
Leo hii, hata panapokuwa hakuna nafasi kwa sisi kuabudiwa, ni muhimu kumpa Mungu utukufu, kuliko kuwafanya watu wengine watupe utukufu wakati walipaswa kumwangalia Mungu.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:31-35, je metali hizi zina sifa gani?
Dhahabu ni ya thamani zaidi, nzito zaidi, na laini zaidi. Fedha ni ya pili, na chuma ni ya mwisho. Bila kuangalia uwezekano kuwa sanamu za dhahabu zilikuwa zinafunikwa kwa dhahabu, hazikuwa za dhahabu halisi, jambo hili lilionyesha kuwa Himaya ya Babeli ingeweza kuonekana kuwa bora zaidi, yenye utulivu zaidi, na isiyoweza kutikiswa. Himaya ya Uajemi ilikuwa na maasi kutoka kwa Wagiriki, Wamisri, na maasi ya toka ndani ya nchi. Himaya ya Kigiriki (Makedonia) iligawanyika sehemu nne mara baada ya kifo cha Alexanda Mkuu. Himaya ya Rumi ilikuwa na changamoto nyingi zaidi kuliko himaya nyingine, na ilionekana kuwa yenye usalama kidogo zaidi (miongoni mwa maasi ya Wagaulu, Wakaarthaginia, Wajerumani, Wahuna, nk.) lakini ilikuwa ndio yenye nguvu zaidi. Kulikuwa na metali nyingine ambazo hazikuelezwa kwenye ndoto hii. Vile vile, kuna himaya nyingine ambazo hazijatajwa hapa, lakini hazikuwatawala Wayahudi.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:35a, je upepo uliowapeperusha unaweza kuwa unawakilisha kitu gani?
Upepo hapa si muda uliopangwa tu, bali huenda ilikuwa ni utendaji wa Mungu katika historia kutimiza kusudi alilolipanga.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:35b, je mlima ulioijaza dunia nzima ulikuwa ni kitu gani?
Huu unaweza kuwa ni ufalme wa Mungu, ulioanzishwa na Yesu Kristo. Huyu ni Yesu anayeyaangamiza mataifa. Jambo hili linatimizwa katika vita vya kThis is fulfilled at the Battle of Har-Magedoni kwa mujibu wa 1001 Bible Questions Answered, uk.291-292.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:37-44, je hizi falme nne zilikuwa zipi kwenye "sanamu kubwa sana kuliko binadamu" na mlima?
Hizi ni himaya za Babeli (karibu mwaka 605-538 KK), Uajemi ya Kigiriki (karibu mwaka 538 KK), Ugiriki/Makedonia (karibu mwaka 333 KK), na Rumi. Vifuatavyo ni vidokezo vitatu vitakavyotusaidia kupata jibu.
1. Hizi hazikuwa himaya zozote zile nne, lakini himaya zilizohusiana na Wayahudi na zilichukua madaraka ya moja toka kwa nyingine. Hivyo, himaya za India, China, Mongoli, na himaya za ulimwengu mpya hazihusiki hapa.
2. Daniel 2:36-39 inaonyesha kuwa himaya ya Babeli ya wakati wa Nebukadneza ni ya kwanza. Hivyo, Himaya ya Misri haiwezi kuwa moja ya hizo nne, kwani ilikuwepo kabla ya Babeli, ingawa iliendelea kuwepo kwa namna fulani hadi wakati wa Waajemi. Vivyo hivyo, Himaya ya Waashuri si moja ya hizo nne kwani iliangamizwa kabisa kabla ya wakati wa Nebukadneza.
3. Yesu Kristo, kama mfalme wa wafalme, atasimamisha ufalme wake wakati wa himaya ya nne.
Kitabu cha mwenye kushuku kiitwacho Asimov’s Guide to the Bible, uk.603 kinasai kuwa himaya za Umedi na Uajemi zilichukuliwa kuwa himaya mbili, na himaya ya nne ilikuwa ya Makedonia ya Alexanda. Asimov huenda akawa anasema hivi kwa sababu anaamini kuwa Kitabu cha Danieli kiliandikwa baada ya Alexanda kutwaa madaraka (huenda ilikuwa baadaye sana hadi mwaka 165 KK. Asimov anadai). Hata hivyo, Himaya ya Umedi haikuwahi kuwa tofauti na Waajemi, kama ambavyo Himaya ya Rumi ilikuwa tofauti, kabla, wakati wa Julias Kaisari, na hata baada ya hapo.
SWALI:
Kwenye Daniel 2:37-44, je Himaya ya Umedi na Uajemi zilikuwa mbili tofauti badala ya moja?
Hapana, kwani kama Encyclopedia of Bible Difficulties, uk.293 inavyotukumbusha, Daniel 5:28 iko wazi kabisa. Mwandishi alijua kuwa uthibiti wa ufalme ulihama kutoka Himaya ya Babeli kwenda Himaya ya Ugiriki ya Kigiriki, si kutoka kwa Wamedi kwanza (ambao Waajemi waliwashinda kabla ya wakati huu) na baadaye kwenda kwa Waajemi.
USIKOSE SEHEMU YA SABA: Kwenye Daniel 2:38, nini inaweza kuwa ni sababu ya Danieli kusema kuwa Nebukadneza alitawala wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW