Friday, January 5, 2018

KWANINI MUNGU ALIUMBA MALAIKA?


Yeye Muumba ni mwenye uweza na utukufu hata asiweze kukaribiwa na mwanadamu katika namna alivyo. Yeye peke yake asiyepatikana na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, wala hakuna mwandamu aliyemwona wala anaweza kumwona. (Timotheo 6:16). Kwa kuwa malaika wao hawana upungufu kwa hiyo wanatenda kwa ajili ya Mungu wakimwakilisha yeye wanapowasiliana na wanaume na wanawake. Wao hufanyika faraja kati ya ufa mkubwa kati ya utukufu na ukamilifu wa Mungu wa Mbinguni na dhambi damu anayekufa katika sayari hii. malaika wao ni wa milele (yaani, hawafi). Umilele wao ni wa namna moja na ule Yesu aliounena wakati aliposema: Lakini wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwenngu ule na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewei; wala hawawezi kufa tena; kwa kuwa huwa sawa sawa na malaika nao ni wana wa Mungu kwa vile walivyo wana wa ufufuo (Luka 20:35,36). Lakini Yesu alisema hivyo, kwa namna moja na Malaika (watoto au "wana" wa Mungu) wanaishi milele na ni wa jinsia moja,kwa hiyo pia wale watakaoitwa "wana" na mabinti wa Mungu wakati Yesu atakaporudi watawezakuishi milele na hawataoa au kuolewa.
Waefeso 6: 12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Kwenye maisha yetu ya Ufalme tumefahamu sana kuhusu Jeshi la malaika wabaya na nguvu zao za giza lakini tumesahau kujifunza na kulitumia jeshi letu la Malaika watakatifu.
Tulijifunza kwenye Biblia kazi ya jeshi hili la Malaika watakatifu nahizi ni Baadhi ya sheria zao.
Mathayo 26: 53 “Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?”
Luka2: 13 “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema,”
Mwanzo 32: 1 “1 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye.Naye Yakobo alipowaona, alisema, Hili ni jeshi la Mungu. Akapaita mahali pale, Mahanaimu. Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.”
Zaburi 148: 2 “Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.”
Waebrania 12: 22 “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,”
Tumejifunza kwamba unapookoka unaingia kwenye Ufalme wa Mungu na huko unakutana na majeshi ya Ufalme ambao ni Malaika watakatifu. Tumejifunza kwamba malaika ni polisi wa Ufalme na pia ni wanajeshi wa Ufalme lakini kama hujui kuwatumia unakuwa hufanyi kitu ndani ya Ufalme. Tumeona pia kuna mambo mengine ambayo sisi tunafanya kama wana wa Ufalme, kuna mambo mengine ambayo malaika wanayafanya na kuna mambo mengine Neno la Mungu linayafanya na sio sisi. Kwa mfano:-
Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."
Maana yake ni sisi tunaokanyaga si Mungu, Unaweza kumkuta mtu anamwomba Mungu ashuke aje akibariki chakula chake na ashuke amlinde usiku kucha kitu ambacho hakiwezekani kwa Mungu kutoka kwenye kiti chake cha Enzi kwenda nyumbani kwa mtu kumlinda. hivyo ndivyo tulivyokuwa tukiamini lakini sasa tumeshafahamu maarifa kwamba siri ya Nguvu zetu Kuwa ndani ya Ufalme wa Mungu kuishika katiba yake ambayo ndiyo inatupa maelekezo ya namna ya kutenda hapa duniani.
Ufunuo 12: 12 “Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”
Wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo ina maana ndani ya Ufalme kuna silaha inayoitwa Damu ya mwanakondoo ambayo tunaweza kuitumia kushinda kila tatizo ‘unapokuwa kwenye maombi unakuwa unaitumia damu ya Mwanakondoo kushinda’, kwenye Maandiko imeandikwa neno la Mungu ni nyundo ivunjayo mawe vipandevipande, ni Upanga uuwao kuwili. Ukishafahamu sheria hii ndipo sasa unaamua kuitumia kupenya sehemu yeyote.
Pia tumejifunza kwamba tunayo silaha ya Malaika ambao ni watumishi wetu na tunao uwezo wa kuwaagiza kwenda mahali popote kutenda kazi.
USIKOSE SOMO LA "SHERIA YA MALAIKA ANAYEWEZA KUFUNGUA MILANGO"
Shalom

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW