Saturday, February 3, 2018

INJILI YA UMASKINI MAKANISANI IMETOKA WAPI KAMA SI KWA SHETANI?

No automatic alt text available.
UMASIKI NI NINI?
Umaskini (kutoka neno la Kiarabu) ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi ya binadamu kama vile chakula, maji salama, huduma za afya, mavazi na nyumba kutokana na kukosa uwezo wa kuvinunua. Hii pia inajulikana kama umaskini uliokithiri au ufukara.
Kwa maana nyingine, umasikini ni ile hali ya mtu kukosa pesa au mali ya kumiliki, kukosa pesa ya kufanyia shughuli za kimaendeleo, kwa mfano elimu, biashara n.k
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” YOHANA 1:12
Biblia inatuambia kuwa, wote walio mpokea Yesu aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. Sasa, iweje Mungu Baba MWENYE UPENDO awe tajiri na wewe mtoto wake uwe maskini wakutupwa?
Hakika kuna Injili ya upotofu ambayo inafundishwa Makanisani. Eti, Mkristo kuwa na Fedha au Mali au Tajiri basi wewe huwezi kuuona Ufalme wa Mbinguni. Je, hii Injili ua UMASKINI AU WOKOVU WA UMASKINI ni wa Kibiblia?
UNAFAAMU KUWA, MUNGU ANATAKA KUKUPA UTAJIRI WAKE?
“Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU, NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)
Biblia inasema Yesu Kristo Mungu Mkuu alifanyika maskini ili atufikie hata tulio maskini tupate kuwa matajiri na kumiliki pamoja nao. Neno kufanyika maskini haina maana alikuwa maskini, Yesu wa Nazareti ni tajiri kule kuja duniani ni kama alikuja katika umaskini kwani utajiri na ufahari wa mbinguni ukilinganisha na dunia, dunia inahesabiwa ni kama maskini, hakuna kitu huku utajiri wa kweli katika vyote u mbinguni na unapatikana tu kupitia Yesu kristo wa Nazareti.
HUDUMA YA YESU ILIKUWA TAJIRI ILE MBAYA, JE, MCHUNGAJI WAKO NA KANISANI KWENU NI MATAJIRI KAMA ALIVYO KUWA YESU?
Biblia katika Yohana 12:6 inasema; Yuda alisema hivyo si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. – INA MAANA HUDUMA YA YESU WA NAZARETI WALIKUWA MATAJIRI KIASI AMBACHO HATA YUDA PAMOJA NA KUIBA KWAKE HAWAKUPUNGUKIWA KITU YAANI NI KAMA VILE KUCHOTA MAJI BAHARINI YATAISHAJE?.
Luka 5:29-30; Baadaye Lawi mwana wa Alfayo akafanya karamu kubwa kumkaribisha Yesu wa Nazareti nyumbani kwake. Watoza kodi wengi walikuwa miongoni mwa watu wal ioalikwa, 30 Basi baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria ambao walikuwa kundi moja wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu wa Nazareti wakisema, “Mbona mnakula na kunywa na wenye dhambi?” – LAWI MWENYEWE ALIKUWA TAJIRI LAKINI AKATAJIRISHWA ZAIDI KATIKA KUMTUMIKIA YESU WA NAZARETI.
Matendo 28:30; Kwa muda wa miaka miwili Paulo aliishi katika nyumba ya kupangisha akiwakaribisha wote waliokuja kumwona.- MTUME PAULO ANATHIBITISHA PIA KWAMBA KUMHUBIRI YESU WA NAZARETI NI UTAJIRI KATIKA KILA IDARA.
Marko 10: 23-25; Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!”. Wanafunzi wake wakashtushwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akasema tena, “Wanangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu. Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”- KAMA WASINGEKUWA MATAJIRI WANAFUNZI WA YESU WASINGESHITUSHWA NA KAULI YAKE HIYO.
Mpendwa mwana wa Mungu nakutakia baraka na heri za Mbinguni sasa na daima na milele. Tumsifu Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.
USIKUBALI KUFUNDISHWA INJILI POTOFU YA UMASKINI KANISANI KWAKO. ANZA KUKIRI KUWA WEWE NI MBARIKIWA NA TAJIRI. ANZA KUKUBALI KUWA MUNGU ALIKUUMBA WEWE UWE MMILIKI WA UTAJIRI NA SIO UMASKI AMBAO NI MTEGO WA SHETANI.
Shalom,
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW