Saturday, March 2, 2019

MUNGU NI NANI NA ALITOKEA WAPI?

Image may contain: one or more people and text




Hili ni swali nzuri sana. Kuna majibu mengi sana kwa hili swali. Watu wengine husema "Hakuna Mungu." Jibu lako kwa swali hili, litatambua jinsi unavyo wajali watu wengine. Tena jibu lako litaonyesha ni wapi utakapoishi baada ya hapa duniani. Jinsi tunavyo amini Mungu ni nani, hudhibitisha kama tunaabudu Mungu wa kweli au sisi wenyewe. Kama tunampenda Mungu, basi inatupasa tuwapende watu wengine. Kuna dini kubwa tatu hapa duniani. Sote hufundisha mafundisho tufauti. Kwa hivyo zote tatu haziwezi kuwa za ukweli.

Mungu wa kweli ndiye Muumba wa vitu vyote. Hana mwanzo wala mwisho. (Zaburi 90:2) Yeye ndiye Chanzo cha habari njema inayopatikana katika Biblia. (1 Timotheo 1:11) Kwa kuwa Mungu ndiye aliyetuumba, tunapaswa kumwabudu yeye peke yake.​—Soma Ufunuo 4:11.

Musa aliandika hivi: ‘Ee Mungu, kabla ya kuzaliwa kwa milima, ao kutokezwa kwa dunia na inchi yenye kuzaa kana kwamba kwa maumivu ya kuzaa, tangu wakati usio na kipimo mupaka wakati usio na kipimo wewe ni Mungu.’ (Zaburi 90:1, 2) Nabii Isaya naye alisema hivi: ‘Je, haujajua ao, je, haujasikia? Mungu, Muumba wa miisho ya dunia, ni Mungu mupaka wakati usio na kipimo’! (Isaya 40:28) Vilevile, barua ya Yuda inaeleza kwamba Mungu amekuwapo “kwa umilele wote uliopita.”—Yuda 25.

Mungu ni roho, kwa asili isiyoonekana (Yohana 4:24). Mungu ni Mmoja, lakini Yeye yupo kama watu watatu-Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu (Mathayo 3: 16-17). Mungu ni asiye na mwisho (1 Timotheo 1:17), hauwezi kulinganishwa (2 Samweli 7:22), na hawezi kubadilika (Malaki 3: 6). Mungu yupo kila mahali (Zaburi 139: 7-12), anajua kila kitu (Mathayo 11:21), na ana nguvu zote na mamlaka (Waefeso 1; Ufunuo 19: 6).

Mungu (Elohim) wa pekee Mmoja ndiye Mungu wa kweli. Kabla yake Mungu hakuumbwa awaye yote, wala baada yake hatakuwepo yeyote mwingine. (Isaya 43:10) masomo haya yanayolenga katika kutufundisha kumjua Mungu yakijikita zaidi katika kutufundisha jinsi tunavyoweza kumjua Mungu,na Kunyenyekea kwa Kicho Kwake na Kumwabudu yeye Mungu Mmoja wa Kweli wa pekee.

Mungu ni nani? — Tabia yake

Hapa ni baadhi ya sifa za Mungu kama ilivyofunuliwa katika Biblia: Mungu ni wa haki (Matendo 17:31), mwwenye upendo (Waefeso 2: 4-5), mwenye kweli (Yohana 14: 6), na mtakatifu (1 Yohana 1: 5). Mungu anaonyesha huruma (2 Wakorintho 1: 3), huruma (Warumi 9:15), na neema (Warumi 5:17). Mungu anahukumu dhambi (Zaburi 5: 5) lakini pia hutoa msamaha (Zaburi 130: 4).

Kulikuwa na wakati ambapo hakuna kitu cho chote kilicho ishi, yaani nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, ila Roho wa Mungu aliyekuwa Mmoja. Alikuwako tangu milele. Tangu mwanzo, alikuwako Yeye wa Pekee, hakuhitaji kitu cho chote ili kupata Nguvu au Uhai. Huyu ndiye Mungu Mmoja na wa Kweli. (Yohana. 17:3:1Yonana 5:20) Ni Mungu wa Milele (1 Timotheo 6:16). Hii ina maana ya kwamba ni Mungu asiyekufa. (Mungu asiyepatikana na mauti)

Mungu ni nani? — Kazi Yake

Hatuwezi kuelewa Mungu mbali na matendo Yake, kwa sababu kile Mungu anachotenda hutoka kwake. Hapa kuna orodha ya kazi za Mungu, zilizopita, zilizopo, na za baadaye: Mungu aliumba ulimwengu (Mwanzo 1: 1; Isaya 42: 5); Anashikiria kikamilifu ulimwengu (Wakolosai 1:17); Anafanya mpango wake wa milele (Waefeso 1:11) ambayo inahusisha ukombozi wa mwanadamu kutoka kwa laana ya dhambi na kifo (Wagalatia 3: 13-14); Anawavuta watu kwa Kristo (Yohana 6:44); Anawaadhibu watoto Wake (Waebrania 12: 6); Na atahukumu ulimwengu (Ufunuo 20: 11-15).

Hapo mwanzo Mungu (Elohim) alianza Uumbaji. Lakini kabla ya kuanza Uumbaji wa cho chote, Mungu alijua ni nini atakachokiumba na kwa namna gani atakavyoumba. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Alijua hata mwisho wa uumbaji wake wa kila kitu. Kwa kila kitu ambacho kilitokea kuwepo, Mungu (Elohim) alijua jinsi ya utendaji wa kazi wa kila kiumbe katika uumbaji na uhusiano kati ya kila kimoja na kingine.

Mungu (Elohim) ni Alpha na yeye ni Omega (Ufunuo 1:8) Yeye ni wa Pekee alikuwako tangu Mwanzo na wa Milele, kwa hiyo ni Alpha, au Mwanzo. Yeye ni Omega kwa sababu yeye atakuwa wa mwisho katika vyote alivyo viumba. Uumbaji unaendelea kwa sababu ya Yeye. Uumbaji umejikita juu Yake na Yeye Ndiye yote katika wote.

Kabla ya kitu cho chote kuwepo, Mungu alijua atakacho kiumba na kwa namna gani. Alijua kila kitu kitakavyokuwa. Alijua kabla, matokeo na mwisho wa kila kitu. Hakuna cho chote kilichofichika au kilichofanyika kwa siri ambacho Mungu hakukijua kabla ya Uumbaji kuanza. Mungu alijua kila kitu (1Yoh. 3:20). Tendo hili la Mungu kujua kila kitu yaani kujua yote linaitwa hekima kuu ya Mungu (Omniscience). Mungu hakutaka msaada wa kitu cho chote, kutoka kwa ye yote kumsaidia yeye katika kufikiri, kufanya maandalio, au kufanya hesabu kabla ya uumbaji. Aliweza yeye mwenyewe kufikiri na kufanya hesabu ya kila umbo na aliweza kuona ni njia ipi ambayo kila chaguo lake lingeweza kutekelezwa.

Mungu ni Mweza wa yote Omnipotent. (Mwenye Nguvu na Mamlaka). Hakuna kitu ambacho hawezi kukifanya kikamilifu kutimiza mapenzi ya mpango wake. Yeye anajua yote yanawezekana kwake, na anajua njia sahihi ya kuumba vitu mbalimbali.Kila kitu kilichoumbwa kiliandaliwa na kuthibitishwa, kudhihirika tangu mwanzo. Huo ni pamoja na Uumbaji wetu sisi. Kila kitu kilionyesha maana katika kutenda kazi njema hata mwisho.

Mungu alijua ni jinsi gani vitu vingeweza kutengenezwa, na kwa namna gani na kwa idadi gani na kadhalika. Elimu hii ni kweli; Mungu ni Kweli (Kumbukumbu 32:4). Mungu aliweza kuumba ulimwengu na vitu vyote bila kubahatisha au kujutia matokeo yake. Kwa hiyo, mapenzi yae yalileta nuru ya utimilifu wake katika ukweli (Mungu ni Kweli) Kwa asili au kitabia Yeye hana makosa yo yote (Yaani ni Mkamilifu Mtakatifu na kazi yake haina makosa kiasili na kitabia) Mungu hawezi kutenda kosa kwa sababu ya uweza na uhodari wake mkubwa katika utendaji wake. Humuwezesha kuepukana na majuto katika hekima yake kuu ya kujua yote, inamfanya Mungu kuwa Mkamilifu (Mathayo. 5:48).

Kabla ya kuanza Uumbaji, Mungu alijua ya kwamba kazi yake yote itakuwa kamilifu na njema. Alijua ni nini kilichokuwa chema sana, kwa sababu Mungu alipenda Uumbaji uwe kama yeye Mwenyewe na kuwa Nuru kama yeye Mwenyewe alivyo nuru. Mapenzi ya mwisho ya Mungu ni wema (Zaburi 25:8) Chanzo cha wema wote hutoka kwake. Wema wote hutoka kwake. Mtu mmoja aliposema yakuwa Kristo ndiye Mwalimu Mwema, Yesu alijibu, “ kwa nini unaniita Mimi Mwema? Mungu tu ndiye Mwema” (Mathayo. 19:17; Marko. 10:18, Luka 18:19).

Maandiko hayo yanatuonyesha kwamba Mungu ni ‘Mfalme wa umilele,’ kama vile mtume Paulo anavyoeleza. (1 Timotheo 1:17) Hilo linaonyesha kwamba Mungu amekuwako siku zote, hata iwe tunafikiria miaka ngapi iliyopita. Na ataendelea kuwapo wakati unaokuja. (Ufunuo 1:8) Kwa hiyo, kwa kuwa amekuwapo milele hilo linahakikisha kwamba yeye ni Mweza-Yote.

Sababu gani tunaona kuwa ni vigumu kuelewa wazo hilo? Kwa sababu maisha yetu ni mafupi, tunaelewa wakati kwa njia tofauti kabisa na namna Mungu anavyouelewa. Kwa sababu Mungu ni wa milele, kwake miaka elfu ni kama siku moja. (2 Petro 3:8) Kwa mfano: Je, panzi anayeishi tu siku 50, anaweza kuelewa urefu wa maisha yetu wa miaka 70 ao 80? Hawezi kabisa kuelewa! Hata hivyo, Biblia inaeleza kwamba tuko kama panzi inapotulinganisha na Muumbaji wetu Mkubwa. Hata uwezo wetu wa kufikiri unaonekana kuwa kidogo sana unapolinganishwa na uwezo wake. (Isaya 40:22; 55:8, 9) Kwa hiyo, kuna utu ao namna ya kuwa ya Mungu ambayo wanadamu hawaelewe kabisa.

Hata ikiwa wazo la kwamba kuna Mungu wa milele linaweza kuwa gumu kuelewa, tunaona kwamba wazo hilo linapatana na akili. Ikiwa kuna mutu fulani aliyemuumba Mungu, mutu huyo anapaswa kuwa ndiye Muumba. Lakini, Biblia inasema kwamba ni Mungu tu ndiye ‘aliyeumba vitu vyote.’ (Ufunuo 4:11) Zaidi ya hilo, tunajua kwamba wakati fulani ulimwengu haukuwa. (Mwanzo 1:1, 2) Ulimwengu ulitoka wapi? Muumbaji wake alipaswa kuwa kwanza. Aliishi pia mbele ya kuumbwa kwa viumbe vyote vyenye akili, kama vile Mwana wake muzaliwa-pekee na malaika. (Ayubu 38:4, 7; Wakolosai 1:15) Kwa hiyo, ni wazi kwamba aliishi kwanza peke yake. Haiwezekane kwamba aliumbwa kwa sababu hakuna kitu kilikuwapo ambacho kingemuumba.

Mungu ni nani? — Uhusiano na Yeye

Katika Mtu wa Mwana, Mungu akawa mwili (Yohana 1:14). Mwana wa Mungu akawa Mwana wa Mtu na hivyo ni "daraja" kati ya Mungu na mwanadamu (Yohana 14: 6, 1 Timotheo 2: 5). Kwa njia ya Mwana tu tunaweza kuwa na msamaha wa dhambi (Waefeso 1: 7), upatanisho na Mungu (Yohana 15:15, Warumi 5:10), na wokovu wa milele (2 Timotheo 2:10). Katika Yesu Kristo "ukamilifu wote wa Uungu huishi katika hali ya mwili" (Wakolosai 2: 9). Hivyo, kwa kweli kujua Mungu ni nani, tunapaswa kufanya ni kuangalia Yesu.

Kuwapo kwetu na kuwapo kwa ulimwengu wote muzima kunahakikisha kwamba kuna Mungu wa milele. Yule aliyeumba ulimwengu wetu mukubwa, Yule aliyeweka sheria za kuuongoza, anapaswa kuwa alikuwapo sikuzote. Ni kwa sababu hiyo tu ndipo alipulizia vitu vingine vyote pumuzi ya uzima.—Ayubu 33:4.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW