Friday, July 14, 2017

BWANA EMMANUEL YOHANA NA MKEWE KATHERINE EMMANUEL WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUPIKA WAKATI WA MFUNGO WA RAMADHAN, ZANZIBAR

Image may contain: one or more people and outdoor



Kikundi cha misaada cha Kikristo kimefahamishwa kuwa, Watanzania Watatu waishio Zanzibar wamekamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa kupika chakula na kula wakati wa mfungo wa Ramadhan.
Christian Solidarity Worldwide (CSW) imesema Emmanuel Yohana, na mkewe Katherine Emmanuel na mwanamke mwingine aliye julikana kwa jina moja la Khadija, walikamatwa Juni 16, 2017 wakiwa nyumbani kwao Zanzibar wakati wanawake hao wakikaanga Samaki.
Kutokana na CSW, Wakristo hao waliambiwa kuwa, wamevunja Sheria za Nchi kwa kupika na kula mchana wakati wa mfungo wa Mwezi wa Ramadhani.
Baada ya Kanisa lao kufahamu hivyo, waliwasiliana na vitengo maalumu na kupinga tuhuma hiza, kwasababu Zanzibar si nchi ya Kiislam na Wakristo wana haki ya kula mchana.

YESU KRISTO NI MWENYEZI MUNGU

Image may contain: text


YESU KASEMA KWA MDOMO WAKE KUWA YEYE NI BWANA MUNGU, ALFA NA OMEGA NA MWENYEZI MUNGU.
Ufunuo 1:8 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Aliyeko na aliyekuwako na ata kayekuja, Mwenyezi Mungu.”
Hakika kuna raha kuu unapo mfuata Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwenyezi Mungu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

YESU KRISTO NI MUNGU MWENYE NGUVU

Image may contain: text


Isaya 9: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Biblia hakika imekamilika na haina shaka ndani yake. Imemtabiri Yesu miaka 520 KABLA YA KUJA DUNIANI.
Biblia haibabaishi wala kosea na ndio maana Mitume wake waliotumwa na Yesu mwenyewe waliweza kumtabiri mapema kabla ya kuja kwakwe.
Barikiwa sana na endelea kumfuata Yesu Kristo ambaye ni MSHAURI WA AJABU, MUNGU MWENYE NGUVU, BABA WA MILELE NA MFALME WA AMANI.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

QURAN YATHIBITISHA KUWA, YESU NI ZAIDI YA MUHAMMAD


Image may contain: one or more people, people sitting, meme and text



KINACHOMFANYA YESU ASIWE SAWA NA MUHAMMADI, NI HII AYA YA QURAN 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
فاطر (22) Faatir
Wala hawalingani walio hai na maiti. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
Hapo 👆 Tunaambiwa hawalingani walio hai na Maiti,
YESU YEYE YUPO HAI 👇
Ufunuo 1:17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
MUHAMMADI KAFA 👇
( قُلْ تَرَبَّصُوا فَإِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُتَرَبِّصِينَ )
الطور (31) At-Tur
Sema: ngojeni na mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongojea (sifi mimi peke yangu, nanyi mtakufa vilevile)
YESU YEYE AMEWEZA KUWASIKILIZISHA SAUTI WALIO MAKABURINI 👇
Yohana 11:38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne.
40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?
41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.
42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.
43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.
44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
MUHAMMAD YEYE AMEAMBIWA KUWA HAWEZI KUWASIKILIZISHA SAUTI WALIOMO MAKABURINI 👇
( وَمَا يَسْتَوِي الْأَحْيَاءُ وَلَا الْأَمْوَاتُ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُسْمِعُ مَن يَشَاءُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ )
35:22
............. Hakika Mwenyezi Mungu humsikilizisha amtakaye. Wala wewe si wa kuwasikilizisha walio makaburini.
Cha ajabu LEO waislamu wamekuwa mahodari wa kuwasomea maiti maneno ya kuwaambia
Abdallah tukiondoka hapa Watakuja malaika nao watakuuliza
"Mola wako nani?" SEMA! "mola wangu ni Allah"
"Nabii wako ni nani?" sema, "Nabii wangu ni Muhammadi "
Sasa ikiwa tu kipenzi cha Allah ameambiwa hana uwezo wa kuwasikilizisha waliomo makaburini, ninyi huo uwezo wa kumzidi mtume wenu mmeutoa wapi?
Imeletwa kwenu na: Abel Suleiman Shiliwa

YESU KRISTO ALIKUWA NA UTUKUFU WA MUNGU KABLA YA DUNIA KUUMBWA

Image may contain: text


Yohana 17:5 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
"Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe hata kabla dunia haijaumbwa."
Unapo isoma Biblia kwa context zake, lazima utakuwa Mkristo papo hapo. Lakini ukiisoma Biblia kwa akili zinginze za ajabu ajabu, utabakia mfia dini na wala huto urithi ufalme wa Mungu.
Yesu anasema:
1. Baba nipe utukufu nilio kuwa nao pamoja nawe hata kabla ya dunia kuumbwa.
2. Yesu anakiri kuwa alikuwa na UTUKUFU WA MUNGU.
3. Yesu anakiri kuwa alikuwepo kabla ya DUNIA KUUMBWA.
4. Yesu anakiri kuwa Baba yake na yeye wana UTUKUFU ULE ULE.
5. Yesu anakiri kuwa YEYE NA BABA YAKE waliishi kabla ya dunia kuumbwa.
SASA KWANINI NISIMFUATE YESU MWENYE UTUKUFU WA MUNGU NA ALIISHI HATA KABLA YA Kuubwa DUNIA?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

MASHOGA WA KIISLAM WAFUNGA NDOA

Image may contain: one or more people and closeup


Image may contain: 2 people, people smiling

Image may contain: 2 people

Jahed Choudhury, 24, alifunga ndoa ya Kishoga na mkewe Rogan mwenye miaka 19 huko Uingereza.
Choudhury aliye taka kujiua kwa sababu ya "bullying", alimpata mkewe Rogan wakati akiwa analia huko Darlaston, Uingereza.
Ndoa yao ilibarikiwa na Imamu na Shehe wa huko huko Uingereza.
Kwa habari kamili ingia hapa

ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAPONYWA

Image may contain: one or more people and text


Nabii Yoeli alitabiri kuwa, “Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la Bwana ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama Bwana alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao Bwana. (Yoeli 2:32)
Mtume Paulo alitilia mkazo unabii huu aliposema,
“Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka” (Warumi 10:12-13).
Kila anayeliitia Jina la Bwana Yesu kwa imani anaponywa na, anaokoka kwa kuwa ndani ya jina hili la Yesu Kristo mna uponyaji na wokovu kwa kila amwaminiye Yesu Kristo.
Lakini mtume Paulo anauliza swali muhimu, ambalo ni muhimu kulitafakari, anasema, “Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?” (Warumi 10:14)
Hili jambo ni kweli. Huwezi kumwita mtu usiyemwamini. Hii ina maana ya kuwa ikiwa tunataka watu waliitie jina la Yesu Kristo ili waokoke na kuponywa madhaifu yao, inatubidi tufundishe na kuhubiri juu ya Yesu na jina lake.
Ndiyo maana Bwana Yesu Kristo alimwambia anania ya kuwa Paulo “ni chombo kiteule kwangu, ALICHUKUE JINA LANGU mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.” (Matendo ya mitume 9:15).
Biblia inasema pia kuwa, “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, AKAWAHUBIRI KRISTO. Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia Kwa sauti kuu; Na watu wengi waliopooza, Na viwete, wakaponywa. Ikawa furaha kubwa katika mji ule” (Matendo 8:5-8)
Smith Wigglesworth aliyekuwa mhibiri wa inili nchini uiengereza miaka ya 1930 aliwahi kushuhudia katika mahubiri yake kuwa siku moja aliitwa kwenda kumuombea mgomjwa mmoja wa kifafaaliyekuwa amezidiwa hata kushindwa kuamka. Anasema watu wa eneno lile hata ndugu zake yule mgonjwa walikuwa wamekata tama. Waliona ndugu yao atakufa kwa ugonjwa huo, kwa hiyo ilimchukua muda Bwana Smith Wigglesworthkupata walio tayari kushirikiana naye katika kumwombea mgojwa yule.
Mwishowe alifanikiwa kuwapata na anasema walikizunguka kitanda cha yule mgonjwa na wakaanza kuliitia Jina La Yesu kwa pamoja wakisema “Yesu, Yesu, Yesu…” kwa kulirudia rudia jina hili. Baada ya kulitia jina la Yesu kwa muda hivi, anasema nguvu za Mungu zilishuka kitandani mwa yule mgonjwa, zikamtingisha mgonjwa na kitanda chake.
Yule mgonjwa akapona saa ile ile, akavaa nguo na kutoka nje. Kijiji kizima kilitaharuki na kushangaa kilipomuona mtu yule amepona. Smith Wigglesworth alipoona watu wamekusanyika hivyo wakishangaa, alichukua Biblia yake akahubiri, na watu wengi waliokoka na kutubu siku ile.
Ni muhimu ufahamu kuwa muujiza unaofanyika kwa Jina la Yesu Kristo unawavuta watu kwa Yesu Kristo, wamwamini na kumfuata. Ndiyo maana imeandikwa juu ya Yesu Kristo kuwa;
“Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya” (Yohana 2:23)
siku moja nilikuwa katika sehemu Fulani nikifundisha juu ya Jina La Yesu Kristo. Mwisho wa somo nilisema wanaotaka kujazwa na Roho Mtakatifu na wanene kwa lugha mpya pamoja na wagonjwa waje mbele. Watu wengi walikuja mbele.
Niliwaambia kuwa hatutaomba neno lolote zaidi ya kuliitia jina la Yesu kwa pamoja na kwa kulirudia rudia. Kwa pamoja tukaanza kuliitia jina la Yesu tukisema kwa sauti, “Yesu, Yesu, Yesu….”
Muda haukupia mwingi tukiwa bado tunaliitia Jina hili nikasikia toka upande wangu wa kushoto sauti ya mengi yakiporomoka. Nilijua hii ni ishara ya uwepo wa Roho Mtakatifukwani mahali tulipokuwa hakukuwa na mto wowote karibu, wala mvua ilikuw hainyeshi. Baadaye nilipowaeleza watu juu ya sauti hiyo ya maji mengi, kuna wengine waliosema kuwa pia waliisikia.
Tulipoendelea kuliitia Jina la Yesu Kristo, wagonjwa walipona, waliokuwa na mapepo walifunguliwa, na wengine walijazwa Roho mtakatifu na kuanza kuzungumza kwa lugha mpya! Ishara na miujiza mingi ilifanyika kwa Jina la Yesu Kristo!
Kumbuka Yesu Kristo alisema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya” (Marko 16:17-18).
Shalom,
Max Shimba mtuma wa Yesu Kristo.

UTHIBITISHO WA MISTARI ILIYO FUTWA KWENYE QURAN

Image may contain: one or more people
Ndugu msomaji,
Kama Quran imekamilika kama jinsi Waislam wanavyo dai, kwanini Muhammad alifuta mistari kwenye kitabu cha Allah?
Kama Quran ni maneno ya Allah, je, nani alimpa mamlaka Muhammad kufuta aya za Allah?
Je, hii Quran imekamilka au haijtakamiliak, maana sasa tunafahamu kuwa kuna aya zilifutwa na Muhammad bila ya ruhusa ya Allah.
Huu ni Msiba. Soma ushahid hapa chini.
"Baada ya hapo, Mungu alitufunulia mstari uliokuwa miongoni mwa ile iliyofutwa baadaye." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.416 uk.288.
"Anas bin Malik alisimulia: ... Walifunuliwa wale waliouawa Bi’r-Ma’una, mstari wa Kurani tuliozoea kuukariri, lakini badaye ulifutwa. Mstari wenyewe ulikuwa: ‘Wafahamishe watu wetu kuwa tumekutana na Bwana wetu. Amefurahishwa nasi na ametufurahisha.’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 19 na.69 uk.53. Tazama pia Historia ya al-Tabari juzuu ya 7 uk.156.
Kumbukumbu nyingine za mistari iliyofutwa ni Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 8 na.57 uk.45, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 184 na.299 uk.191, na Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.421 uk.293 zote zinarudia kitu hicho hicho kuhusu mstari huo huo.
Wakati fulani Muhammad aliafikiana na kusema kuwa kuhusiana na mabinti wa Allah kwenye Sura 53:19 "sala ya ya kuombea ilipaswa kutumainiwa." Muhammad alisema tunapaswa kutegemea msaada wa sanamu hizi tatu.
Wafuasi wa Muhammad walishangazwa kuwa amesema hivi. Baadaye, Muhammad alibadilisha msimamo wake na kusema kuwa Shetani alimdanganya. Mistari hii ilibatilishwa au kutolewa. Wanazuoni wa Kiislam wanaiita mistari hii "aya za Shetani." Inafurahisha kusoma maelezo ya Waislam kuhusu namna ambayo nabii wa kweli angeweza kusema hivi.
MASWALI:
1. Kwanini Allah aliruhusu Shetani kumdanganya Nabii wake?
2. Kama Muhammad aliweza kudanganywa na Shetani, je, tutaiamini vipi Quran ambayo imejaa shaka?
3. Je, kuna aya ngapi ambazo ni za Shetani kwenye Quruan, ikiwa sasa tunafahamu kuwa, Shetani na yeye alikuwa anateremsha aya zake kwa kupitia Jibril huyo huyo?
4. Kwanini Waislam wanakataa ukweli wa Mabinti wa Allah ambao Muhammad aliuukubali?
5. Kwanini Muhammad alishindwa kutofautisha maneno ya Allah na Shetani na kudhani ni mtu huyo huyo anasema?
MABINTI WA ALLAH
Uarabuni kabla ya Muhammad, kabila la Muhammad, Quaraysh, lilimwamini Mungu aitwaye Allah (au Al’Ilah) aliyekuwa na mabinti watatu walioitwa Al-Lat, Al-Uzza, na Manat.
" ‘Urwa alisema, ... kuhusiana na Ansar aliyezoea kumdhania Ihram kuwa anaabudu sanamu anayeitwa ‘Manat’ ambaye walizoea kumwabudu kwenye sehemu iliyoitwa Al-Mushallal..." Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 26 (Hija) sura ya 78 na.706 uk.413.
"Mstari huu ulifunuliwa kwa kuhusiana na Ansar aliyekuwa anamdhania Ihram kuwa sanamu Manat ambaye aliwekwa karibu na sehemu iliyoitwa Qudaid..."Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 27 (‘Hija ya Umra) sura ya 10 na.18 uk.11. Al-Lat, Al-Uzza wameelezewa Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 74 (Kitabu cha Kuomba Ruhusa ya Kuingia) sura ya 52 na.314 uk.209; juzuu ya 5 na.375 uk.259
Hakika Quran sio kitabu cha Mungu na kimejaa shaka kubwa kubwa.
Leo tumejifunza tena kuwa Quran sio kitabu cha Mungu, na zaidi ya hapo, Allah alikuwa na Mabainti watatu.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries

BIBLIA INAKATAZA USHOGA

Image may contain: 1 person, beard
Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga?
Je, Ushoga ni dhambi?
Ndugu msomaji,
Leo, watu wengi kupitia viongozi fulani wa dini hawashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja. Hata hivyo, Biblia iko wazi kuhusu jambo hilo. Inatuambia Mungu aliumba mwanamume na mwanamke na kwamba alikusudia ngono ifanywe kati ya mume na mke tu. (Mwanzo 1:27, 28; 2:24) Hivyo, haishangazi kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.—Waroma 1:26, 27.
Waislam mara nyingi wamekuwa wakisema na kuwashutumu Wakristo, eti, Ukristo unaruhusu ushoga, huku ikifahamika kuwa, hakuna aya hata moja inayo ruhusu huu uchafu.
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Neno la Mungu kama lisemavyo kwenye Biblia linasisitiza kila mara kwamba ushoga na usagaji ni dhambi (Mwanzo 19:1-13; Mambo ya Walawi 18: 22; Warumi 1:26-27; Wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wanadamu wanajinenea kuwa wenye hekima na kupumbazika. Mtume Paulo ameeleza vizuri katika Waroma1:21-27.
Mungu amewaacha wafuate akili zao. Kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao ,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.Waroma1:28
Watu wengine wanasema kwamba ushoga upo kwenye chembe za urithi. Wengine wanasema kwamba mtu hujifunza zoea hilo. Si kusudi la makala hii kujadili ikiwa zoea hilo ni la kurithiwa au ni la kujifunza. Kwa wazi, kusema kwamba ushoga unasababishwa na jambo fulani hususa haingekuwa kweli. Inaonekana kwamba kama ilivyo kwa mazoea mengine, ni vigumu kufahamu chanzo cha zoea hilo.
Hata chanzo kiwe nini, jambo muhimu ni kutambua kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.
Mungu hakuumba mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga.
Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (Warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
JE, UNAWEZA KUISHINDA TAMAA HII YA USHOGA?
Unaweza kuepukaje kujihusisha na ngono ya watu wa jinsia moja?
 Kwanza Mtupie Mungu mahangaiko yako yote kupitia sala, ukiwa na uhakika kwamba ‘anakujali wewe.’ (1 Petro 5:7; Zaburi 55:22) Mungu anaweza kukuimarisha kwa kukupa amani “yenye ubora unaozidi fikira zote.” Amani hiyo ‘itaulinda moyo wako na nguvu zako za akili’ na kukupa “nguvu zinazopita zile za kawaida” ili usitende kulingana na tamaa zisizofaa. (Wafilipi 4:7; 2 Wakorintho 4:7) Sarah, ambaye alihofia kwamba anavutiwa na watu wa jinsia zote mbili, anasema: “Kila wakati ninapopatwa na hisia hizo, mimi husali; na Yehova hunitegemeza. Nisingeweza kukabiliana na tatizo hilo bila msaada wake. Sala ndiyo msaada wangu mkubwa!”—Zaburi 94:18, 19; Waefeso 3:20.
 Pili Jaza akili yako mambo ya kiroho yenye kujenga. (Wafilipi 4:8) Soma Biblia kila siku. Usidharau uwezo wake wa kuongoza akili na moyo wako daima. (Waebrania 4:12) Kijana mmoja anayeitwa Jason anasema: “Biblia—kutia ndani maandiko kama vile 1 Wakorintho 6:9, 10; na Waefeso 5:3—imenisaidia sana. Mimi husoma maandiko haya kila wakati tamaa mbaya zinaponijia.”
 Tatu Epuka ponografia, yaani picha au habari za kingono na propaganda za ngono kati ya watu wa jinsia moja ambazo zinaweza kuchochea mawazo yasiyofaa.* (Zaburi 119:37; Wakolosai 3:5, 6) Sinema na vipindi fulani vya televisheni pia huendeleza wazo la kwamba ngono kati ya watu wa jinsia moja ni mtindo mwingine tu wa maisha. “Maoni yaliyopotoka ya ulimwengu yaliathiri sana akili yangu, na kufanya nichanganyikiwe kuhusu hisia za kuvutiwa na watu wa jinsia yangu,” anasema Anna. “Sasa mimi huepuka kabisa kitu chochote au mtu yeyote ambaye anaunga mkono ngono kati ya watu wa jinsia moja.”—Methali 13:20.
 Nne Zungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako. (Methali 23:26; 31:26; 2 Timotheo 1:1, 2; 3:10)
MAMBO YA KUFIKIRIA
 Kwa nini Mungu hushutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja?
 Utafanya nini ikiwa unakabiliana na hisia za kuvutiwa kingono na mtu wa jinsia yako?
 Unaweza kuongea na nani ikiwa unahangaishwa na hisia za kufanya ngono na mtu wa jinsia yako?
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Ushoga ni dhambi na umekatazwa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org.

YESU ATABIRI KUWA MUHAMMAD NI MTUME NA NABII WA UONGO

Image may contain: meme and text
Ndugu msomaji,
Mara nyingi Waislam wamekuwa wakisema kuwa, eti, Yesu alitabiri kuja kwa Muhammad, pale alipo sema kuhusu Roho wa Kweli, la hasha.
Nabii ni mtu gani?
Nabii ni mtu aliyeteuliwa rasmi kwa vigezo vya Kiungu ili kuleta ujumbe wa Mungu kwa wanadamu, kwa maneno mengine nabii ni msemaji wa siri za Mungu.
Nabii: Ni mtu ambaye ni msemaji wa Mungu (a mouthpiece of God) .Husimama kati ya Mungu na binadamu, mwenye jukumu la kupeleka ujumbe wa Mungu kwa watu. Nabii anapokuwa msemaji wa Mungu, huvuviwa na Roho wa Mungu, bila ujumbe wake kuwa na makosa. Nabii hujizuia kabisa utashi wake, nafsi yake, na mawazo yake, anapokuwa anatoa ujumbe wa Kinabii toka kwa Mungu. Wakati mwingine Mungu mwenyewe hutia maneno yake vinywani mwao (Kum 18:18, Yer 1:9). Nabii ni mtumishi wa Mungu (Zekaria 1:6) na mjumbe wa Mungu 2 Nyak 36:15).
Ni kweli kuwa Yesu alitabiri kuja kwa manabii, lakini kamwe hakusema lolote kuhusu utume wa Muhammad zaidi ya kukiri kuwa watu wenye sifa kama za Muhammad ni Mitume na Manabii wa Uongo.
Miongoni mwa wanadamu wanaoitwa nabii na mtume, ni mtu aitwaye Muhammad s.a.w ibn Abdullah, ibn Abdu Mutallib, ambaye ni mtume na nabii katika dini ya Kiislamu.
Pengine wewe msomaji wa somo hili unaweza kushangaa ni kwa vipi sisi ambao si Waislamu bali Wakristo tuanze kuhoji habari za Muhammad s.a.w mtume wa Waislamu? Jibu lake ni kwamba kitabu cha Qur’an kinachotumiwa na Waislamu kimetutaja sisi Wakristo mara 62 kikitutaka kuupokea, kuuamini na hatimaye kuufuata ujumbe wa Muhammad s.a.w kwa madai ya kuwa yeye ni nabii na mtume wa mwisho hata kwetu Wakristo, aliyetumwa na Mungu.
YESU ATABIRI KUHUSU MTUME WA UONGO AMBAYE NI MUHAMMAD
Tahadhari ya Bwana Yesu: Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani alituonya kuhusu kuwatambua manabii na mitume wa uongo kabla Muhammad hajazaliwa (amezaliwa 570 B.K), wala kabla Uislamu haujaanzishwa na Muhammad mwaka 610 B.K, wala kabla ya kuwepo kitabu kinachoitwa Qur’an. Tunayasoma maonyo hayo ya Bwana Yesu katika
Mathayo 7:15-16 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali, mtawatambua kwa matunda yao”.
Mathayo 24:11-13 “Na manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi na kwasababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka”.
Yesu katika Ufunuo alisema kuwa watakuja Manabii na Mitume wa Uongo.
Ufunuo 2:2 Nayajua matendo yako na taabu yako, subira yako, na kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume nao sio, ukawaona kuwa waongo.
Je, Muhammad ni nabii wa Mungu?
Je, Muhammad anasifa za nabii wa Mungu?
Hebu endelea na somo hapa chini:
JINSI YA KUMFAHAMU NABII WA UONGO:
Kwa hivyo Muhammad ni miongoni mwa hao Mitume ambao ni waongo, ambao sisi kama Wakristo yatupasa kuutambua uwepo wao hapa Duniani, kwani tumeshapewa angalizo la kuwatambua hawa wanaojiita Mitume na Manabii, hali ya kuwa ni waongo
1 Yohana 4:1-3
1 Wapenzi msiamni kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu: kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; KILA ROHO IKIRIYO KWAMBA YESU KRISTO AMEKUJA KATIKA MWILI, YATOKANA NA MUNGU, 3 Na Kila roho isiyomkiri Yesu, haitokani na Mungu. Na HII NDIO ROHO YA MPINGA KRISTO ambayo mliskia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Vigezo hivi tulivyopewa na Biblia Takatifu kuwajua manabii na mitume wa uongo ni muhimu sana tukavichunguza katika maisha ya wale wanaoitwa nabii au mtume
Kila nabii na mtume ambaye yeye hakubali kuwa Kristo alikuja katika mwili, kwa maana kuwa Mungu alidhihirishwa katika mwili, hiyo roho yaani huyo nabii si ambaye anatokana na Mungu, huyo ni Nabii anaetokana na shetani, kwa mujibu ya maandiko Matakatifu, Kristo alidhirishwa katika mwili.
1 Timotheo 3:16 Na Bila shaka siri ya utauwa ni kuu, Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulikana kuwa na haki katika roho,
Akaonekana na Malaika, akahubiriwa katika mataifa. akaaminiwa katika ulimwengu, akachukuliwa juu katika utukufu,
SASA KAMA MNATAKA KUAMINI KUWA KWELI Muhammad ni nabii na mtume wa uongo, waulizeni wafuasi wake,
SWALI LA KUPIMA UNABII WA MUHAMMAD:
Je! Kwa mujibu wa uislamu, Wanakubali kuwa Mungu alikuja kwa njia ya mwili wa kibinadamu na kuonekana?
Wakikubali, basi tambueni kuwa Muhammad ni mtume wa kweli, na wakikataa basi mjue kuwa Muhammad ni nabii na mtume wa Uongo.
SIFA ZA NABII WA KWELI:
Nabii wa kweli hupata ufunuo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu:- 2Petro 1:20-21.” Mkijua neno hili kwanza,ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu;bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.
LAKINI MUHAMMAD YEYE ALIPATA UNABII KWA NJIA HII, SOMA
Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Je, wapi katika Injili au Taurat au Zaburi tunasoma kuwa Manabii na Mitume katika Biblia walipata kwa njia ya homa na kukiri kuchezewa na mashetani kama Muhammad wa kwenye Quran?
1 Petro1:10-11 “Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta tafuta na kuchunguza chunguza ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi na wakati wa namna gani ulioonywa NA ROHO WA KRISTO ALIYEKUWA NDANI YAO ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaokuwako baada ya hayo…..” (maneno ya msisitizo kwa herufi kubwa ni ya mwandishi)
Ufunuo 19:10 “Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndiyo roho ya unabii”
Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza mitume na manabii. Katika kitabu cha Ufunuo 2:1-2 “ Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao siyo ukawaona kuwa waongo”
Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia katika kundi la manabii na mitume wa uongo.
Mungu awabarikisana, na tuendelee kujifunza kweli, na kweli itatuweka huru.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
For Max Shimba Ministries Org.

An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance

  Title: An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance Au...

TRENDING NOW