Monday, December 14, 2015

YESU KRISTO AMEKUPA UTAJIRI

Watu wengu wanafikiri kuwa, Mungu aliwaumba ili wawe watu wa kawaida tu, la hasha, Mungu amekuumba wewe ukiwa Tajiri. Ukisoma kuhusu Adam katika Kitabu cha Mwanzo, utaona kuwa, Mungu alimuumba Adam na Hawa baada ya kuumba dunia na kila kitu. Baada ya Adam na Hawa kuubwa, walikabidhiwa kila kitu kilichopo hapa duniani. Huo ni Utajiri mkubwa sana. Soma. Mwanzo 1: 28 Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.” 29Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. 30Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo.
UNAONA: Mungu alimpa kila kitu Adam na Mkewe Hawa. KUMBE ADAMA NA HAWA WALIKUWA MATAJIRI. Je, wewe unasubiri na kungoja nini? Muamuru Shetani akurudishie mali zako zote kwa Jina la Yesu.
Mithali 3:16; (Yesu kristo Mnazareti) ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na Heshima katika mkono wake wa kushoto.
MAANA YA TAJIRI:
Tajiri ni yule mtu mwenye mali nyingi na mwenye moyo wa kusaidia wenye uhitaji na anayefaidi mali zake kwa amani kuu na sio tu kumiliki na kutawala mali nyingi. Huyo ndiye Tajiri katika Bwana anayesomeka pajini mwa uso wake hata pasipo kujua utajiri anaomiliki. Lakini ile kuwa na roho mtakatifu ni utajiri unaothihirika hadi mwilini. Kama ilivyokuwa kwa Mfalme Sulemani (2 Mambo ya Nyakati 1:15) inasema; "Mfalme Sulemani alifanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe ule wingi wake huko Yerusalemu na mierezi akafanya kuwa kama mikuyu iliyoko shefela kwa kuwa mingi". Hii yote inatokana na kuwa na Bwana Yesu wa Nazareti ya kwamba ni utajiri utajirishao wengi na sio tu muhusika yaani ni utajiri usio binafsi na ndiyo utajiri wa kweli unaomaanishwa.
Biblia katika Waefeso 3:8-11 pia inasema kwa habari ya Mtume Paulo; “Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote, kusudi, sasa kwa njia ya kanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguni wapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi. Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu."
“Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU, NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)

Wednesday, December 9, 2015

SHETANI LA ULAFI KATIKA UISLAMU

Ndugu msomaji,
Leo ningependa tujifunze kidogo kuhusu roho ya ulafi ambayo inawasumbuwa ndugu ztu katika Adam. Hebu tusome Biblia kama ushahidi.
Wafilipi 3: 19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.
Walafi wao wamesha amua kuabudu chakula na mungu wao ni matumbo yao. Mtu mlafi akiona chakula, basi yeye hula kwa haraka haraka na kujaza tumbo lake mpaka anavimbiwa. Ulafi ni dhambi kama ilivyo sema kwevye Wafilipi hapo juu. Ulafi ni kuabudu tumbo.
Mithali 23: 20 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Watu wanao kula nyama kwa Pupa mpaka wanavimbiwa na kushindwa kutembea, hao wana roho chafu ya ulafi, na ni dhambi kuabudu chakula au kuwa mtumwa wa chakula au mtumwa wa tumbo lako.
Kuna dini fulani wao wanapo dai kuwa wanafunga siku thelasini, huwa wanabadilisha masaa ya kula na kula usiku kucha mpaka wanavimbiwa matumbo yao. Hiyo dini ni dini ya walafi na wanatenda dhambi, huku wao wakifikiria kuwa wanafunga kwa Allah wao.
Wagalatia 5: 16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
26 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.
Kama Neno la Mungu linavyo sema kuwa, tusiwe na tamaa za mwili, maana mwili wetu ni hekalu la Mungu. Ikimaanisha kuwa Roho Mtakatifu anaishi ndani ya mwili wetu, na hivyo, ni vyema tuutunze. Ulafu ni roho kutoka kwa Shetani na kula mpaka kuvimbiwa ni dhambi na ni kuabudu chakula na matumbo yetu.
1 Wakorintho 6: 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Basi mpendwa, usiongozwe na tamaa za mwili bali ongozwa na Roho aliye ndani yako.
Leo tumejikumbusha kuwa, Ulafi ni roho kutoka kwa Shetani na ni dhambi.
1. Kwanini Waislam wanakula usku kucha wakati wa mfungo wa Ramadhani?
2. Kwanini Allah amewaruhusu kula usiku kucha na kuwakalisha na njaa mchana kucha, je huko si kubadilisha masaa ya kula?
3. Mbona Yesu wa Biblia alipo funga, yeye hakula Daku?
Hakika kubadilisha masaa ya kula na kula usiku kucha ni ulafi, na ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu.
Max Shimba Ministries

JINSI YA KUENENDA KWA ROHO

Wagalatia 5:16 “Basi, nasema enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili”Hapa tunaona Paulo anawaagiza wagalatia kwamba waenende kwa Roho na lengo kubwa ni ili wasizitimize tama za mwili.
Lengo la waraka huu mfupi ni kukueleza namna unavyoweza kuenenda kwa Roho, na hii ni kwa sababu Yesu mwenyewe alisema ni heri mimi niondokeili aje mwingine msaidizi huyo Roho wa kweli. Na 
kama tunaye Roho mtakatifu ni lazima tujue ni kwa namna gani tutaenenda kwa roho?Neno la Mungu/ Mungu anaposema, enendeni kwa Roho ana maana hii:-
(a) Kila unalolizungumza, lizungumze chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Yohana 12:49-50. Yesu mwenyewe hakunena neno lolote kwa shauri lake, bali kila ambalo baba alimwambia kupitia Roho mtakatifu. Hivyo hata wewe
kama unafundisha, unahubiri, unaonya hakikisha unachokisema Roho mtakatifu ndiye amekuruhusu ukiseme. Usiseme kitu cha kwako halafu ukasema Roho mtakatifu amekuongoza.
(b) Tii uongozi wake .Yohana 16:13 “ lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli; atawaongoza awatie kwenye kweli yote…….” Moja ya kazi za Roho mtakatifu ni kutuongoza na kututia kwenye kweli yote. Hivyo kuenenda kwa Roho maana yake ni kutii katika yale anayotuambia maana hata yeye haneni kwa ridhaa yake isipokuwa yale anayoyasikia kutoka kwa Mungu.

SOMO: MAOMBI YA CHUMVI YA KUVUNJA LAANA NA MAAGANO YA UKOO


Jinsi ya kuvunja Roho za laana na maagano kwenye ukoo wenu, maana watu wengi wameshindwa kufikia malengo na hata kukata tamaa kwa sababu ya maagano na laana za kabila zao, leo hii Mungu anakwenda kukuvusha, chumvi uliyoishika enaenda kukugeuza na kuangalia familia yako wapi imetoka na wapi inaelekea.
Habari ya ukoo ni sawa na lugha ya kabila bali siyo lugha ya Taifa, Mungu hakuumba msomi aliumba kabila ndio maana hata baadhi ya mapepo hayawezi kutoka mpaka ya sikie lugha ya kabila la kwenu.usiangalie wapi umetoka maana Mungu wetu hahukumu umefanya dhambi ngapi, bali wewe upo kwenye nafasi gani?
UFUNUO WA YOHANA 7:1 ‘’Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wowote.’’
Maandiko yanasema Malaika walisimama pande nne wakizuia upepo usivume kwa ajili ya makabila kumi na mbili na kila pembe alisimama malaika mmoja.
kwa hiyo uwe na uhakika kwenye ukoo wa kwenu, hiyo nafasi ambayo alitakiwa asimame Malaika lakini sasa yamesimama mapepo ambayo yamezuia pande nne za ukoo wenu kusitokee upenyo wa maendeleo ya fedha na uchumi.
Kwa maana nyingine kusimamishwa kwa ukoo wa kwenu halafu tunashuhudia mnazika watu kuanzi miaka themanini na kuendelea na naghafla mkaanza kuzika kuzika chini ya kiwango hicho mjue kuna Roho nyingine zimewaingilia kati na zinauwa mmoja baada ya mwingine, na hata wale walioendelea bado hawajakufa kiroho lakini fedha zao zinaendelea kutumika na wale wanaendelea kifedha na watoto wao wamekufa, jua kuna matatizo kwenye familia nzima na unajaribu kutoa sadaka , kwenda kwenye maombi lakini tatizo bado linaendelea.
Mwanangu maombi ya siku moja hayawezi kubadilisha jahazi lililokuwa limezama, lazima ujipange sawasawa na kanuni ya Bwana inayosema natafuta mtu atakaekuwa mlango wa mimi kupita ili nipige na nisizuru ukoo iliyo baki nyuma.
Tunapo ongelea pepo haimaanishi ukoo wenu umefungwa bali kuna roho ambayo ni mlango unaokaribisha mapepo,maana kama roho ya Yuda ilijiunganisha na shina la Daudi na shina la Daudi likajiunganisha na Yesu, Uwenauhakika roho ya nyumbani kwenu itajiunganisha na mapepo.
UFUNUO 7,9,10 “Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila Taifa, na kabila,na jamaa na lugha wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za mwana –kondoo,wamevikwa mavazi meupe,wana matawi ya mitende mikononi mwao. wakilia kwa sauti wakisema Wokovu una Mungu wetu aketiye katika keti cha enzi, na mwana kondoo.’’
Mungu anayasikia maombi yako usifikili wingi wa dhambi zako, maandiko yana sema, Adamu pamoja nakufanya dhambi lakini alimsikia Mungu alipo mwita Adamu uko wapi? Mungu hajishuhulishi na dhambi ulizo fanya bali atakuuliza nafasi yako ipo wapi? aliyokuweka kama Habakuki , maana atasimama katika zamu yake na atamuona Bwana atakacho mjibu.
UFUNUO 5:2 “Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu,Ni nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi,wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu,wala kukitazama.’’
Maandiko ya natuambia kisha nikamuona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma,kimetiwa muhuri saba.
Kwa niaba ya F.J Kilawa
Max Shimba Ministries

MAOMBI YA KUPINGA MAGONJWA, VIFO, AJALI NA UHARIBIFU KATIKA MAISHA YAKO

1. Baba, katika jina la Yesu, naangusha kila mbinu za kishetani zinazozuia mafanikio yangu, katika jina la Yesu.
2. Nakataa na kupinga magonjwa ya kila aina katika nyumba yangu na familia yangu, kwa jina la Yesu.
3. Imeandikwa katika Zekaria 2:8 ya kwamba “Yeye anayenigusa mimi anagusa mboni ya jicho la Mungu”, hivyo, ninalisimamia Neno hili na kupinga kila nguvu inayosababisha magonjwa na upotevu wa fedha zangu katika jina la Yesu.
4. Nasimama kinyume na ajali na vifo katika familia yangu na ndugu zangu katika jina la Yesu.
5. Nawafunika watu wa familia yangu, kijiji changu na nje ya kijiji kwa damu ya Yesu. Ninawalinda na kuwaongoza kila mmoja kwa jina la Yesu.
6. Ninaamuru kila kinachoharibu mtaji na biashara yangu kufa mara moja katika jina la Yesu.
7. Ninaificha fedha yangu yote katika damu ya Yesu na kamwe adui hawezi kuigusa.
8. Baba, katika jina la Yesu, nasimama katika Neno kama mtoto wa Mungu niliyeketishwa mahali pa juu pamoja na Kristo, na ninatangaza kuwa mikutano ya kipepo juu ya maisha yangu na fedha yangu haitafanikiwa, katika jina la Yesu.
9. Namfunga kila anayeharibu fedha yangu nyumbani na sehemu yangu ya kazi katika jina la Yesu.
10. Wewe pepo uliyetumwa kuharibu biashara na fedha zangu, ninakufunga na kukutupa kwenye shimo la giza katika jina la Yesu.
11. Ninaamuru moto wa Roho Mtakatifu kumlamba kila mmoja aliyesimama kinyume na biashara na mafanikio yangu katika jina la Yesu.
12. Ewe mlima uharibio, ninakuangusha na nianaamuru usambaratike, katika jina la Yesu. 13. Ninaificha biashara, ofisi, fedha na miradi yangu yote katika damu ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. Amen.
14. Bwana, ninaomba upendeleo wako katika maisha yangu ili niweze kufanikiwa.
15. Upendeleo wako unizunguke kadiri ya Neno lako, katika jina la Yesu.
16. Bwana, naomba kuunganishwa na watu watakaonisaidia kufikia ndoto zangu kwa jina la Yesu.
17. Oh, Bwana, naomba ufanye njia kwa ajili yangu hata pale pasipo na njia katika jina la Yesu.
18. Baba, naomba niunganishe na mtu ambaye atakuwa msaada mkubwa katika kuyafikia mafanikio yangu katika jina la Yesu. 19. Baba ninaamini ya kwamba kila ninapokanyaga ninapamiliki sawasawa na na Neno lako, hivyo naomba univike vazi lako la upendeleo katika jina la Yesu.
20. Asante Bwana Yesu kwa kuwa umefanya sawasawa na nilivyokuomba katika jina la Yesu.
Amen.

MAOMBI YA HATARI


UTANGULIZI
Maombi ya hatari ndiyo ni sahihi. Kichwa cha habari kinaogopesha katika mtazamo wa kwanza, lakini maelezo yake ni matamu, naamini matamu kuliko asali. Huwezi kueeleza kwa undani maana ya maombi ya hatari mpaka utakapokua unafanya. Haya ni maombi ambayo ulimwengu mzima umekuwa ukiyatamani, kila mtoto wa Mungu anapaswa kuomba haya ili kuweza kumweka shetani pamoja na mapepo yake kule wanakostahili.
Unapokuwa umeomba maombi haya katika Roho na kweli, utakuwa unamwambia shetani 'IMEKWISHA'' mimi niko nje ya kambi yako. Hebu turudi kwenye jarada hili la kitabu hiki tuone kwanza nyundo nzito na yenye hatari inavyoharibu kijibanda kwa nguvu isiyo kifani na utaweza kuona kufuli (kitasa) na mlango wa kijibanda vinavunjwa vipande vipande kwa ile nyundo. Ukitazama kwa uangalifu zaidi, utamwona mtu akikimbia kutoka kwenye kibanda akiwa huru kabisa.
Hivi ndivyo maombi haya ya hatari yalivyomweka mtu huru kutoka kwenye vifungo vya shetani na mapepo yake. Maombi ya hatari ni nguvu na uwezo mkuu wa Roho Mtakatifu unaona hivi na kuangamiza nguvu za giza zilizopo dhidi yako. Maombi haya ukiyatumia, utakuwa huru kutokana na vigongo na mashambulizi ya kishetani yanayo kuzunguka. Kamwe usinisifu mimi, baada ya maombi haya, bali mpe Mungu, Yesu na Roho Mtakatifu utukufu wote, ambao ndiyo walioniwezesha kuyafahamu maombi haya.
Kabla ya maombi yako hayajawa na hatari unapaswa kwa mtu wa hatari unapokuwa mtu wa hatari ndipo utakapoweza kuomba maombi ya haraka na utakapoomba maombi ya hatari UPAKO WA HATARI uatanza kutiririka, na mambo ya hatari yataanza kufanyika katika ulimwengu huu na katika ulimwengu wa Roho.
MAPAMBANO YA KIHEKIMA
Kama tutajua nafasi yako ndani ya Kristo, ndipo utakapojua haki yako. Ukijua haki yako unauwezo wa kutumia haki yako, shetani na mapepo yake watakimbia.
Maombi ya hatari yanashambulia kiini cha matatizo yako. Hii ni njia nzuri ya kufanya nashambulizi. Unapokishinda kiini cha matatizo, sehemu nyingine ya hilo tatizo huwa inakufa. Unapotaka kuua mmea, unachotakiwa ni kung'oa shina lake na mti huo utakufa. Ikiwa tu utakata matawi, bila kung'oa shina hilo shina unaweza kuchipua tena. Hivyo inachotakiwa ni kuikata mizizi na mmea utakufa kabisa.
Maombi ya hatari ni aina ya maombi ambayo yanamlazimisha shetani na majeshi yake kuhama kwa nguvu na Roho Mtakatifu, hata kwama hawataki kuhama. Maombi haya yanaangamiza nguvu zote za shetani kuanzia ngazi za chini hadi ngazi za juu. Maombi ya hatari kama yanavyoitwa humfanya mtu wa Mungu kuwa huru kutokana na kutawaliwa na nguvu za shetani. Maombi haya huleta ukombozi kwa kila mtu wa Mungu
Maombi ya hatari huondoa na kuharibu kila laana maagano na makubaliano dhidi ya mtu wa Mungu. Tukitumia ujasiri tunaopata kwa njia ya Roho Mtakatifu, tunaweza kujiletea ukombozi sisi wenyewe tuapoomba maombi haya.
Maombi ya hatari hayampi shetani nafasi ya kuaingilia maisha yetu au maendeleo yetu. Maombi ya hatari ni maombi ya nguvu yanayopaswa kuombwa na watu wa Mungu wenye nguvu. Maombi ya hatari hutangaza VITA dhidi ya nguvu za giza zinakuzunguka na ufalme wa shetani mwenyewe.
Maombi haya yanakufanya kuwa zaidi ya mshindi; kila mtu wa Mungu anahitaji maombi haya ili awe mshindi wakati unaposhindwa kuishi maisha ya ushindi.
Fellowship, vikundi bya Kikristo, Makanisa na huduma zinahitaji aina hii ya maombi kwa ajili ya ushindi na kuwafanya waumini wake kukombolewa kwa jina la Yesu.
i. Biblia inasema utakuwa kiumbe kipya kiroho (2 Wakoritho 5:17)
ii. Ni lazima uwasamehe wote wakikukosea
Kama ulivyokwesha kujulishwa maombi ya hatari ni nini? Inakufahamisha juu ya maombi haya kwa uangalifu, maombi haya siyo ya mkato bali ni maombi yenye nguvu, kwa sababu ufalme wa Mungu hutekwa na wenye nguvu (MATHAYO 11: 12)
JINSI YA KUOMBA MAOMBI HAYA

VUNJA VIFUNGO, MAAGANO, NA MIKATABA YA KISHETANI MAISHANI MWAKO

Kutoka 23:32 ''Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.''
Agano ni kitu kikubwa sana, Agana la kipepo ni mapatano ya kishetani, ni mikataba ya kishetani na MUNGU hataki tuingie agano lolote na shetani wala mawakala wake.
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaidia familia yako.
Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.
Isaya 57:8 '' Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona. ''
-Maagano mabaya ni jambo baya sana ndugu. kama zamani uliwahi kuingia maagano ya kishetani basi kimbilia kanisani ukaombewe maana maagano ni mkataba na ukiingia mkataba na shetani mwishowe anaweza kukuangamiza tu na uzima wa milele ukaukosa.
Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.
Aliyahidhirisha haya kwenye kitabu cha nabii Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana Mungu i juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.
Vunja uhusiano wako na hiyo miungu pamoja na kazi zake na agano lililofanyika kati ya familia au ukoo wako na hiyo miungu. Kila unapotamka mwisho wake sema kwa sababu nimesamehewa. Ipo mistari mingi ya kuvunja maagano lakini mimi nitakupa kifungu hiki cha mstari katika kuvunja maagano na mapoozo ya aina yoyote. “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta” Isaya 10:27

JINSI YA KUTOA PEPO WABAYA/CHAFU

Maana ya neno pepo linamaanisha, pepo mbaya, shetani, mwovu, mharibifu na mwangamizi. Hao ni malaika waliomuasi Mungu wakatupwa duniani. “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na Yule joka (Shetani), Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, Yule wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Ufu 12:7-9.
1. Ili kutoa pepo, kuna mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa:
Ni lazima uwe na nguvu za Roho Mtakatifu.Tunaweza kujifunza kwa Yesu alivyoweza kutoa pepo kwa uwezo na nguvu za Roho. Imeandikwa, “…..awaaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36.
2. Kutoa pepo kwa jina la Yesu. Aliye na amri na mamlaka ya kutoa pepo ni mkristo ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo……” Math 16:17. Wale ambao bado hawajamwamini Yesu na kuokoka, Si vyema kujaribu kutoa Pepo kwa sababu hatatoka, vile vile wanaweza kushambuliwa na hao walio na Pepo, kama wale wana wa Skewa, Kuhani Mkuu.
“.....wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nakuapisha kwa Yesu, Yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, Kuhani Mkuu, walifanya hivyo..... na yule mtu aliye pagawa na pepo wachafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.” Mdo 19:13-16.

Saturday, November 28, 2015

NAMNA YA KUMWITA,KWENDA NA KUMUOMBA MUNGU ILI AKUSIKILIZE.

Yeremia 29:12 “Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza”.

Utangulizi 

Watu wengi wamekuwa wakitamani maombi wanayoyapeleka mbele za Mungukusikilizwa.Watu wanaomba kila aina ya maombi inayowezakana maadam Mungu asikie na kuwaokoa kutoka kwenye shida waliyonayo au kuwapa haja za mioyo sawasawa na uhitaji wao.

Wapo wanaoomba na wanaona majibu yao yanajibiwa lakini pia lipo kundi jingine kubwa ambalo wanaona kama vile Mungu amenyamaza, amewaacha, hawasikii, au wanajiona kama vile Mungu amewakataa na kuziona ahadi za Mungu kwamba si za kweli na mbaya zaidi wengine wamefika mahali pa kumwacha Mungu kwa sababu ya kushindwa kuvumilia majibu kutoka kwa Mungu na hivyo kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo yao. 

Wapo walioomba kuhusu watoto, ndoa zao, afya zao,ajira,biashara,Elimu zao nk. Walipoona katika fahamu zao Mungu hajibu basi wakaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji,wachawi na kwa miungu mingine kutafuta msaada huko.

Sasa ili Mungu aweze kusikiliza au kujibu maombi yako huenda kuna mambo mengi ya msingi ambayo mwombaji anapaswa kuyajua na kuyatendeakazi. Sasa baada ya kuona maombi mengi ninayoomba na pia ambayo wana wa Mungu pia wanaomba hayajibiwi ili nilazimu nimuombe Mungu anifundishe vizuri kuhusu hili neno.

Hivyo hayo ninayoenda kukushirikisha ni sehemu ya yale ambayo Mungu amekua akifundisha naamini na wewe yatakusaidia maana nimeona yakinisaidia binafsi pamoja na wale ambao Mungu amenipa kuwafundisha kwa njia nyingine.

Lengo la ujumbe huu ni kukupa maarifa yatakayokusaidia kuomba maombi ambayo wewe mwenyewe.Pindi unapoomba utakua na uhakika Mungu anakusikiliza kwa wakati  huo.Zaidi ujumbe huu umekusudia kukufundisha namna unavyoweza ukapeleka maombi mbele za Mungu.

Siku moja nikiwa chuoni mwaka wa kwanza majira ya tisa jioni,nilikua nikipandisha ngazi kuelekea chumbani kwangu ambacho kilikua ghorofa ya tatu juu kabisa.Wakati naanza kupandisha zile ngazi nikasikia mtu ananiuliza ndani yangu 

Je hivi Mungu huwa anaitwaje?Anaendwaje?Anatafutajwe?Anakaribiwaje? Nilipofika chumbani nikaanza kutafakari haya maswali na baadae ndipo nikapata hii mistari katika Yeremia 29:12-13 inayosema “Nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza 13 nanyi mtanifuata na kuniona,mtakaponifuata kwa moyo wenu wote.”Baada ya kuisoma vizuri ndio nikagundua karibu maswali yale yote yalitoka hapa.

Mungu anasema nanyi mtaniita, sasa na mimi nikuulize swali, hivi umeshawahi kujiuliza Mungu tunamwitajemwitaje? Tunamwendeaje? Na tunamtafutaje. Usiishie kusema Mungu ameseam nikaribieni nami nitawakaribia, umneshawahi kujiuliza anaposema tumkaribie yeye yuko wapi? Na pia tunamkaribia kwa namna gani? Sasa hayo ndio maswali yaliokuwa yakinijia.

Picha ambayo Mungu alitaka niipate kwenye zile ngazi ni hii, nifikirie kwamba kile chumba kule juu ndiko aliko yeye yaani mbinguni. Sasa baada ya kufikiria hivyo ndio niwaze na nijiulize amesema nimuite nimwendee nimtafute n.k Sasa hivi ndio ninamwitaje, ninamwendeaje na ninamtafutaje? Nilipozidi kutafakari hiyo mistari roho mtakatifu akanifundisha yafuatayo:
kwanza alinionyesha makosa matatu ambayo watoto wake mara nyingi tumekuwa tukiyafanya wakati wa maombi. Na ningependa na wewe uyajue kwa maana itakusaidia ili bado unayafanya basi usiyafanye tena.


Kosa la kwanza, 
Kuomba kinyume au nje ya mapenzi ya Mungu.
1 Yohana 5:14 inasema Na huu ndio ujasiri tulionao kwake ,ya kuwa,tukiomba kitu sawa na mapenzi yake atusikia” Moja ya tafsiri za kiingereza inasema “We are certain that God will hear our prayers when we ask for what pleases him” Kosa kubwa ambalo tumekuwa tukilifanya mara nyingi ni kuomba vitu au mambo ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.

Anaposema sawasawa na mapenzi ya Mungu maana yake ni lazima ujue kwanza nini ni mtazamo au mawazo ya Mungu juu ya hilo unalotaka kuliombea. Maombi ni kuzungumza au kusemezana na Mungu kwa Kumwambia yale ambayo amesema kwenye neno lake kuhusu haja zako wewe.

Kwa lugha nyingine usiombe kitu ambacho hujui nini Mawazo ya Mungu juu ya hicho kitu. Mawazo ya Mungu juu ya kila haja ujyonayo yako ndani ya Neno lake .Hivyo ni lazima Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yako ili unapoomba uombe kulingana na ahadi zake na pia sawa na kile alichokisema.

Zaidi pia wengi wanapotaka kuomba huenda kuhusu ndoa,kanisa,Ajira,watoto ,biashara nk huwa wanomba kimazaoea. Maana yake ni hii wengi wamezoea ninpoombea ndoa nitaombea amani,upendo ,furaha nk Sasa sina maana hayo maombi hayafai ila ninachotaka ukipate ni hiki hoja unazozipeleka mbinguni hakikisha umefunuliwa na Mungumwenyewe.Maana yake Mungu ndiye akupe mambo ya kuombea kuhusu nchi ,ndoa,biashara yako nk.


Kosa la pili, 
Kukosa utulivu na uskivu wa rohoni wakati wa maombi na baada ya maombi.
Sikiliza Mungu anayo mambo mengi ya kukuambia wewe kuliko yaje wewe uliyonayo wewe kumweleza yeye. Chungu hakiwezi kumwambia mfinyanzi kwamba ulinumba kwa kazi hii tu, bali mfmyazi ndiye mwenye mengi kuhusu kile chungu. 

Ndio maana Yesu anasema si ninyi mlionichagua mimi bali ni mimi niliyewachagua njnyi (Yohana 15:16),Sasa watu wengi sana wana bidii nzuri ya maombi wanaweza wakakaa hata masaa matatu mfululizo na hata zaidi wanamuomba Mungu tu.

Katika mda huu wote wao ndio wanaojieleza na mara wanapomaliza ni kusema Ameni na kuondoka.Hii ni picha ya mtoto anayekuja kwako kama mzazi anasema baba/mama naomba hela ya daftari, nauli na ya kula shuleni, pia naomba uninunulie suruali nk. Sasa kabla wewe hujamjibu yeye ameshafungua mlango na kuondoka.sasa kibiblia ndiko kunaitwa kukosa utulivu na usikivu wa rohoni mbele za Mungu.


Mara zote unapoomba jifunze kuwa na wakati wa kutulia kusikiliza Mungu naye anasema nini.Kwenye utulivu ndiko Mungu anakosema sio kwenye kelele maana anjua hamwezi kusikilizana.Soma Isamwel 3:1-10 utaelewa ninachokisema hapa.Mungu alisema na Samweli alipotulia.


Kosa la tatu, 
Kumuomba Mungu wakati tayari umeshajitafutiajibu la shida uliyo nayo.

Hili ni kosa jingine kubwa ambalo wana wa Mungu wamekuwa wakilifanya. Wengi wana mahitaji mbalimbali.Wapo watu wengi ambao kweli wanaomba kwa kumaanisha mbele za Mungu na wengine hata kufunga kwa masaa mengi lakini tatizo lao katika fahamu zao wameshafanya uamuzi wa nini watafanya baada ya maombi yao.sasa hata Mungu akikushirikisha mawazo yake si rahisi ukamwelewa kwa sababu tayari kwenye nafsi na ufahamu wako kuna jibu na Biblia inasema Aonavyo mtu katika nafsi yake ndivyo alivyo.

Sambamba na hilo, kosa linalofanana na hili ni wale watu wanaomwomba Mungu afanye kama vile wao waonavyo kataka nafsi zao. Yaani wanamtaka Mungu akubaliane na Mawazo yao na njia zao juu ya shida au haja walizo nazo wao wenyewe.

Na jambo hili tunalielewa vizuri tunaposoma katika Kitabu cha Luka 9:12 -17 .Habari za wanafunzi wa Yesu pindi njaa ilipokuwa ikiwauma watu wakati Yesu anaendelea na mkutano. Wao walimwambia Bwana waage watu wakajijinunulie chakula vijijini na mashambani, wao walidhani hili ndilo jibu la njaa ya watu. Hawakufikiri kwamba sio wote wenye pesa za kununua chakula, Kuwaaga watu kungemaanisha Yesu aache kufundisha nk. Sasa jibu la njaa ya wale watu halikuwa kama wanafunzi walivyowaza na walivyotaka bali jibu lilikuwa kwa Yesu kufanya muujiza wa kubariki mikate mitano na samaki wawili vitosheleze watu wote 5000.

Sasa baada ya kuwa tumeona hayo makosa makubwa matatu tuangalie Mungu anaposema nanyi mtaniita,mtakwenda na kuniomba,nami nitawasikiliza ana maana gani?.

Katika mstari huu kuna mambo makubwa matatu yamezungumziwa.


Moja ni MTANIITA,mbiIi MTAKWENDA NA KUNIOMBA, tatu ni NAMI NITAWA

SIKILIZA.
Jambo la kwanza ni ,
Mtaniita.
Ukisoma kitabu cha Yeremia 33:3 anasema “Niite,nami nitakuitikia ,nami nitakuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua. Mungu ansema utakapomwita yeye atafanya mambo mawili.Moja atakuitikia na mbili atakuoyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua.

Maana yake ni hii, kukuonyesha mambo makubwa,magumu usiyoyajua ni kukufunulia mambo ambayo ulikuwa huyajui katika lile ulilomuita.Hivyo basi kumuita Mungu ni kumuomba au Kumtaka Mungu akufunulie mambo makubwa na magumu usiyoyajua kuhusu shida au hitaji au haja uliyonayo mbele zake. Mfano unamuita Mungu akufunulie ndoa yako jinsi ilivyo, nini kinaendelea usichokijua, nini ukiombee, nini hakijakaa sawasawa kwenye hiyo ndoa k.
 Hivyo basi unapotaka kuomba juu ya jambo lolote lile ni vizuri kwanza ukamuita Mungu juu ya hilo jambo.Maana yake muombe Mungu akupe picha kamili ya hilo unalotaka kuliombea,akufunulie jinsi lilivyo ili ujue uanzie wapi kuomba.,kama ni ndoa,nchi,mke au mme mtarajiwa,Huduma yako nk.


Jambo la pili 
Mtakwenda na kuniomba.
Sasa baada ya kuwa umemuita Mungu kinachofuata ni kwenda na kumuomba Mungu. Anaposema mtakweda na kuniomba ana maana mtaanza kuomba sawasawa na vile nilivyowaonyesha au nilivyowafunulia wakati mliponiita katika haja zenu.Hivi ulishawahi kujiuliza ni mambo gani makubwa na magumu ambayo Mungu atakuonyesha_pindi utakapomuita?. Kumbuka tulikotoka tumeona Kumuita Mungu ni kumfanya Mungu akufunulie mambo usiyoyajua kuhusu hitaji lako ili ujipange vizuri kuyaombea.

Sasa kwenda na kuomba maana yake ni kuomba sawasawa na vile Mungu alivyojifunua kwako kuhusu hitaji ulilonalo.Utakapoomba namna hii ndiko kunaitwa kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu maana yake unaombea mambo ambayo Mungu anataka uyaombee kwa wakati huo. Kwa lugha nyepesi jifunze kuomba mambo ambayo Mungu anakuongoza kuyaombea. Labda nitoe mifano michache ndio somo litaeleweka vema.

Mfano wa kanza huenda mnaombea mgonjwa au mtu aliyefungwa na mapepo. Ni kweli Biblia imesema mtaweka mikono juu ya wagonjwa nao watapata afya. Sasa si kila mgonjwa ni wa kuweka mikono na kuanza kukemea ugonjwa au mapepo, kuna magonjwa mengine yanasababishwa na mawazo yaani tatizo ni mtu mwenyewe, Mwingine huenda ni kwa sababu ya kujeruhiwa nafsi yake na mwingine huenda ni kwa sababu ya dhambi, na mwingine huenda mikataba aliyoingia mwenyewe na mapepo na huenda mengine ni Mungu mwenyewe ameruhusu Shetani aguse afya ya huyo mtu kama alivyomruhusu shetani kwa Ayubu nk..

Saa nafikiri mpaka hapa umeshaona si wagonjwa wote utakawawekea mikono watapona. Hivyo ni vema umuite Mungu akufunulie nini cha kufanya, mwingine atakuambia huyu anahitaji ushauri tu wala si maombi,mwingine anaweza kukuambia huyu ametenda dhambi hii na hii akizitubia nitamponya, na mwingine atakuambia huyu hicho ni kipimo chake mpe tu neno la uvumilivu na Ushindi,Mwingine atakuambia huyu ndugu mwenyewe au wazazi wake waliingia mkataba na mapepo hivyo vunja kwanza mktaba huo nk.

Mfano wa pili,huenda mnaombea kanisa lenu. Ni rahisi kusema tumuombe Mchungaji ndani ya kanisa,mara tuombee kamati ya ujenzi tuombe Mungu kuhusu ujenzi nk.Kweli ni maombi mazuri lakini una uhakika Mungu kwa wakati huo anataka muombee hayo mambo.Huenda kuna roho ya mpinga Kristo ina vamia washirika au kuna maajenti wanajiingiza kwa siri makanisani na kuwapofusha macho ninyi mnakazana kuombea ujenzi. Maana yangu ni hii ikiwa wewe ni mchungaji au kiongozi wa maombi katika kundi lolote lile ni vema kila wakati kumuita Mungu akupe mambo ya kuombea kwa wakati huo. Mungu atakufunulia nini unachotakiwa kuombea kwa wakati huo.

Nina ujasiri na ninachokisema kwa sababu siku moja tukiwa katika kambi la vijana.Nilikuwa kwenye timu ya maombi ya hilo kambi.Ndani ya hiyo timu tulikuwa na wajumbe wa shetani kutoka kuzimu yaani maajenti (vibaraka wa shetani).Hawa jamaa walikuwa wakiomba na kufimga kuzidi masaa yale tuliyokuwa tukifunga sisi.Na wakati wa kuomba walikuwa wanapendekeza tuombee na kukemea roho ambazo hazifanyi kazi katika lile eneotulilokuwepo. Na walikuwa wanajita watumishi wa Mungu.Nina uhakika wa habari hii kwani Mungu alinifungua macho tukaomba na nguvu za Mungu ziliposhuka mmoja wo akasema “sisi ni wajumbe wa shetani kutoka kuzimu,tulitumwa kuleta uharibifu lakini katika yale tuliyotumwa tumeshindwa kuyatekeleza”.

Nakuambia tangia siku hiyo ndipo nilipofunguka macho yangu ya ndani na kuanza kuhitaji uongozi wa Mungu katika yale tunayoomba kila siku.Hujawahi kuona Kiongozi wa maombi anasema jamani hee tutaombea hili na hili na hili,lakini mnapoanza kuomba unakuta Mungu anakuongza kuombea vitu vingine kabisa ?

Kumbuka siku zote katika kila unaloliomba ,mwambie Mungu nifunulie zaidi kuhusu mambo ya kuomba kuhusu hili jambo.lwe ndoa,kanisa,mkutano au semina,Watoto,elimu nk Sasa nimalizie kwa kusema kuomba kwa namna hii ndiko Kibiblia kunaitwa kumtafuta Bwana.Sikiliza huwezi kumtafuta mtu mahali asikopatikana.Unapomtafuta Bwana ni lazima umtafute kwenye maeneo yake yaani kule anakopatikana.Sasa kunaitwa kumtafuta Bwana kwa sababu umeomba kulingana na ufunuo wake

Ni imani yangu kuwa baada ya kuwa umesoma ujumbe huu basi naamini umeshapata maarifa ya kukusaidia katika kumtafuta Bwana na hivyo kwa jambo lolote utakalotaka kuomba siku zote utaomba kwanza ufunuo wa Mungu juu ya hili jambo.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nawe.
Na: Patrick Samson Sanga

JIFUNZE KUMILIKI MAJIBU YA MAOMBI YAKO

Yoshua 13:1-7
Utangulizi,
Katika dunia ya leo watu wengi sana wamekuwa wakitumia muda wao mwingi ikiwa ni pamoja na kufanya maombi ya kufunga na kuomba ili kumuomba Mungu awabariki, awaponye, awalinde kwa kifupi awajibu mahitaji yao waliyonayo mbele zake siku zote. Wapo waliokuwa hawazai wamezaa, vipofu wameona, wasioajiliwa wameajiliwa, biashara za wengi zimefanikiwa, ndoa nyingi Mungu ameziponya, wapo waliotaka kuolewa au kuoa na Mungu amewapa waume na wake wazuri.
Sasa hao hao watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika kuomba Mungu awatendee miujiza katika maisha yao, imefika mahali wanaona yale ambayo yalikuwa ni majibu ya Moambi yao shetani ameyavamia na kuleta balaa zaidi na limekuwa pigo kubwa sana kwa wana wa Mungu. Na kwa sababu hiyo wamejikuta wakimlalamikia Mungu kama vile wana wa Israeli na imefika mahali pa wengine kuona kama Mungu hawezi na hivyo kumuacha.
Tatizo la haya yote ni kwamba wakristo wengi hawana tabia ya au mazoea ya kumiliki mujibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Huenda ulikuwa huna mtoto na Mungu amekupa kuzaa mtoto, sasa huyo mtoto ndiyo jibu lenyewe kutoka kwa Mungu. Sasa ni lazima ujifunze kumiliki huo muujiza wa mtoto, sasa si mtoto tu bali ni pamoja na ajira, ndoa, uponyaji, kanisa, Nchi, Biashara nk.

An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance

  Title: An Academic Critique of Internal Contradictions in the Quran with Reference to Eschatological Descriptions of Hell’s Sustenance Au...

TRENDING NOW