Friday, July 8, 2016

MUHAMMAD AWAAGIZA WAISLAM WOTE KUVAA VIATU WAKATI WANASWALI MSIKITINI


KUMBE KUVUA VIATU NI UTAMADUNI WA WAYAHUDI.
“Nabii wa Allah akatuambia: Msiwe kama Wayahudi wanao Swali bila ya Viatu au viatu vyao vya ngozi (khufoof).” (Abu Dawood, 652; classed as saheeh by al-Albaani in Saheeh Abi Dawood, 607).
Kumbe utamaduni wa kuvua viatu ni wa Wayahudi na sio WAISLAM WANAO KOPIA KILA KITU. Huu ni MSIBA MKUBWA SANA.
SASA TUMSOMEA NABII WA ALLAH:
SOMA UTHIBITISHO HAPA:
Anas ibn Maalik (may Allaah be pleased with him) aliuiza, Je, Mtume Muhammad (PBUH) aliomba huku akiwa amevaa Viatu? Alinijibu NDIO” (al-Bukhaari, 386; Muslim, 555).
Endelea uone kwanini Muhammad alivua viatu mara moja:
Ngoja niwaletee hadith ya Abu Saeed al Khudri alisema: Wakati nabii wa Allah alipo kuwa anaongoza swala kwa Maswahiba wake, alivua viatu vyake na akaviweka upande wa kushoto. Maswahiba wake walipo muona, nao wakavua viatu vyao. Nabii wa Allah alipo maliza kuongoza swala, akawauliza Maswahiba wake, kwanini walivua viatu vyao? Wakamjibu, sisi tumekuona wewe ukivua viatu vyako, na sisi tukafanya hivyo. Nabii wa Allah (amani iwe juu yake) akasema: Jibril (PBUH) alikuja na akaniambia kuwa kulikuwa na uchafu kwenye viatu vyangu. Lakini nyie mnapo kuja Msikitini, vichunguzeni Viatu vyenu na kama mkiona uchafu kwenye Viatu vyenu, basi, safisheni au toeni huo uchafu na muombe huku mkiwa mmevaa Viatu. (Abu Dawood, 650; classed as saheeh by al-Albaani in Saheeh Abi Dawood, 605).
Kumbe basi Muhammad alikuwa anavaa viatu alipo kuwa Msikitini isipokuwa mara moja tu alipo ambiwa na Jibril kuwa viatu vyake vina uchafu.
WAISLAM, KWANINI HAMFUATI MAAMRISHO YA MUHAMMAD YA KUVAA VIATU MSIKITINI NA MNAENDELEA KUFUATA UTAMADUNI WA WAYAHUDI WA KUTO VAA VIATU?
Natanguliza pole kwa Waislam.

No comments:

JIWE JEUSI LA MAKKA

 

TRENDING NOW