Monday, October 10, 2016

MUNGU WA ISRAELI HAKUAHIDI KITABU KIPYA TOFAUTI NA INJILI YA YESU

Na Masudi FK:
Kitabu chochote tofauti na Injili ya Yesu sio ujumbe wa Mungu wa Israeli YAHWEH. Injili ndilo litafundishwa kwa mataifa yote, litahukumu na litaokoa ulimwengu siku ya mwisho ... HAKUNA HAJA YA KITABU WALA UJUMBE MPYA.
-
KABLA YA INJILI YA YESU, MUNGU YAHWEH ALITUMA SHERIA (TORATI) NA MANABII.
Injili ya Mathayo 11:13
<Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana>
-------
MUNGU YAHWEH ALITUMA INJILI KWA KUTIMILIZA TORATI NA MANABII
Mathayo 5:17
<Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.>
--------
INJILI ITAHUBIRIWA KATIKA ULIMWENGU WOTE MPAKA MWISHO WA DUNIA.
Injili ya Mathayo 24:14
<Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Chukizo la Uharibifu>
-----------
MUNGU YAHWEH ALITUMA INJILI ILI KILA MTU AWE NA UZIMA WA MILELE
Injili ya Yohane 3:16
<Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.>
-----------
NENO YA YESU ALINENA NDILO LITAHUKUMU ULIMWENGU SIKU YA MWISHO
Injili ya Yohana 12:48
< Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.>
-------
YESU ALITHIBITISHA KWAMBA MSAIDIZI AMBAYE MUNGU ALIAHIDI ATAFUNDISHA MANENO YA INJILI.
Injili ya Yohana 14:26
<Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.>
----------
MTU YOYOTE AKIHUBIRI MANENO TOFAUTI NA INJILI YA YESU ALAANIWE
Wagalatia 1:9
<Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.>
-----
KUAMINI BILA KUCHUNGUZA NI DHAMBI ... MANABII WA UONGO NI WENGI DUNIANI
1 Yohana 4:1
<Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.>
------
.
MASWALI YA MUHIMU
----------------------------------------
1- Manabii wengi walijitokeza duniani na vitabu tofauti na Injili baada ya kufa kwa Yesu... Walipata wapi vitabu hivyo?
2- Kama Injili ya Yesu ndilo litaokoa, litahukumu ulimwengu na litaubiririwa mpaka mwisho... Ni nini umuhimu wa kitabu kipya au ujumbe mpya?
2. Dini nyingi yalitungwa na manabii duniani.. Waumini wanaabudu Nani kama manabii hawakutumwa na Mungu wa Israeli?
Mungu awabariki sana.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW