Friday, August 26, 2016

ETI BIBLIA INATAJA MASHEHE KWAHIYO INAUNGA MKONO UISLAM, THUBUTU

Wahubiri wa ‘injili potofu’ wa Kiislamu wanaendelea kuhaha kuhalalisha Quran kupitia Biblia. Nasema ‘kuhaha’ kwa sababu hakika kabisa wana juhudi kubwa mno lakini inasikitisha kwa sababu hakuna hata siku moja waliyowahi kusema jambo lenye ukweli kibiblia linalounga mkono quran kama wasemavyo wao – Mungu ni shahidi yangu. Mara waseme Muhammad ametabiriwa kwenye Biblia; mara waseme Yesu aliposema kuwa ataletwa Msaidizi basi alimaanisha Muhammad, n.k. Ni kituko kimoja baada ya kingine. Na wanayemdanganya ni wao wenyewe pamoja na Wakristo wachache wasiojua Biblia.
Kwa msingi huohuo, wanasema eti Biblia imewataja Mashehe; na kwa hiyo kwao huo ni ushahidi kuwa uislamu ulikuwapo tangu zamani.
Acha ninukuu hoja ya mmoja wao kama ilivyo, kuhusiana na suala hili, kisha kama kawaida, utaona jinsi hoja hiyo inavyosambaratika mbele za nuru ya Kristo, yaani neno lake.
Mtu huyu anasema:
"Swali kwenu nyinyi ambao hamjabahatika kuwa waislam, yaani Wakristo. Kama uislam uliletwa na muhammad s.a.w, vipi masheikh watajwe ndani ya agano la kale?
“Ndivyo walivyosimama mikutano miwili yao walioshukuru nyumbani mwa mungu, na mimi, na nusu ya mashehe pamoja nami.” (Nehemia 12:40)
Mkristo jiulize mwenyewe hili swali; mashehe ni viongozi wa dini ipi? waislam...!? au wakristo?"
Mwisho wa kunukuu.
Hapa huyu ndugu wa Kiislamu anaongea kwa ujasiri kabisa na kwa kituo. Na unaona kabisa kuwa moyoni mwake anawaza, “Hapa leo nimewapata Wakristo. Lazima waone kuwa Uislamu ndiyo dini ya kweli.”
Na hivi ndivyo ilivyo kwa hoja zao ZOTE kuhusiana na Ukristo. NI UONGO; NI UONGO; NI UONGO!! NI UPOTOVU MTUPU!!

Na mimi nilimpatia jibu fupi tu na rahisi. Kwanza nikamwambia acha nikupatie maana ya neno ‘Shehe’ kutoka kwenye kamusi ya Kiswahili.
Sheke: mtu mwenye elimu yadini ya kiislamu amabye agh uifundisha kwa watu wengine. pia Shekhe, sheihk
Shehe: Mzee anyeheshimiwa kwa busara kwa busara yake na mashauri anayotoa.
Kama inavyoonekana hapo juu, kuna maana mbili. Na ni wazi kabisa kuwa, kwa ufahamu wa kawaida kabisa, muktadha wa aya hii ya Nehemia haiongelei maana ya kwanza ya neno hili. Kwanza, wakati Nehemia anaandika, Uislamu haukuwapo. Uislamu ni wa juzijuzi tu; miaka 600 baada ya Yesu kuondoka duniani.
Kisha nikamwambia, soma pia aya hiyo kwa Kiingereza. Imeandikwa hivi: “So stood the two companies of them that gave thanks in the house of God, and I, and the half of THE RULERS with me”
Hilo neno ‘mashehe’ limeandikwa kama ‘rulers’ yaani viongozi. tafsiri zingine zinatumia neno Elders, yaani wazee. Na hii ndiyo maana inayoendana na ile ya pili kwenye kamusi, yaani wazee wenye busara.
Hitimisho
Usidanganywe na tafsiri za Biblia zinazotolewa na Waislamu (siongelei tafsiri za quran; hilo ni suala jingine). Tafsiri za Biblia zinazotolewa na Waislamu ni uongo na upotoshaji mtupu kwa asilimia 100. Kila wanachosema kuhusu Biblia ni kifungo kinachowapeleka watu kuzimu kama wakikiamini.
Ukiwaamini, utakuwa umetupa taji yako; na umeuza uzaliwa wako wa kwanza kwa ujira wa kunde kama Esau.
Bwana Yesu anasema:
“Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.” (Ufunuo 3:11)
Kaa chonjo; adui anahaha kila mahali kukuibia uzima wako wa milele.
Tafakari
Hoji mambo
Chukua hatua

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW