Saturday, October 1, 2016

QURAN NA BIBLIA ZATHIBITISHA KUWA PAULO NI MTUME WA MWENYEZI MUNGU LAKINI MUHAMMAD NI MTUME BANDIA
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAM.
Kwa mujibu wa Biblia manabii na mitume wanathibitishwa kwa njia ya miujiza.
Kutoka 14:21” Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari,BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki,usiku kucha,akaifanya bahari kuwa nchi kavu”.
Matendo 19:11-12 “Mungu alifanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida . Hata wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake magonjwa yao yakawaondokea, pepo wachafu wakawatoka”. Tazama pia Matendo 16:16-18, 20:7-12 na Matendo 13:6-12.
Qur’an nayo inathibitisha kuwa manabii na mitume ni lazima wafanye miujiza.
Qurani 40:78 Suratul Al-Muumini [Waumini] inasomeka “Na kwa yakini tumewatuma mitume kabla yako wengime katika wao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia na haikuwa kwa mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”
Muhammad hakupewa kufanya muujiza wowote ili kuthibitisha madai ya unabii na utume wake.
Qur’an 29:50 Suratul Al-Ankabuut (Buibui). “Na walisema “Mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa Mola wake? Sema miujiza iko kwa Mwenyezi Mungu tu (akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi), nami hakika ni mwonyaji mbainishaji (dhahiri tu).” (Taz. Qur,an 6:35-37 13:7,)
Katika Qur’an iko aya ambayo tunapaswa tuitafakari wote kwa pamoja. Katika Surat An-Nisaa, (wanawake), 4:79 “Wema uliokufikia unatoka kwa Mwenyezi Mungu na ubaya uliokufikia unatoka nafsini mwako, mwenyewe umefanya mambo hata yakakufika hayo. Nasi tumekupeleka kwa watu kuwa mtume na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha (hapaitajiwi shahidi mwingine)”
Aya hii inaonesha kuwa Muhammad mtume wa Waislamu, alipelekwa kwa watu kuwa mtume, huku Mwenyezi Mungu akiwa shahidi tu. Siku zote shahidi si mtendaji bali ni mwonaji tu wa tendo lililotendeka.
Hoja yetu tungependa kuwajua hao watu waliompeleka Muhammad kwa watu ni akina nani? Kwa sababu tumeona kule nyuma baada ya Muhammad kutoka pangoni, mkewe Bi. Khadija anamwambia Muhammad kuwa “utume huo!!!!!!! Na Bwana Waraqah ibn Naufal akimwambia Muhammad kuwa “ basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu” kabla ya Qur’an .Je hao si wale “Nasi tumekupeleka” wanaotajwa kwenye aya hiyo hapo juu? Tafakari!!
Muhammad alikuwa nabii wa uongo na mtenda dhambi kubwa kubwa na hakufanya miujiza.
Lakini Mtume Paulo alifanya miujiza mingi sana.
Ndio maana huwa nasema Uislam ni dini ya kutengeneza tu.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW