UTATA MKUBWA SANA NA KUPINGANA NA KUGONGANA KWA QURAN:
Je, Uovu unatoka kwa Shetani, au sisi binadamu au kwa Allah?
Quran inakujibu kuwa, kila kitu kinatoka kwa Allah.
Quran 4:78
Sema: Kila kitu kimetoka kwa Mwenyezi Mungu.
Sasa Quran inachakachua na kusema sio kila kitu kinatoka kwa Allah.
Quran 4:79
Jema lolote linalokupata linatoka kwa Mwenyezi Mungu.
lakini ubaya wowote unaokupata unatoka kwako mwenyewe.
Quran 4:82
Je, hawaitafakari Qur'ani?
Lau kuwa imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
bila ya shaka wangekuta humo khitilafu nyingi.
Bila shaka mambo maovu ni sehemu ya "vitu vyote", na ikiwa "vitu vyote vimetoka kwa Allah" basi maovu pia yanatoka kwa Allah, na mwandishi wa Qur'an hawezi kupitisha hatia na kuwalaumu wengine. kama inavyofanywa katika aya ya 79.
Inafurahisha kwamba Muhammad angejipinga mwenyewe ndani ya aya mbili mfululizo na kisha kuandika aya tatu baadaye kwamba hitilafu ni ishara kwamba haitoki kwa Mungu.
Lakini mada hii bado haijaisha.
Quran 38:41
Mkumbuke Mja wetu Ayubu, tazama alimwomba Mola wake Mlezi.
"Shetani amenitia dhiki na mateso!"
Sasa tuna mtu wa tatu anayejiunga na shindano la kuwajibika. Je, uovu unatoka kwetu? Je, unatoka kwa Shetani? Au umetoka kwa Allah?
Yoyote mawili kati ya hayo yanapingana, lakini hasa mawili ya kwanza (4:79, 38:41) yanapingana na ya tatu (4:78) kwani Allah alidai kwamba vitu vyote vimetoka kwake.
Kwa hakika, sehemu hizo hapo juu ni mwanzo tu wa matatizo yaliyotajwa katika Qur’ani na Hadithi kuhusu suala la kuamuliwa kabla, hiari, na jukumu la dhambi.
Ndio maana naendelea kusema Allah hajaumba kila kitu na Allah sio Mwenyezi Mungu.
Shalom,
Dr. Max Shimba for Max Shimba Ministries
No comments:
Post a Comment