Sunday, September 16, 2018
ALLAH KASEMA MUHAMMAD SIO ROHO MTAKATIFU
ALLAH KASEMA MUHAMMAD SIO ROHO MTAKATIFU
ISA BIN MARYAM HAKUPEWA MUHAMMAD BALI ROHO TAKATIFU QURAN 2:87.
WAISLAM WAWEWESEKA KWA NDEREMO NA KU-PANIC
Tuanze kwanza kwa kusoma aya za Biblia:
Hubiri la kwanza la Yesu baada ya kutoka kufunga siku 40 jangwani linatangaza habari njema ya Yesu. Katika Luka 14:18-19 Yesu anatangaza huduma yake kwa kusema;
“Roho wa Bwana yu juu Yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwaletea maskini habari njema.
Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika”
ISA BIN MARYAM HAKUPEWA MUHAMMAD BALI ROHO TAKATIFU QURAN 2:87.
Qurani nayo pia inakubaliana na ukweli huu kwamba Yesu alitiwa nguvu kwa Roho Mtakatifu. Sura ya 2:87 tunasoma kwamba;
“…na tukampa Isa mwana wa Mariam miujiza mingi na tukampa nguvu kwa Roho Takatifu…”
Je, ina maana Isa Bin Maryam alitiwa nguvu kwa Muhammad kama wanavyo dai Waislam?
Kama dai la Waislam eti Muhammad ni Roho Takatifu, kivipi alikuwepo wakati wa Isa Bin Maryam?
Je, Muhammad aliishi wakati wa Isa Bin Maryam?
Quran hapa inatueleza kwamba Yesu alipewa miujiza mingi. Miujiza hii ni kama ilivyotangazwa na Yesu mwenyewe katika Luka 4:18-19. Katika Quran Sura ya 5:110 tunaona baadhi ya miujiza hii aliyopwewa Yesu ni kuponya watu.
“(Kumbuka) Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Mariam! Kumbuka neema yangu juu yako, na ujuu ya mama yako, nilipokutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu katika utoto na utu uzima. Na nilivyokufunza kuandika na hekama na Taurati na Injili. Na ulipotengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, na ulipowaponyesha, vipofu na wakoma kwa idhini yangu, na ulipowafufua wafu kwa idhini yangu…”
KAMA MUHAMMAD NI ROHO TAKATIFU, KIVIPI ALIKUWEPO WAKATI WA ISA BIN MARYAM ALIYE KUWEPO MIAKA 630 KABLA YA KUZALIWA KWAKE MUHAMMAD?
Kwanini Allah hakusema Isa Bin Maryam alitiwa nguvu kwa Muhammad bali Roho Takatifu?
Kama Muhammad ni Roho Takatifu kama wanavyo dai Waisam, je, alikuwepo wakati wa Isa Bin Maryam?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?
Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...
TRENDING NOW
-
Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kil...
-
Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaid...
-
Adui anakuja kuiba, kuua na kuharibu kila kitu chetu, ni lazima kuwa tayari kupambana na maadui, tujue silaha zetu, na kutumia neno la Mun...
-
Twakusalimu kwa mara ingine katika jina tukufu na takatifu la Yesu Kristo Bwana wetu. Twazidi pia kukushukuru kwa ajili ...
No comments:
Post a Comment