Friday, September 21, 2018

KWANINI SURA YA KWAZA KWENYE QURAN NI AL-FAATIH'A NA SIO SURAT AL - A'LAQ (96) ILIYO TEREMSHWA KWANZA?

Image may contain: people sitting
KWANINI SURA YA KWAZA KWENYE QURAN NI AL-FAATIH'A NA SIO SURAT AL - A'LAQ (96) ILIYO TEREMSHWA KWANZA?
TUNAPO SEMA QURAN IMEJAA SHAKA NA SI MALI KITU HUWA HATUTANII
Sura ya kwanza ya Quran kuteremkani ni Surat Alaq yaani ya 96 na kwa nini sio sura ya kwanza kimpangilio kwenye Quran?
Imezungumzwa na kusimuliwa vizuri katika Hadith ya bibi 'Aisha (r.a)kama ifuatayo:
Bibi 'Aisha (r.a) amesema:" Kilichoanza katika Wahyi wa
Mtume (s.a.w) ni ndoto za kweli. Alikuwa Mtume (s.a.w)
haoti chochote isipokuwa kilitokea kama alivyoota. Kisha
akaona ni bora kujitenga. Akawa anakwenda Jabal Hira
kujilinda na maovu. Basi alikuwa anakwenda Jabal Hira
akifanya ibada masiku mengi na alichukua masurufu kwa ajili hiyo. Masurufu haya kila yalipokwisha alirudi tena kwa Bibi Khadija, aliyemtayarishia masurufu kama yale (ya kwanza) mpaka ikambainikia haki akiwa pangoni Hira. Pale alipomjia Malaika (Jibril) humo pangoni akamuamrisha kusoma,
Mtume (s.a.w) alijibu: "Sijui kusoma". Alinibana kwa nguvu.
mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha
tena kusoma na nikajibu: Sijui kusoma: Kisha akanibana tena kwa nguvu kwa mara ya pili mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha tena kusoma. Nilijibu tena, "sijui kusoma". Akanikumbatia tena kwa nguvu kwa mara ya tatu mpaka nikahisi mashaka, kisha akaniachia na akasema:
"Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba
mwanaadamu kwa pande la damu. Soma na Mola wako ni
Karimu sana.Ambaye amefundisha kwa msaada wa
kalamu.Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa
hayajui." (96:1-5)
Mtume wa Mwenyezi Mungu alirejea na Wahy huu, huku
akitetemeka kwa khofu aliyokuwa nayo. Alikwenda kwa mkewe Khadijah na akamhadithia yale yote yaliyomtokea kisha akasema;
"Nakhofia kuwa kuna kitu kinaweza kunitokea". Khadijah alijibu:
"Hapana! Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu,
hatakufedhehesha. Unakaa vizuri na kuwafanyia wema ndugu na jamaa zako, unawasaidia masikini na fukara, unawakirimu wageni na unawasaidia waliokabiliwa na matatizo."
Kisha Bibi Khadijah alimchukua Mtume (s.a.w) mpaka kwa bin-ami yake, Waraqa bin Naufal bin Asad bin Abdul Uzza, ambaye alikuwa Mkristo. Waraqa wakati huo alikuwa mzee sana na alikuwa hawezi kuona tena. Khadijah alimuambia Waraqa "Sikiliza hadithi ya mpwa wako, Ewe Bin-ami yangu" Waraqa aliuliza, "Ewe Mpwa wangu umeona nini?" Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuhadithia habari yote kama alivyoona. Waraqa akasema:
"Huyu ni yule mtunza siri (Malaika Jibril) ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kwa Mussa. Natamani ningelikuwa kijana na kuishi mpaka wakati huo watu wako watakapokukataa na kukufukuza." Mtume wa Mwenyezi Mungu akauliza:
"Watanifukuza?" Waraqa akajibu kuwa watafanya hivyo na
akasema, "Yeyote aliyekuja na kitu kama hicho ulichokuja nacho alifanyiwa uadui na watu wake, na ningejaaliwa kubakia hai mpaka siku hiyo watu wako atakapokufukuza, ningelikusaidia kwa hali na mali." Lakini baada ya muda mfupi Waraqa alifariki na Wahyi mwingine ulikawia kuja kwa kipindi kirefu. (Sahihi Bukhari)
Mpangilio wa Qur-aan na majina yake yamepangwa na nani?
Majina Ya Sura za Quran yalitoka wapi na yaliteremshwa lini?
Kwanini uumbaji upo kwenye Sura ya 96 na sio ya kwanza kwenye Quran?
Nini maana ya neno Qur'aan?
Kwanini Quran ina Juzuu 30?
Kwanini Surat At Tawb haikuanza na Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi [ Surat At-Tawba[AL-BARA'AT]?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW