Tuesday, January 17, 2017

KWA NINI NAKATAA KUWA MUISLAMU?


Image may contain: text

Katika ulimwengu wa leo kuna njia nyingi za kutumaini. Furaha ya milele na Mbinguni vina hubiriwa kila mahali. Hata hivyo kuna dini na imani nyingi tofauti, filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo (furaha ya milele) vinatofautiana. Na kila mmoja katika tofauti hizo za dini au imani na filosophia na mawazo juu ya tumaini hilo; anaamini ya kuwa amesimama katika ukweli.
ALLAH AMEKWISHA WAHUKUMU WAISLAM WOTE KUINGIA JEHANNAM:
Katika Surat Maryam, Quruan inasema kuwa (19) 71.72. wala hapana yoyote ila mwenye kuifikia Jehanamu, maana ni wajibu wa Mola wako umekwisha kuhukumiwa, nasi tutawaokoa wale wamchao na kuwaacha madharimu hali wamepiga magoti.
Quruan inakiri kuwan kila MUISLAM amekwisha hukumiwa kuingia Jehannam kwa maana huo ndio wajibu wa Allah kuwaingiza WAISLAM Jehannam. Allah anaendelea kusema kuwa, yeye atawaokoa Waislam baada kuingia Jehanam.
Je, haya madai ni kweli?
WAISLAM WOTE KUINGIA JEHANNAM:
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jehannamu wadhalilike.
Katika Surat Ghaafir Allah anaendelea kusema kuwa Waislam wote wataingia Jehannam. Mimi kama Mkristo siwezi kuipenda dini hii ambayo teyari Allah wake amesha toa hukumu ya kwenda Jehannam kwa wote wanao ufuata Uislam.
Zaidi ya hapo, katika Surat Maryam, Allah ameshindwa kutueleza ni kivipi atawatoa watu Jehannam, bali ameweka madai tu kuwa atakuja huko na kuwatoa Waislam.
ALLAH NA YEYE KUIJAZA JEHANNAM KWA MGUU:
Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 371
Imeletwa kwenu na Anas:
Nabii wa Allah alisema: Watu watatupwa katika Jihannam, na Jihannam itasema. "Je, hakuna watu zaidi wa kuingia huku Jehannam?" (50.30) Mpaka Allah atakapo weka Mguu wake Jehannam, na Jihannam itasema, Inatosha, inatosha (qat! qat!)
Katika Sahihi hadith hapo juu, tumesoma kuwa, naye Allah atauweka mguu wake Jihannam, kwasababu Jehannam bado ilikuwa inaita watu waingie huko na au labda ilikuwa bado haija jaa.
Je, wapi tumesoma kuwa Allah aliutoa Mguu wake Jehannan?
Wapi aya ambayo inatuambia kuwa Allah aliingia huko ili awatoe Waislam ambao teyari walisha hukumia kwenda Jehannam kutokana na Surat Maryam?
Ndugu wasomaji, Njia ya kwenda Mbinguni haipitii Jehannam kama ambavyo Allah anadai kwenye Surat tulizozisoma hapo juu. Jehannam haipo pembezoni mwa Mbinguni kama Allah anavyo wafundisha Waislam.
BIBLIA INAKUJIBU:
Biblia ina jibu swali hilo ikisema kamwe waliotumia njia ya motoni kutaka kutokea peponi kamwe hawataiona.
Luka 16:24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
Hii aya ya Biblia inatuhakikishia kuwa, kuna sehemu mbili ambazo zitakuwa na au Walio mwabudu Mungu au wali mwabudu Shetani. Biblia haisemi kuwa wote wataingia Jehannam alafu Mungu atakuja huko Jehannam na kuchukua watu wake, la hasha.
Neno la Mungu linaendelea kusema kuwa: Mithali 16:25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Ndugu msomaji. Biblia imesha tufundisha kuwa mwisho wa njia ya Allah (Surat Maryam 72-73) ni Motoni ambako kumesemwa katika Mithali 16:25.
Ndugu zanguni, hii ni moja sababu nyingi zinazo nifanye niukatae Uislam, maana teyari umesha hukumu wafuasi wake na kuwasweka Jehannam.
Sasa, mimi kama Mkristo kwanini niupende Uislam ambayo unapeleka watu Jehannam?
Karibu kwa Yesu ambako kuna uzima wa Milele. Yohana 14: 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Na kwa mujibu wa Neno la Mungu, Yesu Kristo ndiye NJIA, Mtu hawezi kuja kwa BABA pasipo kupitia kwake (Yohana 14:6).
Kuna wengi hawajui kuwa Yesu Ndiye Hii Njia Nyembamba Iendayo Uzimani…
Hawa akili zao zimetiwa GIZA na Ibilisi (mungu wa dunia hii aka Allah) Ili Isiwazukie Nuru Ya Wokovu, wakamwamini Yesu aliye Utukufu wa Mungu na Sura Ya Mungu (2 Wakorintho 4:3-4).
Hatua ya pili mara baada ya kujua kwa Yesu Ni Njia Kweli Na Uzima na ya kuwa alikufa Msalabani kuchukua DHAMBI na Uovu Wako, lazima sasa UKUBALI ukweli huu moyoni mwako, UAMINI moyoni na kukiri waziwazi kwa kinywa chako ili uweze kupata Wokovu na pia khesabiwa haki (Warumi 10:9-10).
Tunapomwamini Yesu na kazi ya Msalaba, tunachukua SEHEMU YETU YA UKOMBOZI toka Msalabani, na kuimilki kisheria.
wako watu wengi wanaijua njia [Wametimiza Hatua Ya Kwanza] lakini kwa kweli hawaja chukua hatua ya KUYATOA maisha yao kwa Yesu, yaani kuingia kwenye Njia, yaani KUOKOKA!
Watu wengi tuliomo nao kwenye madhehebu na Dini zetu ni watu ambao wako hatua ya kwanza. Lakini lazima uchukue hatua ya pili, uingie kwenye Njia
“Yeye atakayenikiri mbele za watu nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye Mbinguni, bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye Mbinguni,” Mat. 10:32-33.
Yesu Kristo Mwana wa Mungu hakika ndiye, “Njia na Kweli na Uzima.” Hakuna atakaye okoka isipokuwa kwa njia ya Yesu Kristo. Kama ukimwamini Yesu leo na kumtii ujue ya kuwa furaha na amani na uzima vita kuwa vyako; sio katika ulimwengu huu tu, bali na katika ulimwengu ule ujao.
Hizi ndizo sababu chache kwanini nakataa kuwa Muislam.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Max Shimba Ministries Org

1 comment:

Unknown said...

Endeleeni kujifariji

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW