Tuesday, January 10, 2017

MUHAMMAD ALIKUWA NA UGONJWA WA KUSAHAU SAHAU

Image may contain: text
Katika Sahihi Al-Bukhar Vol vi hadithi nambari 556-558 zinamuelezea Muhammad naye Nabii wa Allah alivyokuwa ni mmoja kati ya watu waliosahau aya na sura za Qur’an. Tazama Qur’an 87:6-7. tena Sahihi al-Bukhari Vol vi hadithi nambari 530-557. sijawahi kusoma wala kusikia habari za Nabii yeyote wa Mungu wa kweli aliesahau ujumbe wake.
Maana sisi Wakristo tunasoma katika 2Petro 1:20-21 maneno haya.
“Mkijua neno hili kwanza ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu bali mwanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu”.
Kwa hiyo kwa maana ya maneno haya tunakuwa na shaka na imani ya Kiislamu kuwa Nabii anasahau aya na sura za ujumbe wa Mungu.
Sababu nyingine ambayo ni ya kushangaza ni kuondoshwa kwa baadhi ya aya kwa makusudi tu. Imeelezwa katika Sahihi al-Bukhari Vol vi hadithi nambaro 8 na 527 jinsi Sayyidina Umar alivyoziondoa sura za “ HAFD” na “KHAL’A”. Inasemekana sura hizo zilihifadhiwa na Ibn Ka’b. katika maelezo ya mwanazuoni mmoja Ibn majah yanasema katika heke heka ya mazishi ya Muhammad aya zingine ambazo zilihifadhiwa uchagani mwa kitanda cha bibi Aisha zilikuwa na mnyama wa kufugwa. Hii inashangaza sana, inanishangaza mimi hasa kutokana na yale wayasemayo kinyume na Ukristo. Maana ni wepesi wa kusema kudharau, kubeza na hata kutamka maneno yasiyofaa kwa Wakristo. Ukisema wewe utasikia tu huyo anamkashifu Mtume! Mara nyingi sana hujiuliza mbona Waislamu wengi katika mihadhara humkashifu Yesu tena hadharani? Isitoshe Mtume Paulo kwao amekuwa kama taka taka jinsi wanavyomtukana na kumdharau. Sijasikia watu wanapopiga kelele wakionya na kuwaambia waache kumkashifu Mtume.
Waislamu wengi na wanadamu mamia kwa maelfu kila siku wanamtukana Mungu kwa matendo yao, lakini sijawahi kusikia Waislamu wakiandamana na kuwaonya watu waache mara moja laa sivyo watasusia kila kitu kwa wale ambao wamehusika. Je, huyu Muhammad amekuwa bora kuliko Mungu? Nimechunguza kwa miaka mingi kwamba ukiongea lolote juu ya Allah hutasikia Waislamu duniani wakidai lolote, lakini ukiongea juu ya Muhammad tegemea nlipuko wa Waislamu wakikuzomea karibia dunia nzima. Wakianza mtu mashuhuri au kikundi cha watu mashuhuri hawa wengine watafanya bila kuuliza wala kufikiri. Jambo la kutisha lile ambalo mtu anafedha ambazo fedha hizo si zake bali ni za YEHOVA. Yeye atazitumia kwa kuweka dau eti yule atakaye muua mtu fulani kwa kumsema Muhammad nitampa kiasi fulani cha fedha. Na Waislamu wengine wakishangilia na pengine wakimuombea dua kwa Allah.
Kwa maana hiyo hiyo ukiwaambia ukweli kama haya niyasemayo utasikia wewe hujui, Qur’an siyo mchezo bwana!! Lakini ukiwauliza kwa nini aya za Qur’an zilikuwa katika mchago wa kitanda cha Aisha mke wa Muhammad? Hapo utakosa jibu la msingi. Na kwa wale ambao hawakusoma wataona haya niyasemayo hayakuandikwa katika vitabu vya Kiislamu.
Katika Qur’an Sura 5:48 Surat maida kuna maneno haya ya Allah.
Sisi ndiyo tulioshusha mawaidha haya na sisi ndio tutakao yalinda.
Je, maneno haya ambayo Allah ameyasema yana ukweli gani?
Maana tunajifunza katika mikasa mbali mbali za kupotea kabisa sura na aya za Qur’an kwamba mpaka sasa hazipo kabisa. Je, sisi tunajifunza nini? Je, kama kweli Qur’an ni maneno ya Mungu aliyehai zingewezaje sura na aya zake zipotezwe kabisa kwa mikono ya wanadamu na isiwepo kumbukumbu? Nitakupa mfano mmoja ili upate kuthibitisha kuwa maneno ya Mungu aliye hai hayawezi kupotea kwa mikono ya wanadamu na Mungu asiyalinde. Katika Yeremia 36:1-4 na 21-32 Hapo tunasoma kisa cha mfalme mmoja ambaye alichukizwa na maneno ya Mungu yenye kumuonya akaamuru liletwe na kulikata kwa kijembe hadi lote likamalizika. Lakini mfalme aligundua kuwa kama ataviacha vile vipande watu wangeviokota na kuviunganisha na neno hilo la Mungu aliye hai likaendelea. Mfalme akaamuru vile vipande vichomwe moto vyote.
Mfalme alijua kuwa kwa kufanya hivyo atayafuta kabisa maneno ya YEHOVA. Lakini tunaposoma katika mstari wa Sura hiyo hiyo tunasikia maneno haya:
Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia hapo mfalme hapo mfalne alipokuwa amekwisha kulliteketeza Gombo lile na maneno yote ya kwanza aliyoyaandika Baruku yaliyotoka katika kinywa cha Yeremia akasema: Haya twaa wewe Gombo lingine ukaandike ndani yake maneno yote ya kwanza yaliyokuwa katika Gombo la kwanza ambalo Yehoyakimu mfalme wa Yuda ameliteketeza.
Mungu hakuridhika kuona maneno yake yanapotezwa na mwanadamu. Akaamuru kuyarudisha maneno yale yale ambayo mfalme alichukizwa nayo.
Swali ambalo Waislamu wote wangejiuliza iweje maneno ya Allah yapotee tu hata yasiwe na kumbukumbu? Tunamuaminije yule yule aliyeshusha maneno ya Qur’an kuwa anauwezo wa Kimungu?
Katika hili mimi nimeona mambo mawilli muhimu.
1. Kutoaminika kwa madai ya sura 5:48, kupotea kwa sura na aya kadhaa ambazo Allah anadai alizishusha kuwaonesha sio kuaminika tu bali kukosa uwezo na mamlaka ya Kiungu (Divinity Authority) ya kutunza aya alizo ahidi kuzilinda.
2. Kuhusu madai ya Allah ya NASKH na MANSUWKH yaani aya moja inaweza kufutwa na nyingine hii ni ulaghai wa kibinadamu ili kutoa nafasi ya kubadilisha mambo kwa madai ya kwamba Mungu amesema.
Kwa mfano aya nyingi katika Qur’an inasemekana ni maneno ya watu mbalimbali. Nitakukumbusha tena jambo hili. Katika Sahihi al-Bukhar Vol vi musnad Harba Vol I Saifa ya 23-24 inamtaja sana Ibn Hanbal akimkaririAnnas akisema:
Umar bin Khatab baba mkwe wa Muhammad alisema nimekubaliwa mambo matatu. Nikasema ewe Mtumme wa Allah lau kama tungeweka kisimamo cha Ibrahimu ndipo ilipoteremka aya ya kuweka kisimamo cha Ibrahimu. Tazama Sura 2:125 Surat Bakara.
Neno la Kiarabu la WAAFAQTU (Yaani nimekubaliwa) katika hadithi hiyo lilionesha kuwa Umar bin Khatab alitoa pendekezo kuwa Qibla ya Waislamu kiwe Al-Kaaba na sio kwamba badiliko lile lilitoka kwa Allah Mungu wa Waislamu. Je, mashekhe hili mmnasemaje? Je, kisa cha aya hii ya 125 ya Surat Bakara ni Sahihi aliyosema Bukhari katika hadithi aliyoipokea? Kama sawa basi wapasheni Waislamu waiojua ukweli huu. Na kama siyo sawa toweni ukweli kinyume na yale ambayo Bukhari ameyapokea.
Ikumbukwe katika Sahihi Muslimu Vol:I hadithi 525 na 527 inaeleza kuwa miezi 17 tangu Muhammad ahamie Makka Waislamu walisali huku wameelekea Yerusalemu sawa na Wayahudi. Lakini ilipofika aya ya 125 ya Surat Bakara Qibla kilibadilika na kuwa Al-Kaaba.
Je inatupasa kusemama nini? Ya kusema ni haya: Ashukuriwe Umar bin Khatab kwa pendekezo lake lililomfanya Allah ahamishe Qibla kukipeleka AL-kaaba.
Si hilo tu Umar bin Khatib alilopendekeza bali anasema nikasema ewe Mtume wa Allah hakika wake zako wanaingia nyumbani hali vichwa vyao havijafunikwa? Ndipo alipoamrisha wavae Hijab. Hapo napo ndipo ilipoteremka aya ya kuvaa Hijab sura 33:59. Hili ni pendekezo la Umar na Allah akalikubali.
Haya ni baadhi tu ya mambo yanayoonesha kuwa madai ambayo wanadai Waislamu dhidi ya Wakristo hayana ukweli wowote.
Uislamu kamwe hata siku moja hauwezi kabisa kuufananisha au kuwa na nafasi ya kusema lolote juu yake. Uislamu na Ukristo ni sawa na watu wawili waliovaa nguo mmoja nguo nyeupe isiyo na doa na mwingine amevaa nguo nyeusi iliyo na uchafu wa grisi ya magari. Yohana aliwaona hao waliovaa nguo katika maoni anaandika katika Uf 7:13-18. katika mlango huo anajibiwa na wale wazee maalumu lile swali alilouliza. Akaambiwa hao waliovaa nguo nyeupe ni wale ambao wamepokea wokovu na nguo zao wamezifua kwa damu ya mwana kondoo. Nini maana yake? Ni kwamba hao ni Wakristo waliokubali kulitii neno la Mungu na kuamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu.
Bahati mbaya Wakristo tunapoongelea kuwa Yesu ni mwana wa Mungu Waislamu wasiosoma wale wanaofikiri mambo yaliyo nje ya mwilli wanauliza Mungu alioa lini?
Mke wake ni nani? Inashangaza kweli. Mungu kutamka yeye mwenyewe kuwaambia watu wale wa kwanza kwamba Yesu ni mwana wake aliyependezwa naye hana maana ya kuzaa. Nia ni kuwafundisha watu katika mazingira yao. Mtu anapokujulisha kwamba huyu ni mwanangu maana yake ujumbe wowote atakao muagiza huyo mtoto wake kwako lazima utauamini kwasababu umetoka kwa baba yake. Mungu alitufundisha katika mazingira yetu. Waislamu kwasababu wao huwaza sana mambo ya kimwili ya kidunia utasikia Yesu sio mwana wa Mungu. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa. Je, ni nani anayepinga hayo mambo ya kidunia. Wakristo wanaamini kuwa Mungu hakuzaa kidunia wala hakuzaliwa kidunia. Lakini kiroho akatamka kuwa Yesu ni mwana wake aliyependezwa naye tumsikie yeye.
Njoo kwa Yesu upate kupona.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW