Tuesday, March 14, 2017

ISA HANA UFAHAMU WA MAMBO MBALIMBALIkatika Al-Lu’lu’ war- Marjan,kitabu cha 3 Hadithi na 1528 uk.883 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema “Issa Ibn Mariam (a,s) alimwona mtu anaiba akamuuliza umeiba? akasema hapana ,Naapa kwa Allah ambaye hakuna mola isipokuwa yeye .Issa (a.s) akasema nimemuamini Allah na limeniongopea jicho langu”.

YESU ANAYAJUA YOTE
Yohana 1:47-48 “ Basi Yesu akamwona Nathanael anakuja kwake, akanena habari zake “Tazama Mwizraeli kweli kweli hamna hila ndani yake. Nathaeli akamwambia umepataje kunitambua? Yesu akajibu akamwambia, Kabla Filipo hajakuita ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona”

Yohana 2:24-25 “ Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe aliyajua yaliyomo ndani ya mwanadamu”
Shalom
Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. 

No comments:

 

TRENDING NOW