Sunday, March 19, 2017

UTATU NI UPENDO

Image may contain: text


Yehova anaonyesha upendo wake kwa kutumia Utatu. Hebu ungana nani na uone jinsi upendo wa Mungu ulivyo kwa Mwanadamu.
(a) Baba – Yohana 3:16
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”
(b) Mwana- Efeso 5:25
“Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili yake.”
(C) Roho Mtakatifu – Rumi 15:30
“Ndugu zangu nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kwa upendo wa Roho jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu”
Hoja inayohusu Utatu Mtakatifu iko wazi sana unaposoma Maandiko Matakatifu na ukiyafanya ndiyo dira yako .
Yesu mwenyewe alipokuwa hapa duniani alisema
Yohana 15: 24 “ kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine wasingalikuwa na dhambi ,lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu na kutuchukia “
Swali la ufahamu : Hao watu pale walikuwa wanamuona nani? Baba au Yesu au walikuwa wana muona Yesu ambaye ni Baba? Tafakari.
Katika Yohana 16:13-16
“Lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari zake .Yeye atanitukuza mimi kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari .Na yote aliyonayo Baba ni yangu kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu kuwapasheni habari .Bado kitambo kidogo nanyi hamtaniona”.
Swali la ufahamu: Yesu yuko mbinguni na bado tena yuko duniani pote akiwa nani?
Matendo 20:28
“ Jitunzeni nafsi zenu na lile kundi lote nalo ambalo Roho Mtakatifu amewaweka nyinyi kuwa waangalizi ndani yake mpate kulilisha Kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe”
Swali la ufahamu:
“Aliyesulubiwa msalabani ni Mungu,Yesu au Roho Mtakatifu? Bila shaka ni Yesu Kristo”
- Kwanini Kanisa lisiwe mikononi mwa Yesu aliyesulubiwa? Ni kwa sababu Mungu ,Baba,Mwana,na Roho Mtakatifu ni umoja (1 Yohana 5:6-7)
- Mwana amemtukuza Baba duniani (Yoh 17: 4)Baba amewaketisha mwana katika mkutano wake wa kuume wa kiti chake cha enzi mbinguni.
- (Ufunuo 22:1, Marko 16:19)
- Mwana amempa Roho Mtakatifu kazi ya kulitunza kanisa ambalo Mungu alilinunua kwa damu yake.
Ayubu 11:7-10
“ Je wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikiria upeo wa huyo mwenyenzi? Ni juu mno kama mbingu waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni kufanya nini wewe cheo chake ni kirefu kuliko dunia ni kipana zaidi ya bahari”.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW