Wednesday, March 29, 2017

YEHOVA KWA KIARABU NI YAHUH ( يهوه ) NA SIO ALLAH


Ndugu msomaji,
Ninaendelea kuweka ukweli kuhusu Allah ambaye sio Yehova na wala hajawai sema yeye ni Yehova kwenye Quran yake.
Wakati Biblia inatumia jina la Yehova kwa zaidi ya mara 9000, Allah yeye anasema hivi kwa Muhammad:
"Jua ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Allah..." (Qur’an. 47:19)
Unaona Allah anavyo likwepa jina la Yehova? Sasa tujifunze maana ya neno "JINA" . Waislam wengi kama sio wote hawajui tofauti ya JINA na [Jina la Sifa/wasifa kama Rais].
NINI MAANA YA JINA?
Ngoja kwanza nieleze kiurefu maana ya "JINA" na ASILI YAKE:
Kila mtu au kiumbe au Malaika ana jina lake na jina hilo linabeba kitu kikubwa sana.
Chimbuko ya neno ‘’jina’’ linatokana na neno la kigiriki liitwalo ‘’Sum’’
‘’Sum’’ maana yake ni ukumbusho au kumbukumbu. Ukumbusho au Sum kama ilivyoandikwa katika Biblia ya Kigiriki maana yake ni jina.
-Kwa hiyo maana ya kwanza ya jina/sum ni ukumbusho ambao mtu au kiumbe au Malaika anapewa.
-Jina/sum maana yake ni alama ya pekee ambayo anapewa mtu au kiumbe au Malaima ili kumtofautisha na wengine.
-Jina/sum ni zawadi ya pekee ambayo mtu au Malaika au Kiumbe anapewa.
Vigezo vya kumpatia mtu jina hutofautiana.
Majina mengine huwakilisha heshima ya kipekee.
Wafilipi 2:9-11( Kwa hiyo tena MUNGU alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa MUNGU Baba. )
Majina mengine huwakilisha sifa ya huyo anayepewa jina .
Mfano rais wanchi ni [jina la sifa] ambalo anapewa mhusika.
Majina mengine ni kuonyesha mamlaka mfano [Askari ni jina ambalo linaonyesha mamlaka].
Kwa sababu ya tabia Fulani Fulani baadhi ya majina hutokea.
Mfano mwingine JEHOVAH SHALOM maana yake MUNGU ni Amani yetu hili ni jina jema ambalo linatokana na sifa ya MUNGU katika kuleta amani kwa watu wake.
SASA TURUDI KWENYE MADA YETU: YEHOVA KWA KIARABU NI YAHUH ( يهوه ) NA SIO ALLAH
Nini tafisri ya YEHOVA KWA KIARABU?
Kutokana na Tovuti ya Serikali ya Saudi Arabia ya AL TAFSIRhttp://www.altafsir.com/ Jina la Yehova kwa KIARABU NI YAHUH ( يهوه ). Umeona kuwa Kumbe Yehova sio Allah wa Waislam. Sasa, kwanini Waislam wanalazimisha kuwa Allah ni Yehova?
Majina yana tafsiri yake na yana utaalamu wake wa kuyafsir.
Mungu wa kwenye Biblia anaitwa Yehova (Jehovah/Yahweh) kwa zaidi ya mara 9000. LAKINI Allah hajaitwa kwa jina la Yehova kwenye Quran yake hata mara moja. Kama Allah ni Yehova kwanini Quran imekataa kumwita hivyo?
Mungu vile vile anaitwa Elohim kwenye Biblia kwa zaidi ya mara 2500, LAKINI hilo Jina la Elohim halipo kwenye Quran ya ALLAH.
Yehova ni Jina la Mungu ambalo kwa Kiingereza anaitwa Jehovah na kwa Kiebrania anaitwa יהוה (YHVH) na kwa Kiarabu anaitwa ( yahuh ) au ( يهوه ). ngoja niweke kwa urahisi ili wafuasi wa Muhmmad waelewe;
1. Kiebrania = יהוה (YHVH)
2. Kiingereza = Jehovah
3. Kiswahili = Yehova
4. Kiarabu = yahuh ( يهوه )
Umeona kuwa Tafsir ya Yehova ni YAHUH kwa KIARABU na sio ALLAH. Ingia hapa http://translation.babylon-software.com/…/to-arabic/jehovah/kwa msaada zaidi.
Ndugu msomaji, kwa mara nyingine tean, tunaendelea kuona utofauti wa Allah ambaye ni MPINGA YEHOVA na Mwenyezi Mungu ambaye ni Yehova. "Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako Yehovah, ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote". (Zaburi 83:18)https://www.wordproject.org/bibles/sw/19/83.htm#0
Kutoka 6: 6 Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
Ndugu zanguni,
Kama bado hamuelewi kuwa Yehova ambaye ni YAHUH kwa Kiarabu sio Allah, basi wewe umeamua mwenyewe kwenda kwenye njia iliyo potea ya Jehannam.
ALLAH SIO YAHUH NA HAJASEMA HIVYO KWENYE QURAN.
ALLAH SIO YEHOVA NA HAJASEMA HIVYO KWENYE QURAN.
Nawakaribisha Waislamu wote kwa Mungu wa Kweli anaye itwa YEHOVA.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
Footnotes
http://ivarfjeld.wordpress.com/…/apostasy-40-born-again-ch…/
http://en.wikipedia.org/wiki/Bible_translations_into_Arabic
Correspondence with Robert Morey, Ph.D. May 11. 2012
http://www.islam-watch.org/…/Muhammad-Killing-Jews-of-Banu-…
Correspondence with Robert Morey, Ph.D. May 11. 2012
Correspondence with Bill Warner May 21, 2011
Winning the War with Radical Islam. Robert Morey Ph.D. Christian Scholar Press 2002 p.14.
Bukari Hadith vol.5 book 59 ch.13 no.362 p.241
Correspondence with Craig Blomberg, Ph.D. May 8, 2012
Ibid.
http://www.juancole.com/…/riots-by-some-muslims-in-malaysia…
http://www.adherents.com/Religions_By_Adherents.html
Correspondence with Messianic Rabbi R. Drebenshedt May 11. 2012
http://www.islamicity.com/Mosque/99names.htm
http://www.maxshimbaministries.org/

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW