Friday, March 17, 2017

JE MUHAMMAD ALIKUNYWA POMBE?

Image may contain: 1 person, outdoor
Je Muhamad hakunywa pombe au Quran imekataza pombe hilo ndo swali la kujiuliza. Ukipitia aya za Quran na hadithi za Muhamad utakuta mtume saw alikunywa pombe na pia Quran inaunga mkono na kuruhusu jambo hilo. Bila shaka kuna baadhi ya watu watapinga na kutoa maneno ya kashfa pamoja na matusi lakin lazima ukweli uwekwe wazi. Ingawa baadhi ya madhehebu ya kikristo yanaruhusu pombe lkn leo tutaangalia khs ngd zetu waislam ambao mda mwingi wanawarahumu wakristo eti wanaruhusu pombe.
Kabla ya yote ebu tutazame aya zinazokataza pombe ktk Quran
Quran 2:219. Wanakuuliza juu ya ULEVI na kamari. Sema: Katika hivyo zipo dhambi kubwa namanufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Nawanakuuliza watoe nini? Sema: Kilicho chepesi. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya zake mpate kufikiri.
Hilo neno dhambi katika baadhi ya tafasiri za kiingereza limetumika Harm km ifuatavyo na ktk tafasiri ya kiarabu hamna neno dhambi ktk aya hiyo …….
Kwahiyo katika aya hii hakuna amri ya kukataza pombe moja kwa moja, huko mbele tutaona zaidi, ingawa hiyo aya ilikuwepa waislam na muhamad bd waliendelae kunywa pombe.
Quran 4 :43. Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali MMELEWA,………
Hii aya haikatazi pombe bali inatoa ushauri juu ya waislam ambao walikuwa wana Sali huku wamelewa.
Aya zinazoruhusu pombe ktk Quran
Quran 16: 67. Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ULEVI na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili
Quran 47:15. Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya ULEVI yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?

Je hadithi za mtume Muhammad zinasemaje kuhusu pombe?
Hadithi au Sunnah ni maneno na vitendo ambavyo Mtume Muhammad alikuwa akisema au akifanya katika kipindi chake cha utume. Hadithi hizi ni moja ya miongozo ya imani kwa Waislamu. Hadithi hizi zinajumuisha pia mambo aliyoyaona, kuyasikia au kuyatenda katika muda wa utume. Na hadithi zilikamilika chini ya usimamizi wa Makhalifa wa Abbasid miaka 200 baada ya muhamad kufa.
Muhammad atumia mvinyo mkali:
Sahihi Muslim 3753:'' Sisi tulikuwa pamoja na Mtume wa Allah, na Yeye Mtume wa Allah alikuwa na kiu na mtu mmoja akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, Je, UNATAKA KUNYWA MVINYO? Mtume Muhammad akasema: NDIO. Basi yule Mtu alikwenda kuleta mvinyo. Mtume wa Allah akamwambia: Lete MVINYO ULIO MKALI ILI NINYWE; Basi Mtume wa Allah alipo kunywa ule MVINYO MKALI ALILEWA"
Biblia ishaonya vileo kabla ya muhamad, na muhamad anadai anasadikisha ya manabii waliopita, swali halishindwa kusadikisha ayah ii ifuatayo mpaka akanywa mvinyo mkali? Tazama…
Isaya 5:22 Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;
Muslim-3721 Mtume wa Allah alikuwa anatumia chombo(bakuri) cha jiwe kunywea mvinyo.
Mithali 23:31,32 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu.Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
(Muslim-AlHayd-451). Aisha alikuwa anammiminia mvinyo mtume wa Allah asubuhi na usiku na pia alikuwa anampelekea ndani ya msikiti.
Malaika nao wanakunywa mvinyo
Kuna habari katika Uislam ya malaika walikuwa wanamuliza mwanamke maswali lakini Yule mwanamke hakuwajibu maswali yao mpaka wanywe pombe, nao wakanywa pombee wakalewa na kuua mtoto. (Musnad Ahmad- Musnad almukathareen-5902)
RAFIKI ZAKE MUHAMMAD WALIKUWA WALEVI
Hamza alikunywa mpaka Muhammad akaogopa maana alilewa mpaka akawa kama mwendawazimu. (Bukhari-V,4-B,53-324)
Anas Bin Malek alikuwa akitumika kuwahudumia watu mvinyo (Muslim: 23.4884, 4886)
Mujahedeen walikunywa pombe na kulewa ktk vita vya Uhud. (Bukhari-V4, B52, Nr 70)
Makhalifa (warithi) wa muhamad wanywa pombe (the protectors of Islam)
Yazid I (680-683): alikuwa mtoto wa Muawiyah. Alilewa kila siku mpaka akapata jina la Yazid al-Khumur, Yazid mlevi.
Abd al-Malik (685-705): Alikuwa anakunywa pombe mara moja kwa mwezi; alikuwa anakunywa san asana mpaka inambidi atumie dawa za kuzuia kutapika ili aendelee kuitunza pombe yake aliokunywa.
Al-Walid I (705-715): Alikunywa na kulewa kila siku.
Hisham ((724-743): Alikunywa mvinyo kila ijumaa baada ya swala..
Al-Walid II (743-744): Mtoto wa Yazid ’. Aliogelea kabisa ktk ziwa la pombe mpaka akashindwa kujitambua kabisa mpaka alikuwa aki shuti vipande vya Quran kwa kutumia upinde na mshale.
Pia Khalifa wa Abbasid al-Mamun aliyetawala mwaka 813-833 baada ya Muhammad alikuwa mlevi wa mvinyo kila siku.(Hitti, p.306). Na Makhalifa wa Abbasid ndo waliokusanya hadithi nyingi za muhamad, na pmj na hadithi mashuuri sana ya sahih Bukhar ilikamilika mwaka wa 830-840, miaka 200 baada ya muhamad. Na pia ndio dola ya kwanza ya kiislam(makhalifa) baada ya Rashidun na Ummayed kaliphate kupiga marufuku pombe. Kwaiyo kuanzia Muhamad mpaka ukhalifa wa Abbasid bado waislam walikuwa wanakunywa pombe.
Rejea: ( Mishkah, vol. ii, pp.172-3;; Sahih Bukhari, ibn Hanbal, Musnad (Cairo, 1313), vol.i, pp. 240,287, 320 vol. vi, p.232 (History of the Arabs; Philip K. Hitti, ch. xxvi, p.337)
HITIMISHO
Tumeona jinsi Quran na vitabu vya Allah vinavyojipinga vyenyewe kuhusu pombe, mara inakataza mara inaruhusu, pamoja na kutoa ahadi za ulevi kwa watakao fika ktk pepo ya Allah. Kwaiyo Quran haina jibu la moja kwa moja juu ya pombe. Pia tumeona jinsi mtume wa allah muhamad alivyokunywa pombe pmj na wafuasi wake. Tumeona jinsi malaika wa Allah walivyo kunywa pombe. Na pia tumeona waislam waliendelea kunywa pombe baada ya muhamad mpaka ilivyokatazwa na makhalifa wa Abbasid miaka 200 baada ya muhamad. Kwaiyo nawaonya waislam wote kabla hamjawakosoa wakristo kwa jambo lolote mvichunguze vitabu vyenu kwanza. Maana huko vitabuni mwenu kuna viroja vya kutosha ambavyo mamuma wa kiislam hawavijui. Neno la Bwana linasema ktk Mika 2:11 Mtu akienda kwa roho ya uongo, akinena maneno ya uongo, akisema, Nitakutabiria habari ya mvinyo na kileo; mtu huyu atakuwa nabii wao watu hawa.
Bwana Yesu anasema Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.(Marko 1:15) na Mtume Petro anakazia hapo kwa kusema Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 2:38
Karibuni Kwa Yesu waislam
Bwana Yesu apewe sifa
Shalom,
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW