Tuesday, March 14, 2017

ISSA A.S HANA HADHI YA KUABUDIWA NA BINADAMU YEYOTE.

Qur’an, Suratul Al-Maidah, 5:116 “ Na (kumbukeni) Mwnyezi Mungu atakaposema: “Ewe Isa bin Maryam! Je ,wewe uliwaambia watu: ‘Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu’?” Aseme (Nabii Isa): “Wewe umetakasika na kuwa na mshirika, hainijuzii mimi kusema ambayo si haki yangu (kuyasema, kwa kuwa ni ya uongo), kama ningalisema bila shaka ungalijua ; unayajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako; hakika Wewe ndiye ujuaye mambo ya ghaibu.
YESU ANASTAHILI KUABUDIWA NA WANADAMU NA MALAIKA
Mathayo 2: 2 “yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? kwa maana tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.”
Yohana 9: 35 “ Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yesu akamwambia Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Akasema, naamini, Bwana, akamsujudia.”
Filipi 2:10-11 “ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.”
Ebrania 1:6 “ Hata tena amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu Malaika wote wa Mungu.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

 

TRENDING NOW