Friday, July 21, 2017

KWANINI WANAHISTORIA NA DUNIA NZIMA INATUMIA B.K NA K.K?

Image may contain: text, outdoor and nature



Baada ya Kristo (B.K)
Kabla ya Kristo (K.K)

Yesu alibadilisha mwenendo wa historia. Hata tarehe kwenye gazeti lako la leo inathibitisha kwamba Yesu wa Nazareti aliishi ulimwenguni karibu miaka 2,000 iliyopita. Maandishi kwa Kiingereza "B.C." yanasimamia nyakati kabla ya kuzaliwa kwa Kristo; vilevile maandishi "A.D." yanasimamia nyakati baada ya kuzaliwa kwa Kristo.

Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani.

Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK

Kabla ya Kristo (KK), Hiki ni kipindi cha kihistoria ambacho kinahusisha matukio ya kihistoria ambayo yametokea kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo.

Kwanza katika matukio ya kihistoria Waroma hawakuwa na mwaka sifuri. Na hivyo miaka kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa ilikuwa ikisomwa kutoka juu kuja chini. Kwa mfano, (480-340 K.K) .

Lakini jamii lazima ifahamun kuwa Neno K.K [B.C] lenye maana ya (Before Christ “BC”), lilikuwa ni msingi wa usomaji wa kalenda ambayo ilifuata kalenda ya Walatini ambao walifuata misingi ya Ukristo. Na ifahamike kuwa sio kila mtu alikuwa mfuasi wa dini ya Ukristo kwa wakati huo, hivyo kwa wale wasio fuata msingi ya Ukristo waliamua kuita matukio ya kihistoria kwa namna yao.

Hivyo wapo walioita B.C wakimaanisha “Before Common”. Lakini pia lazima tufahamu kuwa, kuna wakati ambao matukio ya kihistoria yanawakilishwa kwa herufi ndogo “b.c” tambua kuwa tukio hilo la kihistoria limekadiriwa. Kwa ujumla huu ndio mfumo uliokuwepo ukitumika kusoma matukio ya kihistoria kabla ya kiuzaliwa Yesu Kristo.

Pia kuna kipindi kinachofahamika kama Baada ya Kristo (A.D). tunaposema A.D hiki ni kifupisho cha Anno Domini, neno la kilatini lenye maana ya Mwaka wa Bwana au ( in the year of lord), kulingana na mfumo wa kalenda ya Warumi kwa kipindi hiko. Na kihistoria neno hili lilitumika katika kipindi cha karne ya 6 baada ya Kristo. Usomaji wa kalenda kwa kurejerea kuzaliwa kwa Kristo, ulianza pale bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la DIONYSIUS EXIGUUS, ambaye alifanikiwa kuhesabu miaka kwa kuanzia kipindi ambacho Yesu Kristo alizaliwa.

Hii yote ni kumtukuza Yesu Kristo na kuthibitisha kuwa hakuna kama Yesu Mungu Mkuu.

Tarehe yako ya kwenye simu yako ya leo inashuhudia uwepo wa Yesu Kristo

Tarehe yako ya Kuzaliwa inashuhudia kuwa Yesu alikuwepo na ndio msingi mkuu wa kalenda yetu.

Wafilipi 2: 10 ili kwa jina la Yesu, kila goti lipigwe, mbinguni na duniani na kuzimu; 11 na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW